Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akifungua mkutano huo
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanchama wa chama hicho
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Clemence
Tara baada ya kujiunga na chama hicho.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepitisha mpango mkakati wake wa kuelekea kushika dola mwaka 2015 kwa kumega madaraka ya makao makuu katika kanda kumi. Maazimio hayo yalipitishwa na Kamati Kuu (CC) juzi kwa agenda moja kubwa ambayo ni kupitisha mpango mkakati wa mwaka 2013 ili kushinda chaguzi zote kuanzia serikali za vitongoji, vijiji na mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015.
Akizungumza na wajumbe wa kikao cha dharura cha Baraza Kuu jana, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema kuwa mpango mkakati huo umelenga kufanya mabadiliko ya uongozi kuanzia ngazi ya taifa kwenda katika majimbo na kukipanga upya chama hicho kwa mustakabali wa taifa. “Mtakumbuka kwamba wakati tunakianzisha chama chetu, tulizungumzia sera ya majimbo na kuainisha kazi zake…sasa tumeanza kupanga kazi zenyewe kwa kugawa majukumu katika kanda kumi. “Tunataka tuishi vile tunavyosema kwa kuwa katika miaka mingi ya kuwa chini ya uongozi wa serikali ya CCM, wananchi wamekuwa wakiamriwa mambo yao na kundi dogo la watu wanaojikusanya sehemu moja ya nchi, hilo kwetu si mfano bora wa uongozi,” alisema.
Mbowe aliongeza kuwa katika miaka 20 ya kuhimili misukosuko ya kisiasa chama hicho kimejifunza mengi na sasa kiko tayari kushika dola ndio maana wameanza kugawa majukumu kwa wananchi kupitia uongozi wa kikanda. Alisema kuwa wamejiandaa kwa mashambulizi ya aina zote na sasa jukumu kubwa la kila kanda litakuwa ni kuhakikisha kila mwananchi anaiunga mkono CHADEMA katika eneo atakalokuwa.
Mwenyekiti huyo alitaja kanda hizo na mikoa husika kuwa ni
- Kanda ya Ziwa Magaharibi (Mwanza, Geita, Kagera),
- Ziwa Mashariki (Mara, Simiyu, Shinyanga),
- Ziwa Magharibi (Kigoma, Tabora, Katavi)
- Kati (Singida, Dodoma, Morogoro).
- Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Ruvuma, Iringa),
- Kusini (Lindi na Mtwara),
- Mashariki (Pwani, Dar es Salaam na Tanga),
- Kaskazini (Kilimanjaro, Manyara, Arusha),
- Pemba na Kanda ya Unguja.
Mbowe alisema katika kuhakikisha vikosi hivyo vinafanya kazi zake vizuri, kila kanda itajengewa ofisi, kununuliwa magari, pikipiki na vifaa vyote vya ofisini na za mikutano. “Lengo la mkakati huo pia ni kuhakikisha CHADEMA inasimama katika chaguzi zote bila kupingwa…tunataka CCM ndiyo ipingwe katika chaguzi na hili tutalifanikisha,” aliongeza.
Katika suala zima la Muungano, Mbowe alisema uwepo wa serikali tatu hauepukiki kwa kuwa tayari Tanzania Visiwani wameshakuwa na serikali yao hivyo ni jukumu la Watanzania Bara kupata serikali ya Tanganyika na kisha kuwepo na serikali ndogo ya Muungano. Alisema serikali tatu inawezekana ikiwa viongozi wataacha unafiki wa kusema muungano utavunjika huku tayari wakitoa uhuru wa Zanzibar kuwa na Rais, bendera na wimbo wao ya taifa. Tunawaunga mkono wenzetu Wazanzibar katika kupigania uhuru kamili na kwa sasa sisi ndio tunaoonekana wa ajabu kushindwa kuuliza serikali ya Tanganyika,” alisema.
Mbowe pia aligusia tume huru ya uchaguzi akisema serikali ihakikishe Watanzania wanapata tume hiyo kwa kuwa tayari hata viongozi wa chombo hicho wameshatoa maoni na kutaka wapewe uhuru wa kufanya kazi.
Alisema serikali kama inafikiri kuwa CHADEMA itaingia katika uchaguzi wa 2015 ikiwa chini ya tume iliyopo sasa watakuwa wanajidanganya na badala yake watalazimisha upatikanaji wa tume hiyo.
SHITAMBALA KUONGOZA MAANDAMANO WANANCHI 5000 KUMVAA KANDORO KUPINGA KUHAMISHWA
MJUMBE
wa Halmashauri kuu CCM Taifa Bw.Sambwee Sitambala
,asema yatakuwa
ya amani bila Vurugu
,asema sera
ya CCM ni kutetea wananchi
MJUMBE wa Halmashauri
kuu CCM Taifa Bw.Sambwee Sitambala anatarajiwa kuongoza
maandamano ya amani ya wananchi zaidi ya 5000 wa
mtaa wa Gombe kusini kwenda kwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya
kwa ajili ya kupinga amri ya kutaka kuwahamisha kwenye nyumba
zao na eneo hilo kupewa watu wengine.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kwisha kwa mkutano wa wananchi hao diwani
wa Kata ya Itezi jijini Mbeya Bw.Frank Mayemba ambaye
pia ni mjumbe wa Mkutano mkuu Taifa CCM alisema kuwa
katika maandamano hayo watashirikiana na
Bw.Shitambala kuongoza hadi kufika kwa mkuu wa Mkoa.
Alisema kuwa wananchi
hao ambao zaidi ya asilimia 90 ni wanachama wa CCM walifikia hatua
hiyo baada ya kuona hawasikilizwi katika kilio chao ambacho
wamekuwa wakitoa kwa Jiji la Mbeya kuwataka kutowagusa kwa kuwa walipewa maeneo
hao kihalali baada ya kubadilishwa matumizi yake ya awali ambayo
yalikuwa viwanda.
Bw.Mayemba alisema
kuwa kutokana na hali hiyo wamedhamiria kudai haki yao kwa mkuu wa
Mkoa ambaye ndiye msimamizi wa Halmashauri zote Mkoa wa Mbeya
ambapo kutokana na hekima yake walisema kuwa wana imani kuwa
atawasaidia kuwasikiliza ombi lao na kusitisha zoezi hilo ambalo
ni athari kubwa kwa wananchi hao.
Alisema kuwa
wananchi hao baada ya kupewa viwanja hivyo wamekaa katika eneo hilo kwa
zaidi ya miaka 20 na hivyo kisheria kuwa wamiliki haklali wa
maeneo haio wasio takiwa kubughudhiwa na hivyo kushangaa wakati wote
wanapoambiwa kuwa watahamishwa na maeneo yao kupewa watu wengine.
"sisi
tunasema kama viongozi wa chama hakika
hatutakubali suala hili kwa kuwa ni wamiliki halali wa eneo
hili na hivyo kama wanataka kugawa basi tuweke mkataba ambao
watatugawia sisi na wala si wengine kama wanavyotaka kufanya
sasa hawa wataalam."alisema.
Naye
Bw.Shitambala ambaye pia ni Kaptain wa jeshi mstaafu na mwanasheria
maarufu alisema kuwa ataongoza maandamano hayo ya amani hadi kwa
mkuu wa Mkoa na hakuna vurugu itakayotokea kwa kuwa CCM
ni chama kinachohamasisha amani na utulivu na hivyo wao
wataonesha mfano.
Kada huyo wa CCM ambaye
awali alikuwa mwenyekiti wa CHADEMA kabla ya kumamia chama
hicho alisema kuwa wataomba vibali polisi kwa ajili ya kulinda maandamano
hayo na kamwe hawatachoma barabara kama wanavyofanya wengine
ambnapo watapata nafasi ya kumweleza mkuu wa Mkoa hoja
zao zinazopinga kuondolewa katika eneo hilo .
Alisema yeye kama mkazi
aliyejenga eneo hilo ni dhambi kubwa kuona wananchi wenzake na yeye
akiwemo wakinyanyaswa na hivyo kupelekea hasira kali kwa
chama hali ambayo alisema kuwa katika mkutano mkuu wa chama
na vikao mbali mbali wamekubaliana kupinga hali hiyo na
kuwapa haki yao wanachama .
Kwahisani ya Charles Mwakipesile Mbeya
lugarawa kujengewa chuo cha vetaMh Deo akimuonyesha eneo la ujenzi wa Chuo Mkurugenzi mkuu veta Ndg. Zebadieli Mushi lenye ukubwa wa hekali sabini. Mh Deo akimkabidhi zawadi ya kuku Mkurugenzi mkuu wa Vyuo vya veta Tanzania Mkurugenzi wa Vyuovya veta nchini akiongea na wananchi wakijiji cha Ludewa juu ya ujenzi wa chuo cha veta katika kijiji chao kwaniaba ya wana Ludewa. Mh Deo Filikunjombe akiongea na wananchi wa kijiji cha shaulimoyo walipo ijiwa na mkurugenzi wa vyuo vya veta Tanzania kuwathibitishia ujenzi wa chuo cha veta wilayani Ludewa.Ndg.Zebadieli Moshi SHAHIDI AIOMBA MAHAKAMA KUMWONDOA NCHINI MWEKEZAJI KAPUNGA
Na
Venance Matinya
KESI
inayowakabili Wawekezaji wa shamba la Kapunga Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa
imechukua sura mpya baada ya mashahidi kujitokeza na kuiomba mahakama iwaamuru
wawekezaji hao kuondoka.
Akitoa
ushahidi wake mbele ya hakimu Michael Mtaite wa mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa
wa Mbeya, Shahidi Daison Tonyela(50) Mkazi wa Kijiji cha Kapunga akiongozwa na
Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa alidai mahakamani hapo kuwa tangu
Mwkezaji apewe eneo hilo hana uhusiano mzuri na wanakijiji.
Alisema
tangu mwekezaji huyo apewe eneo hilo amekuwa akiwanyanyasa wakazi wa Kapunga
kwa kuwafungia njia na kubomoa matofali na madaraja kitu kinachoonesha
Mwekezaji kutotoa ushirikiano na wanakijiji.
Alidai
Mahakamani hapo kuwa kutokana na Mwekezaji huyo kumwaga dawa inayodaiwa kuwa
sumu katika mashamba hayo tayari
wameingia hasara kubwa kutokana na kukosa mazao hali iliyopelekea kushindwa
kuishi kutokana na njaa.
Aliongeza
kuwa yye binafsi amepata hasara iliyopelekea kushindwa kuwapeleka shule watoto
wake kutokana na kukosa fedha ambazo angezipata baada kuuza mpunga ambao
angekuwa amevuna kabla ya kuharibiwa na mwekezaji huyo.
Shahidi
huyo anayedai kuharibiwa kwa shamba lake lenye ukubwa wa ekari 4 ambalo
angeweza kuvuna zaidi ya gunia 20 kwa kila Ekari huku gunia moja angeuza kwa Shilingi Laki
mbili.
Aidha
aliiomba mahakama hiyo kumwamuru mwekezaji huyo kuwalipa fidia wananchi
kutokana na hasara waliyoipata ikiwa ni pamoja na kufukuzwa katika eneo hilo na
kuwaachia wananchi.
Hata
hivyo kesi hiyo iliahirishwa hadi Machi
5, Mwaka huu ambapo mashahidi wengine wataendelea kutoa ushahidi wao hali
iliyokubaliwa na upande wa utetezi chini ya wakili Vicent Mtavangu.
Awali
Wawekezaji hao watatu raia wa Afrika kusini walifikishwa mahakamani
kwa kosa la kumwaga sumu kwenye mashamba ya mpunga ya
wakulima 153 wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
Mashtaka
ya awali yalisomwa mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya
mjini Girbeti Ndeuluo, na mwendesha mashtaka mwanasheria wa serikali, Achiles
Murisa ambaye alidai kosa hilo lilitokea
January 12/2012.
Achiles
aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni WalderVeemad, Segeer Backer na Andress Dafee
ambapo wote ni wafanyakazi wa kampuni ya Kapunga rice.
Alisema,
watuhumiwa wamefanya kosa hilo wakati wakipiga dawa katika mashamba yao kwa
kutumia chombo cha usafiri wa anga (ndege).
Alisema,
dawa hiyo inasemekana ilipitiliza hadi kwenye mashamba jirani na kufanya
uharibifu kwenye mazao yaliyokuwa shambani.
KATIKA vijiji vya Totowe na Mbuyuni hakuna serikali. Ni utawala binafsi. Huku ni katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
Kwani Sera ya Afya ya mwaka 2007 inasema wajawazito kote nchini watapata huduma bure kabla na wakati wa kujifungua. Lakini hayo hayaonekani katika vijiji hivyo. Pamoja na kuwepo zahanati katika kata ya Totowe, wanawake kwa mamia wanasukumana wakitafuta kupewa huduma ya uzazi kwa wakunga wa jadi ambao serikali haijawatambua. Hilda Said Kawinga (80), mkazi wa kijiji cha Malangali mpoa kata ya Totowe ni mkunga kwa miaka 30. Anaishi katika banda la vyumba viwili ambavyo anaita sebule na chumba cha kulala. Kwa umri wake Hilda hatetemi mikono. Kwa rekodi za sasa, ameweza kusaidia wajawazito 70 kujifungua katika kipindi cha miezi 10 (Januari hadi Oktoba mwaka 2012). Kijiji cha Totowe kipo umbali upatao kilometa zaidi ya 100 kutoka Chunya mjini. Hapa ndipo wajawazito wanaita kwa jina la kirafiki, “nyumbani salama,” kutokana na kujifungua salama na kuondoka kwa kicheko na watoto wao mikononi. Hapa ni nyumbani kwa Hilda. Pale kuna mafiga Ndilo jiko. Kuna kuni. Hapa kuna vyombo vya kupikia. Alipokaa mwandishi kuna mkeka na ndiyo sehemu inayotumika wakati wa kusaidia wajawazito kujifungua. Wajawazito wakija, basi hakuna mgeni. Bibi Hilda hana mkasi. Hana vyombo vya kisasa kama vya zahanati, kituo cha afya au hospitali kwa huduma za uzazi. Hana kitanda. Hana godoro wala mipira ambako wajawazito hujilaza wakati wa kujifungua. Lakini hapa ndipo wanawake wanamiminika kwa huduma ya uzazi na wanaondoka na watoto wao salama. Akiongea kwa sauti nyembamba anasema, “Ninamworodhesha kila anayejifungulia hapa katika daftari langu. Nafanya hivi ili kuisaidia serikali kupata takwimu endapo watazihitaji; ingawa tangu nimeanza shughuli hakuna kiongozi wa serikali aliyewahi kuja kuangalia wala kuuliza kuwa ninafanyaje kazi.” Hilda anajigamba kwamba alipata ujuzi kutoka kwa mama na kuongeza, “…kwa watoto wangu sikuwahi kujifungulia hospitali; ilikuwa kazi ya mama. Hapo ndipo nilijifunzia kazi tena bila vifaa vya kisasa. Sharti kuu ni kuwa msafi tu.” Hivi sasa anasema anapokea wajawazito 10 kwa mwezi na kila mmoja anaondoka kwa kicheko. Tangu aanze kazi hii, hakuna mtoto wala mama aliyepoteza maisha akiwa mbele yake. Bibi Hilda ni kama mkunga mwingine Agripina Frederick Sikanyika wa kijiji cha Mbuyuni wilaya ya Chunya. Tofauti ni kwamba Agripina ametenga nyumba rasmi kwa wajawazito kulala na kujifungulia. Agripina, mwenye umri wa miaka 37 anafahamika sana kwa jina la “Mama Namwinji.” Anasema imemlazimu kuwaachia nyumba wajawazito wanaokwenda kwake kwa ajili ya kusubiri kujifungua kutokana na idadi yao kuongezeka kukicha. Kulia ni Mkunga Agripina Sikanyika akimkabidhi mtoto mmoja wa wajawazito waliotoka kujifungua nyumbani kwake
Katika kipindi cha miezi 10, Januari hadi 9 Oktoba 2012, Mama Namwinji
amehudumia wajawazito 212. Alianza huduma kwa wajawazito mwaka 2000.
PICHA: Mwonekano wa Nyumba inayotumika kujifungulia wajawazito kwa Mkunga Agripina Mama Namwinji. Kitu kimoja kimemkwaza Mama Namwinji. Watoto wawili kati ya 212 waliozaliwa mwaka jana walikuwa na ulemavu. Ilikuwa Septemba 15, 2012 wakati mwanamke mmoja alipojifungua mtoto mwenye sikio moja, mguu mmoja, mdomo na pua vikiwa vimeungana. Mtoto huyo alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa. Mkokoteni unaokokotwa na Punda hutumika pia kubebea baadhi ya wajawazito kwenda katika kituo cha afya cha Mbuyuni na kwa Mkunga wa jadi Mama Namwinji Siku iliyofuata, Septemba 16, 2012 alizaliwa mtoto aliyekuwa na kichwa kikubwa chenye umbile la kichwa cha ng'ombe lakini mwenye kiwiliwili cha binadamu. Mkunga amesema hawezi kutoa majina ya waliojifungua “watoto wa ajabu” kwa alichoeleza kuwa ni siri ya wazazi wao na aliyekuwepo. Mama Namwinji akionesha mkeka aina ya Msengele anaotandika wanapojifungulia wajawazito wanapofika kwake Changamoto anazokabiliana nazo Agripina hazina tofauti na zile za Bibi Hilda na wakunga wengi wa jadi nchini. Hana kitanda, hivyo huwalaza wajawazito kwenye mkeka wa matete (maarufu kama Msengele). “Hii ni hatari kwa sababu wanaweza kupata magonjwa hasa kipindi cha masika,” anasema Agripina. Kama Hilda, Agripina naye anaorodhesha wajawazito katika daftari maalum, ingawa yeye anachukua hatua zaidi kwa kuangalia kadi za kliniki na kuzijaza mara wanapojifungua. Anasema pamoja na kuwepo kwa kituo cha afya jirani cha Mbuyuni (Chang’ombe), lakini wajawazito wengi wanakimbilia kwake kwa madai kwamba wakienda hospitalini wanaweza kufanyiwa upasuaji. “Wapo ambao walikwenda hospitalini wakafanyiwa upasuaji, lakini walipofika hapa katika uzazi wao mwingine wameendelea kujifungua bila upasuaji,” anasema. Kama ilivyo kwa Bibi Hilda, Agripina naye anasema huwa hatozi kiwango chochote cha fedha kabla na baada ya mjazito kujifungua, ingawa wote wanakiri kwamba akinamama au ndugu zao “…huleta chochote walichojaliwa kama asante.” “Wanawake wengi Tanzania wanakufa kipindi cha ujauzito au baada ya kujifungua ndani ya siku 40. Hii ni hatari sana,” anasema Dk. Magoma akiwa anafundisha waandishi wa habari Tanzania wanaobobea katika habari za afya ya uzazi akiwemo mwandishi wa makala haya na kuongeza kuwa, kwa upande mwingine, watoto wanakufa ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya kuzaliwa huku akibainisha kwamba asilimia 57 ya wanawake wote wanaojifungua hawahudhurii kliniki. Mtafiti wa Masuala ya Afya nchini, Dk. Kahabi Ganka Isangula, anasema zaidi ya wanawake 300,000 wanafariki kila mwaka wakati wa kujifungua au wakati wa kipindi cha ujauzito kutokana na sababu mbalimbali huku 800 kati yao wakifa kwa “matatizo yanayoweza kuzuilika.” Kati ya vifo hivyo, asilimia 99 hutokea katika nchi zinazoendelea hasa vijijini kwa watu maskini ambapo wajawazito wengi hutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua. Anashauri wanawake wajifungulie katika vituo vya afya akieleza kuwa moja ya changamoto kwa huduma za wajawazito, “ni kutoa kondo la nyuma ambalo linahitaji utaalamu.” Hata hivyo, Dk. Isangula hapingi matumizi ya wakunga wa jadi katika kuhudumia wajawazito. Anasema, “…hakuna ubaya wowote kwa wanawake kujifungulia kwa wakunga wa jadi, tatizo linakuja katika upatikanaji wa vifaa vinavyomwezesha mkunga wa jadi kumhudumia mama mjamzito katika hali ya usalama.” Naye Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka hospitali ya mkoa wa Mbeya, Prisca Butuyuyu, anasema wanatambua kuwepo kwa wakunga wa jadi na kwamba watoto wote wanaozaliwa huko wanawahesabu kuwa wanazaliwa nyumbani kwa sababu hakuna mwongozo wa wizara unaowatambua wakunga wa jadi. Sera ya Afya ya mwaka 2007 inaagiza kwamba wajawazito wapewe huduma bure katika sehemu zote za huduma ya afya. Je, hawa wanaojifungulia kwa Hilda na Agripina wanapata huduma gani au huduma inayotajwa haiwahusu? Je, kama wajawazito hawapati huduma, wakunga wanasaidiwa vipi au wanawezeshwa vipi na serikali ili wafanye kazi yao kwa ustadi na weledi ambao tayari umedhihirishwa kwa kuhudumia mamia kwa mamia ya wajawazito waliojifungua salama? Majibu kwa maswali haya yako mikononi mwa serikali.
Mungu ibariki Tanzania
MBEYA
Serikali yasikia kilio cha watoto
Na, Gordon Kalulunga, Mbeya
SERIKALI imesikia kilio cha wanafunzi wa shule za Msingi
hasa darasa la kwanza na la pili katika shule za serikali kwa kuwapunguzia
masomo.
Wanafunzi hao wamerejeshewa mfumo unaowasaidia kujua kusoma
na kuandika ujulikanao kwa jina la KKK yaani kusoma kuandika na kuhesabu.
Uchunguzi uliofanywa na Mtandao wa www.kalulunga.blogspot.com ambao uliwahi
kulipoti kuhusu mlundikano wa masomo kwa wanafunzi hao hali iliyokuwa
inachangia wengi wao kuhitimu darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika.
Masomo yaliyokuwa yakifundishwa kwa wanafunzi wa madarasa
hao kutokana na mfumo wa kila waziri anayekuwepo madarakani kubadili mitaala
bila kushauliana na walimu ni pamoja na somo la Kiingereza, Kiswahili,
Hisababti, Stadi za kazi, Tehama, Haiba na michezo na Sayansi.
Baadhi ya walimu waliohojiwa wamethibitisha
kurejeshwa kwa mfumo huo wa KKK katika shule za Msingi tangu shule zilipofungua
Januari 14, mwaka huu.
Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa bado kuna mfumo mbaya wa
elimu hapa nchini ambapo wanafunzi wanafundishwa kwa Lugha ya Kiswahili lakini
wakati wa kuajiliwa wanasailiwa kwa Lugha ya Kiingereza.
KUNDI LA WANANCHI WAFANYA VURUGU NA UHARIBIFU MTAA WA ISENGO KATA YA IZIWA. MBEYA
ABDURAHMAN KINANA AONGOZA SEKRETARIETI YA YA CCM KUKAGUA MRADI WA UJENZI DARAJA LA MTO MALAGARASI MKOANI KIGOMA
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ndugu Abdurahman Kinana akimsikiliza Meneja
mradi wa ujenzi wa Daraja la mto Malagarasi Bw. Jung- Sik Yu kutoka
nchini Korea wakati akikagua ujenzi wa Daraja hilo Mkoani Kigoma jana
katika ziara ya Wajumbe Sekretarieti ya CCM wanaotembelea mkoa huo na
kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongea nao kusikiliza kero za wananchi.
Daraja la Malagalasi ambalo
linagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 78 za Tanzania lina
urefu wa mita 275 na linatarajiwa kukamilika Oktoba 16 mwaka huu ambapo
linatarajiwa kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete, Kushoto ni Nape Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na uenezi wa CCM.
Meneja
Mradi wa Ujenzi wa daraja la Malagarasi Bw. Jung Sik- Yu akimuonyesha
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana jinsi eneo hilo lilivyosumbua
wakati wa utekelezaji wa mradi huo kutokana na kuwa na majimaji wakati
mwingi.
Wananchi
wa Uvinza wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika mji
huo na kuhutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana.
Wananchi wa Tarafa ya nguruka wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana hayupo pichani wakati wa mkutano huo
Msanii Dokii akiimba katika mkutano huo uliofanyika tarafa ya Nguruka.
Katibu wa Halmashauri Kuu Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha- Rose
Migiro akicheza na mmoja wa wazee wa tarafa ya Nguruka wakati
Sekretarieti hiyo ilipopokelewa kijijini hapo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
akiongozana na Asha Baraka Mjumbe wa NEC CCM wilaya ya Uvinza mara baada
ya kuwasili katika tarafa ya Nguruka jana.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga ngoma
sambamba na wasanii wa kikundi cha ngoma cha Nguruka.
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman
Kinana akikagua kipande cha Barabara kinachounganisha madaraja hayo
wakati alipokagua ujenzi wa Daraja la Mto Malagarasi mkoani Kigoma jana,
aliyeongozana naye ni Meneja Mradi Bw. Jung-Sik Yu.
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman
Kinana akizungumza jambo na Bw. Kadudu Issa Tawfiq mkazi wa eneo hilo
ambaye alielezea faida za ujenzi wa daraja hilo katika maisha ya watu wa
Kigoma.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akiongoza wajumbe wa Sekretarieti ya CCM
wakati walipokagua ujenzi wa Daraja la mto Malagarasi jana.
Hiki ni moja ya vipande vya daraja la mto Malagarasi chenye urefu wa mita 200
|
No comments:
Post a Comment