Sunday, July 28, 2013

KAZI ZA SHAMBA MUHIMU SANA VIJANA WENZANGU

NAELEKEA SHAMBANI IKIWA NI SIKU YA MAPUMZIKO YA KAZI ZA KIOFISI LEO NIKAZI YA KUTUMIA NGUVU HAPO NI DALAJA LA MTO KYALA MJINI TUKUYU WILAYANI RUNGWE NIKAKUTA DARAJA LETU LIMEBOMOKA
SEHEMU YA SHAMBA LA MITI
NIMEFIKA SHAMBANI KWANGU NIMEKUTA MITI IMEZINGILWA NA MAJANI NA MIIBA KAZI IKAANZA

NIPO NA KAMANDA WANGU WA KAZI
KAZI INAENDELEA
ANGALAU THERUTHI YA SHAMBA ANGALAU NIMEFYEKA MIBAA NA MANYASI ILA SASA NAHAKIKISHA WIKI HII NAPATA NAFSI YA KUSHINDA SHAMBANI HUKU ILI KUWEKA HARI YA USAFI MAANA TUNAELEKEA KIANGAZI NA MITI INATAKA HEWA SAFI ILI KUKUA NA KUNENEPA ILI BAADAE TUNAPOVUTA TULIE KIVULINI
KAZI NA DAWA MWENYEJI WANGU MZEE MWASOMOLA KANILETEA MAJI YA KUNYWA

HAPO NIKIPATA CHAI YA ASUBUHI

HUKU SHAMBA MWENYEJI WANGU MZEE MWASOMOLA ANATENGENEZA MKAA NA GUNIA ANAUZA TSH ELFU TISA, KIUKWELI KWA WAKAZI WA MJINI HII NI AJABU KUONA GUNIA LA MKAA KUUZWA KIASI HIKI KIDOGO LAKINI MAISHA YANASONGA
MZEE MWASOMOLA NA MKEWE WAKINIAGA KWA FURAHA SANA NA HAWA WAZEE WANGU NAWAPENDA SANA KWAKUWA WANANITUNZIA SANA MASHAMBA YA HUKU MUNGU AWABARIKI SANA KWA MOYO WA UPENDO KWANGU
LEO NI KUTEMBEA KWA KWENDA MBELE HAPO NIKIVUKA MOJA YA MADARAJA MANNE NINAYOYAPITA NIENDAPO KATIKA MASHAMBA HAYA MAWILI YA MITI
NIMECHOKA SANA HAPO SASA SAFARI ISHAANZA KUWA NGUMU UKIZINGATIA KAZI NGUMU YA SHAMBA NA KUTEMBEA, NA HUKU NIMEPATA MAJI TU NA MUA LAZIMA KUPANDA MLIMA UONE KAZI
KARIBUNI NYUMBANI SASA NIMEFIKA.
.......................................................................................................................

BAADA YA KUFICHUA UWEPO WA MBEGU NA DAWA FEKI MBEYA, WAKAGUZI WANUFAIKA KWA RUSHWA

DAWA FEKI NA MBEGU ZA MAZAO ZAZAGAA MBEYA Mkuu wa wilaya Mbeya Norman Sigalla

*Wakulima wauziwa unga wa matofali kama dawa
*Mahindi yapakwa Coper kulaghai wakulima

DAWA feki zimezagaa katika maduka mbalimbali ya pembejeo za kilimo mkoani Mbeya na kuendelea kutajirisha wafanyabiashara wasio waaminifu, imebainika.

Uchunguzi wa kina uliofanywa kwa miezi sita sasa, umebaini kuwepo kwa dawa feki za kuhifadhia nafaka hasa mahindi na maharage.

Wafanyabiashara hao, ambao baadhi yao kwa sasa hawakamatiki kutokana na utajiri walioupata kwa njia hiyo, wamefikia hatua ya kusaga matofali yaliyochomwa  kisha unga wake kuhifadhiwa kweye mifuko kama dawa za kuulia wadudu wanaoharibu mimea na matunda ya Kahawa.

Dawa aina ya Red Copper baadhi ya wafanyabiashara wanauza kwa ujanja unga wa matofali ya kuchomwa kisha kuweka unga huo kwenye mifuko na kuuza kwenye maduka yao huku Copper ya kuhifadhia mbegu za pamba wanauza kama Copper ya kutibu magonjwa ya kahawa aina ya CBD.

Copper hiyo wakulima wakiikoroga kwenye maji inatuama kwasababu siyo Copper halisi ya kuchanganya na maji lakini wengi wanaitumia kwasababu ni bei rahisi na hawana elimu ya kutosha kuhusu dawa hizo.

Kwa upande wa mbolea, wanachukua mbolea aina ya minjingu ya punje na kuweka katika mifuko ya Dap kwani Dap ina bei kubwa kuliko minjingu.

Wanafanya hivyo kwasababu mkulima anapotumia mbolea hiyo hawezi kugundua mpaka pale mazao yatakapokuwa yameanza kuharibika yakiwa shambani.

Mbegu za mahindi, wamekuwa wakichukua mahindi ya kawaida na kuyachanganya na Copper ya kuhifadhia mbegu za pamba na kopa ya kawaida kisha kuhifadhi kwenye mifuko ya makampuni ya utafiti na kuwauzia wakulima.

Kuwepo kwa mchezo huo mchafu kwa ajili ya kujitajirisha unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara, mtaalam wa masuala ya pembejeo kutoka kampuni ya Bager, Alex Swilla anathibitisha kuwepo kwa mchezo huo mchafu huku serikali ikiendelea kufumbia macho.

Anasema mbali na mbolea na mbegu hizo kuchakachuliwa, wafanyabiashara hao pia wanachakachua na sumu ambapo jina la sumu linalokuwepo kwenye kopo ni tofauti na dawa inayokuwemo ndani.

‘’Kwa upande wa sumu, wanachukua dawa aina ya Sumision na kuweka katika makopo ya sumu aina ya Daksban’’alisema Swilla.

Alisema hali hiyo imeendelea kushika kasi kutokana na mambo mawili, likiwemo suala la rushwa kwa wakaguzi au wakaguzi hao kutokagua kabisa maduka ya pembejeo hizo za kilimo ama kukaa muda mrefu bila kufanya ukaguzi hali ambayo inawapa mwanya wafanyabiashara hao kuendelea na mchezo huo.

Hata hivyo, imebainika kuwa kutokana na ubora wa pembejeo za ruzuku kutoka serikalini, baadhi ya wafnyabiashara hawakuwauzia wakulima kutokana na bei yake kuwa kubwa hivyo mbolea hizo waliziuza kwa bei kubwa tofauti na maelekezo ya serikali lakini serikalini hakuna aliyejali.
.................................................................................................

No comments: