Saturday, February 2, 2013

RAIS KIKWETE AKAMILISHA USAJILI WA KITAMBULISHO CHA TAIFA

j1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha kwa ajili ya Kitambulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho cha Taifa nyumbani kwake asubuhi ya leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013.

j2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini baada ya  kuthibitisha maelezo yake binafsi kwenye Fomu ya Kitambulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho hicho  nyumbani kwake jijini Dar es salaam  leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bwana Dickson E Maimu.
j3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipigwa akichukuliwa alama vidole wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho cha Taifa nyumbani kwake asubuhi ya leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013. 
 PICHA NA IKULU
 

HOTUBA YA MHE RAIS KIKWETE YA MWISHO WA MWEZI JANUARI 2013

h1
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, TAREHE 31 JANUARY, 2013
Utangulizi
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyo ada naomba tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwenye Rehema, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kuzungumza kwa mara nyingine kwa kutumia utaratibu wetu huu mzuri wa mawasiliano baina ya Rais na wananchi wa Tanzania kila mwisho wa mwezi.  Siku ya leo nitazungumzia safari yangu ya Ufaransa, Uswizi na Ethiopia.  Pia nitazungumzia ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam.
Safari za Kikazi Nje ya Nchi
Ndugu Wananchi;
         Safari yangu ya Ufaransa, Uswizi na Ethiopia ilikuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu.  Nchini Ufaransa licha ya kuimarisha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi zetu, tumepata wawekezaji wengi wakubwa wenye nia thabiti ya kuja kuwekeza hapa nchini.  Pia tumekubaliana kuanza mazungumzo ya kuwa na mpango mwingine wa ushirikiano.  Mpango wetu wa sasa ulioanza mwaka 2006 uliisha mwaka 2010.  Mpango ule ulitusaidia sana kuboresha huduma za maji katika miji ya Utete mkoani Pwani na Mpwapwa mkoani Dodoma.
         Katika mkutano wa Kongamano la Uchumi wa Dunia uliofanyika Davos, Uswizi, tumehakikishiwa ushirikiano katika kuendeleza juhudi zetu za kuleta mapinduzi ya kijani ili tujihakikishie usalama wa chakula na kupunguza umaskini vijijini na kukuza uchumi wa nchi yetu.  Aidha, tulipata bahati ya kushirikishwa katika mjadala wa kuanzishwa kwa programu kubwa ya kuzisaidia nchi za Afrika kutatua matatizo ya upatikanaji wa umeme.  Naamini programu hiyo ikitekelezwa na wakubwa kuheshimu kauli na ahadi zao itakuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Ndugu Wananchi;
         Nchini Ethiopia tulishiriki katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika na katika kikao cha African Peer Review Mechanism (APRM) ambapo taarifa ya tathmini ya utawala bora ya Tanzania na Zambia iliyofanywa na APRM ilijadiliwa.  Kwa jumla hatuna mahali tuliponyooshewa kidole kuwa tunafanya vibaya.  Tumepongezwa katika mambo mengi na tumepewa ushauri kwa baadhi ya maeneo waliyoona hatuna budi kuyaboresha.  Nilipata nafasi ya kusema ambayo niliitumia kufafanua baadhi ya mambo yaliyokuwamo kwenye taarifa.  Niliwashukuru na kuahidi kuufanyia kazi ushauri uliotolewa.  Tathmini ya nchi yetu ilipitishwa kwa kauli moja.
Vurugu za Kupinga Gesi Kusafirishwa Kutoka Mtwara
Ndugu wananchi;
Kama mtakavyokumbuka tarehe 8 Novemba, 2012 kule Kinyerezi, Wilaya ya Ilala hapa Dar es Salaam, niliweka jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara na Songosongo kuja Dar es Salaam.  Karibu na mwishoni mwa Desemba, 2012 kukafanyika maandamano mjini Mtwara kupinga ujenzi wa bomba hilo.  Katika maandamano yale na baadaye kwenye kauli za wanasiasa na wanaharakati yakatolewa madai kuwa gesi hiyo itumike kwa maendeleo ya Mtwara na kwamba yale yanayotakiwa kufanyika Dar es Salaam yafanyike Mtwara.  Pia, zilitolewa shutuma nyingine dhidi ya Serikali eti kuwa kwa miaka mingi imewasahau na haiwajali wananchi wa Mikoa ya Kusini na ujenzi wa bomba hilo ni muendelezo wa hayo. Kauli mbalimbali za wanasiasa na wanaharakati ni kama vile ziliongeza mafuta kwenye kaa la moto na kuuchochea mpaka kukatokea matukio yaliyotusikitisha na kutshtua sote.  Baadhi ya ndugu zetu wamepoteza maisha na mali za watu na Serikali kuharibiwa. 
Ndugu Wananchi;
Katika hotuba yangu ya kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013, tarehe 31 Desemba, 2012, nililisemea jambo hili.  Leo mwezi mmoja baadae, napenda kusisitiza mambo mawili.  Kwanza kwamba, si kweli kuwa Serikali inapuuza Mikoa ya Kusini.  Na pili, kwamba kujenga bomba la kuipeleka gesi Dar es Salaam hakuinyimi Mikoa ya Mtwara na Lindi fursa ya kunufaika na gesi iliyopo Mtwara.

NAPE AUMALIZA UPINZANI RUNGWE MPYA

 Katibu waItikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Nape Nnauye ametembelea Kijiji chaRungwe Mpya kilichopo kata ya Rungwe Mpya Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kufanya shughuli mbalimbali za Chama ikiwa ni pamoja na Kuweka jiwe la Msingila Ofisi ya CCM kijijini hapo na kuhutubia mkutano wa hadhara wa wananchi wa Kata
  hiyo pamoja na Kata ya Asante Nyerere.
 Baada yakuweka Jiwe hilo la Msingi, Nnauye alikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa Chama hicho kutyoka katika kata za Asante Nyerere pamoja na Rugwe Mpya, wanachama
ambao wamerejea CCM kutoka vyama vya upinzani hasa NCCR Mageuzi na Chadema.
Aidha Nape pia alipata fursa ya kuzungumza na Wajumbe wa Nyumba Kumi wa chama hicho, Wazee pamoja na Vijana waendesha Bodaboda mjini Kasulu.

Pichani juu ni Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Rungwe
Mpya na Asante Nyerere katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
Kijiji cha Rungwe Mpya kilichopo Kata ya Rungwe Mpya Wilaya ya Kasulu
Mkoani Kigoma.
 Nape akikabidhi kadi kwa wanachama wapya.
 Baadhi ya Kadi zilizorejeshwa.
Mkuu wa Wilaya Kasulu, Danny Makanga akicheza ngoma wakati wa mapokezi hayo ya Nape Kijijini hapo.
 Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiweka jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Ofisi ya CCM Kijiji cha Rungwe Mpya Wilayani Kasulu.
 Nape akiangalia jengo hilo la CCM
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Kata ya Asante Nyerere, Yohana
Seif akizungumza katika mkutano wa hadhara mara baada ya kurejea CCM.
Katibu
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (katikati) akisalimiana na Diwani
wa Kata ya Rungwe Mpya, Moris Mahabula wakati wa Mapokezi ya Katibu
huyo. Kushoto ni Katibu wa Mwenezi wa Mkoa wa Kigoma, Zubery Mabie.
Akina mama wakishangilia ujio wa Nape kijiji cha Rungwe Mpya.
Nape akiwa na Mjumbe wa NEC, Kasulu, Daniel Nsanzugwanko.
Kutoka
kulia ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Kigoma, Zubery Mabie, Mjumbe wa
NEC Kasulu, Daniel Nsanzugwanko, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kasulu wakisikiliza kwa makini
maswali kutoka kwa wajumbe wa Shina wa CCM Kasulu.
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisikiliza hoja mbalimbali za wajumbe hao.
Wajumbe hao wakifuatilia kikao hicho na Katibu wa Itikadi na Uenezi.
Wanachama wakila Kiapo cha CCM Kata ya Rungwe Mpya.
Burudani ya ngoma kutoka kikundi cha akina mama.
 

Dkt. Migiro afanya ziara wilaya mpya ya Buhigwe Mkoani Kigoma 

by John Bukuku 

Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea maeneo hayo na kuweza kujionea changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo wananchi hao ikiwa ni pamoja na kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Kimataifa litakalowanufaisha wakazi wengi wa wilaya hiyo ambao wako kando kando ya Mto Maragarasi unaopakana na nchi jirani ya Burundi.Dkt. Migiro pia amewaasa wananchi wa maeneo hayo kuwa na umoja,mshikamano na upendo ili kuweza kuhimarisha mambo mbali mbali ya Wilaya.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha waliokuja kumpokea.
Wananchi wa Kijiji cha Buhigwe wakimuaga Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa CCM katika Kijiji cha Mnanila,Wilayani Buhigwe.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa Kijiji cha Mnanila kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati akiendelea na Ziara yake ya kutembelea Kata zote zilizopo wilayani humo.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wa Ziara yake ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwapungia watoto wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa Kijiji hicho jana.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Buhigwe ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakati wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi (kulia) akikabidhi Taarifa ya Utekelezani wa Ilani ya Uchaguzi kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akipokea ripoti ya Chama Wilaya ya Buhigwe,kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Buhigwe,Bi. Bennosa Mjema.Katikati ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo,Ndg. Elisha Bagwanya
Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Buhigwe wakimsikiliza Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro aliekuwa kwenye Ziara ya kutembelea wilaya hiyo jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akicheza ngoma ya asili ya kabila la Waha sambamba na Bibi Buchiro Edmas Kapina wakati wa Ziara ya kutembelea wilaya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma jana.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akilakiwa kwa shangwe na kinamama wa Kijiji cha Kilelema.
Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Kilelema,Everist Samson akisoma taarifa ya kijiji kuhusiana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kijiji hizo zikiwemo zile za kuvamiwa na majambazi wanaotoka nchi jirani ya Burundi.Kijiji hiki kipo mpakani kabisa mwa Tanzania na Burundi kwa kijiji cha Buhema Mkoani Lutana,nchini Burundi.
 
Wananchi wa Kijiji cha Kilelema kilichopo kwenye Wilaya Mpya ya Buhigwe,Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kilelema,Benedict Samson Mahuta (kulia) akitoa ufafanuzi juu ya eneo la Soko kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati),alietembelea eneo litakalojengwa soko la Kimataifa katika Kijiji hicho cha Kilelema.
Picha ya Pamoja na Watendaji wa Kijiji cha Kilelema.
Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro (pili kulia) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe,Ndg. Gishuli Mbegesi Charles (kushoto) kuelekea kwenye eneo la mpaka wa Tanzania na Burundi unaotenganishwa na sehemu ya Mto Maragarasi.
 
 
Muungano ukivunjika nini kitatokea?

seif 43e19
Katika mfumo gandamizi watawala wakitumia system zao za propaganda potofu wameweza kuteka fikra za watu kwa sababu maalumu za kulinda nafasi zao: Ukisema ukweli mweupe usiokuwa na doa hata chembe moja, basi utaambiwa aidha wewe ni Mchochezi au una Jaziba! Haya maneno mawili ni silaha kubwa sana ya tawala gandamizi kote duniani, na maneno haya yamesaidia sana
kuwadhibiti wale wote wanaopenda kudai haki zao au haki za watu wengine. Watawala wanapowagandamiza raia hawaelewi kabisa kwamba wao ndiyo wanaoweka jiwe la msingi wa Uchochezi, lakini wale wanaoonewa na kugandamizwa wanapotaka kujinasua toka mikononi mwa wagandamizaji, tayari wameshaonekana wanataka kutoka, hivyo neno linalotumiwa ili kuwadhibiti ni “Uchochezi” ! Sasa mchochezi hapo ni nani!? Mchochezi ni yule anayeukataa Ugandamizaji, au Mchochezi ni yule Anayemgandamiza mwenzie!? Hapa huhitaji kusomea sheria ili ujibu maswali haya.
Wakati wa utawala wa Idd Amin waandishi wa habari walioandika kwamba Amin anauwa watu; utawala wake uliwaita waandishi hao kwamba ni wachochezi! Viongozi wa kidini waliokemea mauaji ya Idd Amin waliambiwa wana ni Wachochezi na wana Jaziba! Jella anaposema nchi hii kuna mbegu mbaya ya udini ambayo inaharisha amani ya nchi hii; anaambiwa aache Jaziba!  Na wakati mwingine anaweza kutokea mwanasiasa akasema niache Uchochezi!
Mwaka 1990 kuna mcheza sinema mmoja wa Kimarekani Spike Lee alicheza sinema inayoitwa “Do the Right Things”, sinema hii inaonyesha jinsi mfumo gandamizi ulivyokuwa unawagandamiza watu weusi na kujiona kwamba wapo sahihi kufanya hivyo; na watu weusi nao badala ya kufuata taratibu za kisheria, wao wakaamua kupata haki kwa kutumia nguvu; na katika mazingira kama haya wote walipoteza: Wagandamizaji na Wagandamizwaji! Ndiyo maana sinema hii inatufundisha kwamba kila mtu afuate sheria; watu wote wapo chini ya sheria moja bila ya kujali imani za dini zao, rangi zao, elimu zao, kazi zao, makabila yao, uwezo wao kifedha au nyadhifa zao.
Kutumia Maneno ya Jaziba au Uchochezi tukidhani ndiyo tunadumisha Amani na Utulivu kama tulivyozoea kusema; tutakuwa hatupo sahihi asilimia mia moja; bali usahihi ni kutafuta chanzo cha tatizo na kuangalia ni namna gani tunaweza kulitatua bila ya kuidhuru jamii inayotuzunguka.
Wote tumezaliwa hapa hapa, tumesoma hapa hapa, tunaishi hapa hapa, tunafanya kazi hapa hapa, tunazeekea hapa hapa, tutastaafu hapa hapa, tutafia hapa hapa, na tutazikwa hapa hapa, lakini hatujui mambo ya hapa!
A. Ukishabikia Udini, ukajiona kwamba dini yako ni bora kuliko dini zingine, basi jua kwamba Dhehebu lako halikubaliki!
B. Ukishabikia Dhehebu, ukajiona dhehebu lako ni bora kuliko madhehebu mengine, basi jua kwamba Kabila lako halikubaliki!
C. Ukishabikia Ukabila, ukajiona Kabila lako ni bora kuliko Makabila mengine, basi jua kwamba Elimu yako haikubaliki!
D. Ukishabikia Elimu, ukajiona Elimu yako ni bora kuliko Elimu za wengine, basi jua kwamba kazi zako hazikubaliki!
E.  Ukishabikia Kazi, ukajiona Kazi zako ni bora kuliko kazi za wengine, basi jiandae kwa lolote, na kwa wakati wowote kwa vile Wanakitengo wapo kazini watakutafutia tu sababu na watakubana!
Dr. Jella
Post a Comment