Friday, April 4, 2014

ZIARA YA KINANA SUMBAWANGA VIJIJINI LEO, MAELFU WAFURIKA MKUTANO KATA YA ILEMBO, AZINDUA NA KUCHAGIA MIRADI YA SHULE, ZAHANATI, KITUO CHA POLISI, MSAFARA WAKE WAZUIWA NJIANI NA WANANCHI MARA KADHAA

Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi, katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika  ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa,

CCM,Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya watu, katika kijiji cha Ilemba, kata ya Ilemba, alipohutubia wananchi katika kata hiyo akiwa katika  ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia za kuzitatua katika wilaya Sumbawanga Vijijini mkoani Rukwa, leo Aprili 3, 2014. ©2014 theNkoromo Blog

Maelfu ya wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Kijiji cha Ilembo wilaya ya Sumbawanga Vijijini  ©2014 theNkoromo Blog

inayoonyesha wananchi wengi kuridhishwa na utendaji kazi wa Kinana, mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa kiongozi huyo katika kata ya Ilembo wilaya ya Sumbawanga Vijijini wakiwa na bango la kusifu uchapakazi huo wa Kinana

Kinana akimpa kadi ya CCM, mwanachama mpya Eva Thomas, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Ilemba, Sumbawanga Vijijini. Zaidi ya wanachama wapya 250 wa CCM, walikabidhiwa kadi

Abdulrahman Kinana na Mjumbe wa NEC Balozi Ali Karume wakiingia kwenye Uwanja wa mkutano huo.

UVCCM wakiimba kwaya wakati wa mkutano wa Kinana, kijiji cha Ilemba

Kinana akifurahia vijana wakati wakicheza ngoma kumlaki alipowasili uwanja wa mkutano katika kata ya Ilembo 
Kinana akisaidia kuweka dirisha kwenye bweni la wasichana shule ya sekondari, Ilembo Sumbawanga Vijijini wakati wa ziara yake katika wilaya hiyo. 

Kinana akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Vijijini kwa kufanikisha usimamizi wa ilani ya CCM kwa kujenga bweni hilo la wanafunzi katika shule ya sekondari ya Kata ya Ilembo wilayani humo. 

Kinana akishiriki ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ya Ilemba, Sumbawanga Vijijini. Ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji na bati 50 kumalizia ujenzi wa kituo hicho

Kinana akifungua shina la wakereketwa la Vijana wa UVCCM la Makoko, katika Kijiji cha Ilemba

Kinana akizindua shina la Vijana la Makoto, Ilemba Sumbawanga Vijijini

Msafara wa Kinana ukipita kwenye mto kutokana daraja kuharibika katika barabara ya kutoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini.

Wananchi wa Kijiji cha Milepa A wakimshangilia Kinana baada ya kusimamisha msafara wake wakati akitoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini
 
Wananchi wamesimamisha njiani msafara wa Kinana wakati akitoka Kata ya Ilembo kwenda Sumbawanga mjini

 
Vijana 
Kalakala Kata ya Muze wakisakata ngoma kumpokea Kinana alipowasili eneo hilo akiwa njiani kutoka  Ilembo kwenda Sumbawanga

Wananchi wa Kijiji cha Kalakala, Kata ya Muze wilaya ya Sumbawanga Vijijini, wakimshangilia  baada ya kutangaza kuchangia mifuko 100 ya saruji na bati 100 ujenzi wa zahanati  ya Kata hiyo 

Kinana akiwashukuru wananchi wa Kijiji cha, Kata ya Muze baada ya kumlazimisha kuzungumza nao licha ya kufika eneo lao saa moja jioni, wakati akitoka Kata ya Ilembo wilaya ya Sumbawanga Vijijini kwenda Sumbawanga mjini
Post a Comment