USAFIRI KWA KWENDA USHIRIKA, KATUMBA, KIWIRA, MASOKO, MBAMBO, LUFILYO NA LWANGWA HAPA NDIO STENDI KUBWA YA DALADALA ZINAPOANZIA KUELEKEA KUNAKOHUSIKA |
MIUNDOMBINU MIBOVU YA STENDI YA TUKUYU MJINI HUKU HALMASHAURI IKIWA INACHUKUA USHURU KILA SIKU WA SOKO NA DALADALA TSH 500/= KWA MAGALI MADOGO NA MAGALI MAKUBWA NI SH 1000/= KWA SIKU |
BAADHI YA WAFANYAKAZI WA UJENZI WA BARABARA WAKIFURAHIA KAMERA YA KINGOTANZANIA |
Standi hiyo
imeonekana kuwa na mashimo yaliyojaa maji machafu na matope
yanayosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika wilayani Rungwe na
kusababisha kero kwa watumiaji wa standi
hiyo.
Ubovu wa standi hiyo unatokana na Halmashauri ya
wilaya ya Rungwe kubadilisha matumizi ya uwanja wa mpira wa miguu wa Tukuyu na
kuwa soko la wamachinga na standi ya daladala bila maandalizi ya kuufanya uwe
sehemu inayoweza kustahimili matumizi ya magari na wafanyabiashara.
Uwanja wa mpira
uliogeuzwa kuwa standi na soko unapelekea madereva kupaki magari bila mpangilio
na kufanya standi ionekane kuwa ni ndogo ukilinganisha na matumizi ya eneo
hilo,pia kufanya abiria wapate shida katika standi hiyo hivyo huwalazim abiria
kushuka nje ya standi.
Barabara zinazofanyiwa matengenezo ni
zile barabara zote zinazotokea keepleft na ile ya kutoka Makandana barabara kuu
kwenda hospital ya wilaya ya Rungwe ya
Makandana kwa kiwango cha rami na zile zilizo nje ya Tukuyu mjini kama barabara ya kutoka Bagamoyo kwenda Katumba kipitia Lubiga na
barabara ya Majengo au Bujinga kwa kiwango kisicho cha rami.
Baadhi ya
barabara zimeanza kuharibika mara baada ya kumaliza kumwaga mchanga na kushindilia na kufanya zirudi katika muonekano wa mwanzo, na zingine
kumeguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Wakizungumza na kingotanzania watumiaji wa stend ya Tukuyu kwa maana ya madereva na wamachinga wamesema kila siku halmashauri ya Rungwe inachukua ushuru kwa kila mfanya biashara wa soko na kwa kila Gali linapotoka stendi hapo. Hivyo hadi sasa ubovu wa miundombinu ya stendi inatokana na watendaji wa halmashauri kutoichukulia maanani stendi kwa kuifanyia ukarabati zaidi ya kujipatia pesa bila ya kufanya ukarabati wa stendi ya daladala Tukuyu.
Katika
kutaka kujua zaidi kuhusu muafaka wa standi hiyo na barabara zinazoendelea
kujengwa mhandisi wa wilaya alikataa
kuongea na mwandishi wa Habari kwa madai kuwa hana
ruhusa ya kuzungumzia hayo na wala wao si wasemaji na kuelekeza kuwa
mkurugenzi ndie mwenye uwezo wa kuzungumzia hayo na kutoa kibali cha wao
kuzungumza,
Kingotanzaniaikafika ofisi ya Mkurugenzi na lakini ofisi ya mkurugenzi imesema kuwa kwa sasa muda wa kuongea nawe haupo (mda
tuliofika ofisini kwakwe) hataweza kuzungumza wala kuonana na mtu kwani anaenda kukagua miradi ya maendeleo vijijini.
TUMAIN OBEL
KINGOTANZANIA
No comments:
Post a Comment