Tuesday, April 9, 2013

MTOTO LISTA MWAKANYAMALE MIAKA NANE MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI SHULE YA MSINGI YA ISANGE MWAKALELI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA AUAWA KIKATILI KWA KUKATWA KICHWA NA KUTOLEWA VIUNGO VINGINE NA MWILI WAKE KUPATIKANA MTONI BAADA YA SIKU NANE TANGU KUPOTEA KWAKE

WANANCHI WA MWAKALELI ISANGE WAKISHUHUDIA MWILI WA LITA MWAKANYAMALE BAADA YA SIKU SABA KUUTAFUTA BILA YA MAFANKIO

SIKU YA NANE AMBAYO NI JANA MBWA ANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA POPI ALILEJEA KIJIJINI HUKU AKIBURUZA MHUU HUU WA MAREHEMU KITU KILICHOWASHITUA WANANCHI NA KUANZA KUFUATILIA  HADI SEHEMU YA TUKIO WALIPOKUTA KIWILIWILI NA HUKU MBWA WAWILI WALIOKUWA WAKALI WAKIULINDA MWILI HUO

KIWILIWILI KISICHO NA KICHWA NA MHUU MMOJA NA MKONO MMOJA KILIPATIKANA KANDOKANDO YA KIJITO CHA MAJI KALAMISI KITONGOJI CHA ISANU KATIKA KIJIJI CHA ISANGE MWAKALELI

KIWILIWILI KIKIWA KIMEGANDAMIZWA NA JIWE MKONO MMOJA NA HAPO MHUDUMU WA MOCHWALI YA TUKUYU AKIJIANDAA KUTOA HUDUMA YA KUSITIRI MWILI HUO

KIPANDE CHA TAYA KILIPATIKANA KATIKA ENEO HILO
MMM DUNIA NA WATU WAKE WAKATIRI KIASI HIKI?
MGUU ULIOPATIKANA KIJIJINI
ULINZI ULIIMALISHWA KIJIJINI HAPO
NDUGU WA FAMILIA YA MAREHEMU LISTA MWAKANYAMALE
MWILI UKIANDALIA TAYARI KWA MAZIKO
PAMOJA NA MVUA KUBWA KUNYESHA WANANCHI WA ISANGE MWAKALELI WALIVUMILIA NA KUENDELEA NA MKUTANO AMBAPO MWISHO WALIAMUA KUPIGA KURA ILI KUWABAINI WAHUSIKA WA MAUAJI YALIYOFANYIKA

AFISA MTENDAJI WA KIJI CHA ISANGE ANYAMBEGE MWANGOMO ALIONGOZA ZOEZI LA KURA NA WATU SITA WAKAPATIKANA JAPO WANNE WALIPATA MOJAMOJA NA HUKU WAWILI WAKIPATA KURA NYINGI NA KUKABIDHIWA KWA POLISI NA KUONDOKA NA NAO
WALIBAINIKA KUSHIRIKI MAUAJI HAYO NI LAMECK MWASYEBULE NA SANGA MWAKYOMA AMBAO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MAHOJIANO ZAIDI



 BONDE LA MWAKALELI LIMEKABIRIWA NA MAUAJI YA KUTISHA SANA KWA KUWAUA WATOTO WADOGO KIKATIRI IKIWA NI MAUAJI WA WATOTO WATATU NDANI YA SIKU MUMI NA NNE WATOTO WATATU WAMEUWAWA WAKWANZA AKIWA NI DEBORA RIZIKI ALIYEUWAWA NA BABA YAKE MZAZI KWA KUMZIKA AKIWA HAI NA WAPILI AYUBU MWAKALENGELA ALIYE UWAWA KWA KUKATWA KICHWA NA KIWILIWILI CHAKE KUTUPWA HUKU KICHWA KUTOPATIKANA HADI LEO

MAREHEM AYUBU MWAKALENGELA ALIYE UWAWA KWA KUKATWA KICHWA


DR STAPHORD AKIFANYA UCHUNGUZI WA MWILI WA AYUBU
Photo
MTOTO WA MIAKA 3 DEBORA RIZIKI ENZI ZA UHAI WAKE NA CHINI NI SIKU ALIPOFUKULIWA SEBURENI KWA BAB YAKE AKIWA AMEMZIKA WKIWA HAI
Photo: MKASA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .

KATIKA MIKAKATI ILIYOPITISHWA NA WANANCHI HAO MWA ISANGE MWAKALELI NA JAMII YOTE YA BONDE LA MWAKALELI WAMEKUBARINA KUENDELEA NA ULINZI WA SUNGUSUNGU MASAA 24 PIA KUANGALIA SANA WAGENI WANAO INGIA NA KUTOA KIJIJINI HAPO KWAKUWA HAYA MAUAJI YAMEKITHIRI SANA SIO RAHISI KUVUMILIWA 

PIA WAMEIOMBA SERIKALI KUTOA USHIRIKIANO KWAKUWA TANGU MAUAJI HAYA YAANZE WANANCHI WAMESEMA HAWAJAWAHI KUMWONA KIONGOZI YEYOTE WA NGAZI YA JUU HASA WILAYANI KUJA KUJUMUIKA NAO JAPO HATA POLE KITU KINACHOWAPA HOFU WANANCHI HAWA WA MWAKALELI KUTOFANIKIWA KATIKA MIKAKATI YA KUUMALIZA MTANDAO HUU WA MAUAJI YA WATOTO WASIO NA HATIA

KINGOTANZANIA IMEONGEA NA DAS WA WILAYA YA RUNGWE  MOSES MWIDETE AMESEMA KUWA KIKAO CHA ULINZI NA USALAMA KIMEKAA NA WANAFUATILIA NA HUKU UPEREREZI UNAENDELEA WA KINA KWA KUBAINI KIINI CHA TATIZO NA WALIO HUSIKA KUKAMATWA NA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA

NA KINGOTANZANIA

0752881456

................................................................................................................................................................

..........................................................................................................................................................................

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

RPC MBEYA KAMANDA DIWANI

WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
                                               KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 08.04.2013 MAJIRA YA SAA 09:20HRS HUKO ENEO LA CHAMSALAKA – CHIMALA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA . GARI T.627 AEA/T T346 AUE AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA ABDU S/O OMARI,MIAKA 43,MBENA,MKAZI WA IRINGA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MARIAM D/O INCHAGI,MIAKA 18,MUWANJI,MKULIMA MKAZI WA CHIMALA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI . MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA CHIMALA MISHENI . DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA RUNGWE -  AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA KUSABABISHA   
                                      KIFO NA MAJERUH.
MNAMO TAREHE 08.04.2013 MAJIRA YA SAA 11:30HRS HUKO ENEO LA NUMBER ONE BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.520 BDZ AINA YA TATA MALI YA KAMPUNI YA BONITE BOTTLES LTD MOSHI  LIKIENDESHWA NA DEREVA AINEA S/O ELIA @ SYANGA,MIAKA 38,MCHAGA,MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI T.451 CBV AINA YA KING AITWAE  SIKITU S/O ELIA ,MIAKA 38,MSAFWA, MKAZI WA MCHANGANI KIWIRA  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO  NA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE FRED S/O SIGARA,MIAKA 28,MSAFWA,MKULIMA MKAZI WA NDAGA TUKUYU AMBAYE AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE . CHANZO NI MWENDO KASI . MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA IGOGWE MISHENI . DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA MBEYA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MNAMO TAREHE 08.04.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA 1. DEBESHA S/O ABUSHA,MIAKA 23 NA 2. ADINA S/O ALABAYO,MIAKA 24 WOTE RAIA WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI . MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO TARATIBU ZINAFANYWA ILI KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI . KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO  KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWEMO WAGENI KUTOKA NJE YA NCHI ILI HATUA  ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.
                                                      [ BARAKAEL MASAKI - SSP ]
   KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
...........................................................................................................................................................

Asilimia 26.5 wanawake hufanya mapenzi kinyume na maumbile

3 bfb73
Wakati idadi ya wanawake wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ikiongezeka, asilimia 26.5 ya wanawake Tanzania wamebainika kuwa wanafanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mfumo wa uzazi unaharibika
Watafiti wanabainisha kuwa kitendo hicho licha ya ukweli hakifai kwa vile kinaharibu mfumo wa uzazi, kina athari kubwa mno kwa mwanadamu, mojawapo ni ikiwemo uwezekano mkubwa wa wahusika kuambukizana virusi vya Ukimwi kwa vile hakuna vilainishi, hivyo kusababisha michubuko ambayo ndio njia kuu ya kuambukiza vijidudu hivyo.
Mtafiti Mwanasayansi, Irene Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini Tanzania (NIMR) alitoa ripoti hiyo hivi karibuni hapa jijini Dar Es Salaam.
Mremi akiwa na jopo la watafiti kutoka NIMR anasema kuwa wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi na Kuogopa kupata Mimba.
 Vilevile alizitaja sababu nyingine za wanawake kufanya mapenzi kwa njia hiyo ni kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
Sampuli za utafiti
Utafiti huo ulikusanya sampuli kutoka katika mikoa ya Dar es salaam, hasa maeneo ya Kinondoni, Tanga, Makete na Siha.
 Mremi anasema “Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu wa bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani
Katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao walihusishwa katika utafiti huo.
Imani potofu kwa wanaume
Wanaume waliohojiwa wamesema wanafanya kwa ajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maaambukizi ya VVU, kitu ambacho ni uongo, kwani huko ndiko kwenye kuchangia ukimwi kwa haraka zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote. 
CHANZO MWANANCHI
..............................................................................................................................

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Mbunge wa Iramba magharibi,Mwigulu Lameck Nchemba  kutoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma Aprili 9, 2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_1528 
Waziri Mlkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Mkiwa Adam Kimwanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 9, 2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: