Mchungaji
wa kanisa linalojulikana kwa jina la Calnel Centre Mchungaji Elia Ambakisye
Jongo alijikuta katika mzozo mkali na aliyedai kuwa ni mke wake baada ya
kumtuhumu kuwa ni mchawi.
|
Sabina Lameck mke wa mchungaji anaedaiwa kuwachwa sababu ya uchawi |
Katikati mama mzazi wa mchungaji Elia Jongo wakiwa katika kikao hicho |
Baadhi ya wazee wa kanisa wakiwa makini kusikiliza kisa hicho |
Huyu ndiye muumini wa kanisa hilo anayedaiwa kutaka kuolewa na mchungaji Elia pia muumini huyu ni mzee wa kanisa hilo |
Mchungaji elia na dada yake wakiwa makini kumsikiliza mchawi wake |
Askofu wa kanisha hilo laiyejulikana kwa jina moja la Pasta Lugito |
Hili ndilo kanisa la Calnel Centre mbeya lipo katibu na kiwanja cha ndege mwanjelwa Mchungaji wa kanisa linalojulikana kwa jina la Calnel Centre Mchungaji Elia Ambakisye Jongo alijikuta katika mzozo mkali na aliyedai kuwa ni mke wake baada ya kumtuhumu kuwa ni mchawi.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea juzi katika kanisa hilo lililopo Airport Jijijini
Mbeya baada ya Mchungaji huyo kupokea ujumbe mfupi katika simu yake ya mkononi
kutoka kwa Mwanamke anayedai alikutwa mke wake ambaye waliachana miaka mine
iliyopita.
Mchungaji
huyo akiwa mbele ya wazee wa kanisa, Familia yake, waumini pamoja na wanahabari
alisema sababu ya kuwakusanya watu hao kumetokana na mwanamke huyo
aliyejulikana kwa jina la Sabina Lameck akitaka kutubu kwa mabaya aliyomtendea
mumewe.
Hata
hivyo baada ya mwanamke huyo kupewa nafasi ya kuanza kujieleza alianza
kumtuhumu muumini wa kanisa hilo kuwa anauhusiano na mchungaji ambaye ni mumewe
wa ndoa ambapo pia alidai kuwa mwanamke huyo alichukua nguo za mchngaji na
mkewe kwa madai ya kupeleka kwa mganga ili kusudi awasaidie warudiane.
“
Ninachotaka ni huyu mwanamke kurudisha nguo zangu kwa sababu alizichukua ili
apeleke kwa mganga kwa nia ya kunisaidia mimi nirudiane na mchungaji lakini
badala yake naona dawa hizo zimemsaidia mwenyewe hadi anataka kuolewa yeye,”
alisema Mwanamke huyo.
Kwa
upande wake mchungaji Jongo alimtuhumu mwanamke huyo kuwa ni mshirikina na
kwamba sababu ya kutengana naye ni kutokana na mwanamke huyo kuzaa na mwanaume
mwingine nje ya ndoa hali aliyosema alidhalilishwa kama mchungaji.
“
Huyu mwanamke ni mshirikina maana tangu tutengane alianza kunivurugia huduma
ambapo waumini walianza kupungua kanisani nayeye kwenda kwa waganga wa kienyeji
kwa lengo la kunivurugia huduma” alisema mchungaji huyo na kuongeza.
“
amekuja leo hapa baada ya kusikia mimi nataka kuoa muumini wangu ambapo yeye
ameanza kumzushia kuwa ni mshirikiana kitu ambacho si cha kweli lakini kama
kuna ukweli wowote utajulikana kwa sababu Mungu yupo,” alisisitiza Mchungaji
huyo.
Hata
hivyo usuluhishi huo haukufika mwafaka baada ya kuibuka kwa malumbano hali
iliyomlazimu msimamizi wa usuluhisho huo Askofu wa kanisha hilo laiyejulikana
kwa jina moja la Pasta Lugito kuahilsha mazungumzo hayo huku wakimpiga marufuku
mwanamke huyo kukanyaga katika makazi ya mchungaji.
Picha na Mbeya yetu
Hili ni Bunge la hoja au vioja?
Tunaelekea
kuzoea bunge la vioja badala ya hoja.mfano,ni kuwa kuna baadhi ya
wabunge wanapeleka hoja kuwa bunge lisionyeshwe live.hakya ya nani!
.Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa
taarifa kwa wabunge (kawapo pichani) jana mjini Dodoma kuhusu kuundwa
kwa kamati itakayokwenda mkoani Mtwara kusikiliza maoni ya wananchi wa
mkoa huo kuhusu tatizo la suala la gesi
Baadhi
ya wabunge wakifuatilia masuali na majibu katika kikao cha mkutano wa
kumi mjini Dodoma leo,
Baadhi ya wabunge wakisalimiana baada ya kuahirishwa kwa kikao leo mjini Dodoma,
Mbunge
wa( Monduli )Edward Lowassa ((kulia) akimsikilza Mbunge wa Bariadi
Mashariki John Cheyo Kushoto) katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo,
(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Naibu
Waziri Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia , January Makamba akijibu
hoja za wabunge zinazohusu wizara yake Bungeni leo- Dodoma, (Picha na
Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Je, Wana Mtwara wamekubaliana na waziri mkuu wa Tanzania ndugu pinda?
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wafanyabiashara wa Mtwara kuhusu
mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara, Januari 28, 2013.
Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia.(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya
Wafanya biashara wa Mtwara wakinyosha mikono kuomba nafasi ya kuchangia
katika mazungumzo kati yao na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu mgogoro
wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara, Januari 28, 2013.(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Serikali Yataja Manufaa kwa Wana-mtwara Gesi Ikipelekwa Dar
Na Mwandishi wa Thehabari.com
SERIKALI imetaja manufaa na faida
ambazo wanatarajia kuzipata wananchi wa Mtwara pamoja na Lindi endapo
gesi itasafirishwa kwenda Jijini Dar es Salaam.
Imesema Mkoa wa Mtwara ndipo
utakapo jengwa mtambo mkubwa wa kusafishia gesi hiyo kabla ya
kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa matumizi ya uzalishaji
umeme na matumizi ya moja kwa moja viwandani.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alipokuwa
akizungumza katika Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha
Radio One jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri huyo ameweka wazi
kuwa mkoani Mtwara licha ya Serikali kupanga kujenga viwanda vingine
kadhaa, inajenga mtambo wa megawati 250 ambao utakuwa ukizalisha umeme
na mwingine kujengwa mkoani Lindi eneo la Somanga Funga utakao kuwa
ukizalisha megawati 520.
Akifafanua zaidi Simbachawene
alisema eneo la Mikindani katika Kijiji cha Msijute mkoani Mtwara
kinatarajiwa kujengwa kiwanda kikubwa cha saruji Afrika Mashariki na
Kati chenye uwezo wa kutoaji ajira kwa watu 6000 jambo ambalo ni manufaa
ya Wanamtwara.
Alisema pia tayari kuna
wawekezaji wa viwanda vya mbolea wamejitokeza kujenga viwanda mkoani
Mtwara na Serikali itaviacha vinu vya kuchimba na kusindika gesi eneo
hilo jambo ambalo bado ni manufaa makubwa kwa wananchi.
KATIBU MKUU WA UVCCM MARTIN SHIGELA ASHIRIKI SHUGHULI ZA KILIMO NA KUKAGUA MIRADI KIGOMA VIJIJINI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM, UVCCM Bw. Martin Shigela akishiriki
katika kupalilia shamba la Karanga katika kijiji cha Nkungwe Tarafa ya
Mabembe Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembelea na kujionea
shughuli mbalimbali na kukagua miradi inayotekelezwa na wananchi kwa
pamoja na Serikali jana.
Sekretarieti ya CCM ikiongozwa na
katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana iko mkoani Kigoma kwa ajili
ya kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na sherehe za
miaka 36 ya chama hicho zinazotarajiwa kufanyika Februari 3 kwenye
uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo, kulia ni Bi Fatma mmiliki wa na
kushoto ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akisalimiana na
wananchi wa kijiji cha Nkungwe wakati alipotembelea katika kijiji hicho
jana
Katibu
Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akikabidhiwa zawadi ya
mihogo na Bi Asha Ibrahim mara baada ya kutembelea shamba lake jana,
.Kijiji hicho cha Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa kilimo cha muhogo bra
katika mkoa wa Kigoma.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akiongozana na
Bw.Khamis Bitese Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini mbele yake
wakati akikagua shughuli za ukulima wa kisasa katika kijiji cha Nkungwe
Kigoma Vijijini, Kijiji hicho cha Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa
kilimo cha muhogo bra katika mkoa wa Kigoma.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimsaidia Bi. Asha
Ibrahim kufukia mbegu ya Viazi, huku viongozi mbalimbali wa CCM wilaya
ya Kigoma Vijijini wakishuhudia tukio hilo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimkabidhi
zawadi ya shilingi elfu 10,000 mtoto Rehema huku mama yake akimsaidia
wakati alipotembelea na kujionea shughuli za kilimo katika kijiji cha
Nkungwe jana
Viongozi mbalimbali wakikagua kivuko cha Mto Ruchi katika kijiji cha Nkungwe jana.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akivuka katika kivuko
cha Mto Ruchi kwa kutumia Baiskeli huku akiwa ameonozana na viongozi
mbalimbali wa CCM wilaya ya Kigoma Vijijini pamoja na watendajiwa kijiji
hicho jana inaelezwa kwamba watu wengi walipotea maisha kwa kuliwa na
Mamba kabla ya kujengwa kivuko hiki.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Martin Shigela akimenya muhogo ili
kutafuna kidogo mara baada ya kununua kwa mmoja wa wakulima Kijiji cha
Nkungwe ndicho kinachoongoza kwa kilimo cha Muhogo mkoani Kigoma
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akiagiza jambo kwa
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kigoma Bw Peter Msanjila wakati
alipotembelea kata ya Mwanduga jana kulia ni Khamis Bitese Mwenyekiti wa
CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akizungumza na
wanafunzi wa shule ya msingi ya Kabanda katika kijiji cha Chabwimba jana
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akisalimiana na
wananchi mara baada ya kuwasili katika Kata ya Mabembe.
Wananchi wa kijiji cha Mabembe wakimsikiliza mwenyekiti wa UVCCM katika Kata ya Mabembe kwenye mkutano wa ndani
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM Martin Shigela akicheza na msanii
chipukizi wa kijiji cha Mabembe ambaye ni mlemavu wakati alipotembelea
na katika Kata ya Mabembe
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika kata ya Mwanduga Kigoma vijijini jana
Mjumbe
wa NEC CCM kupitia Wilaya ya Uvinza Asha Baraka akiwa katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika Kata ya Mwanduga Kigoma jana kulia ni Khamis
Bitese Mwenyekiti wa CCM Kigoma Vijijini na katikati ni Peter Msanjila
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kigoma.
Martin
Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akihutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika jana kwenye kata ya Mwanduga Wilaya ya Kigoma vijijini
Matin
Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akipata maeleo kutoka kwa Khamis
Bitese Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembele
na kukagua ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi ya Kabanda.
Martin
Shigela Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa akipata maeleo kutoka kwa Khamis
Bitese Mwenyekitiwa CCM Wilaya ya Kigoma Vijijini wakati alipotembele
na kukagua ujenzi wa numba za walimu katika shule ya msingi ya Kabanda.
Huu ndiyo mto Ruchi unaotenganisha kijiji cha Nkungwe na mashamba ya
wanakijiji hao uliosababisha mauaji ya wananchi kadhaa kutoka na kuliwa
na Mamba kabla ya kujengwa kwa kivuko hicho.
|
No comments:
Post a Comment