Fursa za uwekezaji
zinazidi kutolewa kwa kiasi kikubwa nchini ikiaminika kuwa uwekezaji ndio
utakao tufanya tutoke katika nchi zinazoendelea na kuwa nchi za uchumi wa kati.
Hayo yameonekana baada ya Waziri wa Nishati na Madini kutembelewa na Waziri wa chuma
wa nchini India Mr. Dileep Raj Singh
Chaudhary aliyefika kutafuta nafasi za uwekezaji kwa
kampuni za india zinazoweza kuwekeza katika sekta za nishati na madini na
kuokelewa kwa moyo na wenyeji wake.
Profesa Muhongo
ameahidi kuwa na ushirikiano mzuri na nchi hiyo na kwamba wataoneshwa ramani
zenye maeneo muhimu kwa ajili ya shughuri za uwekezaji katika sekta za madini
na nishati.
Pia amesisitiza kuwa
ushirikiano baina ya nchi hizo haujaanza leo kwani toka kipindi cha uhuru
wahindi walitumika sana katika shughuri za maendeleo ikiwa ni pamoja na
kufundisha.
Muhongo amesema,
pamoja na uwekezaji huo, ni lazima serikali ya Tanzania iwe na hisa kwenye
makampuni yatakayofika ili kuwekeza nchini ili rasilimali za nchi ziwe za
manufaa kwa taifa na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wake
Waziri wa Chuma India Bw. Dileep Raj Singh
Chaudhary amefurahishwa na
mapokezi mazuri na kwamba kwa upande wao wako tayari kuwekeza katika madini ya
makaa ya mawe, manganese, gold, diamond na chuma.
Pamoja
na hayo imeelezwa kwamba katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini ndugu,
Eliakim Maswi watasani makubaliano ya kushirikiana kiutendaji na Katibu Mkuu wa
India.
.............................................................................................................
MAHAFARI YA PILI YA DIPROMA YA UUGUZI CHUO CHA UUGUZI NTC TUKUYU WAHITIMU 56 WAFANIKIWA KUMALIZA MAFUNZO YAO TAYARI KUWAHUDUMIA WATANZANIA
SHEREHE ILIANZA KWA MAANDAMANO YALIYOANZIA TUKUYU MJINI HADI CHUO CHA NTC TUKUYU KILICHOPO MAKANDANA |
SHEREHE ILIANZA KWA MKUU WA CHUO NOLASCA MTEGA KUWAKARIBISHA WAGENI WAALIKWA |
ADISON EMMANUEL AKISOMA RISALA KWA NIABA YA WAHITIMU WA DIPROMA YA UUGUZI |
MR MANGA KUSHOTO AKIONGOZA KIAPO CHA UKUNGA KWA WAHITIMU |
WASHA TAA YA UPENDO |
KIAPO KWA WAKUNGA |
SHARIF HAMIS (WA KWANZA KITAARUMA DARASANI) |
ROSEMARY ARROKO (NIDHAMU BORA KATI YA WAHITIMU) |
NEEMA SADDI ( WATATU KITAARUMA DARASANI) |
PICHA YA PAMOJA NA MGENI RASM PAMOJA NA WAKUFUNZI WA CHUO CHA WAUGUZI TUKUYU NA WAPILI KWA MBELE UPANDE WA KUSHOTO NI PILLI KIMATA AMBAYE NI MRATIBU WA MAFUNZO YA UUGUZI TANZANIA |
WAHITIMU WAKAKABIDHIWA VYETI |
MZAZI AKIMPONGEZA BINTI YAKE ESTER HAULE KWA KUHITIMU DIPROMA YA UUGUZI |
PAULINA BROWN AKIFURAHI NA DADA YAKE BAADA YA KUHITIM DIPROMA YA UUGUZI |
FAMILIA YA MAREHEMU MCHUNGAJI MWAIKENDA WAKIFURAHIA PICHA YA PAMOJA NA KIJANA WAO LUGANO MWAIKENDA ALIYESHIKA CHETI |
ANDIKENI HABARI ZA UCHUNGUZI ZAIDI ACHANENI NA HABARI ZA SEMINA NA MIKUTANO- MWOLEKA
Na Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
WAANDISHI wa habari hapa Nchini
wameaswa kuhakikisha kuwa wanajiwekea utatibu wa kuandika zaidi habari
za uchunguzi kuliko kurtegemea habari za semina na mikutano kwani habari
za mikutano na semina bado hazitoi majawabu na changamoto kwa jamii
Endapo kama waandishi wa habari
wa Tanzania wataweza kujiwekea utaribu wa kuandika habari ambazo zina
uchunguzi wa kutosha basi watakuwa ni chanzo kikubwa sana cha maendeleo
ya Nchi
Hayo yalielezwa Jana na Anjelo
Mwoleka ambaye ni Mkurugenzi wa Jambo Arusha Publisher wakati akiongea
na wahitimu wa fani ya uandishi wa habari katika chuo cha uandishi wa
habari Arusha (AJTC) katika maafali ya sita ya chuo hicho yaliyofanyika
chuoni hapo.
Aidha Mwoleka alisema kuwa kwa
sasa kuna wimbi kubwa la waandishi wa habari a wanajihusisha zaidi na
masuala ya habari za Semina na kuachana na habari za kiuchunguzi hali
ambayo wakati mwingine ina nyima haki za msingi za jamii kwa kuwa
waandishi wa habari wana nafasi kubwa sana ya kuibua maovu yanaoendelea
kwenye Jamii
Alifafanua kuwa habari za
uchunguzi ndani ya Nchi ya Tanzania ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi
hivyo basi wana habari hawapswi kukimbia na badala yake wanapswa kuzipa
kipaumbele kikubwa ili kuweza kuruhusu changamoto kwenye sekta zote
kujilikana
“kuwa mwandishi wa habari sio
lazima uwe unajua ratiba za mikutano za kila siku bali kuna maana kuwa
unapaswa kujua na kutambua kuwa unatakiwa lkuwa mchunguzi na hapo ndio
kazi yako itakuwa na manufaa makubwa sana kwa jamii hivyo basi habari za
muhimu zinatakiwa kupewa kipaumbele tena kikubwa sana ili nchi ya
Tanzania iweze kufika mahali ambapo inatakiwa kufika kama zilivyo nchi
nyingine ambazo zimeendelea duniani”aliongeza Mwoleka
Awali wahitimu wa mafunzo hayo ya
uandishi wa habari katika ngazi ya cheti, na shahada walisema kuwa
pamoja na kuwa chuo hicho kimewalea katika maadili mazuri lakini bado
wanakabiliwa na uhaba wa vifaa kama vile Kompyuta, na Kamera kwa ajili
ya mazoezi.
................................................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment