Thursday, February 7, 2013

TAARIFA YA POLISI KUHUSIANA NA KUWAWA WAKIGOMBANIA MWANAMKE MTAA WA ITIJI NONDE MBEYA



MWILI WA MAREHEMU DANIEL MWASALEMBA 30 UKIWA UMELALA KWENYE MAJANI BAADA YA KUTOLEWA NDANI MAREHEMU AMECHOMWA VISU KISA NI UGOMVI WA KUGOMBANIA MWANAMKE AITWAE ELIZABETH MICHAEL
ANAYEDHANIWA KUSABABISHA KIFO  CHA DANIEL  AMEJULIKANA KWA JINA MOJA TU PETER YEYE NI MWENYEJI WA SUMBAWANGA NA NA NIMWOSH MAGARI YA KAMPUNI YA MABASI YA SUMRY JIJINI MBEYA AKIWA AMEPATA KIPIGO TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI
HAPA PETER AKIOKOLEWA NA WANAUSALAMA WALIOWAHI ENEO HILI LA TUKIO LEO HII
HIKI NDICHO CHUMBA ALIMOUWAWA MAREHEMU DANIEL
NDUGU WA MAREHEMU WAKIANGUA KILIO MARA BAADA YA KUONA MWILI WA NDUGU YAO DANIEL
HAKIKA ILIKUWA KAZI KUBWA SANA KWA POLISI KUMUOKOA PETER ANAEDHANIWA KUMUUA DANIEL KUMUOKOA KATIKA MIKONO YA WANANCHI WENYE HASIRA KALI KAMA UNAVYOONA WENGINE BADO WANA MAWE MKONONI
ANAEDHANIWA KUMUUA DANIEL AKIWA AMELALA CHINI BAADA YA KIPIGO KIKALI TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI
POLISI TAYARI WAMEUCHUKUA MWILI WA MAREHEMU DANIEL  HABARI KAMILI MBEYA YETU ITAZIDI KUKUJUZA KWANI BADO TUPO ENEO LA TUKIO

PICHA NA KAMANGA WA MBEYA YETU
MNAMO TAREHE 08.02.2013 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO KATIKA MTAA WA ITIJI KATA YA ITIJI JIJI NA MKOA WA MBEYA. DANIEL S/O MWASALEMBA,MIAKA 18,KYUSA,MKULIMA MKAZI WA ITIJI ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA  KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI UPANDE WA KUSHOTO NA  PETER S/O BOSCO,MIAKA 25,MFIPA,MPIGA DEBE,MKAZI WA ITIJI. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA  UKIWA UCHI KANDO YA BARABARA. CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI BAADA YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA KUMGOMBEA MWANAMKE ELIZABETH D/O MICHAEL, MIAKA 18,KYUSA,MUUZA POMBE ZA KIENYEJI KATIKA KILABU KIITWACHO MUSOMA MKAZI WA ITIJI. KABLA YA TUKIO MAREHEMU NA MTUHUMIWA AMBAO WOTE WALIKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA ELIZABETH D/O MICHAEL WALIPIGANA KILABUNI HAPO TAREHE 07.02.2013 MAJIRA YA SAA 21:00HRS WAKIMGOMBEA MWANAMKE HUYO KISHA KUAMULIWA NA WATEJA WENGINE NA MTUHUMIWA ALIONDOKA NA MWANAMKE HUYO HADI NYUMBANI KWA MWANAMKE NA KUANZA KUMPIGA.  
 HATA HIVYO ELIZABETH D/O MICHAEL  ALIFANIKIWA KUKIMBIA NA KURUDI KILABUNI AMBAPO ALIKUTANA NA MAREHEMU NA KUMWELEZA TUKIO HILO  AMBAYE WALIKUBALIANA  KURUDI WOTE NYUMBANI KWA MWANAMKE HUYO. MAJIRA YA SAA 01:30HRS MTUHUMIWA PETER S/O BOSCO ALIRUDI NYUMBANI KWA ELIZABETH D/O MICHAEL NA KUMKUTA MWANAMKE HUYO  AKIWA NA MAREHEMU CHUMBANI HIVYO ALIWAFUNGIA  MLANGO KWA NJE NA KWENDA KUTAFUTA KISU NA ALIPORUDI ALIVUNJA MLANGO KISHA UGOMVI BAINA YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA ULIANZA UPYA NA MTUHUMIWA ALIMCHOMA MAREHEMU KISU KIFUANI  UPANDE WA KUSHOTO  NA KUSABABISHA MAREHEMU KUDONDOKA CHINI HUKU DAMU NYINGI ZIKIMTOKA NA  MTUHUMIWA KUTOWEKA.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI ZAIDI. MTUHUMIWA PETER S/O BOSCO AMEKAMATWA KWA USHIRIKIANO BAINA YA POLISI NA WANANCHI WA ENEO HILO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI KWA KOSA LA MAUAJI. AIDHA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUGOMBEWA  ELIZABETH D/O MICHAEL  ANAENDELEA  KUHOJIWA  POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI. AIDHA ANATOA RAI KWA WENYE  NDOA/MAHUSIANO  YA KIMAPENZI KUWA WAAMINIFU KWA WENZI WAO ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA NA PINDI WANAPOKUWA NA MIGOGORO/MATATIZO WATUMIE NJIA YA MAZUNGUMZO KUMALIZA/TATUA MATATIZO/MIGOGORO  YAO.


[DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MNAMKUMBUKA MWANAMKE ALIYEMLISHA MTOTO KINYESI NA KUSABABISHA MKONO WA MTOTO HUYO KUKATWA, HUKUMU YAKE TAREHE 18/2/2013

WILVINA MKANDALA  AKIWASONYA NA KUWAKEJELI WAKAZI WAMAJENGO MBEYA WALIOKUJA KUSIKILIZA KESI YAKE KWA KUWAAMBIA MMEACHA KUKAA MAJUMBANI MWENU MMEKUJA KUFUATA UMBEYA TU NIACHENI KUNIFUATAFUATA HUKUMU YA WILIVINA MKANDALA ITATOLEWA  TAREHE 18/2/2013

BAADHI YA WAKAZI WA MAJENGO NA WAANDISHI WA HABRI WAKIMSHANGAA WILVINA  MKANDALA
MAHAKAMANI HAPO JANA


WILVINA MKANDALA SASA NI MJA MZITO

SIKU YA HUKUMBU MBEYA YETU ITAKUWEPO MAHAKAMANI

PICHA NA Jem
KIHUMBE WATOA ELIMU YA AFYA NA USHAURI NASAHA KUHUSU UKIMWI. SOKONI TANDALE MJINI TUKUYU WILAYANI RUNGWE
 
DADA BETH AKIWA KAZINI ANASUBIRI WATEJA WA KUPATA USHAURI WA AFYA MIE NILIKUWA MOJA WAPO WA KUPATA SHULE

RAS, MFANYA BIASHARA WA MAEMBE ANASEMA BIASHARA YA MATUNDA NDIO IMEMFANYA ASOMESHE WATOTO NA KUJENGA NYUMBA ANAAWAASA VIJANA KUTOKAA VIJIWENI KUPIGA KETE NA ULEVI

SOKONI LEO TANDALE TUKUYU MJINI

BEI NAFUU KIASI HIKI LAZIMA KILA MTU APATE KIASI SINIA LOTE 1200/=

WADAU WAUSAFIRI WA BODABODA TUKUYU MJINI WILAYANI RUNGWE WAKISUBIRI WATEJA


DUKA LINALOTEMBEA NO VAT WALA USHURU HAPO

LEO AJABU SANA NIMEKUTANA NA RAFIKI YANGU PATRICK HAJALEWA? MAANA SIKU HIZI?

ELIMU POPOTE IPO CHA MSINGI KUONGEZA UAMINIFU TU ILI TUWE SALAMA

KUTOKANA NA MITANDAO NET KUWA CHINI SANA NIMEJIGUNDULIA MIE OFISI YANGU KUWA GHOROFANI

HIKI KILINGE KIPO TUKUYU WE ULIZA LAX KWA DAUDI TU

LEO NIMEKUTANA NA RASHID MKWINDA MWANDISHI WA HABARI, MITAA YA NYAMA CHOMA MAENEO YA LAX
KARIBU NYAMA JAPO SIKU MOJA MOJA UNAPATA HII KITU

WAKAZI WA DSM HIZO NDIZI ZINAKUJA HUKO SAFARI INAANZA LEO USIKU HUKU MKUNGU MMOJA NI TSH 1500.


KARIBUNI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA MJIONEE MAAJABU YA MUNGU

ZIWA KISIBA (MASOKO) WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA
ZIWA NGOSI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA. KATI YA MAAJABU KUMI NA TISA YANAYOPATIKANA WILAYANI RUNGWE MAYA MAZIWA NI SEHEMU YA MAAJABU YALIYOAINISHWA KAMA SEHEMU KUU YA UTALII. MAZIWA HAYA YAPO JUU YA MILIMA NA HAYANA SEHEMU YA KUINGILIA MAJI WALA MAJI KUTOKA HATA KUPUNGUA KWA KINA CHA MAJI WALA KUONGEZEKA

No comments: