Monday, February 4, 2013

MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM

 

22 
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Jakaya Kikwete akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 36 ya CCM zilizofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma na kuhudhuriwa  na wananchi mbalimbali waliojitokeza kushiriki katika sherehe hizo.
Wawakilishi wa vyama rafiki vya CCM kutoka nchini Burundi CNDD kinachotawala nchini humo, na PPRD kinachotawala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
16 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza katika maadhimisho hayo.
23 
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akizungumzia mikakati ya Serikali katika maadhimisho hayo juu ya urejeshaji wa huduma za treni katika kituo cha Reli ya Kati cha Kigoma.
14 
Kikundi cha ngoma kutoka nchini Burundi kikitumuiza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
15 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika maadhimisho hayo katika uwanja wa Lake Taganyika.
2 
 Rais Jakaya Kikwete akiangalia picha zilizochorwa zikimuonesha yeye na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM
5 
Rais Jakaya Kikwete akiangalia ndizi zinazozalishwa mkoani Kigoma katika banda la wakulima wa ndizi kutoka mkoa huo.
6Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa mkoa wa Kigoma waliojitokeza kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya CCM kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
7 
Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
8 
 Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtunza mmoja wa wasanii wadogo wa kikundi cha ngoma kutoka nchini Burundi kilichoshiriki katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.
9 
Rais Jakaya Kikwete akiangalia vikundi vya ngoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Lake Tanganyika kwa ajili ya kushiriki katika maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi CCM  Kutoka kushoto ni Makamu Mweyekiti Bara Mzee Philip Mangula, Naibu Katibu Mkuu Bara Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana.
10 
Wananchi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
11 
Vijana wa Chipukizi wa CCM wakipita kwa Gwaride la Heshima na Utii mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
13 
Vijana wa Chipukizi wakiimba wimbo wa Kwaya katika maadhimisho hayo.
18 
Msanii Diamond akiongoza kundi lake katika kutoa burudani kwa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo.
20Mwanamuziki Diamond akiwaburudisha wananchi kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma katika maadhimisho ya miaka 36 ya CCM mjini Kigoma leo.

WITHOUT MOTHER ORGANIZATION NA BEZ MAMY KUSAIDIA UKARABATI NA UJENZI WA MADARASA YA SHULE ZA MSINGI WILAYA YA MBALARI, CHUNYA NA RUNGWE

Madarasa ya shule ya msingi kisa wilayani Rungwe yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa watu wa Jamhuri ya Czech kupitia shirika la Without Mother (Tanzania) kwa kushirikiana na Bez Mamy (Czech Republic) 
Mratibu wa miradi ya Bez Mamy Africa na Mwenyekiti wa Without Mother Organization kulia Bw Chris Zacharia akiwa na Vituko Issa  Mkuu wa shule ya msingi Simike Wilaya ya Mbarali wakijadili mpango wa kumalizia jingo la darasa la awali ambalo wananchi walishindwa kulimaliza
Without Mother organization|Bez mamy wakiwa na Kamati ya maendeleo ya shule ya Msingi Ilenge wilaya ya Rungwe baada ya mjadala wa kuifadhili shule hiyo kuboresha majengo na kuiwekea umeme kwa ajili ya kuanzisha mafunzo ya computer shuleni hapo
Mratibu wa Miradi ya Bez Mamy Africa na Mwenyekiti wa Shirika la Without Mother Bw Chris Zacharia akitambulishwa kwa wazazi na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ilenge akiwa na Mratibu wa miradi ya Shule wa Bez Mamy Eliška Nováková kushoto na mratibu wa Elimu kata ya Kimo wilaya ya Rungwe
 Bi Maulicia Mkusa kulia

Darasa la chekechea la shule ya msingi Galaula linalojengwa kwa ufadhili wa watu wa Jamhuri ya Czech kupitia shirika la Without Mother (Tanzania) kwa kushirikiana na Bez Mamy (Czech Republic)

Picha chini Mratibu wa Miradi za Shule wa Shirika la Bez Mamy Eliška Nováková akikagua majengo ya nyumba za waalimu katika shule ya Msingi Mahango wilaya ya Mbarali. Majengo hayo yaliyokuwa yanajengwa kwa nguvu za wananchi wamesimama baada ya wananchi kukosa uwezo wa kuyaendeleza
 
 

NCCR-MAGEUZI YAIBOMOA CHADEMA MBEYA.
-Viongozi na makada zaidi ya 20 wang’oka

Moses Mwasubira, ambaye alikuwa mwenezi wa Chadema wilaya ya Mbeya akikabidhiwa kadi ya NCCR na 
Mmoja wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye inadaiwa kuwa ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo wake wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na kung’ara mkoani 
Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda,
 Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

 Aliyewahi kuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi , Januari 20 mwaka huu Eddo Mwamalala, alisema wanachama hao waliomfuata ni mtaji mkubwa wa kuhakikisha inakimaliza chadema mkoani hapa.CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimesema taifa limepoteza muelekeo kutokana na viongozi wake wengi waliopewa dhamana ya kuongoza kushindwa kutimiza wajibu wao, hali ambayo imesababisha wananchi kuishi katika mkanganyiko mkubwa.

Hayo yalisemwa jana, Jijini hapa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Double J, mbele ya waandishi wa habari, Danda alisema ili taifa liweze kupiga hatua za kimaendeleo ni lazima liwe na siasa safi na uongozi bora.
Alisema kutokana na dhana hiyo kukosekana kwa viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza kumesababisha kuliacha taifa na wananchi wake wakiishi katika mkanganyiko mkubwa unaotokana na kupanda kwa gharama za maisha.
“Vyakula vimepanda, kadhalika nauli…. Kwa ujumla gharama za maisha imepanda sana nahii yote imesababishwa na taifa kukosa watu wa kufanya siasa safi ambazo zingetuletea viongozi bora” alifafanua Danda.


Alisema msingi pekee wa taifa kupata maendeleo ni rasilimali watu ambayo imejengwa kwa kupewa elimu, hivyo kitendo cha serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kukosa mitaala ya elimu ni inaonesha taifa lilivyokosa muelekeo.
“Rasilimali watu ni muhimu katika mchakjato wa maendeleo kuzidi hata hayo madini, lakini umeona kilichotokea juzi pale bungeni…. Mwenyekiti wetu (Jems Mbatia-NCCRA-Mageuzi) alichokieleza na kilichotokea”.


Aliongeza kuwa licha ya CCM iliyoiweka serikali madarakani kujipambanua kwa itikadi ya ujamaa na kujitegemea, lakini serikali hiyo imeshindwa kuisimamia hivyo kufanya taifa kushindwa kujitegemea na badala yake limegeuka kuwa ombaomba.
Alisema hali hiyo inajidhihirisha kwenye bajeti ya serikali, kwani zaidi ya asilimia 40 ya bajeti hiyo inategemea msaada wa wafadhili jambo linalokinzana na mfumo wa itikadi yake iliyojiwekea kama malengo wakati ikitafuta dhamana ya kupewa nafasi ya kuongoza nchi.
Kwa upande wake mwakilishi wa kundi la wanachama 21 waliohamia ndani ya NCCR-MAgeuzi, Moses Mwasubira, ambaye alikuwa mwenezi wa Chadema wilaya ya Mbeya Mjini, alisema wamefikia uamuzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Miongoni mwa sababu hizo ni kudai kuwa uongozi wa taifa wa Chadema kushindwa kujenga Demokrasia ya kweli ndani ya chama kwa kukumbatia ufisadi wa kutumia vibaya ruzuku ya chama na kuwaacha wa mikoani wakifanya kazi kubwa ya kuchangisha fedha.
Uongozi mbaya wa Katibu Mkuu wa chama hicho taifa,Dk.Willbroad Slaa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, kushindwa kusimamia katiba ya chama hicho katika kutatua migogoro, badala yake wakitumia na kuamini kuwa kufukuza wanachama tena kwa majungu ndio suluhisho la kukijenga na kukiimarisha chama.
Lakini pia walilalamikia chama hicho kujaa utashi wa nguvu ya umma na kulazimisha maandamano, migomo vitu ambavyo si vya lazima na kwamba kamwe hiyo si njia sahihi na malengo ya kweli ya kutafuta ukombozi.


Naye mmoja wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye inadaiwa kuwa ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo wake wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na kung’ara mkoani hapa.
Kwa upande wake aliyewahi kuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi , Januari 20 mwaka huu Eddo Mwamalala, alisema wanachama hao waliomfuata ni mtaji mkubwa wa kuhakikisha inakimaliza chadema mkoani hapa.


Na Moses Ng’wat, Picha na Mbeya yetu
 
 
Post a Comment