Kutokana na kuibuka kwa mgogoro kati ya Serikali, madiwani, wananchi na wazee wa mila CCM iliunda Tume ya Nchemba kuzungumza na kusikiliza maoni ya wananchi.
Tume hiyo ilifanya mkutano na wananchi Kijiji cha Olorien Magaiduru, Tarafa ya Loliondo juzi,ikiwahusisha pia Mbunge wa Simanjiro Christopher ole Sendeka na Mbunge wa Longido, Michael Laizer.
Katika mkutano huo Nchemba alisema CCM inatambua wazi maslahi ya wananchi ndiyo maslahi ya taifa na kamwe hakuna maslahi ya taifa ambayo si maslahi ya wananchi.
Nchemba aliwataka wananchi, wazee wa mila na madiwani kutoogopa matamshi ya Waziri Kagasheki badala yake Chama kinaangalia uzito wa tatizo.
“Nitapeleka taarifa ya Kamati ya siasa, viongozi wa vijiji, mila na itakayotoka hapa. Wiki ijayo timu niliyokuja nayo na viongozi wenu tutakwenda kumuona Katibu Mkuu ili tumuone Waziri Mkuu,”alisema Nchemba.
Naye Sendeka alisema: “Nimepata fursa ya kujua jinsi wananchi wa Loliondo walivyojipanga, kutoka kijiji cha Piyaya, Arash mpaka Ololosokwani.
“Mashariki ni makazi, Magharibi Hifadhi ya Serengeti na mifugo ya kuchunga inayoelekea mwelekeo mmoja. Hili halikuwa la bahati mbaya ni matumizi bora ya ardhi.”
Alisema mwaka 2009 Bunge lilipitisha Sheria namba 5 ya Uhifadhi, katika sheria hiyo Bunge lilifuta maeneo ya uhifadhi na uwindaji unaotaratibiwa kote nchini.
....................................................................................................................................
WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINDA AWATAKA WATANZANIA KUPENDANA NAKUDUMISHA AMANI
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda amewataka wa Tanzania wapendane na kuishi kama
watoto wa baba mmoja na kuondoa tofauti za kidini ambazo zina weza
kuliingiza taifa katika matatizo makubwa waziri Mkuu ametoleamfano wa
hivi karibuni ambao badhi ya wakristo na waisilamu walianza kugombana
kwa ajili ya uhalali wa kuchinja nyama , amesema watanzania hawana budi
kuheshimu imani za wenzao kwani miaka ya nyuma watu walikuwa
wakishirikiana kiasi kwamba huwezi kujua tofauti ya mkristo na mwisilamu
kwa vile watu walikuwa wanapendana nakuheshimu dini ya mwenzao , Hivyo
amewaomba viongozi wa dini kusaidia kurudisha upendo ambao ulikuwepo
amesema amefurahishwa na kuona hata viongozi wa dini ya kisilamu Kuwepo
kanisani katika ibada ya kubariki ndoa ya Bwana Philip Mangula na Bibi
Yolanda Kabelege amesema watu wanjombe ndio mfano wa kuigwa
Waziri
mkuu ameyasema hayo alipokuwa amehudhuria sherehe ya kubariki ndoa ya
Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Mh. Philip Mangula na Mwalimu Yolanda
Kabelege ambayo imefanyika katika kanisa la Kilutheri Mkoani Njombe
Naye
Katibu mkuu wa CCM Mh. Abdurahamani Kinana aliwapongeaza wana ndoa hao
kwa kuamua jambo la kufunga ndoa kwani hata vitabu vitakatifu vinasema
nyumba iliyo katika ndoa hata mungu huibariki nakuipa amani
Sherehe
hiyo imefanyika siku ya jumamosi Aprili 6. 2013 mjini Njombe ilhuduriwa
na viongozi wa dini ,vyama ,Serkali na mabaozi pamoja na wana njombe
Pichani katikati ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kngine waliohudhuria
katika harusi hiyo mjini Njombe jana, Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdurahman Kinana wakiwa pamoja na wageni we Picha na Chris
Mfinanga
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana wakipiga picha pamoja na Maharusi baada ya kubariki ndoa yao.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana wakiwapongeza maharusi
Bwana
Harusi Mzee Philip Mangula akimshukuru Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
mara baada ya kumaliza kutoa nasaha zake katika ndoa hiyo takatifu.
.....................................................................................................................................
WASANII MBEYA WAZINDUKA WAANZISHA SHIRIKISHO LA WACHEZA FILAMU MKOA WA MBEYA
MWENYEKITI WA MUDA WA SHIRIKISHO LA
WAIGIZAJI MKOA WA MBEYA SAMWEL MWAMBOMA AKIZUNGUMZA AZMA YA KUWAKUTANISHA
WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA KATIKA KIWANJA CHA CITY PUB MBEYA
|
KATIBU WA MUDA WA SHIRIKISHO LA
WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA SADY MWANG'ONDA AKIZUNGUMZIA MIKAKATI YA WASANII
KUJIKWAMUA KATIKA KAZI ZAO ZA SANAA YA UIGIZAJI MKOA WA MBEYA
|
BAADHI YA WASANII WA SANAA YA
UIGIZAJI MKOA WA MBEYA WAKIWA KATIKA MKUTANO ULIOWAKUTANISHA WAIGIZAJI KATIKA
UWANJA WA CITY PUB JIJINI MBEYA
|
BAADHI YA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA
WAKIWA WAMESIMAMA DAKIKA MOJA KWA AJILI YA KUMKUMBUKA MSANII MWENZAO STEVEN
KANUMBA ANAYETIMIZA MWAKA MMOJA TANGU AFARIKI DUNIA APRIL 7 MWAKA JANA
|
BAADHI YA WASANII WALIPATA MUDA WA KUWAULIZA MASWALI VIONGOZI WAO WA MUDA NA KUCHANGIA MADA MBALI MBALI KATIKA MKUTANO HUO |
BAADHI YA VIONGO ZI WA WAKIHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI
WASANII wa Filamu Mkoani Mbeya
wameaswa kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kuaminiana ili kuifanya kazi zao
kujulikana kitaifa na kupata masoko mengi ikiwa ni pamoja na kujiongezea
kipato.
Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti
wa Muda wa Shirikisho la Filamu Mkoa wa Mbeya, Samwel Mwamboma ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Kituo cha kusambazia Filamu cha Sam Video Centre cha Jijini Mbeya
Mwamboma alisema Mkoa wa Mbeya
unawasanii wengi sana na wazuri tofauti na Dar Es Salaam lakini wameshindwa
kujulikana kutokana na kukosa ushirikiano na uaminifu unaosababishwa na
ubinafsi ndiyo unaosababisha kutofanikiwa wala kujulikana kwa wasanii
licha ya kushiriki katika Filamu nyingi.
“ Wasanii mkiwaamini
watayarishaji wa Filamu, Wasambazaji, Waongozaji, Wapiga Picha na Waandaaji
kazi zetu zitafika mbali sana lakini mkiwa wabinafsi hatutaendelea kabisa”
Aliosema Mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa Lengo la Kuanzisha
Shirikisho la wacheza Filamu Mkoa wa Mbeya ni kuleta Umoja ili kazi za Wasanii
wa Mkoa wa Mbeya zijulikane na kupendwa na watazamaji ili Wasanii wakubwa
kutoka Dar Es Salaamu watamani kufanya kazi nao na siyo Wasanii wa Mbeya
kutamani kuigiza na Wasanii wakubwa.
Kwa Upande Katibu wa Muda wa
Shirikisho hilo Sadi Mwang’onda alisema kuwa moja ya vitu vinavyosababisha kazi
za wasanii wa Mkoa wa Mbeya kuonekana kutokuwa na ubora ni kutokana na kila mtu
kufanya kazi kivyake bila ushirikiano ambapo Watayarishaji, Wasambazaji, Wapiga
picha na wadau kutokuwa na umoja.
Aliongeza kuwa Wasanii wa Mkoa wa
Mbeya wanakutana na Changamoto nyingi ambazo ni ukosefu wa Mitaji hivyo
kuwaomba Wakazi wa Mkoa wa Mbeya wenye mitaji kuwekeza katika Soko la Filamu
ambapo aliongeza kuwa kama wasanii wako tayari kuhakikisha Mwekezaji ananufaika
na hajutii kuwekeza kwenye Filamu za Wasanii wa Mkoa wa Mbeya.
Aliitaja Changamoto Nyingine kuwa
ni kukosekana kwa Elimu miongoni mwa Wasanii ambapo wengi wao wamekosa elimu ya
kawaida ya darasani ili hali wengine kutokuwa na ufahamu juu ya kitu
wanachokifanyia maigizo, kutokana na hilo Katibu huyo amewakikishia Wasanii
kuwa baada ya Shirikisho hilo kutulia atawatafutia Semina na Mafunzo ili wapate
mwanga kuhusu Filamu.
Katibu huyo alizitaja changamoto
zingine kuwa ni pamoja na Wasanii kutofanya utafiti kuhusu kile anachotaka
kukiigiza jambo ambalo linasababisha kazi nyingi kuonekana kama
zinafanana,ukosefu wa matangazo na wasanii wenyewe kutojiamini kutokana na kazi
wanazozifanya hivyo kuonekana ni wababaishaji tu.
Mbali na hayo Mwang’onda
aliwasihi Wasanii waliojitokeza katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Wasanii
zaidi ya 50 kutoka Ndani ya Jiji la Mbeya, Wadau wa Filamu pamoja na Wanahabari
kuwa Wasanii wanatakiwa kuishi maisha ya Heshima kama wanavyoigiza kutokana na
Jamii kuiamini sana kazi za sanaa.
Aidha Katibu huyo alisema ili
Shirikisho lao liweze kuimarika na kuendelea watakuwa wakifanya mikutano ya
mara kwa mara na kuwataka Wasanii hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kukutana
kila wanapopata nafasi na sio kubaguana.
...................................................................................................................................
JK Apanda Pantoni kwenda na kurudi Kigamboni..Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na watoto waliokutana nao kwenye pantoni ya MV Magogoni walipokuwa wakitoka Mji Mwema, Kigamboni, jijini Dar es salaam leo April 7, 2013 walikomtembelea Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakishuka kutoka kwenye pantoni ya MV Magogoni walipokuwa wakitoka Mji Mwema, Kigamboni, jijini Dar es salaam leo April 7, 2013 walikomtembelea Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
PICHA NA IKULU
................................................................................................................................ Serikali iache kutoa uraia kama njugu
Kwa ufupi
Tatizo hapa ni kwamba suala la kutoa uraia limepewa
usiri mkubwa. Ndiyo maana kwa makusudi taarifa inayotolewa na Serikali
kuhusu watu hao inakuwa nusunusu ili kuwachanganya wananchi wenye
pingamizi wasijue pa kuanzia.
Kama kuna suala nyeti kwa taifa ambalo Serikali bado inalifanyia
mzaha, basi suala hilo ni namna uraia unavyotolewa kiholela kwa wageni
pasipo kuwapo mfumo stahiki wa kusimamia mchakato huo. Kwa muda mrefu
sasa, Serikali imekuwa ikiliona suala hilo la uraia kama jambo jepesi
tofauti na nchi nyingi duniani ambazo huliona kama msingi wa usalama na
kitovu cha maendeleo ya nchi hizo.
Hapa tunajaribu kuonyesha jinsi sera ya Serikali kuhusu uraia na uhamiaji inavyoendelea kututesa, ingawa inawezekana kabisa kwamba lipo kundi la watu linaloweza kuwa limefaidika na kuneemeka kutokana na udhaifu wa sera hiyo inayotoa mianya tele kwa vitendo vya rushwa na ufisadi. Hoja hapa ni kwamba Serikali inaendelea kutoa uraia kwa wahamiaji wengi wasiokuwa na sifa za kupata uraia wa Tanzania. Wiki iliyopita, Serikali kama kawaida yake ilitoa tangazo tunaloweza kuliita la kisanii katika baadhi ya magazeti kuhusu watu walioomba uraia wa Tanzania. Pamoja na tangazo hilo kuficha mambo mengi muhimu kuhusu watu hao, linamtaka Mtanzania yeyote anayepinga watu hao kupewa uraia amwandikie Waziri wa Mambo ya Ndani na kutoa sababu kwa nini wasipewe uraia. Hiki ni nini kama siyo kichekesho cha mwaka? Inawezekanaje tangazo lisilokuwa na kichwa wala miguu, kwa maana ya kuwa na taarifa muhimu za waombaji wa uraia lililotoka mara moja tu, tena katika gazeti moja au mawili liwawezeshe Watanzania wengi kuwafahamu watu hao na kuitaarifu Serikali? Je, watawezaje kuwasiliana na Serikali wakati tangazo hilo halionyeshi anuani au simu ya waziri au wizara husika? Serikali kweli ina dhamira ya kuwahusisha wananchi katika mchakato huo wa kuwapa au kutowapa uraia watu hao? Tatizo hapa ni kwamba suala la kutoa uraia limepewa usiri mkubwa. Ndiyo maana kwa makusudi taarifa inayotolewa na Serikali kuhusu watu hao inakuwa nusunusu ili kuwachanganya wananchi wenye pingamizi wasijue pa kuanzia. Na ndiyo maana hata baada ya zoezi hilo Serikali haitoi taarifa kwa umma kuhusu waliopata na walionyimwa uraia. Zoezi la kutoa uraia hufanywa kwa tahadhari kubwa katka nchi nyingi duniani. Kwanza, mwombaji lazima atume maombi akiwa nchini mwake. Hapa tunashuhudia watu wakiingia nchini ovyo na baadaye kuomba uraia. Pili, kuna vigezo vinavyoangaliwa, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa elimu na taaluma yake kwa nchi anayoomba uraia; au umri na uwezo wake wa kiuchumi wa kumwezesha kujitegemea; au sababu za kibinadamu kama kukimbia vita, mateso, na kadhalika. Uzoefu umeonyesha kwamba nchi yetu inatoa uraia kwa watu wazima na tegemezi ambao hawawezi kuwa na manufaa yoyote kwa nchi yetu. Tunatoa uraia kwa watu wanaogeuka wachuuzi na kupigana vikumbo mitaani na vijana wetu wasio na ajira. Hii inatokana na baadhi ya ndugu zao ambao tayari wana uraia wa Tanzania (ambao waliupata kinamna?) kutoa rushwa na kuwawezesha kupewa uraia. Ndiyo maana Tanzania imekuwa kama nchi isiyo na mwenyewe ambayo inajulikana kwa jina la mitaani kama Shamba la Bibi. Tumegundua gesi na hivi punde tutagundua mafuta. Uraia sasa utazidi kutolewa kama njugu, kwani wageni watamiminika ili kufaidi nishati hizo. Tusipokuwa makini tutaiuza nchi yetu. ........................................................................................................................................................ |
No comments:
Post a Comment