MVUA IKINYESHA |
HIYO HAPO JUU NDIO OFISi YA KINGO PRODUCTION & www,kingotanzania.blogspot.com NDIPO WAYA ZILIPOKATIKA NA KUJIKUTA MAISHA YAKO REHANI KWA MLIPUKO MKUBWA NA CHECHE ZA MOTO KUTOKEA |
KIJANA AKAJITOLEA KUINUA WAYA ILI WATU WAVUKE SALAMA |
WATOTO WAKIPITA KWA HOFU |
SASA AMANI MAANA MAFUNDI WA TANESCO WAMEFIKA NA KUZIMA UMEME NA KUENDELEA NA MAREKEBISHO |
MAFUNDI WAKIENDELEA NA KAZI SASA |
Wafanyabiashara na Wanasiasa walioahidi kuisaidia familia ya Mwangosi watakiwa kutekeleza ahadi zao walizoahidi kwa familia mbele ya watanzania .
MKE WA MAREHEM SIKU YA MAZIKO YA MUMEWE AKIMUAGA KWA MALA YA MWISHO |
WACHUNGAJI WAKIONGOZA MAZIKO |
Mkurugenzi wa umoja wa vilabu vya waandishi wa
habari nchini (UTPC) Abubakar Karsan wakati akiongea na waandishi wa habari
mkoani Mbeya.
|
WANAWAKE ILEJE TANZANIA, WAJIFUGULIA CHITIPA NCHINI MALAWI.
HAPA NDIO MPAKANI MWA MWALAWI NA TANZANIA WILAYANI ILEJE |
MCHANA NDIO UNAPITA KWA MWENDO WA TOGWA NA KIPANDE CHA MKATE |
NIKATAMANI KINACHOUZWA HAPO MMMMM PALIKUWA NA TOGWA PAMOJA NA HUKU TANZANIA NI HALAM MALAWI WANAUZA HADHARANI (GONGO) |
SERA ya Afya ya mwaka 2007 haifahamiki wilayani Ileje katika
mkoa wa Mbeya. Ni katika sera hii ambamo inatamkwa kwamba wajawazito nchini
watapewa huduma za afya bure lakini hali sivyo ilivyo, imebainika.
Kama sera inafahamika, basi haitekelezwi. Baadhi ya
wajawazito katika wilaya ya Ileje wanaacha zahanati, vituo vya afya na
hospitali wilayani mwao na kuvuka mpaka hadi nchini Malawi kufuata kinachoitwa
“huduma bora.”katika hospitali inayojulikana kwa jina la Chitipa.
Kuna nini katika hospitali ya Chitipa nchini Malawi hadi
wajawazito wakimbilie huko? Jibu wanalo wanawake na wanaume wa wilayani ileje
akiwemo Neema Mbughi mkazi wa kijiji na kata ya Bupigu ambaye anasema kuwa Pale
hospitali ya Chitipa wajawazito wanaenda bila madishi, karatasi za nailoni
(ambako mjamzito huhala wakati wa kujifungua) wala glovu Kila kitu ni bure,
hata chakula ambacho tunapewa bule kama kimetoka nyumbani.
Wanawake wapatao 27 waliohojiwa na mwandishi wa habari hii, pamoja na
kutofautiana katika mambo mengine, wengi waliafikiana kuwa katika hospitali ya
Chitipa, wauguzi wanatumia “lugha nzuri” inayompa matumaini mjamzito.
Swali ni kwamba Hivi wanapitaje mpakani penye idara ya
uhamiaji? Jibu unalopewa ni kwamba hawapiti mpakani kwenye ofisi za serikali.
Wanapita vichochoroni ambako wanaita “njia za panya.”
Wakifika hospitalini Chitipa wanajieleza kuwa wanatoka vijiji
vya ndani ya Malawi – wengine wakitaja viongozi katika maeneo hayo kuthibitisha
kuwa wanatoka humohumo.
Kuna kichocheo kingine kwa wananchi wa Tanzania kutibiwa na
kujifungulia Chitipa? Katika mahojiano nao walieleza, mmoja baada ya mwingine,
kuwa ikitokea “bahati mbaya” mama au mtoto akafariki na wakati huo
umejitambulisha kuwa anatoka Tanzania, basi maiti inasafirishwa hadi mpakani
bila gharama yeyote.
Katika hospitali za mkoani Mbeya mwanamke hutakiwa kwenda na karatasi la kutandika wakati
wa kujifugua linalouzwa kwa Sh. 3,000, paketi ya glovu Sh. 2000, beseni Sh. 3,000
na kama mjamzito amelazwa bia kujali kuwa ana ndugu au hana, basi hujitegemea
pia kwa gharama za chakula.
Na, Gordon Kalulunga, Ileje
MAONI YA MH. LOWASSA KWA TUME YA KATIBA MPYA
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kukusanya Maoni ya Katiba
mpya,mara baada ya kutoa maoni yake.
YAFUATAYO NI SEHEMU YA MAONI ALIYOYATOA MH. EDWARD LOWASAA:
Kwanza
ningependa kukupongeza wewe mwenyekiti Mh Jaji Warioba pamoja na tume
nzima kwa imani kubwa ambayo Rais ameionesha kwenu, ni kwa kuwapa jukumu
hilo zito na muhimu kwa nchi yetu.
Wananchi
pia wamekuwa na imani kubwa na wamejenga matumaini ya kila kitu kwa
tume hii. Kutokana na hilo wamekuwa wakitoa maoni ambayo mengine
hayahusiani na katiba, yaani siyo ya kikatiba.Pengine na mimi nitakuwa
miongoni mwao, kwa hiyo naomba radhi mapema, iwapo maoni yangu haya
mengine , yataonekana si ya kikatiba.
Katiba
yetu ya sasa ni nzuri, imetuongoza katika umoja na mshikamano wa
kitaifa kwa muda wote huo.Lakini, kutokana na hali ya dunia ya sasa, ni
vyema kuwepo na katiba mpya ili kuendana na hali halisi.
Kuna mambo manne ambayo kwa imani na mtizamo wangu ningependa yawemo katika katiba yetu ijayo.
1.ELIMU BURE
Moja
ya haki za mtoto ni kupata elimu. Ningependa suala la elimu bure ya
sekondari liwemo kwenye katiba yetu. Katiba itamke wazi kuwa elimu ya
sekondari ni bure.Nchi yetu bado ina idadi kubwa ya watu wake ambao ni
masikini.
Uwezo
wao wa kipato ni mdogo.Naamini kabisa hili linawezekana na serikali
inaweza kugharimia elimu ya sekondari ikawa bure. Hii itatoa nafasi ya
kujenga taifa lijalo lenye idadi kubwa ya vijana watakaokuwa wamepata
elimu ya sekondari.Wabunge wenzangu bila shaka wanalijua hili.
Ukweli katika majimbo yetu wazazi wamekuwa wakishindwa kulipia karo ya shule kwa
watoto wao. Wabunge tumekuwa tukibeba mzigo huo japo kidogo. Kwa hiyo,
kifungu cha ELIMU BURE KWA SEKONDARI, kiwepo kwenye katiba.
2.ADHABU YA KIFO-DEATH PENALT
Katiba
ya sasa haisemi wazi kuhusu adhabu ya kifo.Inazungumzia tu haki ya
uhai.Ibara ya 14 ya katiba hii ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya
mwaka 1977 inatamka kiujumla tu kuwa KILA MTU ANA HAKI YA KUISHI NA UHAI
WAKE KULINDWA.
Lakini
, haki hiyo inanyang’anywa na kifungu nambari 196 cha sheria ya kanuni
za adhabu sura ya 16(penal code ,cap 16), kinachotamka kuwa adhabu ya
kifo(death penalty or capital punishment) kwa kosa la mauaji ya
kukusudia.
Adhabu
hiyo hiyo pia utolewa kwa kosa la uhaini.Sasa mapendekezo yangu mimi ni
kwamba kuwe na ibara katika katiba mpya inayotamka wazi kuwa HAKUTAKUWA
NA ADHABU YA KIFO HAPA NCHINI HATA KWA KOSA LA KUKUSUDIA AU UHAINI.
3.MATUMIZI YA FEDHA KATIKA UCHAGUZI
Katika
sehemu nyingi hapa nchini mwananchi kama hana fedha hawezi kugombea
nafasi mbalimbali za uongozi.Katiba mpya iwe na ibara inayofafanua ni
kiasi gani cha fedha ambacho mgombea anaruhusiwa kutumia katika
kampeni.Iainishe ni matumizi gani ya lazima ambayo mgombea hawezi
kukwepa kutumia fedha katika kampeni zake, mfano kuwakusanya wapiga kura
kwenda kupiga kura gharama hizo nani azibebe.
Katiba
ifafanue rushwa ni nini kwenye chaguzi hizi.Au tuwe na mfumo wa
PROPORTIONAL REPRESENTATION ,vyama viwe ndiyo vinaingia kwenye chaguzi
kuwania majimbo na siyo wanachama,huko kila mtu atakuwa anapigania chama
chake kupata kura nyingi ili wapate viti vingi zaidi, pengine hii
itasaidia kuondoa kikwazo cha mtu kuwa na uwezo wa kifedha ndiyo aweze
kuwania uongozi.
4.ARDHI
Kwa
mwanadamu, kunyang’anywa haki ya kutumia ardhi ya nchi aliyozaliwa ni
sawa na kunyanng’anywa haki ya uraia wake. Katiba hii ya sasa inawapa
nguvu wakulima katika suala la ardhi, na kuwasahau wafugaji.
Wafugaji
wamekuwa wakimbizi katika nchi yao, wamekuwa wakitangatanga kutafuta
malisho ya mifugo yao, ile ardhi waliyokuwa wanaimiliki wakiondoka
kutafuta malisho huku nyuma imekuwa ikimilikishwa watu wengine, wakulima
au wawekezaji, hili kwakweli si jambo jema .
Tumeshuhudia
migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.Kwa hiyo, mimi
ningependa katiba hii mpya impe mfugaji haki katika suala la ardhi
kama.Ardhi ya wafugaji ilindwe, ifafanuliwe kikatiba haki yao hiyo. Kuwe
na hali ya 50,50 situation kati ya mfugaji na mkulima katika suala zima
la umiliki wa ardhi,kikatiba!
Dkt.bilal ataka muungano wa serikali mbili katiba mpya
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na ujumbe wa Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Agostino Ramadhan. Mheshimiwa Makamu wa Rais amepata fursa ya kukutana na Tume hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Warioba kabla ya kumruhusu Mheshimiwa Makamu Wa Rais kutoa maoni yake, alimuelezea namna tume hiyo inavyofanya kazi na namna zoezi zima la kukusanya maoni ya mtu mmoja mmoja lilivyofanyika na kisha akaeleza kuwa, tume hiyo inaendelea na zoezi hilo kwa kukutana na makundi maalum sambamba na mtu mmoja mmoja kufuatia umuhimu wa hoja ambazo tume inakutana nazo na hivyo kuhitaji ufafanuzi.
Katika muktadha huo, Jaji Warioba sambamba na kumpa fursa ya kuchangia maoni yake mengine anayopenda alimtaka Mheshimiwa Makamu wa Rais kujikita zaidi katika suala la Muungano kufuatia yeye kuwa na uzoefu wa kiuongozi katika serikali zote mbili yaani ya Muungano sambamba na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumzia suala la Muungano Makamu wa Rais Dkt. Bilal ameieleza Tume kuwa yeye ni muumini wa Muungano wa serikali mbili na kwamba haoni sababu ya kubadili mfumo uliopo kwa kuwa umeipatia tija nchi yetu na kuipambanua kama nchi yenye muungano wa mfano katika dunia. Pia alifafanua kuwa mfumo wa serikali mbili umesaidia kujenga na kudumisha udugu, amani na utulivu baina ya wananchi wa Tanzania Bara na Visiwani kwa kipindi cha miaka 49 sasa.
"Tanzania imechangia kitu kikubwa katika historia, kudumisha Muungano wa mfumo wa serikali mbili kati ya nchi mbili, kubwa na ndogo, jambo ambalo kwa nchi nyingine za Afrika wameshindwa. Kumekuwepo na nchi nyingi ambazo ziliungana na kushindwa kudumu kama tulivyo sisi. Hatuna haja ya kujifunza mfumo mpya wakati tulionao umeweza kudumu," alisema.
Katika ujumbe wa tume uliofika kuchukua maoni ya Mheshimiwa Makamu wa Rais ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Profesa wa Sheria Palamagamba Kabudi, Ndugu Simai Said, Ndugu Assa Rashid, Ndugu Sasmir Kyuki, Ndugu Salum Athuman, Ndugu Juma Mzalau na Mratibu wa Tume hiyo Ndugu Ramadhan Kailima.
No comments:
Post a Comment