Mgombea
ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani
Kikwete akiongea na waandhishi wa habari na kufafanua mambo mbalimbali
katika Ikulu ya Msoga leo ikiwani muda wa lala salama za kampeni katika
uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Jumapili Aprili 6 jimboni humo.
Mgombea
ubunge wa jimbo la Chalinze kupitia Chama cha Mapinduzi Ndugu Ridhiwani
Kikwete akifafanua zaidi mambo kadhaa wakati alipozungumza na waandishi
wa habari katika Ikulu ya Msoga leo.
…………………………………………………………………………………………………………….
Ridhiwani anasema ameingia CCM akiwa na umri wa miaka minne na wakati huo aliiingia kwasababu ya kupelekwa kucheza.
Anasema akiwa CCM na umri wake huo, alipata bahati ya kushiriki katika halaiki na alifanikiwa kucheza gwaride.
Wakati huo alikuwa na umri wa
miaka mitano na wakati huo Rais Jakaya Kikwete alikuwa Monduli akitoa
mafunzo ya Jeshi la Wananchi.
“Wakati nikiwa tayari nimeingia
CCM kama Chipukizi , mzee wangu alikuwa hayupo CCM.Hivyo unaweza kuona
namna ambavyo hali ilivyo.
Alifafanua kuwa mwaka 1984 alikuwa kiongozi wa gwaride Nachingewa lakini pia alifanikiwa kuwa kiongozi wa gwaride mwaka 1987.
“Rama Kisauti na Rajivu Fundikira,
William Lukuvi nilikutana nao Dar es Saalam ambapo kwa wakati huo
waliniambia wanataka kuanzisha gwaride Dar es Salaam.
“Nilikuwa mmoja wapo katika
gwaride hilo, pamoja na wenzangu wengine akiwemo Tamila Makene.Pia
nilikuwa kamanda wa gwaride.Wakati mzee wangu akiwa Naibu Waziri wa
Nishati na Madini.
ENDELEA .........................................
“Wakati huo kulifanyika uchaguzi
wa kumtafuta kiongozi kwa chipukizi wa CCM katika Wilaya ya
Ilala.Niliombwa nigombee lakini nikataa,hivyo nikaombwa kufanya
hivyo.Nikaletewa fomu,sikumbuki kama nilitia saini au kidole
gumba,”anasema.
Historia yake katika CCM ni ndefu na nyenye kukumbuku nyingi za wapi alitoka na hadi alipofika sasa.
Anasema akiwa kidato cha kwanza
akawa mwalimu wa kufundisha chipukizi na ilipofika mwaka 1998 akiwa
kidato cha tano, anakumbuka Rais Benjamin Mkapa anakwenda Iringa , yeye
alikuwa Shule ya Sekondari Mkwawa.
Alisema wakati akiwa katika shule
hiyo, alifuatwa na viongozi watu wa CCM ambapo walimufuata Ridhiwani na
kisha kumuomba atafute vijana wenzake ili kwenda kumpokea Rais.
Alisema ilipofika mwaka 2000,
waliitwa tena kufanya kazi ya kuhamasisha vijana ili kusaidia chama
katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka huo.
“Kwa mara ya kwanza ndio ilikuwa
naingia rasmi katika kufanya kampeni za uchaguzi mkuu ili kuhakikisha
Mkapa anashinda tena urais.
“Mwaka 2001 akiwa chuoni ulitokea
uchaguzi Wilaya ya Bagamoyo, nilifuatwa na Rehema Rashidi akitaka
nigombee uenyekiti.Nilikataa.
“Hivyo akatafutwa Said Mtanda ili agombee nafasi hiyo lakini naye alikataa lakini baadaye akakubali na alishinda,”alisema.
Hata hivyo baada ya kushinda Mtanda aliamua kumchagua Ridhiwani kuwa Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM Wilaya ya Bagamoyo.
Alifafanua katika maisha yote hayo hajawahi kumshirikirisha mzazi wake(Rais Jakaya Kikwete).
Alisema anakumbuka akiwa katika nafasi hiyo ndipo alipoitwa na Rais Kikwete wakati huo akiwa mbunge wa Chalinze.
“Nakumbuka aliniambia wewe ndio
Katibu wa Uhamasishaji Bagamoyo , ndipo aliponiomba nihamasishe vijana
wenzangu kujenga shule ya sekondari Changalikwa.
“Wakati tunajenga shule, huku
chuoni nako mambo yakawa yanakaribia kumalizika.Hata hivyo tukashauriana
na wenzangu kuwa na ndipo tukagombea tena nafasi ya UVCCM Mkoa wa
Pwani,”anasema Ridhiwani.
Anaongeza katika kipindi chote hicho hajawahi kushauriana jambo lolote kuhusu siasa na Rais Kikwete.
“Baada ya kupata nafasi hiyo katika Mkoa wa Pwani, wakati huo tayari bwana Kikwete amekuwa Rais.
“Akiwa Mwenyekiti wa CCM,
Ridhiwani Kikwete alikwenda na wenzake kuzungumza na Rais na ndipo
walipofanikiwa kusaidiwa vifaa mbalimbali vya UVCCM nchima
nzima,”alisema.
Pamoja na yote hayo alisema katika siasa, hana kundi lolote yupo kwa ajili ya wote.
“Nafanya siasa ya kwangu mwenyewe sina siasa ya baba yangu.Nasaidiwa na marafiki zangu.Wananisaidia kwenye mambo mengi.
“Mzee wangu ni rafiki yangu mkubwa sana na ndio mwenye kumwambia kila kinachomhusu yeye hata kile ambacho hawezi kumwambia.
Hata hivyo, alisema kuwa mzee wake(Rais), anapenda wananchi wake na amekuwa akitamani kuona wanafanikiwa katika maisha yake.
“Mzee wangu kwa namna ambavyo namjua na yeye ndio mwenyekiti wa CCM, angeweza kukata jina lake.
“Anajua naweza ndio maana
amekubali nigombee, asingekuwa tayari nikitie aibu chama changu wala
kumtia aibu yeye,”alisema Ridhiwani , ndio mwenye nafasi ya kuamua
Hivyo mzee wake.
litokea nafasi ya kugombea
SAA 4:30 , asubuhi ya Aprili 4
mwaka huu, Ridhiwani Kikwete anaamua kukutana na waandishi wa habari kwa
lengo la kutoa tathimini ya kampeni za Chalinze.
Ridhiwani anapeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa jimbo la Chalinze ambao unafanyika kesho.
Akiwa amekaa katika kiti chake cha
miguu minne,nyumbani kwake Msoga jana, Ridhiwani anatumia nafasi hiyo
kuwakaribishwa waandishi wa habari.
Anaanza kwa kuaambia kuwa hapa ndipo nyumbani kwangu na wageni wangu wote huwa wanafikia hapa.
Baada ya kutoa ukaribisho huo,Ridhiwani anaanza kwa kuelezea mwenendo mzima wa kampeni tangu zilipoanza hadi kufikia jana.
Ridhiwani aanza kuwa kuwashukuru
waandishi wa habari kwa kutenga muda wao na kubwa zaidi namna ambavyo
wamefanya kazi kubwa ya kuuhabarisha umma kuhusu kampeni.
Anasema jamii imetambua mambo mengi ambayo yamezungumzwa kwenye kampeni na kwamba Chalinze ni jimbo kubwa kidogo.
Hata hivyo anasema kuwa jimbo la Chalinze yapo matatizo mbalimbali lakini yote yanaweza kupata ufumbuzi wake.
Anataja matatizo ya Chalinze ambako kwake yeye anaeleza kuwa maji ni tatizo kubwa.
Pili ajira kwa vijana wa Chalinze hawana ajira lakini tatizo la tatu ni afya ambayo bado inasuasua katika jimbo hilo.
Anasema kuwa bado kuna tatizo la zahanati na vituo vya afya lakini wakati huo huo kukiwa pia natatizo la uhaba wa dawa.
Ridhiwani anasema kuna tatizo la miundombinu ya barabara ambayo kwake yeye anaamini atashughulikia.
Wakati huo huo anasema anatambua tatizo la migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.
Anafananua kuwa kuna tatizo la
migogoro kati ya vijiji na vijiji lakini pia maeneo ya watu.Katika eneo
hilo unakuta kuna migogoro ambayo inatokana na eneo la ardhi kuwa na mtu
zaidi ya mmoja.
Kwa lugha nyingine ni kwamba migogoro ya ardhi imegawanyika katika upana wake.
Baada ya kutoa utangulizi huo wa matatizo ya jimbo hilo anatumia nafasi hiyo kuelezea tatizo moja baada ya jingine.
Maji
Anasema hilo ni tatizo kubwa na juhudi za kuhakikisha maji yanapatikana yalianza muda mrefu.
Wanawake na vijana walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji.Tatizo la maji lilisababisha hata ndoa za watu kuvunjika.
Hata hivyo, juhudi za kutafuta
suluhu ya adha ya maji, ndipo ukaja mradi wa maji Chalinze.Mradi huo ni
mkubwa na unatakiwa kupita katika maeneo yote.
Anafafanua kuwa mradi huo wa Wami
unatumia chanzo cha maji cha Mto wa Wami na kwamba, awamu ya kwanza
ulianza kwa kupelekwa Chalinze na Mdaula na vijiji kadhaa ya maeneo
hayo.
Mradi huo ni wa muda mrefu ambapo
anafafanua anadhani ulianza mwaka 1978 na kwamba katika kufanikisha
mradi huo unakwenda maeneo mengi zaidi yakiwemo ya Kata ya Msata,
Kibindu na Miono.
Hata hivyo kuna baadhi ya maeneo ambayo mabomba ya mradi huo yamefika lakini kuna maeneo mengine bado.
Ridhiwani anasema awamu ya tatu ya mradi huo itafika maeneo mengi zaidi ili kuwawezesha wananchi kunufaika na mradi huo.
Pamoja na ufafanuzi huo kuna
baadhi ya maeneo ambayo mradi huo haujakamilika kwasababu tu ya
waliopewa kazi ya kusambaza mabomba wameshindwa kufanya kazi kiwango
kinachotakiwa.
Anafafanua kuwa awamu ya tatu katika mradi huo ni kutoa maji kwenye vijiji na kisha kuvipeleka katika vitongoji.
Pamoja na hayo anasema changamoto
kubwa, chanzo cha maji cha Wami kinakabiliwa na tope ambalo
linasababisha tekeo kuingiza maji ndani ya mtando.
Anasema kuwa kutokana na matope
hayo, mtambo huo ulishindwa kufanya kazi na watalaamu wakashauri kuwa
mtambo uzimwe ili kusafisha mtambo huo.
“Mradi huu unasusua kwasababu tu kuna taka zimeingia lakini kazi inayoendelea ni kutafuta ufumbuzi wa moja kwa moja.
“Tutaangalia namga gani ya kufanya
kama ni kutafuta dawa ya kusafishia maji au kuzungumza na wilaya jirani
ili kutunza chanzo hicho,”anasema.
Ridhiwani anasema ,changamoto iliyopo sasa ni kuhakikisha marambo ya maji yanafufuliwa ili kupunguza tatizo la maji.
Anasema kuna baadhi ya marambo yamesahuulika lakini ni wakati muafaka sasa wa kuhakikisha yanafufuliwa.
Anatoa mfano wa Lulenge na Matuli
ambapo marambo hayo yalitengezwa kwa ajili ya binadamu lakini
kilichotokea ng’ombe na binadamu wakawa wanachangia.
Hiyo ni changamoto kubwa lakini anatumia nafasi hiyo kutoa ufafanuzi kuwa umefika wakati pia wa kuchimba visima vya maji.
Anafafanua kuwa jimbo la Chalinze linavyanzo vingi vya maji ambavyo vikitumika vizuri wananchi watapata ufumbuzi.
“Nataka kuhakikisha tunatafuta
ufumbuzi wa tatizo la maji kwa kusimamia mambo muhimu yakiwemo ya
kuchimba visima, marambo na kutumia vyanzo vingine.
Ajira.
Ridhiwani anasema kuwa ajira ni tatizo kubwa katika jimbo hilo na changamoto kubwa watu wengi wamekosa elimu ya ujasiriamali.
Anasema kuwa kinachotakiwa ni
wananchi kupata elimu ya ujasiriamali inayoweza kumsaidia mwananchi
kutumia ardhi yake katika kupata maendeleo.
Katika eneo hilo anasema kuwa atasimamia vema matumizi ya trekta badala ya jembe la mkono ili kuongeza tija kwa wakulima.
Mwaka 1982 , akiwa mdogo
anakumbuka matrekta ambavyo yalivyotumika kulima zaidi ya 1000 na kazi
hiyo ilifanywa na mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa wakati huo.
Anasema kuwa kauli mbiu yake kwa
wakulima itakuwa ni kuhimiza kilimo cha kutumia trekta na kazi yake kama
mbunge itakuwa ni kusimamia.
“Kupeleka trekta kwa kila kijiji
ni jambo ambalo linawezekana na nitasimamia.Matrekta yanatoka wapi,
mnajua, Suma JKT wanatoa mikopo ya matrekta lakini pia nchi mbalimbali
nazo zinatoa mikopo,”anasema.
Anafafanua anataka kuona njaa
inaondoka Chalinze kwa kutumia mpango wa matrekta na kwamba akipata
ushirikiano mzuri wa viongozi wengine baada ya miaka miwili Chalinze
inaweza kutoa chakula kwa ajili ya mikoa yote.
Hivyo anapozungumzia ajira , anazungumza namna ya kijana kuondokana na ajira tegemezi na badala yake asimame kwa miguu yake.
Anatoa mfano wa eneo la Bwilingu na Pera ambako kuna vijana wengi hawana ajira.
Anasema vijana wengi wa eneo hilo
kazi yao kubwa ni kuuza bidhaa ndogondogo kwa abiria wanaosafiri kwenye
mabasi yanayopita eneo hilo.
Anasema lazima atafute eneo ambalo
vijana hao watafanya kazi zao na katika kuwahakikishia kupata sehemu ya
kufanya biashara ni kujengwa kwa kituo cha mabasi Chalinze.
Anasema kutakapokuwa na kituo cha
mabasi, vijana watakuwa na uhakika wa kufanya biashara zao tofauti na
sasa ambako wanafanya katika mazingira magumu.
“Vijana wanapoteza maisha pale
Chalinze ambako kwa mwaka jana zaidi ya vijana 70 wamepoteza maisha
kutokana na kukanyagwa na magari katika eneo hilo wakati wanafanya
biashara zao,”anasema.
Ridhiwani anasema kupitia kilimo
anataka vijana wapate ajira.Kazi kubwa itakuwa kuwezesha vijana kupata
mitaji ambayo wataitumia kulima kilimo cha mazao mbalimbali.
Pia anataka awe mbunge ambaye atatengeneza mazingira mazuri ya vijana wa bodaboda kumiliki pikipiki.
Ridhiwani, anasema kuwa anataka Chalinze iwe na viwaanda ambavyo vitasaidia kutoa ajira kwa vijana wa Chalinze.
Afya.
Akizungumzia suala la afya anasema
kuwa kwa kutumia Serikali ya Serilali, atahakikisha zahanati zinajengwa
katika vijiji ili kupunguza umbali kutoka eneo moja kwenda jingine.
Anasema kuwa kuna baadhi ya
vitongoji vipo mbali na makao makuu ya vijiji hali inayofanywa wananchi
kutumia muda mwingi kutafuta huduma za afya.
Anafafanua kuwa kazi iliyopo mbele
yake ni kuhakikisha zahanati zinajengwa lakini pia madaktari wanakuwepo
ili kurahisisha upatikanaji wa ajira.
Anafafanua zaidi kuwa , mbali ya
zahanati kuboreshwa anataka kuwepo na mfumo ambao utawezesha kuwa na
madaktari ambao watakuwa wakienda kwenye vitongoji kwa ajili ya kutoa
huduma za afya.
“Lazima tutengeneza mpango wa
kupeleka madaktari kwa ajili ya kutoa huduma za afya.Kuiga jambo nzuri
si dhambi na hili nitalisimamia vema.
Katika eneo hilo la afya anasema
changamoto kubwa ni kuzidiwa kwa vituo vya afya kutokana na idadi kubwa
ya wanaokwenda kupata matibabu.
Anasema kuwa Chalinze ndio imekuwa kimbilio la wananchi wa jimbo hilo na hata wale ambao wanapata ajali za magari.
“Chalinze imezidiwa maana sasa imekuwa kama Hospitali ya Rufaa, idadi ya watu kubwa kuliko uwezo wake.Hii nichangamoto kubwa .
“Nataka tuone ndani ya jimbo la
chalinze tunatanua huduma za afya katika jimbo la Chalinze.Lazima
tujenge zahanati kubwa lakini moja ya malengo yangu ni kuhakikisha
inajengwa hospitali kubwa,”anasema.
Pia anasema katika eneo hilo la afya kuna tatizo la upungufu wa madaktari na katika baadhi ya zahanati hakuna madaktari.
“Unakwenda katika zahanati unakuta
daktari hayupo, ukiuliza amekwenda wapi unaambiwa amekwenda kuchaji
simu.Kinachoonekana kauli ya kwamba kazi hiyo ni wito inaanza
kupotea,”anasema.
Hata hivyo, anasema kuwa kazi iliyopo mbele yake ni kuangalia namna amayo itawezesha madaktari kukaa katika zahanati.
Anasema kwake yeye anataka
kushirikiana na vijiji kuangalia namna ya kutekeleza ilani ya CCM ambayo
inazungumzia ujenzi wa nyumba za madaktari.
Kuhusu afya ya akina mama, anasema , anataka kuwepo na mpango ambao utawawezesha wajawazito kujifungua katika mazingira salama.
Anasema anataka kusimamia ili
kutoka Chalinze iliko na kwamba anataka aone mama baada ya kujifungua
yeye na mtoto wake wanakuwa na uhakika wa kuwa salama.
“Si mara moja, mara mbili akina
mama wanafiriki kwasababu ya kujifungua.Changomoto zipo nyingi ikiwemo
ya umbali mrefu lakini nina uhusiano mzuri na wadau katika eneo hilo.
“Nia yangu ya dhati ni kuona
napambana ili kuhakikisha tunamaliza matatizo yaliyopo katika eneo hilo,
lazima mama na mtoto wawe salama na hili litafanikiwa kuwa kutengeneza
mazingira mazuri ya mjazito kujifungua salama,”anasema Ridhiwani.
Elimu
Ridhiwani anasema kuwa katika eneo hilo kunachangamoto kubwa.
Anasema kuna maeneo ambapo wanafunzi wamefanya vizuri lakini wamekosa mahali pakwenda.
Anasema hawezi kuahidi kusomesha vijana wake lakini anataka kutengeneza mfumo ambao utawawezesha wanafunzi kusoma.
Anasema kupitia fedha za mfuko wa
jimbo anataka kuona anasomesha vijana kati ya 50 hadi 100 kila mwaka ili
wasome na hatimaye kulifanya jimbo la Chalinze kuwa na wasomi wengi.
Anasema anatambua changamoto katika sekta ya elimu.Zipo baadhi ya shule ndani ya Chalinze mazingira yake si rafiki.
Anatoa mfano kuwa kuna shule
ambayo mazingira yake ni magumu kwa mwanafunzi na hata mwalimu lakini
imekuwa kifanya vizuri kwa kipindi cha miaka mitatu.
“Moja ya vitu ambavyo nimepanga
kuvifanya ni kujenga shule hii yote.Hii ni dhamira yangu na itakuwa
mfano mzuri kwangu mimi wa kuilezea shule hiyo.
Hata hivyo anasema, changamoto nyingine katika sekta ya elimu ni walimu ambapo hawatoshi.
Hivyo atahakikisha anafanikisha upatikanaji wa walimu wa kutosha lakikubwa zaidi ni kuboresha mazingira yao.
“Nataka nishirikiane na madiwani wenzangu ili kuhakikisha walimu wanakaa katika maeneo shule.
“Katika eneo la kitaaluma bado
tupo chini , lakini natambua baadhi ya shule zetu za sekondari ikiwemo
ya Shule ya Sekondari Chalinze, Lugoba, Miono na Mbwe zinafanya vizuri
sana.
Barabara
Katika eneo hilo, Ridhiwani anasema kuwa hiyo ni changamoto kubwa kwani barabara nyingi hazipitiki.
Sera ya CCM inaweka wazi namna ambavyo inahitaji vitongoji kuunganishwa na vijiji vyao ili wananchi waweze kufika kwa urahisi.
“Kuna baadhi ya barabara hazipiti
na ushahidi upo, kuna baadhi ya maeneo tulikwama kwa saa sita.Hata hivyo
nieleza tu kwamba waliopita wamefanya kazi kubwa na jukumu lililobaki
ni sisi kuendelea kuziboresha.
Hata hivyo barabara hizo
zimegawanyika maeneo mawili.Zipo barabara ambazo zipo chini ya Tanrods
ambazo hizo kazi yake itakuwa ni kuisimamia Serikali kujenga barabara
hizo.
Anatoa mfano barabara ya kutoa
Muavi kwenda Mkenge hadi Magulumatali ambapo hizo nazo zipo chini ya
Tanrod.Hivyo kwa kushirikiana na viongozi wa halmashauri atasimamia ili
zijengwa.
Hata hivyo anasema mpango wake wa
kwanza , ni kufanikisha barabara hizo ziweze kupita na baadhi ya
barabara zinahitaji madaraja madogo.
“Barabara ambazo zipo ndani ya halmashauri hizi tutazisimamia kwa nguvu zaidi.Tunataka barabara hizi zipitike wakati wote.
“Pamoja na juhudi hizo ni wakati muafaka sasa wa kuhakikisha barabara zinatunzwa vizuri na hilo ni jambo la msingi.
Ardhi
Anaweka wazi kuwa Chalinze kuna jamii mbili ambayo ni wakulima na wafugaji.
Anasema katika kila kijiji na kila kata ambayo amepita amekutana na tatizo la migogoro ya ardhi.
Anasema kuwa imefika mahali ambapo baadhi ya maeneo ambapo hawataki kabisa wamasai na wanasema hadharani.
“Kuna maugomvi mengi ambayo
yametokea, watu wamechomwa visu, mashamba yameharibiwa lakini pia kuna
ng’ombe zimekufa kwasababu baadhi ya wakulima wameamua kuweka sumu
kwenye mashamba yao.Ndipo ambapo hali imefikia hapo,”anasema.
Anafafanua kuwa tatizo la yote
hayo , ni kwamba hakuna mpango bora wa matuzi ya ardhi.Katika eneo hilo
viongozi wameshindwa kufanya kazi ya kutosha ya kuhakikisha makundi hayo
yanazingatia matumizi ya ardhi.
“Jimbo la Chalinze asilimia 35 ya
viongozi wa vijiji, wameondolewa na sababu yake ni moja tu wanafanya
mambo ambayo hayaridhishi wananchi,”anasema.
Anaweka wazi, katika migogoro kati
ya wakulima na wafugaji, kuna baadhi ya watu wamekuwa viburi.Baadhi ya
maeneo mtu anaambiwa asiingize ng’ombe kwenye shamba, bado wanaingizwa.
“Hiyo ni changamoto ambayo
naiona.Suluhu kubwa ya hili ni kupata mpango bora wa matumizi ya ardhi
ili tuondokane na migogoro ya ardhi.
Pia changamoto nyingine katika
eneo hilo la ardhi ni migogoro ya mipaka kati ya kijiji na kijiji ambapo
hiyo imesababisha wananchi kutoelewana.
“Kuna matatizo lukuki ya mipaka,
imefika mahali watu hawaongei .Kuna tatizo la mpaka kati ya Msolwa na
Msata, kuna tatizo la mpaka kati ya kambi ya Jeshi na Kijiji cha Pongwe
Sungura na vijiji vingine vingi tu,”anasema.
Anasema atakachofanya ni kukutana
na viongozi wa vijiji vyote hivyo ili kuzungumzia mipaka hiyo na
ikiwezekana kurudi kwenye mipaka ya asili badala ya ile mipaka
iliyowekwa mwaka 2008 kwa baadhi ya maeneo ya jimbo hilo.
“Pale ambapo kutakuwa ulazima basi
kinachotakiwa ni wananchi kulipwa fidia.kwa kutumia taaluma yangu
nataka nishirikiane na wenzangu kumasimamia haya.
Chalinze ipangwe
Pamoja na yote hayo,Ridhiwani anasema umefika wakati kwa Chalinze kukaa katika mpangilio tofauti na sasa.
Pia anasema kuwa , umefika wakati kwa Chalinze kuwa kituo cha biashara na katika hilo anaona haja ya uwekezaji mkubwa kufanyika.
Anafafanua kuwa Chalinze ikiwa na
mpango mzuri, itapunguza hata msongamano wa magari katika Jiji la Dar es
Salaam, maana Chalinze ikiwa imejipanga vizuri hakutakuwa sababu ya mtu
wa mkoani kufuata bidhaa Dar es Salaam wakati vitapatikana katika eneo
hilo.
Umoja na mshikamano
Ridhiwani anasema kuwa, umoja na mshikamano ni jambo muhimu katika maisha yake.
Pia anasema sera ya CCM
inazungumzia umoja na mshikamano na kwamba ndani ya jimbo la Chalinze
kumeanza kuibuka tabia ya watu kutoangaliana vizuri.
Anasema katika jimbo hilo kumeibuka ukabila,kumeibuka tabia ya kuona hawa wazawa na wengine wakuja.
Anasema katika maisha yake, amekuwa akishuhudia namna ambavyo wananchi wa Chalinze wakiishi kama ndugu na hakukua na ubaguzi.
“Kazi yangu mimi nataka kuona mshikamano unaendelea, nataka niwe na timu ya wazee wa jimbo la Chalinze.
“Nitakusanya wazee wote ambao wanatoka katika kabila zote na makundi yote ya jimbo hili.Naanza kuona mpasuko wa mshikamano wetu
“Watu wamepasuka , imefika mahali watu wanakataana hadharani.Jambo hili kwangu sitaki kuona linaendelea Chalinze,”anasema.
Anasema nia yake ni kuona umoja na mshikamano unaendelea Chalinze.
Anataka kuona watu wanaishi bila kubaguana , na siasa za Chalinze isiwe sababu ya kutofautiana.
“Sina ugomvi na wanasiasa , na
hata kampeni za Chalinze haziwezi kuwa sababu ya kulumbana .Nikiwa
mbunge nataka nilete vyama vyote vya Chalinze ili tushirikiane kuleta
maendeleo.
“Nipo tayari kwa matokeo ya aina
yoyote , kubwa nataka tushirikiane kuleta maendeleo yetu.Maslahi yangu
ni Chalinze na hao wagombea vyama vingine vya siasa nao wanataka
kuijenga Chalinze yetu,”anasema.
Michezo
MOJA ya mambo ambayo mgombea ubunge wa CCM,Chalinze Ridhiwani Kikwete ni kuinua michezo katika jimbo hilo.
Akizungumza katika mikutano yake
mbalimbali ya kuomba kura kwa wananchi wa jimbo hilo,Ridhiwani anaonesha
dhamira njema na kuhakikisha michezo inapewa kipaumbele.
Katika kuhakikisha anafanikiwa
katika eneo la michezo anasema atatumia wadau mbalimbali ili kuwezesha
vijana kushiriki kwenye michezo.
Akizungumzia zaidi kuhusu michezo Ridhiwani anasema CCM imekuwa na sera ya kuhamasisha michezo kupitia viongozi mbalimbali.
Anasema anataka kurudisha kombe la mbunge ili kuwawezesha wananchi kupata fursa ya kushiriki kwenyw michezo.
Anasema jimbo la Chalinze kulikuwa na timu ya Ibo na Nyundo na kwamba anataka kuona timu hizo zinarudi.
Anafafanua inawezekana isiwe kwa majina yale yale ya zamani lakini ni vema timu hizo zikarudi katika jimbo la Chalinze.
Anasema kuwa anafahamu kuwa na
kuna mashindano kwenye kata mbalimbali za Chalinze na kwa kutumia
madiwani hao atakuwa akianzisha ligi ya mbunge.
Anasema anataka kuona timu ambazo
zinakuwa na ushindani kwa kila kata.Wanapofika kwenye ligi ya kombe la
mbunge ushindani unakuwepo.
Ridhiwani anasema malengo yake ni kuona kuna vipaji vipya katika soka ambavyo vinatoka Chalinze.
Hata hivyo anasema changamoto
iliyopo hakuna uwanja wa uhakika katika jimbo la Chalinze hivyo kazi
atakayokuwa nayo ni kusimamia ujenzi wa uwanja.
Anasema kuna kiwanja cha Mwenge
ambacho atahakikisha kinajengwa hata kama kitaanza kuwa na uwezo wa
kuingiza watu 500 na baadae wakaongezwa.
Katika eneo hilo la michezo anasema, kuwa anataka kuona wanawake nao wanashiriki kwenye michezo.
Hata hivyo, anasema kwa kutumia
shule zilizopo katika jimbo hilo kutasaidia vijana kupata nafasi ya
kuonesha vipaji vyao kuanzia ngazi ya chini.
“Chalinze tunazo shule za kutosha
ambazo hizi tukizitumia vizuri tutakuwa na timu zenye ushindani katika
soka na aina nyingine ya michezo.
“Tunataka Chalinze iwe yenye
kusika kwa michezo na hata pale ambapo timu kubwa za Simba na Yanga
ziweze kuchukua vijana wetu kwenye timu zao,”anasema Ridhiwani.
Anafafanua hakuna jambo nzuri kama kuona kijana anasifa kwenye michezo lakini unapouliza anatoka wapi iwe ni Chalinze.
Kwenye mikutano ya kampeni,
Ridhiwani hakusita kuelewa wananchi anavyotaka kusimamia michezo na
amekuwa akitaka vijana kutambua kuwa katika eneo hilo atasimamia makini.
Umoja na mshikamano
Ridhiwani anasema kuwa, umoja na mshikamano ni jambo muhimu katika maisha yake.
Pia anasema sera ya CCM
inazungumzia umoja na mshikamano na kwamba ndani ya jimbo la Chalinze
kumeanza kuibuka tabia ya watu kutoangaliana vizuri.
Anasema katika jimbo hilo kumeibuka ukabila,kumeibuka tabia ya kuona hawa wazawa na wengine wakuja.
Anasema katika maisha yake, amekuwa akishuhudia namna ambavyo wananchi wa Chalinze wakiishi kama ndugu na hakukua na ubaguzi.
“Kazi yangu mimi nataka kuona mshikamano unaendelea, nataka niwe na timu ya wazee wa jimbo la Chalinze.
“Nitakusanya wazee wote ambao wanatoka katika kabila zote na makundi yote ya jimbo hili.Naanza kuona mpasuko wa mshikamano wetu
“Watu wamepasuka , imefika mahali watu wanakataana hadharani.Jambo hili kwangu sitaki kuona linaendelea Chalinze,”anasema.
Anasema nia yake ni kuona umoja na mshikamano unaendelea Chalinze.
Anataka kuona watu wanaishi bila kubaguana , na siasa za Chalinze isiwe sababu ya kutofautiana.
“Sina ugomvi na wanasiasa , na
hata kampeni za Chalinze haziwezi kuwa sababu ya kulumbana .Nikiwa
mbunge nataka nilete vyama vyote vya Chalinze ili tushirikiane kuleta
maendeleo.
“Nipo tayari kwa matokeo ya aina
yoyote , kubwa nataka tushirikiane kuleta maendeleo yetu.Maslahi yangu
ni Chalinze na hao wagombea vyama vingine vya siasa nao wanataka
kuijenga Chalinze yetu,”anasema.
KINGOTANZANIA
No comments:
Post a Comment