Pombe hizo ambazo zipo kwenye makaratasi ya
plastiki, zimezagaa kila kona ya wilaya ya Kyela, Rungwe, Mbeya mjini, Mbeya
Vijijini, Mbarali, Mbozi na Momba huku zikiuzwa bei ya kati ya Sh.100-300 bei
gharama ambazo vijana wengi wanaimudu na wanapokunywa wengi huzidiwa na kuanza
kutokwa na jasho.
Hali hiyo imejidhihilisha baada ya Mwandishi
wa habari hizi kutembelea wilaya ya Kyela iliyopo mkoani Mbeya na kukuta vijana
wengi wakinywa pombe hizo ambazo wamekiri kuwa zinaathari kwa Afya zao.
Wakiongea kwa ombi la kutoandikwa majina yao,
vijana wa eneo la Kasumulu, Kyela Mjini na Ipinda walisema kuwa wengi
wanaotumia pombe hizo hugeuka vituko na wale wanaotumia vyombo vya moto hasa
pikipiki huishia kugonga watu na baadhi yao kupoteza maisha.
’’Pombe hizi ni nzuri kwa bei lakini zina
madhara makubwa kwasababu wengi tumewaona wakitumia pombe hizi huanza kutokwa
jasho jingi katika miili yao jambo ambalo linaonesha kuwa pombe hizi zinakausha
maji mwilini lakini vijana wanashindwa kuiacha kutokana na bei ni ndogo na
hazikatazwi na Serikali’’ alisema mmoja wa vijana waliohojiwa.
Sanjari na hilo walibainisha moja ya athari
iliyowahi kutokea kuwa ni kifo cha kijana mwenzao John Mwakapisye
kilichotokea Julai 20,2010 baada ya kijana huyo kunywa pombe hizo kisha
kuendesha pikipiki na baadaye kupinduka na kujisababishia kifo.
Waliongeza kuwa uwepo wa pombe hizo ambazo
zinatengenezwa na kiwanda cha Bwenda Group Limited kilichopo mjini Lilongwe
nchini Malawi kumetokana na kuadimika kwa pombe iliyojulikana kwa jina la
Kadansana kutoka huko huko nchini Malawi.
Wakielezea kwa kina uwepo wa uholela wa pombe
hizo ambazo wamekiri kuwa huingizwa nchini kwa njia za magendo, walisema kuwa
pombe aina ya Kandasana nayo pia ilikuwa na madhara kwa watumiaji ambapo wengi
wao hasa wanaume walikuwa wakiishiwa nguvu za kiume baada ya kunywa pombe hiyo.
’’Unashangaa hizi Mowa wa Mafumu na Rider!
Mwanzo kulikuwa na pombe ilikuwa inaitwa Kadansana ambayo ilikuwa na athari
kubwa zaidi kwasababu wanywaji hasa wanaume walikuwa wakiishiwa nguvu za
kiume’’ alieleza mmoja wa vijana mjini Kyela.
Uwepo wa pombe hizo hapa nchini ni mwendelezo
wa udhibiti mdogo wa dawa na vyakula hapa nchini hususani mkoa wa Mbeya ambapo
hivi karibuni tuliweka wazi matumizi mabaya ya vidonge vya Crolofenical
kutumika katika pombe za kienyeji huku Mamlaka ya udhibiti wa dawa na chakalu
TFDA wakisema kuwa hawajui lolote.
Kwa upande wake mkaguzi wa TFDA nyanda za juu
kusini Rodney O. Atananga, alisema utaratibu wa kukamata bidhaa
zilizopigwa marufuku nchini na ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu
huhusisha pia Jeshi la polisi na idara ya afya.
Alisema wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa
mara ili kubaini ubora wa bidhaa zilizoko sokoni ili kubaini usalama wake na
kama zinafaa kwa matumizi ya binadamu.
Atananga alisema watu wanaokamatwa na bidhaa
hizo wanafikisha mahakamani kwa sababu ni kinyume na sheria ya chakula na dawa
ya mwaka 2003 ambayo inakataza kuuza na kusambaza bidhaa ambazo
hazijasajiliwa na kupigwa marufuku.
Alisema baadhi ya bidhaa zilizopigwa marufuku
ni vipodozi vyenye viambato vyenye sumu pamoja na vinavyoingia nchini bila
kibali au kusajiliwa.
Aliongeza kuwa bidhaa zenye viambapo vyenye
sumu zinakatazwa kwa sababu zinamadhara kwa mwili wa binadamu ambapo alisema
madara yake hutokea baada ya muda mfupi na mengine huchukua muda mrefu
kujitokeza.
Alisema baadhi ya madhara hayo ni kansa ya
ngozi na damu ambayo hujitokeza baada ya muda mrefu lakini madhara ya muda
mfupi ni uharibifu wa ngozi na wajawazito kuharibu uzio wa ubongo wa mtoto
akiwa tumboni pamoja na kuumwa kichwa.
Kwa sasa pombe kali zilizozagaa mkoani Mbeya
ni pamoja na Zed pineapple spirit, double punch,Assorted sarit, Power na Rider
can.
|
MKUU WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIKAGUA GWARIDE LA KIKOSI CHA KUTULIZA FUJO KATIKA KIWANJA CHA FFU MBEYA HIVI KARIBUNI |
|
MKUU
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMANDA DIWANI AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA MBEYA
KATIKA SHEREHE HIZO ZA WANAFAMILIA WA POLISI JIJINI HAPA |
|
MKUU WA MKOA MBEYA AKIONGE NA WANAFAMILIA WA POLISI |
|
BAADHI YA WAGENI WAALIKWA WAKIMSIKILIZA MGENI RASMI |
|
BAADHI YA ASKARI 21 WALITUNUKIWA VYETI VYA UTUMISHI MZURI KATIKA JESHI HILO LA POLISI |
|
BAADHI WA WANAFAMILIA WA POLISI WAKICHEZA TAARABU UWANJANI HAPO |
|
BAADHI YA WADAU WALITUNUKIWA VYETI VYA USHIRIKIANO MWEMA NA JESHI LA POLISI HAPA KIONGOZI WA DINI AKIPOKEA HATI HIYO |
|
MAKAMPUNI YA ULINZI YA WATU BINAFI PIA WALIPOKEA HATI HIYO YA USHIRIKIANO NA JESHI LA POLISI |
|
MOJA YA WAFANYABIASHARA WA JIJI LA MBEYA JULIUS KAIJAGE AKIPOKEA HATI HIYO |
|
PIA MKUU WA MKOA MBEYA ALIKABIDHI PIKIPIKI KWA JESHI HILO LA POLISI
PICHA NA Jem |
Vurugu tupu Tanzania ni kwa faida ya nani?
Vijana wakazi wa Dumila na vitongo vyake wakiangusha gari aina ya Land
Cruizer T 241 AMS mali ya mfugaji katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro
wakati wa vurugu zilizodumu kwa masaa sita kwa kuweka vizuwizi kwa
lengo la kumshinikiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdera kusikiliza
kero za wakulima. Picha na Juma Mtanda
MAENEO ya mikoa ya Morogoro, Mtwara na Dar es Salaam, jana
yaligeuka uwanja wa fujo na vurugu zilizosababisha vifo, majeruhi na
uharibifu wa mali, huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya
wananchi.
Vurugu hizo zimehusisha wakulima na wafugaji wa
jamii ya Kimasai kwa upande mmoja wa Morogoro, Mtwara Mikindani wananchi
waliizingira nyumba ya Diwani wa Kata ya Mikindani kwa madai ya
kuwahifadhi watu wanaodaiwa kuwa washirikina ndani ya nyumba yake, huku
Dar es Salaam eneo la Kariakoo, polisi na Wamachinga wakipambamba na
Mgambo wa Jiji.
Mkoani Mororgoro mtu mmoja aliyefahamiwa kwa jina
la Mohamed Msigara (60) amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa
baada ya kutokea vurugu kati ya wakulima na wafugaji Kijiji cha Dumila,
wila yani Kilosa, baada ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza mifugo
yao kwenye mashamba ya wakulima yaliyo katika Kitongoji cha Mfulu,
Kilosa.
Pamoja na mauaji hayo, wasafiri waliokuwa
wakitumia Barabara ya Morogoro – Dodoma, nao walionja machungu ya vurugu
hizo, baada ya kukwama kwa saa 5 kutokana na wananchi wa kijiji hicho,
kufunga barabara kwa mawe, magogo ya miti na kuchoma magurudumu ya gari.
Wananchi hao walichukua hatua hiyo huku
wakisisitiza kutaka kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera,
ili kumaliza mvutano huo.
Katika vurugu hizo wanakijiji hao walivunja vioo
vya madirisha ya baadhi ya nyumba tano za kulala wageni, kuharibu gari
dogo aina ya Landcruser pamoja na kupora mali mbalimbali zi nazodaiwa
kumilikiwa na wafanyabiashara wa jamii ya Kimasai.
Kabla ya kufanya uharibifu huo saa 2:30 asubuhi,
wananchi hao walifanya maandamano sambamba na kusimama katikati ya
barabara, hali iliyosababisha polisi kufika eneo hilo kwa ajili ya
kuwadhibiti.
Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU), walifika eneo la
tukio 5:20 asubuhi na kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao kwa kutumia
mabomu ya machozi, hatimaye kufungua barabara hiyo.
Pamoja na barabara hiyo ya Morogoro – Dodoma,
wananchi hao pia walifunga barabara ya Dumila- Kilosa, hivyo kuyafanya
magari yaliyokuwa yakitumia barabara hiyo kukwama kwa zaidi ya saa sita
na kusababisha usumbufu kwa wasafiri waliokuwa wakitumia barabara hiyo.
Wakati vurugu hizo zikiendelea, wafugaji wa jamii
ya Kimasai wakiwamo wanawake na watoto walionekana kukimbilia kwenye
kituo kidogo cha Polisi Dumila kwa lengo la kujihami na kupata msaada wa
polisi kutokana na hofu ya kushambuliwa na wananchi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
aliyekuwepo kwenye eneo la tukio, mkulima aliyefahamika kwa jina Mauya
Hamadi alisema kuwa wananchi wamelazimika kufanya vurugu hizo baada ya
wafugaji wa jamii ya Kimasai kuingiza mifugo kwenye mashamba ambayo
tayari yameshapandwa mazao na kufanya uharibifu.
Alisema kuwa tayari suala hilo walishalifikisha
kwa uongozi wa kijiji, kata, wilaya hadi mkoa, lakini hakuna jitihada
zozote zinazofanywa na viongozi, hivyo kulazimika kumtaka Mkuu wa Mkoa
Joel Bendera, kwenda kuzungumzia suala hilo, ambapo hata hivyo mkuu huyo
wa mkoa hakuwahi kufika eneo hilo hadi walipoamua kufanya maandamano
hayo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati
alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma ili kukagua ujenzi wa
uwanja huo unaofanywa na kampuni ya ujenzi ya Howard Humphrey
Katibu
wa Halmashauri Kuu Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa Dk. Asha Rose Migiro
, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya na Katibu Mkuu wa CCM
Abdurahman Kinana wakielekea kwenye magari tayari kwa kukagua ujenzi wa
uanjwa wa ndege wa Kigoma
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakikagua uwanja wa ndege wa Kigoma leo.
Mafundi wa kampuni ya Howard Humphrey wakiendelea na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma.
Meneja wa uwanja wa ndege wa Kigoma Injinia Clipia Tesha akitoa maelezo
kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana wakati alipotembelea kukagua
uwanja huo akiongozana na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Kulia ni Mkuu
wa mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya na kutoka kushoto ni Dk. Asha
Rose Migiro Katibu wa Halmashauri kuu Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
CCM, Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi CCM na
Martin Shigela Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM UVCCM.
Cleopa
Mpembeni Meneja mradi wa Ujenzi wa Uwanja huo kutoka kampuni ya Howard
Humphrey akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM na wajumbe wa
Sekretarieti ya CCM wakati ujumbe huo ulipotembelea kukagua ujenzi wa
uwanja huo leo
Meneja
wa uwanja wa ndege wa Kigoma Injinia Clipia Tesha akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana
kukagua ujenzi wa uwanja huo leo.
by John Bukuku
No comments:
Post a Comment