Wednesday, January 21, 2015

MAMBO YANAYOWEZA KUSAIDIA KUINUA UCHUMI WAWANANCHI WA RUNGWE MKOANI MBEYA: Christopher Andendekisye

BAADHI YA MAMBO YANAYOWEZA KUSAIDIA KUINUA UCHUMI WA RUNGWE.
ZAO LA NDIZI LINAWEZA KUBADILISHA MAISHA YA WANA RUNGWE.

Nimekuwa kwa muda wa mwaka mmoja nafuatilia namna ambavyo wilaya yetu ya Rungwe inaweza kunufaika na namna ilivyojaliwa kuwa na uwezo wa kustawisha zao la ndizi.
Kitaalamu, imethibitishwa ndizi ina virutubisho vingo zaidi kuliko hata mahindi, ulezi, ngano nk.
Kwa bahati mbaya, Wilaya ya Rungwe, kutokana na kukosa kuwa na viwanda vya kutengeneza bidhaa zitokanazo na ndizi kilimo hakijawa na tija sana.

Kuna umuhimu wa kujenga viwanda maana, tukilima ndizi kwa wingi, na tunaweza kutengeneza unga wa ndizi na kusambaza si nje tu ya nchi, bali hata shule zetu zinaweza kutumia unga huo kwa wanafunzi kama uji, tunaweza kusambaza kwenye supermarket na maduka mbalimbali. 

HILI KWA SASA HALIFANYIKI, LAKINI
 Inawezekana....Rungwe, naamini tutashirikiana kufanya hili, katika eneo moja la kuinua kilimo cha ndizi..ili wakulima wetu wa ndizi wapate faida kuliko ilivyo sasa. Angalia Picha, namna ya ulimaji bora wa zao la Ndizi na namna na kuweza kutengeneza Unga na hizyo hakuna ndizi zinapotea ama kwa kuoza ama vinginevyo. Inawezekana.
Mawazo yanakaribishwa.


 
Christopher Andendekisye
KINGOTANZANIA
Post a Comment