Na: Fredy Azzah
RAIS
Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ameelezea kufedheheshwa kwake
na mgogoro wa gesi, huku akiwataka wananchi na wadau wa maendeleo wa
Mkoa wa Mtwara kusitisha harakati za maandamano na mihadhara. Mkapa
alitaka wakazi hao
kuacha kulumbana na Serikali kuhusu suala hilo, badala yake wajiandae kukaa meza moja nayo kutafuta mwafaka kwa njia ya amani.
Katika
tamko lake alilolitoa Dar es Salaam jana, Mkapa alisema: “Fujo,
vitisho, kupimana nguvu na malumbano siyo masharti ya maendeleo.
“Nikiwa
kama mwana - Mtwara na raia mwema, mpenda nchi, nimefedheheshwa sana na
matukio haya ya siku za karibuni Mtwara. Kwa sababu hiyo natoa wito kwa
wadau wote wa maendeleo ya Mtwara, kusitisha harakati hizi na
maandamano na mihadhara.
“Badala
yake wajipange kukaa pamoja katika meza moja, kupitia historia,
kutathmini mipango, kuchambua kwa kina mikakati ya utekelezaji wake,
hatimaye kufikia mwafaka wa ujia wa maendeleo. Liwezekanalo leo
lisingoje kesho.”
Mkapa
alisema mwenendo wa mazungumzo, maandamano na mikutano ya hadhara
inayoendelea mkoani Mtwara, inaelekea kuashiria kuvunjika kwa amani hali
aliyosema kuwa inajenga kutokuelewana kati ya viongozi wa vyama vya
siasa na Serikali, wananchi na vyama vya siasa na wananchi na viongozi
wa Serikali.
“Mtafaruku
huu haufai kuachwa na kutishia usalama, mipango ya maendeleo siyo siri,
mikakati na mbinu za utekelezaji wake siyo siri,” alisema Mkapa na
kuongeza:
“Maelezo
yake mazuri yanaweza kutolewa yakadhihirisha namna na kasi ambayo
rasilimali zinawanufaisha wananchi wa eneo zilimo na taifa zima.”
Mkapa alisema hali hiyo ni tishio kwa wawekezaji wa ndani na nje, kwani mara zote hawapendi vurugu, fujo na vitisho.
Kauli hiyo ya Mkapa imekuja siku kadhaa tangu kuwapo kwa maandamano na vurugu zinazofanywa na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara wanaopinga gesi kusafirishwa kwenda Dar es Salaam.
Tayari
viongozi kadhaa akiwamo Rais Jakaya Kikwete wametoa tamko juu ya suala
hilo wakionya kuwa halikubaliki kwa kuwa rasilimali hiyo si kwa ajili ya
wana Mtwara pekee.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo aliyalaani maandamano
hayo akisema walioyaandaa wamelenga kuigawa nchi vipandevipande, Chadema
kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kumbana waziri huyo ili aondoe udhaifu
uliopo katika sekta ya nishati.
Desemba
mwaka huu, maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliandamana wakipinga
uamuzi wa Serikali kusafirisha gesi kwa njia ya bomba kutoka hapa kwenda
Dar es Salaam.
Maandamano
hayo yaliyoratibiwa na vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, Sau, Tanzania
Labour Party (TLP), APPT- Maendeleo, ADC, UDP na DP yakishirikisha
wananchi wa wilaya za mkoa huo, zikiwamo Tandahimba na Newala yalianzia
katika Kijiji cha Mtawanya hadi Mtwara Mjini kupitia barabara ya kwenda
Msimbati eneo ambako gesi asilia inapatikana.
MWANANCHI
Rais Obama awasifu Lincoln, Luther King
Obama ambaye ni Rais wa 44 wa Marekani, aliingia
madarakani katika uchaguzi wa kihistoria mwaka 2008 uliomfanya kuwa Rais
wa kwanza mwenye asili ya Afrika katika taifa hilo kubwa duniani.
Sherehe za kuapishwa kwake Ikulu jana zilikuwa za
faragha na zilihudhuriwa na watu wachache maalumu, leo ataapishwa katika
sherehe za jumla zitakazowajumuisha watu wote kwenye Uwanja wa National
Mall.
Katika kiapo chake, Obama atatumia Biblia mbili,
moja iliyokuwa ikitumiwa na Martin Luther King na nyingine ilikuwa
ikitumiwa na aliyekuwa Rais wa 16 wa Marekani, Abraham Lincoln.
Lincoln aliongoza taifa hilo kuanzia Machi 1861 hadi alipouawa Aprili 1865.
Akiwa Ikulu jana, alitumia Biblia iliyowahi kutumiwa na Lincoln, katika sherehe za leo atatumia Biblia ya Martin Luther King.
Lincoln, ndiye aliyeliongoza taifa hilo kipindi kigumu cha kusimamia umoja na kufuta biashara ya utumwa.
Lincoln aliongoza taifa hilo kuanzia Machi 1861 hadi alipouawa Aprili 1865.
Akiwa Ikulu jana, alitumia Biblia iliyowahi kutumiwa na Lincoln, katika sherehe za leo atatumia Biblia ya Martin Luther King.
Lincoln, ndiye aliyeliongoza taifa hilo kipindi kigumu cha kusimamia umoja na kufuta biashara ya utumwa.
Martin Luther King ambaye alikuwa mchungaji na
mwanaharakati wa haki za watu wenye asili ya Afrika nchini Marekani,
aliuawa Aprili 4, 1968, muda mfupi baada ya kutoa hotuba yenye nguvu ya I
have a Dream (Nimeota ndoto).
Hotuba hiyo ikuwa ikieleza ndoto yake kwamba muda
siyo mrefu watu wenye asili ya Afrika watapata nguvu na kupata haki yao
kama raia wa Marekani.
Viongozi hao wawili wana historia ya pekee,
Lincoln ndiye aliyetumia muda wake mwingi akiwa Ikulu ya Marekani
kuhakikisha watu wenye asili ya Afrika ambao walikuwa watumwa
wananasuliwa utumwani.
Luther alikuwa mwanaharakati aliyechochea mabadiliko kwa kushinikiza Serikali kuwapa haki zao za msingi.
Obama aliapishwa rasmi jana ikiwa ni siku ya
kwanza kati ya siku mbili zilizopangwa, leo ataapishwa mara ya pili
katika viwanja maalumu vya Nationa Mall mjini Washington, ambako maelfu
ya watu watapata fursa ya kushuhudia.
Hotuba ya kuapishwa kwake itakayotolewa leo
inatarajiwa kuweka historia mpya, pia kuhitimisha matukio ya siku mbili
hizi za kuapishwa, ataweka wazi mtazamo wake wa kipindi cha miaka minne
ijayo.
Mkusanyiko utakaoshuhudia kuapishwa kwake na
kusikiliza hotuba yake moja kwa moja katika uwanja huo unakadiriwa
kupungua kutoka ule wa watu 1.8 milioni mwaka 2009 na kufikia kati ya
600,000 na 800,000, huku mamilioni wakishuhudia kupitia televisheni.
JAMBO LEO
UKUTA WA KITUO CHA MABASI UBUNGO WAANGUKA NA KUHARIBU MAGARI
Gari
linalosadikiwa kuwa ni la polisi likiwa limeharibiwa vibaya na ukuta wa
kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo Bus Terminal baada
ya nguzo zake kudondokea magari mbalimbali yaliyokuwa yameegeshwa katika
eneo hilo, jumala ya magari 24 yameharibiwa vibaya katika tukio hilo
Bajaji 4 na watu watatu wamejeruhiwa na mkukimbizwa Hospitali.
Mtoto afariki dunia kwa ajali ya Moto...
Mwili wa mtoto huyo ukichukuliwa na polisi kwenda kuhifahiwa na kuchunguza chanzo cha moto huo |
Nyumba hii ndimo alimoungulia mtoto huyo |
Baadhi ya majirani wakiwa katika tukio hilo |
Mtoto Halaika Bushiri (7)
mwanafunzi wa shule ya msingi Mwanyanje iliyopo kata ya Igawilo jijini hapa
amefariki dunia baada ya kuketea kwa moto akiwa nyumbani kwao jana majira ya
saa 7:45 ya mchana, Januari 21 mwaka huu.
Shuhuda wa tukio hilo Recho Jeseph (36) amesema
mtoto huyo aliza kupiga kelele za kuomba msaada mara baada ya kutokea kwa moto
wakati mama wa mtoto Nuru Mlele akiendelea shughuli zake licha ya majira kujitokeza
na kuuzima moto huo.
Katika hali ya kushangaza mama huyo hakuonesha
kustushwa na kitu chochote na wakati tukio hilo aliendelea kufua nguo, hadi
pale majirani walipofanikiwa kuudhibiti moto huo ambao uliteketeza samani za
nyumba yake ikiwemo seti moja ya kochi
Aidha kutokana na juhudi za majirani kushirikiana
ndani ya dakika kumi walifanikiwa kuudhibiti moto huo na kuuzima lakini mtoto
huyo alikuwa tayari ameshafariki.
Hata hivyo licha ya polisi kupewa taarifa majira
ya saa tisa kamiliwalifika majira ya saa kumbi na mbili na robo jioni, eneo la
tukio lenye umbali wa mita mia sita kutoka kituoni, hali iliyowasononesha sana
wananchi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani
amekiri kupokea taarifa za tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa na uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado
unaendelea.
Na Ezekiel Kamanga,Mbeya
MWENYEKITI WA MBEYA PRESS CLUB ALIYE KUJIUZURU KWA NGUVU YA WANACHAMA AKABIDHI OFISI KWA MWENYEKITI WA MUDA
|
No comments:
Post a Comment