Friday, September 5, 2014

HABARI YA KUSIKITISHA: AJALI YA MABASI MAWILI NA GALI DOGO; WATU 36 WAHOFIA KUFA LEO MUSOMA NI MABASI YA MWANZA COACH NA JUMANNE, TUNAOMBA RADHI KWA PICHA

 
 Basi la J4 Express  T677 CYC lililokuwa linatoka Sirari kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la Mwanza Coach T736 AWJ lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Musoma leo asubuhi saa tano. 
 
 Ajali hiyo  imetokea katika katkati ya daraja la sabasaba, Musoma na habari ambazo hazijathibitishwa zinasema zaidi ya watu 36 wamefariki katika ajali hiyo na wengine wakijeruhiwa vibaya.
Tamasha la Fiesta lililokuwa lifanyika leo kwenye uwanja wa Karume limeahirishwa baada ya ajali hiyo amesema Mkurugenzi wa Maendeleo na Utafiti wa  Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba.
 
Ameongeza kwamba wafanyakazi wote wataungana na waombelezaji pamoja na wananchi wote wa Musoma ili kutoa msaada pale utakapohitajika lakini pia kuomboleza pamoja na wana Musoma kufuatia ajali hiyo mbaya
 
 
Baadhi ya maiti zikiwa zimelazwa chini baada ya kunasuliwa kwenye mabasi hayo
 
Post a Comment