Thursday, January 31, 2013

Siri mgogoro wa gesi yafichuka

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari kwenye makazi yake mkoani  Dodoma jana kuhusu hatua zilizochukuliwa kudhibiti vurugu za gesi mkoa wa Mtwara.Kulia ni waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.Picha na Fidelis Felix 
Na: Habel Chidawali, Dodoma na Abdallah Bakari, Mtwara
Madai kwamba gesi hiyo inapelekwa Bagamoyo yalikuwa moja ya ujumbe mkuu uliokuwa umeandikwa kwenye baadhi ya mabango wakati wa maandamano ya Desemba 27 mwaka jana yaliyofanyika Mtwara Mjini, yakiratibiwa na baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani. MOJA ya mambo yaliyoamsha hisia za wakazi wa Mkoa wa Mtwara hadi kushinikiza kwa vurugu wakitaka gesi isitoke mkoani humo, ni taarifa kuwa nishati hiyo ingepelekwa wilayani Bagamoyo, nyumbani kwa
Rais Jakaya Kikwete.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema jana nyumbani kwake mjini Dodoma kuwa, mbali na imani hiyo, amebaini pia kuwa mpasuko ndani ya CCM mkoani Mtwara na harakati za kisiasa ni sababu nyingine iliyochochea mgogoro huo.

Pinda alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mgogoro huo ambao ulisababisha vifo vya watu wanne huku wengine wakijeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa wa mali zikiwamo nyumba za wabunge kuchomwa moto na namna alivyofanikiwa kuuzima.

Waziri Mkuu alifanya ziara ya siku mbili mkoani Mtwara, Januari 25 na 26 mwaka huu na kufanikiwa kuzima mgogoro huo baada ya kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya wadau wa gesi mkoani humo.
“Sasa hili nililitolea ufafanuzi kwa kukanusha kuwa siyo kweli kwamba gesi inakwenda Bagamoyo. Lakini pia baada ya kukaa nao nilibaini kuwa hata viongozi wenyewe wa CCM hawako pamoja,” alisema Pinda na kuongeza:

“Pamoja na hayo nikachukua maelezo kuhusu matatizo yao mengine na nikawaahidi kwamba nitayafikisha katika mamlaka husika ili waweze kuona namna ya kufanya.”

Madai kwamba gesi hiyo inapelekwa Bagamoyo yalikuwa moja ya ujumbe mkuu uliokuwa umeandikwa kwenye baadhi ya mabango wakati wa maandamano ya Desemba 27 mwaka jana yaliyofanyika Mtwara Mjini, yakiratibiwa na baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani.

Pinda alisema viongozi wa kisiasa mkoani Mtwara wakiwamo wabunge, wameonekana kuwa na mpasuko unaosababisha uchochezi kwa makundi ya watu.

Alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Waziri Mkuu, Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Alhaji Masoud Mbengula alikiri chama hicho kumeguka na akataja sababu kuwa ni makundi yaliyotokana na uchaguzi wa ndani uliofanyika mwaka jana.

“Tusiwe wanafiki, ni kweli kuna makundi ndani ya chama… wabunge hawako pamoja na ndiyo hali iliyotufikisha hapa… suala hili lipo wazi kabisa,” alisema Alhaji Mbengula.
Kamati ya Spika hatihati
Akizungumzia Kamati ya Bunge iliyotarajiwa kuundwa na Spika kwenda Mtwara kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi wa huko, Pinda alisema hawezi kuingilia mhimili huo wa Dola isipokuwa atatoa taarifa bungeni na kama Spika ataona wabunge wameelewa, basi ataamua lolote.

“Nitakuwa na nafasi ya kuzungumzia jambo hili ndani ya Bunge na Spika akiona wabunge wamenielewa bila shaka atasitisha lakini akiona bado inafaa ataamua yeye,” alisema.

Kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari jana, kiongozi huyo alifanya mazungumzo na Mawaziri wanaotoka Mkoa wa Mtwara ambao ni George Mkuchika (Utawala Bora) na Hawa Ghasia (Tamisemi) pamoja na wawekezaji wa kutoka China ambayo alisema yalilenga kuwapa halihalisi ya huko.
Nchimbi afunguka
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alisema vurugu hizo zimefikia mwisho na Serikali haitavumilia tena machafuko ya aina hiyo.

Dk Nchimbi alisema timu ya wataalamu ipo Mtwara kuweka mambo sawa na kusema Serikali itatimiza majukumu yake pasi na shaka yoyote na kusisitiza kuwa haiwezi kukubali Tanzania ikawa vipande.
Alisema Serikali inafanya tathmini kujua hali ilivyo Mtwara na ikibidi itasitisha shughuli zote za kisiasa mkoani humo.



Dr.Migiro mkuu mpya chuo kikuu huria


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.

Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania. 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
30 Januari, 2013

TANZANIA INA UHABA WA MAFUNDI SANIFU MAABARA-MULUGO

philipo
NA: GLADNESS MUSHI
 TANZANIA inakabaliwa na tatizo la uhaba wa  mafundi Sanifu Maabara ambapo kwa sasa wanaozalishwa na Vyuo vya Ufundi hapa nchini hasa Arusha Techical College(ATC)ni ndogo sana hali ambayo inafanya baadhi ya shule za Sekondari hapa nchini kukosa ufanisi zaidi na Masomo ya Sayansi. Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa elimu na Ufundi hapa Nchini Bw Philiph Mulugo wakati akiongea na
wadau mbalimbali wa chuo cha ufundi Arusha(ATC)mapema wiki hii
Aidha Mulugo alisema kuwa bado hali si shwari hasa katika sekta hiyo ya mafundi sanifu wa maabara kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi yenye shule za Sekondari zaidi ya 400 wakati wanaozalishwa wakiwa bado ni 15
 Alisema kuwa hali hiyo inasababisha kuwepo na uhitaji mkubwa sana wa mafundi sanifu kwa kuwa ili shule yoyote ile iweze kufanya vema katika masomo ya Sayansi ni lazima kwanza wataalamu hao waweze kuandaa vifaa mbalimbali vya maabara ili kuruhusu wanafunzi wasome vizuri
 Mulugo pia alisema kuwa pamoja na uhaba huo wa mafundi sanifu wa maabara lakini lengo la Serikali la sasa ni kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na  Wataalamu hao ambao wataweza kushirikiana na walimu wa Sayansi hivi karibuni ambapo pia hata Vyuo vya ufundi navyo vinatakiwa kuhakikisha kuwa vinajiwekea utaratibu wa kuzalisha wataalamu wengi zaidi
 Alitoa wito kwa vijana wa Kitanzania kuhakikisha kuwa kamwe hawakimbii fani hiyo badala yake wajiunge na Chuo hicho cha  Ufundi Arusha ili waweze kudahiliwa kama wataalamu  ambapo hali hiyo itaweza kuokoa Jamii ambayo bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalamu hao
 Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt Richard Masika alisema kuwa kwa sasa Jamii inaona Masomo ya Sayansi ni Magumu kwa kuwa hakuna utaratibu wa kuyafundisha kwa vitendo jambo ambalo kwa sasa chuo hicho kimejipanga sana kuweza kujipanga kudahili wahitimu wengi zaidi ili kufanya masomo hayo yasionekane ni magumu
 Dkt Masika alisema kuwa ili masomo hayo yasionekane kuwa ni magumu kwa sasa wamejiopanga kwa kuhakikisha kuwa wanazalisha wataalamu wengi zaidi ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 watakuwa wamezalisha wataalamu zaidi ya 150 ambao wataweza kusaidia sana kuokoa shule zenye uhaba wa watalaamu hao


Nape Nauye akumbusha enzi za tanu yajenga nchi

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye leo ameshiriki katika shughuli za ujenzi wa madarsa katika Shule ya Sekondari Nyasha Wilayani Kasulu.Miongoni mwa Shughuli hizo alizoshiriki ni pamoja na kuunganisha kenchi, kubeba mawe na kupiga ripu chumba kimoja wapo cha madarasa na kumalizia na kupanda mti katika uwanja wa shule hiyo.


kuwa kiongozi muhimu kuwa mfano katika  kufanya kazi kwa vitendo




Ukistajabu ya Musa? ..........

ugomvi wanandoa wafichua makubwa


Emmanuel Kalema akiwa akimezungukwa na wananchi wenye hasira kali.
Wanandoa waliofarakana nchini Uganda wamewashangaza wakazi wa manispaa ya Nakawa, Kisenyi Zone.
Kulitokea kutoelewana baina ya Emmanuel Kalema (32), na mkewe aliyefahamika kwa jina moja la Aisha (28) hivyo mama huyo kuamua kufungasha vitu vyake na kutaka kuondoka na watoto wao ndipo ghafla Kalema aliporopoka kuwa akitaka kuondoka na watoto basi amchukuwe na Yule waliyemuua na kumzika katika msingi wa nyumba yao iliyopo Kireka-Banda.


Maneno hayo yaliushangaza umati uliokuwa ukishuhudia ugomvi  huo hali iliyopelekea watu kumzonga jamaa huyo na kumtaka atoe maelezo vizuri kuhusiana na mauji hayo.
Akiwa chini ya shinikizo la wananchi alisimulia kuwa yeye na mkewe walishirikiana kumuua mtoto wa nje wa mama huyo na kumzika kwenye nyumba hiyo ili waanze maisha mapya ya ndoa.
Baada ya kupata taarifa hiyoi wananchi walichukua majembe na kuanza kuchimba eneo lilitajwa na hatimaye walikuta mfuko wa plastiki ukiwa na mabaki ya mtoto huyo.
Kalema yuko chini ya ulinzi wa polisi na uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea.



Kinana akagua miradi ya maendeleo likiwemo soko la kimataifa la pamoja na ujenzi wa daraja mpakani mwa Tanzania na Burundi, Kibondo mkoani Kigoma.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Jengo la Soko la Pamoja lililokaguliwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mapema leo jioni,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma Magango akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokwenda kukagua Soko la Pamoja  leo jioni.  
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya Mpya ya Kokonko Bwa.Peter Toima (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya
Kibondo/Kokonko Bwa.Juma  Magango (shoto) na baadhi ya Wanachi
wakielekea kukagua  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi
wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya
mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini
vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya
Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na
Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo
unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji
na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya
Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.
Wakielekea kukagua ujenzi wa mradi wa darja la pamoja.
Pichani ni  Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.
 
Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.
 
Mradi huo unaotarajiwa kukamilika februari 20,2013 utagharimu kiasi cha shilingi 260,000,000/=,aidha imeelezwa kuwa mradi huo utatekelezwa kwa awamu nne,awamu ya kwanza imeshaanza ambayo unahusisha ujenzi wa daraja,barabara KM1 inayotoka kwenye soko hadi darajani na hifadhi ya Mazingira,utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia 70% mpaka sasa.

Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na  Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai alipokwenda kukagua mradi  wa ujenzi wa  daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi.
Msimamizi wa Mradi kanda ya Umwagiliaji kutoka Mkoani Tabora,Alfred Swai akitoa ufafanuzi mbele ya Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana kuhusiana na ujenzi wa Mradi wa daraja la Umoja ulioibuliwa na Wananchi wa Kijiji cha Nyabibuye mwaka 2011,ikiwa na lengo la kurahisisha biashara ya mazao ya kilimo na bidhaa nyingine kati ya wananchi wa Nyabibuye na vijijini vya Mishiha nchini Burundi,Mradi wa daraja hilo ni sehemu ya mpaka kati ya Tanzania na Burundi liofadhiliwa na serikali ya Japan kwa ushirikiano  na Serikali ya Tanzania kupitia Tanzania/Japan Food Aid Counterpart Fund.Mradi huo unajengwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia ofisi ya Umwagiliaji na huduma za ufundi kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo na Wananchi wa kata ya Nyabibuye.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye shule ya sekondari ya Nyamtukuza iliopo kwenye Wilaya ya Kibondo,mkoani Kigoma,pichani shoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwa.Amani Ntibakazi. 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mpya ya Kokonko Bwa.Peter Toima pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibondo/Kokonko Bwa.Juma Magango wakikagua ujenzi wa shule hiyo ya  Nyamtukuza 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kushoto akishiriki kwenye ujenzi wa shule ya sekondari ya  Nyamtukuza 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanafunzi wa shule ya sekondari ya  Nyamtukuza mara baada ya kuwahutubia mapema leo mchana,kulia kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwa.Amani Ntibakazi. 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya  Nyamtukuza mapema jioni ya leo,Kinana aliuahidi uongozi wa shule hiyo kuwapa umeme (Solar Pannel )mbili kwa ajili ya kuzalisha umeme shuleni hapo,Kampyuta moja pamoja na Televishen
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akipokelewa na wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko.
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye mkutanno wa hadhara mapema leo jioni na Wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko.
Sehemu ya shamba la Mahindi safi kabisa,ambalo pia Ndugu Kinana aliwahimiza wanakijiji cha Rumashi,kutumia Pembejeo za mbolea kuhakikisha wanapata mazao bora. 
Katibu Mkuu,Ndugu.Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Rumashi kata ya Nyabibuye,jimbo la Buyunga wilaya ya Kokonko mapema leo jioni.



RAIS JOSEPH KABILA WA DRC ATUA DAR KWA ZIARA YA SIKU MOJA

k1 
Ndege iliyomchukua Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
k2 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013
k4 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha maafisa mbalimbali Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013
k6 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
k7 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiendelea kuangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
k8 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Hyatt  Kilimanjaro jijini mchana wa leo Januari 30, 2013
PICHA NA IKULU
 
 
 

WAJASIRIAMALI WALIVYONUFAIKA NA SAFARI LAGER WEZESHWA

Mjasiriamali Elizabeth Chami (26), akioka keki kwenye jiko la kisasa alilozawadiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia promosheni ya Safari Lager Wezeshwa 2012, kwenye karakana yake iliyopo Tabata Mawenzi, Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Mfanyakazi wa karakana hiyo, Happiness akiweka akioka keki kwenye jiko hilo la kisasa.
Mfanyakazi wa Kiwanda cha kutangeneza Shampoo  cha L & V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam, Hashim Hussein akifungasha katoni za bidhaa hiyo. Kiwanda hicho kilisaidiwa chupa 15,000 baada ya mmiliki wa kiwanda hicho Valerian Luzangi (hayupo pichani) kuwa mmoja wa washindi wa promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Luzangi akisaidia kupanga vizuri chupa zilizojazwa shampoo. Kushoto ni mfanyakazi wa kiwanda hicho Stahabu Mwinyi.
Mjasiriamali Valerian Luzangi (38), kulia, akipanga vizuri katoni za shampoo anazozalisha katika kiwanda chake cha L & V Intergrated Firm, kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam juzi. Luzangi alisaidiwa chupa 15,000 baada ya kuwa mmoja wa washindi wa promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012, Kushoto ni mfanyakazi wake, Hashim Hussein.
Wajasiriamali Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha wakiwa sawa mfumo wa umwagiliaji katika moja ya mashamba  zao la matikiti maji ya Kampuni yao ya  Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012
Mjasiriamali Innocent Mberwa akionesha tikiti maji katika moja ya mashamba ya Kampuni yao ya  Tin Wax yaliyopo eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo wa maji wa umwagiliaji baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Wajasiriamali Innocent Mberwa (kulia) na Gosbert Mugisha wakiwa sawa mfumo wa umwagiliaji katika moja ya mashamba  zao la matikiti maji ya Kampuni yao ya  Tin Wax eneo la Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam juzi. Kampuni hiyo ilizawadiwa mfumo huo baada ya kushinda promosheni  ya Safari Lager Wezeshwa 2012,
Baadhi ya vitunguu vinavyozalishwa katika shamba hilo.
 
 

KIKUNDI CHA WATU WACHACHE CHATAKIWA KUACHA KUWAYUMBISHA WANANCHI MRADI WA KDA

picha+kigamboni
Ramani ya mfao jinsi utakavyokuwa mradi wa ujenzi wa mji wa Kigamboni

SAKATA la Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA), limeingia kwenye sura mpya, baada ya Diwani wa Kata ya Kibada (CUF), Juma Nkumbi, kukitaka kikundi cha watu wachache kuacha kuwayumbisha wananchi kuhusu mradi huo.
 
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kikundi hicho kuibuka na kudai kuwa wakazi wa Kigamboni kupitia madiwani wao na wabunge wa Manispaa hiyo ya Temeke jijini Dar es Salaam kuwa hawakushirikishwa  katika mchakato wa ujenzi wa mji huo.
 
Nkumbi alisema wakazi wa kata hiyo, baada ya kukutana hivi karibuni na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na kuwafafanulia kuhusu malipo ya fidia yatakavyokuwa, walielewa ambapo walikubali kuondoka katika maeneo hayo, bali hawataki ubabaishaji katika malipo hayo.
 
Alisema wananchi hao walielezwa jinsi watakavyofaidika na mradi huo ambako kila hekari moja ikiwa ni ardhi tupu italipiwa fidia y sh milioni 147, huku mimemea na nyumba zikiwa na viwango vyake.
 
Kwa mujibu wa diwani huyo, amekitaka kikundi hicho kuacha kuwasemea watu bali iwaache wananchi wajiamulie wenyewe kile wanachokitaka kuhusu KDA.
 
“Tuacheni kuwapotosha wananchi pia serikali ilichukulie suala hili kwa umakini na utekelezaji wake uwe wa haraka ili kurudisha imani ambayo ilitoweka kutokana na ucheleweshwaji na maneno mengi bila utekelezaji wenye tija”alisema Nkumbi.
 
Alisema kikundi hicho hakina ridhaa ya wananchi kwa kuwa hawajulikani wamechaguliwa na nani katika kusimamia madai hayo.
 
Nkumbi alisema madiwani wote wa walikuwa na taarifa kuhusu mpango huo tangu awali sasa siyo kweli kama kulikuwa hakuna taarifa zilikuwepo ingawa waziri hakukutana nao moja kwa moja.
 
Akizunumzia kuhusu mji huo kuwa na mamlaka yake, alisema hiyo ni sawa kutokana na ukweli kwamba kutasaidia katika ujenzi, ambako kama ikitegemewa Hazina, mradi huo unaweza kukwama kutokana sababu za urasimu wa upatikanaji wa fedha.
 
 

KUHUSU HABARI YA WAACHADEMA WALIOTIMULIWA......MDAU ANASEMA

"WALIOMKATAA FREEMAN MBOWE MBEYA WATIMULIWA UANACHAMA":

NDUGU MBOWE HII NCHI IKIWAKA MOTO WEWE NI KUNGURU UTARUKA AU UTAPAA KUELEKEA MAREKANI SISI WENGINE NI MBUNI TUTAJITAHIDI KUKIMBIA ILA MOTO WA MBUGA UTATUANGAMIZA WOTE.

KAULI YA KAMA NOMA NA IWE NOMA NI KAULI AMBAYO ANGEZUNGUMZA SHETANI WALA SI MTU ANAYEJINASIBU KUWA MMEANZA NA MUNGU NA KUMALIZA NA MUNGU.

WAMEKUFA WATU 08 WALIOJITOA MUHANGA ILI KUTEKELEZA KAULI YAKO GESI ISIENDE DAR KUNA MAJERUHI 10 HIVI NI NANI ANAHUDUMIA FAMILIA ZA MAREHEMU, NANI ATAHUDUMIA MAJERUHI MALI ZILIZOHARIBIWA ZA SERIKALI NA WATU BINAFSI NANI ATAZILIPA UNAJUA WEWE NI WA KUSHTAKIWA THE HAGUE TENA MARA MOJA?
 
 
 
 
 
 
Kwa Mwanaume mwenzangu ,usije ukabugi ukampenda mwanamke wa duizaini hii mwanamke ambaye hana muda na wewe na usipomtafuta siku nzima wala hata hashtuki,mwanamke anayejifanya sister duuu hata akili yakukuambia ununue kijiko hana,mwanamke ambaye anaogopa kutambulishwa kwa marafiki au ndugu,mwanamke ambaye anajijali akiwa na shida umsaidie uwe naye karibu akimaliza hana tyme na wewe kabisa,
mwanamke ambaye anapenda pesa kuliko anavyokupenda wewe,

mwanamke anayewaza kununua Kiatu cha Mchechemeo,kununua vipedo tu anapenda kwenda club hawaz kuhusu future ya badaye...mapenzi hayalazimishwi hata uwe na pesa kama Bill Gates huwez kununua Moyo wa mwanamke ili akupende atakuchuna tu alafu ukishaishiwa uhonge Iphone 5 anakukimbia bora uwe na mwanamke wa kawaida ambaye anajali na mwenye heshima kuliko kuwa na mwanamke mzuri alafu anatabia mbovu na hana malengo ya maisha...MANENO YANGU SIYO SHERIA
 
 
michezo

REAL MADRID SARE NA BARCA 1-1

Real Madrid and Barcelona have it all to play for in the second leg of their Copa del Rey semi-final after an entertaining stalemate at the Bernabeu tonight.

Both sides had plenty of chances during an enthralling first half but the opener did not arrive until five minutes into the second period when Cesc Fabregas latched onto Lionel Messi's through ball to fire past Diego Lopez.
Madrid got the equaliser their performance merited nine minutes from time when the game's outstanding performer, Raphael Varane, rose to head home Mesut Ozil's cross.
Level pegging: Raphael Varane (left) celebrates after scoring the equaliser
Level pegging: Raphael Varane (left) celebrates after scoring the equaliser
The big news before the match was the decision of Madrid coach Jose Mourinho to hand a debut to goalkeeper Lopez after he rejoined the club from Sevilla last week as cover for the injured Iker Casillas.
But it was Barca's second-choice goalkeeper, Jose Manuel Pinto, who was first into the action, clawing away Cristiano Ronaldo's dipping free-kick from under his crossbar.
Barca began to take control after that early scare and they could have gone ahead on 13 minutes when a beautiful scoop pass from Andres Iniesta set Jordi Alba free but the full-back skewed his volley well off target.
Opener: Cesc Fabregas pulls the trigger to put Barcelona in front against Real Madrid
Opener: Cesc Fabregas pulls the trigger to put Barcelona in front against Real Madrid
Ronaldo was then inches away from connecting with a Karim Benzema cross, before Xavi struck the crossbar with a free-kick.
The Barcelona midfielder missed another chance to open the scoring on 25 minutes after a terrible backpass from Ricardo Carvalho allowed Fabregas to intercept. The former Arsenal's man teed up Xavi to take aim with the goal gaping only for the impressive Varane to get back and clear off the line.
The hosts started to find more opportunities on the counter-attack as the half wore on and Benzema came within inches of scoring with a volley after being played in by Jose Maria Callejon.
Pure delight: Fabregas celebrates opening the scoring for Barcelona
Pure delight: Fabregas celebrates opening the scoring for Barcelona
Barcelona's Cesc Fabregas (L) celebrates scoring
Dani Alves then made a heroic last-ditch tackle to prevent Benzema and the Frenchman was first to threaten after the break as he cut inside and bent a shot just over, but it was Barcelona who found the net moments later.
A poor clearance from Callejon was seized on by Messi, who laid on the opening for Fabregas to apply a cool finish beyond Lopez.
Varane produced another wonderful challenge to deny Fabregas a second as he bore down on goal, and Madrid should have been level four minutes later as Michael Essien whipped a bouncing cross to the back post where Ronaldo headed just wide.
The Portuguese star was in space at the far post but somehow contrived to miss the target with the goal gaping.

How did he miss? Cristiano Ronaldo should have levelled the score but fluffed his lines
How did he miss? Cristiano Ronaldo should have levelled the score but fluffed his lines
How did he miss? Cristiano Ronaldo should have levelled the score but fluffed his lines
Gerard Pique produced a wonderful challenge to thwart Ronaldo as he tried to connect with Ozil's low cross before Barca had two great chances to add to the scoring as Fabregas shot over from Alves' cutback and Pedro's chip drifted wide.
Barca's failure to kill the game off came back to bite them late on when Ozil swung in a cross from the right and Varane powered a header low into the bottom corner.
The visitors had one final chance to take a lead back to the Nou Camp on February 27 but Lopez stood up well to turn away Alba's effort.
Bullet: Varane heads home the equaliser to ensure the spoils are shared in the first leg
Bullet: Varane heads home the equaliser to ensure the spoils are shared in the first leg
Bullet: Varane heads home the equaliser to ensure the spoils are shared in the first leg 

http://www.youtube.com/watch?v=X-oUPtlRZGY&feature=player_embedded


No comments: