Thursday, January 24, 2013

Sheria ya kusimamia vyombo vya habari

Nembo-ya-Taifa 
Serikali inapenda kuufahamisha umma wa Watanzania kwamba mchakato wa maandalizi ya kutungwa kwa Sheria ya Kusimamia Vyombo vya Habari (Media Services Bill) upo katika ngazi za juu  Serikalini.
 
Mswada huo unatarajiwa  kuwasilishwa  Bungeni wakati wowote baada ya kupitishwa katika ngazi za juu za Serikali.
 
Mswada unaotarajiwa kuwasilishwa ni ahadi ya Serikali tangu mwaka 2007.  Serikali ipo tayari kupokea hoja mbalimbali baada ya kuwasilisha mswada huu Bungeni kwa maana ya kuboresha ikiwemo Haki ya Kupata Habari.
 
Serikali inawataka wadau wa habari na watanzania kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kuhakikisha kwamba Mswada wa Kusimamia vyombo vya Habari unakamilika na kuwa sheria lengo likiwa ni kujenga misingi ya demokrasia na utawala bora.
 24/1/2013
 

President Kikwete and Tony Blair participates in a meeting on Mobilising Private Sector investment in African Energy

8E9U5067 
President  Dr. Jakaya Mrisho Kikwete  speaks during  a World Economic Forum session on “Mobilizing Private Sector Investment in African Energy,” held at World Food Programme  Tent in Davos, Switzerland. On the left  is USAID administrator Dr. Rajiv Shah  and second left is former British Prime Minister Tony Blair.
8E9U5068President  Dr. Jakaya Mrisho Kikwete  speaks during  a World Economic Forum session on “Mobilizing Private Sector Investment in African Energy,” held at World Food Programme  Tent in Davos, Switzerland. On the left  is USAID administrator Dr. Rajiv Shah  and second left is former British Prime Minister Tony Blair.
8E9U5111 
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete  and former British Prime Minister Tony Blair leaves World Food Programme tent in Davos, Switzerland after participating in a meeting on “Mobilizing Private Sector Investment in African energy,” yesterday(photos by Freddy Maro)
 
 

MAULID YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)YAFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MAISARA

IM 6380 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar
Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe
za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana,
na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,(katikati).[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_6367 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji
Khamis,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid
ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
IM   6404 
Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma
Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad
(S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini
Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa
na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu. [Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
IM   6412 
Ustadh Abdulla Hamad wa Chuo cha Kiislamu,akitoa
tafsiri ya Aya za Quran,zilizosomwa na Ustadh Rashid Jaffer wa
Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya
Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja
vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama
hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu. [Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
IM 6374 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Viongozi wa Jumuiya ya Maulid
EL Nabii Zanzibar,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika
sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W)
yaliyofanyika jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
 
 

JAPAN YAIPA TANZANIA BILIONI 28.2 KUBORESHA BARABARA NA KILIMO, MAKUTANO YA TAZARA KUWA NA BARABARA ZA JUU KWA JUU

william_mgimwa

Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
 SERIKALI ya Japan imepatia Tanzania msaada wa shilingi bilioni 28.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ya uboreshaji wa usafiri jijini Dar es salaam na kilimo hapa nchini.

 Msaada huo umesainiwa (leo) jijini Dar es salaam na Balozi wa Japan hapa nchini Masaki Okada kwa niaba ya Japan na Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa kwa niaba ya Serikali ya Tanzania.
 Akizungumza mara baada ya kusaini msaada huo Waziri wa Fedha Dkt . Mgimwa alisema kuwa mradi wa kwanza utahusisha upanuzi wa barabara ya Kilwa na ile ya Bandari ambapo jumla ya shilingi bilioni 20 zitatumika katika kukamilisha mradi huo.

 Aliongeza kuwa mradi mwingine ni ule wa ujenzi wa barabara za juu(flyover) katika makutano ya TAZARA ambapo jumla ya shilingi bilioni moja (1) na milioni 26 zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha mradi huo.

 Dkt. Mgimwa aliongeza kuwa eneo lingine ambalo litanufaika na msaada kutoka Japan ni kuunga mkono sera ya Kilimo kwanza ambapo Tanzania imepata shilingi bilioni sita(6) na milioni 92 kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwepo kwa usalama wa chakula cha kutosha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

 Alisema kuwa upande wa eneo hilo lengo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wa kipato cha chini wanaboresha kilimo ambacho kitawahakikisha uhakika wa chakula wakati wote na hivyo kuondokana na umaskini.

 Kwa upande wa Balozi wa Japan hapa nchini Masaki Okada alisema kuwa wananchi wengi wa Tanzania hasa wakazi wa Jiji la Dar es salaam wamekuwa wakisubiri kwa hamu barabara za juu ili kusaidia kupunguza msongamano wakati wa kuja na kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam.
 Alisema kuwa utakapo kamilika mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la msongamano na hivyo kupunguza saa za mwananchi kusafiri kuja na kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam.
 Balozi Okada alisema kuwa hatua hii itakuwa muhimu katika kukuza uchumi kwani wananchi watakuwa na muda wa kutosha kuzalisha mali kutoka na miundombinu kuruhusu magari kwenda kasi pasipo kikwazo.
 

Sitta:Nitajipima kama Nafaa kuwa Raiswakati ukifika


Na :Leon Bahati-Mwananchi
“Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee,” Akizungumza katika mahojiano

maalumu na gazeti hili juzi, Sitta alitaja mambo kadhaa aliyoeleza kuwa ni ishara ya kukubalika kwake, ikiwamo kuteuliwa na marais wote wanne; Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete katika nyadhifa mbalimbali ikiwamo ya uwaziri. Kauli ya Sitta imekuja baada ya kuwapo kwa minong’ono ya baadhi ya wananchi kumtaja kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kujitokeza kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015

“Ni faraja kusikia watu wakinizungumzia kuwa ninazo sifa (za kuwa Rais). Nami ninaamini ninazo sifa. Wakati utakapofika nitajipima. Kama hali hii itaendelea, basi nitaona ni vizuri nigombee,” alisema Sitta ambaye aliwahi kuwa Spika wa Bunge.

Hata hivyo, alisema hana mkakati wowote sasa wa kuendesha harakati za kutafuta nafasi hiyo kwa udi na uvumba kama baadhi ya wengine (bila kuwataja), wanavyofanya... “Sina sababu za kuanza kutafuta support (kuungwa mkono) wala uundaji wa kamati za ushawishi kwa watu sasa,” alisema Sitta.

Badala yake alisema atasubiri hadi muda wa kuchukua fomu za kugombea utakapofika ndipo atakapojitathmini na kusema endapo atabaini kuwa Watanzania wengi wanamuunga mkono, atachukua uamuzi wa kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Aitahadharisha CCM
Waziri huyo aliwahadharisha wanachama wa CCM kwamba wasipokuwa makini, wanaweza kuipoteza nafasi hiyo ya urais na kwenda kwa vyama vya upinzani.

Alionya kuwa iwapo watamteua mtu asiye mwadilifu, Watanzania hawatamchagua na badala yake watampa nafasi hiyo mgombea yeyote kutoka vyama vya upinzani.

Alisema Watanzania wengi wana werevu wa kutosha kujua watu ambao ni mafisadi na ambao wamekuwa wakitumia fedha zao chafu kwa ajili ya kutaka wakubalike mbele ya macho ya Watanzania. Alisema suala la uadilifu ni moja ya vigezo muhimu ambayo CCM wanapaswa kuvizingatia ili kupata ushindi wa kiti cha urais mwaka 2015.

“Ndiyo maana nilipokuwa mbele ya Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba niliweka wazi kwamba Tanzania tunahitaji kuwa na jopo la kuhoji viongozi na wananchi wawe na fursa ya kuwachambua,” alisema Sitta.

Alisema kinachohitajika Tanzania ni mfumo ambao utajenga mazingira ya kuwa na viongozi waadilifu katika ngazi zote.

Alisema hali hiyo itaepusha mfumo unaoonekana sasa wa viongozi kwenye ngazi mbalimbali kuishi kiujanjaujanja, kujinufaisha na kutojali athari kwa uchumi wa nchi na Watanzania kwa ujumla.

Alitoa mfano wa uzembe uliofanywa na viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambao umesababisha Bandari ya Dar es Salaam kupoteza uaminifu kwa nchi mbalimbali zinazopakana na Tanzania.

Alisema uzembe huo umeifanya Bandari ya Dar es Salaam kuingiza Sh38 bilioni kwa mwezi tofauti na Mombasa ambayo inaingiza Sh300 bilioni.

CCM ni imara?
Akizungumzia miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM, mbunge huyo wa Urambo Mashariki alisema anaamini kwamba chama hicho kimefanya vizuri licha ya kuchafuliwa na watu wachache kutokana na tabia zao za ufisadi.
 
 

Hospitali ya rufaa Mbeya yashitukia ubadhilifu na rushwa

Katibu wa Hospitali  Aisha Mtanda akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa hospitali ya rufaa Mbeya
Mwenyekiti wa kamati ya sherehe Christopher Mwakubombaki moja wa waandaaji wa bonanza hilo
Mratibu wa Bonanza hilo kutoka Kampuni ya Lifetime Venance Matinya 
Meneja wa kampuni hiyo ya LifeTime Entertainment, Emmanuel Madafa, 


KUTOKANA na kukithiri kwa vitendo vya rushwa katika taasisi za Serikali, Hospitali ya Rufaa ya Mbeya imeamua kuandaa Bonanza kubwa la michezo kwa ajili ya kukutana na wananchi ili kukemea vitendo hivyo.
Aidha hali hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kuingiwa na kashfa kwa baadhi ya watumishi wake wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya Kupokea Rushwa kutoka kwa wagonjwa hususani katika kitengo cha Mifupa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, katibu wa Hospitali hiyo, Aisha Mtanda alisema kuwa bonanza hilo ambalo litabeba ujumbe usemao ‘Huduma  bora bila rushwa inawezekana, kemea vitendo vya  vya rushwa, tuungane kutokemeza limeandaliwa na Uongozi wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya LifeTime Entertainment & Marketing Ltd na kwamba bonanza hili litafanyika siku ya Jumamosi(Januari 26, mawaka huu).
Alisema kuwa lengo la bonanza hilo ni kufanya hafla fupi kwa watumsihi wa Hospitali hiyo kwa kuaga mwaka wa 2012 na kuukalibisha mwaka mpya wa 2013, ambalo pia litafanyikia katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu (TIA)tawi la Mbeya.
“Uongozi wa Hospitali tunakusudia kufanya bonanza litakalowakutanisha watumishi wa serikali pamoja na taasisi mbalimbali siku ya Jumamosi Katika bonanza letu litakuwa na ujumbe wa kukemea vitendo vya rushwa vinavyoonekana kushamiri katika sekta mbalimbali,” alisema katibu huyo.
Kwa upande wake Mratibu wa Bonanza hilo kutoka Kampuni ya Lifetime Venance Matinya alisema katika Bonanza hilo kutakuwa na michezo mbali mbali kama vile mpia wa miguu, mpira wa pete, Netboli, Basketi boli, Voleboli, kuvuta kamba, kukimbia kwenye magunia,kukuna nazi na mashindano ya kula.
Aliongeza kuwa taasisi zinazotarajia kushiriki ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Halmashauri ya Jiji, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Madiwani wa Halmashauri wa Jiji, Kampuni ya Bia (TBL), Hospitali ya Rufaa na kitengo cha Benki ya damu salama.
Naye  meneja wa kampuni hiyo ya LifeTime Entertainment, Emmanuel Madafa, alisema kuwa katika mabonanza hayo ni sehemu pekee ya kukutana kwa watumishi mbalimbali na wananchi ili kuweza kuambizana ukweli kuhusu adii mbaya wa rushwa.
Alisema kuwa vitendo vya rushwa haviwezi kukomeshwa endapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa kwa kuambizana ukweli, kwani wananchi muda mwingine wanaweza wakawa wanashawishiwa kutoa rushwa kutoka kwa watumishi bila ya kujua haki zao za msingi na wasijue wapi wanaweza kwenda kutoa malalamiko yao.
“kwenye mabonanza kama haya ni sehemu pekee ya kuweza kukutana wananchi pamoja na watumishi wa Serikali na taasisi mbalimbali ili kuweza kuambizana ukweli kuhusu adui rushwa kwani hawa watu wawili ndiyo wahusika wakuu kwamaana ya mpkeaji na mtoaji,” alisema Madafa.
Hivi karibuni Mmoja wa watumishi wa Hospitali hiyo wa kitengo cha mifupa alikamatwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa mgonjwa aliyekuwa anahitaji kupatiwa huduma ya upasauaji.
 
Post a Comment