Friday, February 1, 2013

WATANO WAFARIKI NA 130 WAJERUHIWA VIBAYA KATIKA AJALI YA ROLI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KWENDA SHAMBA KAPUNGA MBARALI MBEYA

MOJA YA MTOTO MAJERUHI AKIHAMISHWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA MISION CHIMARA NA KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
MOJA YA MAJERUHI AKISUBIRI KUPATA MATIBABU
HILI NDILO ROLI WALIMOPANDA VIBARUA HAO WA SHAMBA LA KAPUNGA

KWELI MUNGU NI MKUU HUWALINDA WATOTO WADOGO HAPA MKUU WA MKOA AKIMPA MOJA YA WATOTO WALIOPATA AJALI
HUYU BINTI NI MWANAFUNZI NAE ALIKUWEPO KWENYE AJALI HIYO 
MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI
HAWA WOTE NI WANAFUNZI WALIKUWA WANAENDA KUFANYA KIBARUA CHA KULIMA KWA MWEKEZAJI KATIKA SHAMBA HILO LA KAPUNGA (AJIRA ZA WATOTO TENA MUDA WA MASOMO)
MAJERUHI 22 WAKIPAKIZWA KATIKA ROLI AINA YA FUSO TAYARI KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
MAJERUHI WAKISAFIRISHWA KWENDA MBEYA
HUYU NDIYE  JOSEPH MWAISANGO AKITOKA KATIKA HOSPITALI YA CHIMALA BAADA YA KUSHUHUDIA NA KUPATA HABARI ZA UHAKIKA MAANA TAARIFA YA AWALI ILITOLEWA KUWA WATU WASIOZIDI 30 WAHOFIWA KUFA KATIKA AJALI SASA TUNAHABARI KAMILI BAADA YA MBEYA YETU KUFIKA KATIKA TUKIO



WATU watano wamepoteza maisha na wengine 130 wamejuruhiwa vibaya  huku hali zao zikiwa mbaya baada ya Lori walilokuwa wakisafiria shambani kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha  Mapogolo kata ya Itamboleo  Wilayani Mbarali Mkoani hapa.
Ajali hiyo imetokea leo saa 1:30 asubuhi ambapo lori hilo  ambalo ni mali ya Mwekezaji wa shamba la Kapunga Rice Project, na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye shamba la mwekezaji huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni wakazi kitongoji cha  Kapunga.
 Lori hilo lenye namba za uasjili T398 BSE Scania Tipa, ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina  Baraka Moreli, lilionekana likiwa katika mwendo kasi na   dereva huyo akiwa na lengo la kutaka kuipita pikipiki  iliyokuwa mbele yake. huku akishangiliwa na vibarua hao ipite ipite hiyo pikipiki haiwezi kutushinda sisi gari kubwa moja ya majeruhi alisema. ndipo walipofika kwenye kona dereva lilimshinda gari hilo na kupinduka
Akiwa Hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika hospitalini hapo alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya ,Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa msaada wa kuongezewa madaktari, kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na uwezekano wa kupata damu kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa kuwasiliana na uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili kuweza kuona namna ya kwenda kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro, alisema kuwa  katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na mwanamke mmoja. watatu wametambuliwa
Samweli Mapugilo mbena 30 mkazi wa Ilembula
Bon Mfupa 27 mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde Mbeya
   Aidha, Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika  ajali hiyo kuwa ni 130 ambapo wanawake ni 40 na wanaume 89 huku idadi ya watoto waliokuwa wameongozana na wazazi wao haikuweza kufahamika kwa haraka.

ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI WAKIWA WAMEFIKISHA MAJERUHI PAMOJA NA WATU WALIO FARIKI HOSPITALINI HAPO
 RIPOTI IKIWA INATOLEWA JUU YA AJALI HIYO HUSSEIN KIF
MMOJA YA ABIRIA WALIOKUWEMO KATIKA AJALI HIYO


 WILAYA YA RUNGWE YAUNDA KAMATI YA  UTALII YAMAINISHA VIVUTIO KUMI NA TISA  AMBAVYO VI VIVUTIO VYA KIPEKEE DUNIANI
MLIMA HUU WA KYEJO WILAYANI RUNGWE KILELENI HAPO PANA UWANJA MKUBWA NA MABWAWA SITA YA MAJI NA KINA BWAWA LAKE LINA MIUJIZA TOFAUTI

ZAO LA NDIZI WILAYANI RUNGWE

MLIMA KYEJO WENYE WANYAMA MBALIMBALI NA UMEGUNDULIKA NA GESI ASILIA AMBAYO WAWEKEZAJI WAMESHAANZA KUJENGA KIWANDA NA UZALISHAJI WA GESI UTAANZA HIVI KALIBUNI


MATUNDA

MBOGAMBOGA KWA WINGI ZA KILA AINA

NDIZI
HAPA NI CHINI YA DARAJA LA MUNGU AMBAVYO MAJI YANAPINA NA JINSI DARAJA LILIVYO CHONGWA KIAJABU
HAPA NI KAPOLOGWE

HAPA DARAJA LA MUNGU LINAVYOONEKANA UKIWA JUU
LEO NIMEPITA KUWAPA SALAM MARAFIKI ZANGU WAJASILIAMALI TUMEFURAHI SANA ILA SIKUBAHATIKA HATA KUNUNULIWA SODA DU HUU MWAKA MGUMU AU NI WATU WAGUMU OK NGOJA TUSONGEE


MANGULA: KIGOMA YA SASA SIO ILE YA ZAMANI

Na
Mroki Mroki, FK BLG Kigoma
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula amewasili
mkoani Kigoma asubuhi hii kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na
kupongeza mabadiliko makubwa yaliyopo mkoani humo hasa Uwanja huo wa Ndege
ambao unaonekana sasa kuwa wa kisasa.
Mangula
ambaye amepata mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nappe Nnauye pamoja na mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho ambaye ni
Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Mkuu wa Mkoa
wa Kigoma, Kanali Mstaafu. Issa Machibya pamoja na viongozi mbalimbali wa chama
na serikali.
Mangula
amesema Kigoma ya sasa si Kigoma aliyo ijua miaka iliyopita na viongozi
wanastahili pongezi kwa maendeleo hayo ya sekta mbalimbali.
“Kigoma
ya leo sio Kigoma ile ya zamani ..uwanja huu wakati ndege inataka kutua
nilitaraji nitasikia matairi ya kihangaika lakini nikashangaa tunakwenda vizuri
tu” alisema Mangula akishangiliwa na wakazi wa Kigoma.
Aidha
amewaambia wakazi wa Mkoa wa Kigoma kutembea kifua mbele kutoka na mafanikio
makubwa yaliyofikiwa hasa katika ujenzi wa uwanja wa ndenge wa kigoma ambao
zamani haukuwa na tabaka la lami ambapo sasa uwanja huo umewekewa tabaka la
lami na kuondoa usumbufu waliokuwa wakiupata zamani wananchi wa Kigoma.
Pia
Mangula amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kupuuza kejeli zinazoendelea
kutolewa na wanasiasa wa upinzani kuwa mkoa wa kigoma umesahaurika kitu ambacho
amesema hakina ukweli kwani mkoa huo sasa umefunguka kwa miundombinu ya
barabara.
Wakati
huo huo, katika kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi ccm,
mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili kesho mkoani hapa kwa
ajili ya maadhimisho hayo yanayotarajiwa kufanyika Jumapili Februari 3, 2013
katika uwanja wa Michezo wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Maandalizi ya sherehe hizo yanaendelea ambapo sasa yamefikia asilimia zaidi ya
themnini na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye pamoja na wajumbe wa NEC
na viongozi wengine wa CCM wanataraji kwenda kukagua maandalizi hayo jioni ya
leo.
Mangula akiteremka katika ndege.
Akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye
 Mangula akisalimiana na Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 
 
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Komred Philip Mangula akisalimiana
na viongozi mbalimbali wa CCM waliofika kumpokea Uwanja wa Ndege Mjini Kigoma
hii leo.
Makamu
Mwenyekiti wa UWT, Dogo Mabruk (kushoto) na Mjumbe wa NEC-Wilaya ya
Uvinza, Asha Baraka pamoja na wanachama wengine wa CCM wakimsikiliza
Mangula.

Vijana wa CCM waliofika kumpokea Makamu Mwenyekiti CCM Bara.

BAADHI YA WANANCHI WANANCHI MBEYA WALALAMIKIA MAKAMPUNI YA VINYWAJI BARIDI KUTOWAJALI AFYA ZAO

HII NI AINA YA SODA  TONIC WATER YA KAMPUNI YA COCA COLA  MBEYA IKIWA NA KILOBA CHA POMBE KALI AINA YA VODKA


WANYWAJI WA VINYWAJI BARIDI  MNAONA HIYOOO



BAADHI ya wananchi ambao ni watumiaji wa vinywaji baridi Jijini Mbeya wameyalalamikia baadhi ya makampuni yanayohusika na utengenezaji wa bidhaa hizo kwa kutozingatia usalama wa watumiaji.
Malalamiko hayo yamekuja kufuatia hivi karibuni mwananchi mmoja aliyoomba kuhifadhiwa jina lake kununua soda aina ya Tonic Water inayotengenezwa na kampuni ya Coka kukutwa ikiwa na karatasi la pombe kali aina ya Vodka.
Soda hiyo ikiwa mpya bila kufunguliwa ilikutwa katika duka moja eneo la Simike baada ya mteja huyo kuuiwa kwa lengo la kiutuimia lakini kabla ya kuifungua ndipo laipogundua uchafu huo.
Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa stori hii  alipewa taarifa na mhusika ambapo walienda moja kwa moja hadi kiwandani Coka eneo la Iyunga Jijini Mbeya na kupokelea na Meneja mauzo wa wilaya(Area sales Manager)
Baada ya kupokelewa na kuelezwa hali iliyotokea meneja huyo aliwapeleka waandishi kwa kitengo cha ubora wa bidhaa ambao bila woga walisema tuwaachie soda hiyo baada ya kuridhishwa kuwa ni mpya na inatoka kiwandani hapo.
Walidai waachiwe soda hiyo ili kuifanyia uchunguzi wa kimaabara katika uchunguzi utakafanyika kwa wiki moja hali iliyoleta sintofaham kwa walalamikaji huku wakihoji uchunguzi gani ufanyike ili hali uchafu unaonekana.
Aidha walidai kuwa pamoja na kukataliwa kubakishwa kwa soda hiyo walisema mlalamikaji hatanufaika na chochote ikiwa na kiwanda kutoathirika na tatizo hilo licha ya kuhusika na kuzalisha bidhaa yenye uchafu.
Hali kama hizo zimekuwa zikiwaathiri watumiaji wa vinywaji hivyo hasa wanaotumia  nyakati za usiku muda ambao si rahisi kwa mteja kugundua hali ya uchafu katika vinywaji.
Hata hivyo mhusika aliyepatwa na janga la soda hiyo kutoka kiwanda cha Coka aliiomba mamlaka zinazohusika kufuatilia hali ya usafi wa vifaa vya kubebea vinywaji hivyo kabla ya kupelekwa sokoni kwa watumiaji ili kunusuru afya za wananchi.

kinana azindua tawi la ccm

katibu
mkuu wa chama cha CCM, Abdurahman Kinanan akifungua pazia kuzindua tawi jipya la chama hicho ndani ya kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema jana jioni.

Jiwe la Msingi lililowekwa na Ndugu Kinana.

Ndugu kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi jipya la chama cha CCM  kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema jana jioni.
Ndugu Kinana akisomewa taarifa kutoka kwa wanachama wa chama cha CCM,mapema jana jioni.
Ndugu Kinana akizungumza na wanachama wa chama hicho sambamba na wananchi wa kata hiyo ya Bunyambo,Ndugu Kinana aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili kukamilisha ujenzi wa tawi hilo jipa la chama hicho.
Ndugu Kinana akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwambu,Wilaya ya Kibondo,Ndugu Kinana alikwenda shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na pia kushiriki ujenzi wake,pia aliahidi kutoa Solar Pannel kwa ajili ya kuzalisha umeme ofisi za walimu,Kompyuta moja,seti ya jezi mbili sambamba na mipira miwili kwa ajili ya shule hiyo.
Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari ya Kuwambu akiwa sambamba na baadhi wa viongozi wa Wilaya na mkoa kutoka chama cha CCM.
Wazee wa chama wa shina,Matawi,kata,Madiwani Wilaya,Wazee pamoja na Jumuiya kwa ujumla wakishangilia jambo kwenye mkutano wao wa ndani uliofanyika kwenye ukumbi wa Vijana,wilayani Kibondo.
Ndugu Kinana akizungumza na Wazee wa chama wa shina,Matawi,kata,Madiwani Wilaya pamoja na Wazee,lengo ikiwa ni kuwasilisha taarifa ya kazi za chama na serikali,Ndugu Kinana ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia shunguli mbalimbali za Vijana sambamba na hilo Kinana ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Milioni tatu kwa ajili ya kuwasaidia Walemavu.Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Vijana,wilayani Kibondo,Mkoani Kigoma.
Ndugu Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo,Emmanuel Gwegenyeza,pichani kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo,Venance Mwamoto pamoja na Kada wa chama hicho,Matoni Nyobeye,mara baada ya kuwasili kijiji cha Kilemba,wilayani Kibondo mapema leo jioni.
Msafara wa Ndugu Kinana pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa chama cha CCM,Mkoa na Wilaya.
Picha na Fullshangweblog

NAPE AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ILAGALA KIGOMA

 


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akiangalia matunda ya Mchikichi ambayo yanaacheshwa katika mapipa kwaajili ya kukamua mafuta ya mawese katika Kijiji cha Ilagala, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

 Wana CCM wa Igalula wakiwa katika kikao cha ndani na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha
Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye akikagua maendeleo ya ujenzi katika Kituo cha afya
Ilagala.
 Nyumba ya Daktari wa Ilagala

No comments: