Dar. Serikali imetangaza mishahara mipya kwa watumishi wa umma
itakayoanza kutumika mwezi huu, huku kima cha chini kikiongezwa kwa
asilimia 41.18 kutoka Sh 170,000 hadi Sh240,000.
Vilevile, mishahara ya watumishi wengine wa umma
imeongezwa kwa wastani wa asilimia 8.41. Waraka namba moja kwa watumishi
wa umma uliotolewa na Katibu Mkuu, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,
George Yambesi Julai 2 mwaka huu, unaeleza kuwa marekebisho hayo ya
mishahara yatahusu watumishi wa serikali kuu na watumishi wa serikali za
mitaa.
Wengine watakaonufaika na marekebisho hayo ni
watumishi walioshikizwa kwenye taasisi za umma na watumishi ambao
watakuwa kwenye likizo inayoambatana na kuacha kazi, kustaafu kazi au
kumaliza mikataba baada ya Julai mosi mwaka huu.
Waraka huo umeonyesha kuwa watumishi wa serikali
ambao wanapata mishahara binafsi isiyo ndani ya viwango vya mishahara ya
serikali hawatahusika na marekebisho hayo.
Mei 29 mwaka huu, Waziri wa Kazi na Ajira,
Gaudensia Kabaka, aliliambia Bunge, kwamba Serikali imekamilisha
majadiliano ya kuongeza kima cha chini cha mshahara katika sekta 12
binafsi, kitakachoanza kutumika rasmi Julai mosi.
Waziri Kabaka alitaja sekta hizo kuwa ni ya
Ujenzi, Shule Binafsi, Nishati, Viwanda na Biashara, Hoteli na Huduma za
Majumbani, Ulinzi Binafsi, Madini, Afya, Uvuvi na Huduma za Majini,
Usafirishaji, Mawasiliano na Kilimo. Kwa mujibu wa Kabaka, mishahara
imepanda kwa kiwango cha asilimia kati ya 21 na 65 huku Afya ikiongoza
kwa kuongezwa ikifuatiwa na sekta ya hoteli na huduma za nyumbani yenye
asilimia 55.
Mei mosi mwaka huu akiwa mkoani Mbeya, Rais Jakaya
Kikwete, aliahidi unafuu wa maisha kwa wafanyakazi kwa kuangalia
uwezekano pia wa kupunguza kodi kwenye mishahara, Lipa Kadiri Unavyopata
(PAYE).
Kuhusu kuongeza mishahara, Rais Kikwete aliahidi
wafanyakazi wote kwamba Serikali itaendelea kuiongeza kulingana na hali
ya uchumi wa nchi. Waraka huo unaonyesha kuwa mishahara mipya kwa
watumishi wa serikali kada ya masharti (operational service), ngazi ya
mshahara na mshahara mpya kwenye mabano ni;
TGOS A
TGOS A 1. (Sh240,000), TGOS A 2. (Sh245,600), TGOS
A 3. (Sh251,200), TGOS A 4. (Sh256,800), TGOS A 5. (Sh262,400), TGOS A
6. (Sh268,000), TGOS A 7.(Sh272,000), TGOS A 8(Sh279,000), TGOS A
9.(Sh284,800), TGOS A 10(Sh290,400), TGOS A 11(Sh296,000), TGOS A
12(Sh301,600), TGOS A 13(Sh 307,200), TGOS A 14(Sh312,800), TGOS A 15(Sh
318,400), TGOS A 16(Sh324,000), TGOS A 17(Sh329,600) na TGOS A
18(Sh335,200).
TGOS B
TGOS B 1. (Sh347,000), TGOS B 2. (Sh356,500) TGOS B
3 . (Sh366,000), TGOS B 4 . (Sh375,500), TGOS B 5. (Sh385,000), TGOS B
6. (Sh394,500), TGOS B 7. (Sh404,000), TGOS B 8. (Sh413,500), TGOS B 9.
(Sh423,000), TGOS B 10. (Sh432,500), TGOS B 11 . (Sh442,000) na TGOS B
12. (Sh451,500).
..........................................................................................................................
TANZANIA TUMETOLEWA MICHUANO YA CHAN
Tanzania
(Taifa Stars) imeshindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani
(CHAN) kwa mara ya pili mfululizo baada ya leo (Julai 27 mwaka huu)
kufungwa mabao 3-1 na Uganda Cranes, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao
4-1.
hdg
Stars
ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009
ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa
Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao
1-1.
Wenyeji
ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo
iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar. Frank Kalanda
alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la
Tanzania.
Bao hilo
halikuonekana kuichangaza Taifa Stars, kwani ilitulia na kufanikiwa
kusawazisha dakika ya 18 mfungaji akiwa Amri Kiemba kutokana na pasi
nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya eneo la mita 18.
Dakika ya
32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho Ngasa
ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba kabla
ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.
Mabao
mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian
Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na
makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi
nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.
Kocha Kim
Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 43 kwa kumuingiza Simon Msuva
badala ya Frank Domayo aliyeumia, na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo
Haruni Chanongo na Vincent Barnabas badala ya David Luhende na John
Bocco. Hata hivyo mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo.
Kikosi
cha Stars kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David
Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd,
Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo,
Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani kesho
(Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
................................................................................................
UFUNGAji MAFUNZO YA AWALI YA POLISI NA UHAMIAJI katika picha
WAZIRI WA
MAMBO YA NDANI YA NCHI MH, Dr. EMMANUEL NCHIMBI AKIKAGUA GWARIDE LA
WAHITIMU WA MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI POLISI WAKATI WA SHEREHE ZA
KUFUNGA MAFUNZO HAYO JANA KATIKA CHUO CHA POLISI MOSHI (CCP). TAKRIBANI
ASKARI POLISI ELFU TATU NA TISINI NA MBILI WALIHITIMU MAFUNZO, WAKIWEMO
ASKARI WA UHAMIAJI HAMSINI NA MOJA
ASKARI
POLISI WALIOHITIMU MAFUNZO, WAKIONYESHA PIKIPIKI INAVYOWEZA KUSAIDIA
KATIKA KUKABILIANA NA WAHALIFU KWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MH,
Dr. EMMANUEL NCHIMBI ALIYEKUA MGENI RASMI KATIKA SHEREHE ZA KUFUNGA
MAFUNZO YA AWALI KWA ASKARI POLISI NA UHAMIAJI JANA MJINI MOSHI.
TAKRIBANI ASKARI POLISI ELFU TATU NA TISINI NA MBILI WALIHITIMU MAFUNZO,
WAKIWEMO ASKARI WA UHAMIAJI HAMSINI NA MOJA
WASANII
WA KIKUNDI CHA NGOMA CHA CHUO CHA POLISI MOSHI WAKITOA BURUDANI JANA
MJINI MOSHI WAKATI WA SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO YA AWALI KWA ASKARI
POLISI NA UHAMIAJI. TAKRIBANI ASKARI POLISI ELFU TATU NA TISINI NA MBILI
WALIHITIMU MAFUNZO, WAKIWEMO ASKARI WA UHAMIAJI HAMSINI NA MOJA. PICHA
NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI.
No comments:
Post a Comment