|
HAPA WAPIGA DEBE NA MADELEVA WA MABASI WAKIENDELEA NA MGOMO WA KUSAFIRISHA ABIRIA KWENDA TUKUYU MBEYA NA KYELA |
|
HAPA NI SAA TANO ASUBUHI KATIKA MJI WA TUKUYU NA HAKUNA USAFIRI KWA KWENDA KYELA WALA MBEYA |
|
SASA KWAKUWA VIONGOZI WAMECHELEWA KATIKA KIKAO WALICHOKAA NA VIONGOZI WA MABASI NA KAMATI YA ULINZI NA UASALAMA YA WILAYA SASA VIJANA WAKAENDA KUCHUKUA XSO ILI KUKATA MITI NA KUWEKA BARABARANI ILI KUZUIA MAGARI YEYOTE KUTOPITA BARABARANI HAPO |
|
GALI YA SERIKALI YA PILI KUTOKA KULIA NAYO IKAJIKUTA INAINGIA KATIKA MGOGORO WA KUZUIWA KUFANYA SHUGHURI ZAKE KWA KUWA LEO NI SIKU YA SHERIA NCHINI NA HII GALI NI YA MAHAKAMA YA WILAYA YA RUNGWE HIVYO KUJIKUTA WANASHINDWA KUFANYA SHUGHURI ZAO |
|
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA RUNGWE MALA IKAWASIRI KATIKA UWANJA WA MPIRA TUKUYU ILI KUONGEA NA WAHUSIKA WA MGOMO HUO. ISHU HAPA NANI AMFUATE MWENZAKE WALIO JUKWAANI AU WAGOMAJI WALIOKO STANDI NA BARABARANI? |
|
BUSALA ZIKAFANYIKA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MADELEVA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA KUWAFUATA WAHUSIKA WA MGOMO NA KUWATULIZA KWAKUWA MAKERERE YALITAWALA KWA KILA MTU KUJIFANYA MUONGEAJI WAKASAHAU KUWA WANA VIONGOZI WAO WALIOWATUMA KUONGEA NA UONGOZI WA WILAYA ILI KUPATA MUAFAKA WA MADAI YAO. 1. |
|
|
KATI YA MADAI YA WAGOMAJI NI KWANINI HALMASHAURI YA RUNGWE WAKAMATE GALI YA GOD IS WILING STAND NA IKIWA INAFANYA SERVICE NA KUILIPISHA FAIN LAKI MBILI NA ALOBAINI NA TANO KWA SABABU YA KUCHAFUA MAZINGIRA? BAADA YA KUWEPO SINTOFAHAM KWA SIKU TATU NDIPO MADELEVA WAKAAMUA KUGOMA KULIPA USHURU STANDI HAPO NA KUDAI KUONEWA KWA KUTOZWA KIWANGO KIKUBWA CHA PESA BILA YA UFAFANUZI, KITENDO KILICHOIBUA MALALAMIKO MENGINE MAWILI KUTOKUWEPO KWA HUDUMA YA CHOO KWA MASAA 24, NA SEHEMU YA KUPUMZIKA WASAFIRI KUVUJA MAJI KIPINDI HIKI CHA MVUA. MADAI HAYO BAADA YA KUPELEKWA KATIKA KAMATI YA USALAMA YA WILAYA MAAMUZI YALIYOAFIKIWA NI KURUDISHWA KWA PESA ZA NYONGEZA KWA MAANA YA USUMBUFU NA ULINZI WA GALI LILIPOKAMATWA TSH 145,000/= NA HAO PICHANI DT WA HALMASHAURI YA RUNGWE MR SHIRIMA AMEKABIDHI PESA HIZO KWA MWENYEKITI WA MADELEVA MKOA WA MBEYA NA MADAI MENGINE KUSHUGHURIKIWA KWA WAKATI HUKU CHOO KIKITAKIWA KUFANYA KAZI MASAA 24 BADALA YA UTALATIBU WA AWALI KUFUNGA IFIKAPO JIONI |
|
MWENYEKITI WA MADELEVA MR MWANDUMBYA AKIONGEA MAAMUZI WALIO KUBARIANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA RUNGWE |
|
SASA MAADA IMEKOLEA NA USIKIVU UMEONGEZEKA |
|
MMOJA WA MADELEVA AKIONGEA KELO YA KUFUNGWA KWA CHOO WAKATI WA USIKU |
|
DIWANI WA KATA YA BAGAMOYO MR MADODI AKIONGEA NA MADELEVA NA KUWASIHI KUANZA KUFANYA KAZI NA KUWAASA KUWA NA UTARATIBU WA KUKAA MEZANI KUONGEA NA VIONGOZI WAO PINDI WANANCHI WANAPOKUWA NA KELO KULIKO KUJICHUKULIA MAAMUZI AMBAYO YANAPELEKEA WASAFIRI WENGINE KUSUMBUKA |
|
KAIMU MKURUGENZI WA WILAYA YA RUNGWE MR MWANSASU AKIONGEA NA MADELEVA HAO KUTII SHERIA BILA SHURUTI KWA KUJIWEKEA UTARATIBU WA MATUMIZI MAZURI YA STANDI KULIKO KUFANYA STANDI YA MABASI KUWA SEHEMU YA MATENGENEZO YA MAGALI |
|
MGOGORO UKAISHA NA KAZI ZIKAANZA. HUU MGOGORO UNAOPELEKEA KUFUNGWA KWA BARABARA UMEKUWA WA NNE TANGU MWAKA JANA KWA WANANCHI KUWA NA SABABU ZAO AMBAZO HAZIHUSIANI NA BARABARA KUU ILA WAO HUKIMBILIA KUFUNGA BARABARA KWA KUWEKA VIZUIZI NA KUCHOMA MATAILI ILI KUSHINIKIZA UONGOZI UWASIKIRIZE KWA HARAKA. KWA MFANO MGOGORO WA KIWILA MWANKENJA KUMWONDOA MADARAKANI MWENYEKITI WA KUJIJI VIJANA WALIJIKUSANYA NA KUCHOMA MATAILI NA KUCHOMA MOTO ZAHANATI YA KIJIJI ILI TU KUMWONDOA MWENYEKITI WAO JE ZAHANATI NI YA NANI NA KWA NINI UCHOME NA KUVUNA PAMOJA NA KUIBA VITU? |
|
VIONGOZI WA MABASI WAKAWA NA KIKAO CHAO CHA KUHITIMISHA MGOGORO HUO |
MKUU WA WILAYA CHRISPIN MEELA AWAONGOZA WAKAZI WA RUNGWE KATIKA SIKU YA SHERIA NCHINI
|
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE AKITETA JAMBO NA DAS MOSES MWIDETE KATIKA SHEREHE HIYO |
|
SHEREHE ILIANZA KWA BURUDANI ILIYO JAA MAUDHUI YA KUPINGA RUSHWA NA UWAJIBIKAJI KATIKA KAZI HASA SECTA YA MAHAKAMA |
|
KWAYA YA SEKONDARI YA BULYAGA |
|
HAKIMU MKAZI WA WILAYA YA RUNGWE MHE, O.H. KINGWELE |
|
MR LEBI G. MWAKATOBE |
|
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE ALIYE MBELE NA NYUMA MWENYE KOTI JEUSI NI MHE, MWAKIPUNGA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA BUSOKELO |
|
SHEREHE ILIANZA KWA DUA NA MAOMBEZI |
|
BAADHI YA WWAFANYAKAZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA RUNGWE |
|
WADAU WA RUNGWE NA MWENYE SHATI JEUPE NI DIWANI WA KATA YA BULYAGA MR MWALUSAMBA |
|
WADAU |
|
MWENYE TAI NI MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA RUNGWE NA MWENYE SHATI JEKUNDU NI MR JEREMIA MENEJA WA PRIDE WILAYA YA RUNGWE |
|
KATI YA VITU VILIVYO CHEKESHA WATU NA KUHUZUNISHA NI MATUMIZI MABAYA YA PESA YA SERIKALI NI PALE MKUU WA WILAYA CHRISPIN MEELA ALIPOKUWA AKIONGEA NA WANANCHI KUHUSU ADHABU MBADALA KULIKO KUWALUNDIKA WATU HATA WENYE MAKOSA MADOGO GEREZANI NA MKUU WA GEREZA AKADAKIA NA KUSEMA KUWA "MKUU PALE KWANGU KUNA MTU AMEFUNGWA KWA WIZI WA KUKU KWA MIEZI SITA HADI MWAKA NA UKIANGALIA GHARAMA YA KUKU NA CHAKULA ANACHOKULA KWA SIKU NI GHARAMA SANA MAANA KWA SIKU MFUNGWA MMOJA ANATUMIA TSH 8000/= JE KWA MIEZI SITA AU MWA HUO ATAKAYO KUWA HAPO KWANGU ATATUMIA SHILINGI NGAPI?" |
|
HIZI NI TABASAM ZA NJE YA MAHAKAMA NGOJA WAWE KAZINI UWAONE WANAVYO KUUWA |
|
KATIKATI YA SHEREHE UMEME UKALETA HITILAFU LAKINI MAFUNDI WA TANESCO WALISHUGHURIKIA NA MAMBO YALIENDELEA KAMA KAWAIDA |
|
KIJANA AKILAP KWA HISIA KALI MAUDHUI YAKE NI KUPINGA RUSHWA MAENEO YA KAZI MAANA WANYONGE WANAONEWA NA WENYE PESA |
|
HAKIMU MKAZI MFAWIDHI WA WILAYA YA RUNGWE AKIONGEA NA WANANCHI NA WADAU NA VIONGOZI KUWASHUKURU KWA KUFIKA KWAO KUJUA NINI MAHAKAM INAFANYA NA KUTAMBUA CHANGAMOTO ZAKE |
|
PICHA YA PAMOJA |
|
PICHA YA PAMOJA YA WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA WILAYANI RUNGWE |
|
MUNGU IBARIKI TANZANIA |
AKIONGEA NA WANANCHI NA WATENDAJI WA MAHAKAMA MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AMEWATAKA WATENDAJI WA MAHAKAMA KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA NA AMEWATAKA WANASHERIA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU KWAKUWA CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA NCHINI ZA MIKATABA MINGI KUWA NA KASOLO NI KUTOKANA NA WANASHERIA KUTOKUWA WAADILIFU NA UZALENDO WA NCHI YAO
PIA AMELITAKA JESHI LA POLISI KUFANYA KAZI KWA KUFUATA UTARATIBU WA SHERIA KULIKO KUWABAMBIKIZA WATU KESI ILI TU KUWAKOMOA AU KUJIPATIA KIPATO KISICHO HARALI KWAO
ZAIDI MEELA AMESEMA WANANCHI WAKIKATAA KUTOA RUSHWA BASI HAKUNA HAKIMU ATAKAYE MFUATA MTU KUOMBA RUSHWA HIVYO AMEKEMEA RUSHWA KUWA NI ADUI WA MAENDELEO KATIKA KILA NYANJA NA KUWATAKA KILA MTU KUWAJIBIKA KATIKA NAFASI YAKE NA KUFUATA UTARATIBU WA SHERIA BILA SHURUTI
MKOANI MBEYA
|
JAJI
MFAWIDHI NOEL PETER CHOCHA AKIJIANDAA KUKAGUWA GWARIDE LILILOANDALIWA
NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA
NCHINI |
|
JAJI MFAWIDHI NOEL CHOCHA AKIKAGUA GWARIDE LA KIKOSI CHA FFU MBEYA |
|
KAIMU
KAMANDA WA POLISI NA MKUU WA MKOA MBEYA PAMOJA NA WATUMISHI WA MAHAKAMA
KUU WAKIWA WANAANGALIA GWALIDE LA KIKOSI CHA FFU MBEYA |
KITAIFA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia leo Februari 6, 2013 katika
maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania
jijini
(PICHA NA IKULU)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman,
Jaji Kiongozi Mhe Fakihi Jundu, Jaji January Msofe, Spika Anne Makinda,
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Mathias Chikawe na Mkuu wa mkoa wa Dar
es salaam Mhe. Saidi Mecky Sadik leo Februari 6, 2013 baada ya kuhutubia
katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya
Tanzania jijini
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mchungaji Christopher Mtikila leo
Februari 6, 2013 baada ya kuhutubia katika maadhimisho ya Siku ya
Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini. Kushoto ni Jaji
Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman
Viongozi
wa dini ya Kihindu wakielekea kwenye kipaza sauti ili kuomba dua leo
Februari 6, 2013 wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya
Mahakama Kuu ya Tanzania jijini. Viongozi wa dini za Kiislamu na
Kiktristo pia walishiriki kwenye maadhimisho hayo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa
Mahakama ya Rufaa leo Februari 6, 2013 katika maadhimisho ya Siku ya
Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania leo Februari 6, 2013 katika maadhimisho ya
Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na majaji wakuu
wastaafu na viongozi wengine leo Februari 6, 2013 katika maadhimisho
ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa dini
pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu Rais wa Mawakili leo Februari 6, 2013
katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya Mahakama Kuu ya
Tanzania jijini
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanasheria
leo Februari 6, 2013 katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje
ya Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu leo
Februari 6, 2013 katika maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini nje ya
Mahakama Kuu ya Tanzania jijini
MNAMO
TAREHE 06.02.2013 MAJIRA SAA
00:30HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA
MWAMBANI – MKWAJUNI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI G.68 PC JAFARI KARUME MOHAMED MIAKA 30,MUHA
WA KITUO CHA POLISI MKWAJUNI
ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO .
CHANZO CHA TUKIO NI MAJAMBAZI
WANNE WAKIWA NA SILAHA
IDHANIWAYO KUWA AINA YA SMG WALIVAMIA KITUO CHA MAFUTA KILICHOPO KIJIJI
CHA MATUNDASI MALI YA SAMORA S/O MUYOMBE
NA KUPORA PESA TSHS 2,200,000/=
WAKITUMIA GARI T.227 BST AINA YA TOYOTA COROLA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA SHABAN S/O MSULE,MIAKA 33,MBENA MKAZI
WA MAKAMBAKO .MAREHEMU AKIWA DORIA NA ASKARI WENZAKE WALIFUATILIA TUKIO HILO NA
KATIKA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI ASKARI HUYO ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA
RISASI UBAVU WA KULIA NA KUKIMBIZWA HOSPITALINI KWA MATIBABU ZAIDI . KATIKA
TUKIO HILO JAMBAZI SHABAN S/O MSULE
ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI .GARI
LILILOTUMIKA KATIKA TUKIO HILO LIMEKAMATWA NA MAGANDA 9 YA RISASI AINA
YA SMG/SAR NA RISASI 6 ZIMEOKOTWA ENEO LA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU ASKARI G.68 PC JAFARI KARUME MOHAMED
UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO .MSAKO MKALI UNAENDELEA CHINI YA UONGOZI WA RCO
MBEYA ROBERT MAYALA – SSP, ASKARI POLISI NA WANANCHI ILI KUWABAINI NA KUWAKAMATA WATUHUMIWA
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU
MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI
ANATOA WITO KWA MTU/WATU WENYE
TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE , VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA.
[ BARAKAEL MASAKI – SSP ]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Stars yaichapa Cameroon 1-0
|
HA HA HA HA WATANZANIA |
No comments:
Post a Comment