MWL LUSEKELO MKUMBWA AFISA ELIMU VIFAA NA TAKWIMU SEKONDARI WILAYA YA RUNGWE AKIONGEA NA KINGOTANZANI KUHUSU SAKATA NA SHULE KUMI NA NNE KUFUNGIWA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI MWAKA 2014 - 2015. |
Shule kumi
na nne za wilayani Rungwe mkoani Mbeya
zimefungiwa matokeo ya kidato cha
pili kutokana na kucheleweshwa kwa ada ya mtihani kutoka kanda kwenda wizarani.
Akizungumzia
sakata hilo Afisa Elimu vifaa na takwimu
wa wiraya ya Rungwe Mwl. Lusekelo Mkumbwa amesema kwamba tatizo limetokea kwa wakaguzi wa kanda kwa kuchelewesha taarifa ya malipo ya ada za mitihani kwenda
wizarani, na kudai kuwa waalimu wakuu wa shule hizo ndio wanaotakiwa
kuwasiliana na kanda moja kwa moja kwa
ajili ya kuhakiki malipo ya ada hizo na si kufika ofisini kwake.
Afisa elimu amezitaja baadhi ya shule zilizopatwa na mkasa
huo na zilizoweza kufika ofisini kwake kuwa ni shule ya Lubala, Tukuyu,
Masukulu,
Bujinga,Mwaji,Mpuguso na Lufingo ambapo shule zilizofungiwa matokeo zimethibitisha kulipa ada ya mitihani hiyo ya
kidato cha pili mwaka 2014.
Kutokana na
tatizo hili la baadhi ya shule kufungiwa matokeo Mwl. Mkumbwa amedai kuwa wemeshindwa kupata takwimu sahihi ya ufaulu wa wanafunzi hao kwa mwaka 2014 na2015
kwani ni shule chache zimepata matokeo ya kidato cha pili ya mwaka 2014 na 2015.
Afisa elimu
sekondari wilayani Rungwe mwl. Mkumbwa ameitaka
wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kuweka utaratibu maalumu na wa kueleweka wa
kushughulikia masuala ya mitihani na sio kuchanganya kanda na wizara kama
walivyo fanya mwaka huu kwani kanda imeshughulikia malipo na wizara kushughulikia mitihani na matokeo ya mitihani
, hivyo kusababisha makosa kama ya kufungiwa matokeo kwa baadhi ya shule.
Mpaka sasa
wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha pili mwaka 2014 hawajaripoti shule
bado wakisubili matokeo ya uhakika kama wataweza kuendelea na kidato cha tatu.
TUMAIN OBEL
KINGOTANZANIA
No comments:
Post a Comment