Sarah
A. Mwaseba
Ndugu wanahabari, salaam!
Ndugu wanahabari, Kwanza hatunabudi
kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ulinzi anaotupatia na uwezo wa kutambua fikra
zetu. Tunawashukuru viongozi wetu wa NCCR - Mageuzi kwa kututambua na kufika
Mbeya ili kutupokea.
Pia tunawashukuru waandishi wa habari
wote kwa kazi nzito inayowafanya muwe maadui na marafiki katika utekelezaji wa
majukumu yenu kwa Taifa letu. Mungu na awajalie ulinzi mkuu katika kutekeleza
majukumu yenu.
Ndugu Wanahabari,
Sisi ni sehemu tu tunaohamia
NCCR-Mageuzi kutoka CHADEMA na vyama vingine. Kimsingi tumetangulia na tumeamua
kujitokeza mbele ya watanzani kupitia kwenu wanahabari ili kuwa mashuhuda wa kisiasa.
Wapo wenzetu wanaohama kimya kimya
kimwili na kifikra. Lakini wapo wengine tuliowaacha huko kwenye matawi yetu
tunakwenda kuwapokea na kuanza nao kazi mpya katika Demokrasia ya kweli na
mfumo bora wa kiutawala ndani ya NCCR Mageuzi.
Wapendwa wanahabari, harakati zetu
zina historia tofauti katika siasa za nchi hii. Wapo ambao leo hii wanarudi
NCCR baada ya kuhama miaka kadhaa iliyopita.
Lakini wapo pia wanaotoka CCM
na CUF. Lengo letu ni kuitoa CCM madarakani na kujenga utawala wa sheria na
Demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyetu.
Kwa furaha kubwa kabisa tunapenda
kuchukua fursa hii kuwatangazia wana Mbeya na umma wa Watanzania kwa kuvunja
ukimya na sasa tunatangza rasmi kujiunga na Chama Cha NCCR- Mageuzi (
National Convention For Construction and Reform- Mageuzi) na tunasema tena
kuwa, tumejiunga kwa hiari yetu kutokana na kuikimbia CHADEMA kwa mambo yake
ambayo kwa uchache tunayaeleza kama ifuatavyo:
·
Uongozi wa kitaifa umefeli kujenga demokrasia ya kweli ndani
ya chama kwa kukumbatia ufisadi wa kutumia vibaya ruzuku ya chama.
Chadema mikoani imebaki ni
kujichangisha fedha kwa kila tukio la ujenzi wa chama utadhani hakuna pesa za
ruzuku na michango ya wafadhili.
·
Uongozi mbovu wa Mhe; Mbowe na dk. Slaa kwa kushindwa
kusimamia katiba ya chama katika kutatua migogoro ya chama na kuishia kuwa na
mbinu ya kufukuza wanachama wema kwa majungu wanayoyajenga wenyewe.
·
A tukisema ukweli wa ouvu wao jamii haiwezi kuamini.
Wanajidanganya!!!! Hii ni ishara ya kufinyanga katiba na kutoiheshimu
dhana ya nguvu ya umma.
·
Chama kujaa utashi wa nguvu ya umma na kulazimisha
maandamano, migomo kwa vitu visivyo na ulazima.
Sisi hatuwezi kuamini pamoja na
watu walio na malengo ya kuleta fujo kitaifa kwa kisingizio cha kutafuta
ukombozi mpya wa taifa.
·
Hatua ya kuwafukuza fukuza viongozi bila kuwasilikiliza
hususani wa nyanda za juu kusini.
·
Dk. Slaa kulipwa mamilioni ya pesa kama mshahara wake na
posho lukuki amejikusanyia na watu anaowataka Makao Mkuu.
·
Akina mama Mbeya walihamasishwa kuwa tuwe tunampokea
mchumba wa Katibu mkuu slaa kama mke wa raisi kumbe ni mwanachama wa kawaida
anayetumia vibaya rasilimali za chama.
·
Uwezo mdogo wa kutekeleza ahadi alizoahidi mbunge wa mjini
‘joseph mbilinyi’ kwa wananchi wa mbeya. Ameacha kuufanya ubunge kuwa ni
taasisi nyeti ya umma na ameamua kuutumia kama jukwaa la muziki na ameonesha
Mbeya hatuna uwezo wa maendeleo ya pamoja.
Wakati wa kampeni aliahidi kujenga mabwawa ya samaki, bandari ya
nchi kavu, vifaa vya hospitalini, benki ya wana Mbeya, umoja wa akina mama,
vikundi vya ujasiliamali vya kijamii, kuinua wasanii wa mbeya, kulifanya jiji
la mbeya liwe mfano wa kuigwa Tanzania.
Pia aliahidi kutatua kero ya elimu
(shule za kata), usafi wa jiji, mpango mzuri wa masoko ndani ya jiji. Lakini
hadi leo hakuna anachofanya zaidi na hata bungeni na kupandikiza chuki za
kukataa kupokea Raisi wa nchi anapokuwa na ziara mkoa wa mbeya.
· Mbunge ameendelea kuchochea wanachama
asiowataka wafukuzwe nafasi za uongozi na anaowataka walindwe.
Aliwahi mwambia DK, Slaa kuwa akimtoa
mwenyekiti wa wilaya ya mbeya mjini basi, yeye anarudisha kadi; masikini bila
kujua mzee wa watu dk. Slaa akamsikiliza na akageuka mbogo kwenye kikao cha
ndani na kuamua kuwalinda waharifu wa siasa za Mbeya na kuwafukuza ambao ‘SUGU’
hawataki. Dk. Slaa alionesha uwezo mdogo wa kudadavua mambo ya maneno ya
majungu.
Tumechukua uamuzi huu mzito wa kuhama
chadema na kujiunga na NCCR-Mageuzi kwa kuwa NCCR kwa matendo kimeonekana kuwa
chama cha UTU na chenye misingi bora ya usawa, uheshimu wa haki za wanachama na
watanzania na chenye mshikamano wa kweli.
S/N
|
JINA MWANACHAMA
|
WADHIFA NDANI YA CDM
|
KATA/TAWI
|
1:
|
Moses Aliko Mwasubili (bulldozer)
|
Katibu mwenezi wa wilaya
|
Mbeya mjini
|
2:
|
Emmanuel Amani Mwangoka (Cash Money)
|
Mpambe wa mbunge/mwanachama
|
Mbeya mjini
|
3:
|
Magrethy John M ota
|
Mjumbe wa kamati tendaji
|
Kata ya Isyesye
|
4:
|
Hosea A. Mwangoje
|
Mjumbe kamati tendaji na MC Kampeni za mbunge – SUGU
|
Mbeya mjini
|
5:
|
Sarah A. Mwaseba
|
Mwenyekiti wa BAWACHA
|
Kata ya Isyesye
|
6:
|
Emmanuel Nehemiah Ngogo
|
Mwenyekiti
|
Tawi la Tawi
|
7:
|
William Swila
|
Katibu mstaafu wa Wazee
|
Mkoa wa mbeya
|
8:
|
Jonathani Mwakalinga
|
Katibu mwenezi wa Kata
|
Kalobe
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Kimepitia migogoro mingi na ya
kutisha lakini bado ni imara na hivyo ni vema watanzania wakajenga imani na
chama Komavu kuliko CHADEMA ya watu wachache na iliyo furika majungu na ukabila
pia haina ukomavu na uzoefu wa migogoro. Migogoro kidogo tu iliyopo wamepoteana
na bado wameandaa migogoro mingi ya uchaguzi wa ndani ya chama.
Imetolewa na sisi:
Majina ya wanaohama toka CHADEMA
kuingia NCCR - MAGEUZI.
|
Mmoja
wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye inadaiwa kuwa
ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi
(Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo wake
wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na
kung’ara mkoani |
|
Mjumbe
wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la
kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
|
|
Aliyekuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi ,
Januari 20 mwaka huu Eddo Makatta Mwamalala.
|
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa Kigoma wakati wa uzinduzi
wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuzindua
ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wananchi wa Kigoma wakati wa uzinduzi
wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za
Tanzania, Uganda na Burundi Bw Phillipe Dongier, wakifunua kitambaa cha
jiwe la msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma
leo Januari 4, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na viongozi wengine baada ya
uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi mbalimbali wakipata maelezo juu ya
ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma toka kwa mhandisi George
Sambaliwakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo
Januari 4, 2013
Msanii
Diamond na kundi lake wakitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa
ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
Mkurugenzi
Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw.
Phillipe Dongier akitoa hotuba kwa kiswahili fasaha wakati wa sherehe
za uzinduzi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo Januari 4, 2013
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya
Muungano eneo la Kibaoni wilayani Uvinza, Kigoma, akiwa njiani kuelekea
mjini Kigoma, akitokea kukagua ujenzi wa daraja la Mto Malagarasi leo
Waziri
wa Habari, Vijana ,UtamaduninaMichezoDkt. Fenella Mukangara akifungua
mkutano wa maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa serikali mjini
Dodoma. Pamoja na mambo mengine amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia
weledi na kutoa taarifa sahihi kwa umma mara kwa mara kuhusu shughuli
mbalimbali zinazofanywa na serikali.
(PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO)
Maafisa
Habari, Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja
naWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya ufunguzi
wa kikao kazi hicho mjini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba
Nkinga akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa Kikao
kazi hicho mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwasilisha mada
kuhusu Mtazamo mpya wa Mawasiliano katika Vitengo vya Mawasiliano
Serikalini wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na Mawasiliano
wa Serikali mjini Dodoma.
Afisa
Habari wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Sarah Reuben
akichangia moja ya mada katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa Serikali mjini Dodoma.
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi chao kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi Mjini Dodoma.
Mmiliki
na muendeshaji wa mtandao wahabari na matukio wa Mjengwa Blog kutoka
Iringa Bw. Majjid Mjengwa akitoa mada kwa maafisa Habari, Elimu na
Mawasiliano wa serikali kuhusu Faida na Changamoto za matumizi ya
mitandao ya kijamii kwa mawasiliano serikalini mjini Dodoma.
NA MWANDISHI WETU,MBEYA.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Kyela kimesema viongozi
wa CHADEMA wanataka kutumia fursa ya uwepo wa mafuta katika tarafa ya Ntebela, kuwachochea
wananchi kufanya fujo.
Kufuatia hilo,kiimewatoa
hofu wananchi kipo makini, na kitahakikisha kinatoa elimu sahihi kwa wananchi
juu ya utafiti wa mafuta uliofanyika hivi karibuni, na kubaini uwepo wa mafuta
katika baadhi ya kata za tarafa hiyo.
Kaimu Katibu wa CCM wilayani humo, Richard Kilumbo,
aliyasema hayo mbele ya Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM,
Sambwee Shitambala, kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.
Kilumbo alisema:”Juzi na jana wenzetu wa CHADEMA wamekuwa
wakiwashawishi wananchi ili tuingie kwenye vurugu kama
ilivyotokea hivi karibuni mkoani Mtwara, baada ya kuonekana wilaya yetu inayo
mafuta na utafiti umefanyika bado taarifa rasmi kutolewa”.
Aliongeza hivyo CHADEMA wanataka kutumia fursa hiyo ya
kuwepo mafuta wilayani Kyela, kuwahamasisha wananchi kufanya vurugu ili
machafuko yatokee wilayani humo kitendo ambacho Chama hakiwezi kukubali.
Kaimu Katibu wa CCM wilaya, aliwataka wananchi kuondoa hofu
juu ya hilo, kwani mwananchi yeyote ambaye eneo lake analolimiliki
likionekana kuwa mkondo huo wa mafuta atalipwa fidia stahili.
Kilumbo alisema wananchi waondoe dhana potofu
inayopandikizwa na viongozi wa CHADEMA, kwani CCM itahakikisha hakuna mwananchi
anayestahili haki yake halafu akadhurumiwa.
Aliongeza Chama kipo tayari kupambana na CHADEMA na vyama
vingine vya upinzani wilayani humo, ambavyo vinajiandaa kufanya kama yale
yaliyotokea mkoani Mtwara wananchi kugomea gesi isisafrishwe kwenda Dar es Salaam.
Kilumbo alisema:”Chama kitapita kata zote ambazo mkondo huo
wa mafuta umeonekana na kutoa elimu sahihi juu ya uwepo wa mafuta wilayani
kwetu…walifanikiwa kuwachochea wananchi wa Mtwara, lakini kwa wilaya ya Kyela
wasahau kwani hilo
halitawezekana kamwe”.
No comments:
Post a Comment