Thursday, January 22, 2015

MKOA WA MBEYA WAIOMBA IDARA YA MAMBO YA KALE KUWAKABIDHI MAKUMBUSHO YA MAMBO YA KALE YA KIMONDO

Wanahabari  wakitazama  Kimondo
Mwanahabari  wa Habari  leo  Iringa na mwenyekiti wa chama  cha waandishi wa habari  mkoa  wa Iringa Frank  Leonard  akitoka  kutazama  Kimondo
Mgeni  akisaini kitabu cha wageni katika  ofisi ya makumbusho ya mambo ya kale  ya  Kimondo Mbeya
Wanahabari wakitoka katika  Kimondo  kulia na Slvanus  Kigomba  (ITV) na kulia ni Iren Mwakalinga (TBC),nyuma yao ni ofisi ya makumbusho  hayo
Mhifadhi  akionyesha  jiko  ambalo  linatumika  eneo  hilo
Nyumba ya  wahifadhi  wa makumbusho ya mambo ya kale ya  Kimondo Mbeya
Mhifadhi  msaidizi  wa makumbusho ya  Kimondo  akiingia katika nyumba  yake
Hii  ndio  nyumba  ya  mhifadhi mkuu na mhifadhi msaidizi wa Kimondo  Mbeya

Mwanahabari  wa ITV Iringa  Slvanus Kigomba  akijipumzisha kando ya  Kimondo
Mwanahabari  wa Star Tv Iringa  Mawazo Marembeka  kushoto akiwa na mzee  wa matukiodaima katika Kimondo
Wanahabari  wakimhoji mhifadhi msaidizi  wa makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo Mbeya  Bw Mussa Nsojo
Hiki  ndicho  kimondo  kina tani 12
Afisa utalii kanda  ya  kusini Tanapa  Bi Risala Kabongo akiwa katika kibao  cha Kimondo
Na MatukiodaimaBlog
MKOA  wa  mbeya   umepania  kuboresha miundo  ya  kituo cha mambo ya  kale  cha  Kimondo wilayani Mbozi mkoani hapa  iwapo Idara ya Mambo ya kale iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii itakubali  ombi la mkoa   huo  kukabidhi  kivutio  Halmashauri  ya  Mbozi.
 
Hatua
hiyo   imekuja  kufuatilia ziara ya  wanahabari  mkoani Iringa
wanaotembelea vivutio  vya  utalii  mikoa ya  Mbeya, Njombe na Iringa
kama  njia ya  kuhamasisha  utalii  mkoa ya nyanda  za  juu  kusini na
pia  kubaini sababu  za  utalii kutokua kwa kasi katika  mikoa   hiyo 
.
 
Mhifadhi
msaidizi  wa  kituo  cha makumbusho ya  mambo ya kale ya  Kimondo
wilayani  Mbozi Bw Mussa Nsojo alisema  kuwa  mbali  ya  watalii wengi
kupenda  kutembelea  eneo  hilo la Kimondo ila miundo  mbinu ya  eneo
hilo si rafiki kwa  watalii kuendelea  kutembelea  kutokana na
serikali  kushindwa  kuboresha  majengo na  eneo  hilo kwa  ujumla.
 
Alisema
kuwa  kimondo  hicho  ambacho mwaka kilipoanguka  eneo  hilo
haufahamiki ila  utafiti wake ulianza kati ya  mwaka 1930 -1931 na
kubainika  kuwa  si  jiwe la kawaida  bali ni sayari iliyoanguka  kutoka
angani  toka  wakati   huo  kimendelea  kupata  umaarufu  wa  watalii
kufika  kutembelea  eneo hilo japo katika  eneo  hilo mazingira  yake ni
mabovu  zaidi.
 
Mhifadhi
huyo  akielezea  historia  ya  kimondo  hicho  alisema  kabla  ya
watafiti  kubaini  kuwa ni  kimondo miaka  ya  nyuma kulikuwa na
wenyeji  ambao walikuwa  wakiishi  eneo  hilo na  mkazi  mmoja
aliyefahamika  kwa jina la Harele  ambae  alikuwa akifanya kazi  ya
uhunzi kuweza kubaini jiwe  hilo la ajabu wakati akitafuta  udongo chuma
kabla  ya  kumega kipande  kidogo na kutengenezea shoka .
 
Alisema
kutokana na wakati   huo chuma kuwa na dhamani  kubwa alipeleka
taarifa  kwa chifu  wa  eneo  hilo na  kulifanya  eneo hilo  kuwa  la
tambiko kabla utawala  wa Waingereza  kuchukua eneo  hilo na
kulihifadhi kabla  ya  serikali ya  Tanzania  kupitia idara ya mambo ya
kale  kuhifadhi  eneo  hilo.
 
Kuhusu
changamoto  kubwa  zilizopo eneo  hilo alisema ni pamoja na kukosekana
kwa  nyumba  bora  za watumishi ,jengo la ofisi  ya makumbusho  kutokana
na kibanda  kilichopo  kutokuwa na sifa ya utalii ,pia miundo mbinu  ya
barabara  kufika  kituoni hapo.
 
Afisa
utalii ofisi ya utalii kanda  ya kusini Bi Risala Kabongo akielezea
kivutio   hicho  alisema  kuwa  ni  moja kati ya  vivutio  visivyo  vya
kawaida  hapa  nchini na kuwa  iwapo  serikali itaboresha  zaidi  eneo
hilo upo uwezekano  wa uchumi  wa  mkoa  wa Mbeya kukua  zaidi  kupitia
kivutio  hicho .
 

Kivutio   hiki kinavutia   zaidi ila ushauri  wangu  kwa serikali ni
kuboresha  miundo  mbinu ikiwa ni pamoja na kutenga eneo la banda la
wageni na eneo la kujenga mahema kwa  wageni…..Kimondo  hiki  kimetoka
katika  sayari ya Mars na  hivyo ni  kivutio  cha ajabu  zaidi”
 
Katibu
tawala msaidizi (miundombinu)  mkoa  wa  Mbeya  Kastory Msigala
alisema  kuwa mkoa  huo  kupitia  kikao  chake  cha kamati ya ushauri
ya  mkoa  kimeiandikia  barua  idara ya mambo ya kale  ili kuipa eneo
hilo  la Kimondo Halmashauri ya  Mbozi  ili  kusimamia kwa lengo la
kuiboresha  zaidi.
 
Kwani
alisema  shida  kubwa ya  Halmashauri  hiyo na mkoa  kushindwa
kuboresha  majengo na miundo  mbinu  inayozunguka  makumbusho hayo ni
kutokana na kutokuwa na mamlaka ya  kufanya  hivyo kutokana na usimamizi
wa eneo  hilo  kuwa  chini ya idara ya mambo ya kale ila pale  idara
hiyo  itakapokabidhi katika serikali ya  wilaya  upo uwezekano wa
wilaya  kusimamia  vizuri  zaidi.
 
Alisema
katika mkoa   huo kuna  jumla  ya  vivutio 13  vilivyotambuliwa
kikiwemo  kivutio   hicho  cha Kimondo  na  kuwa mbali ya  vivutio
hivyo  bado  mkoa  umejipanga zaidi  kutangaza  utalii  kufuatia
ushirikiano mkubwa  uliopo kati ya  mkoa huo na ofisi ya SPANEST  , bodi
ya utlii ,wizara  ya utalii na wadau mbali mbali  kukuza  utalii
mkoani  humo .
Post a Comment