Tuesday, February 12, 2013

MWANAMKE ATIMULIWA KWA KUTUHUMIWA NI MCHAWI ILOLO MBEYA



Zainabu Zuberi mwenye kitambaa cheusi kichwani akiongozana na askari kanzu pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuokolewa na askari hao eneo la tukio ili asishambuliwe na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kuwa ni mchawi


Zainabu Zuberi akituhumiwa kuhusika na ushirikina.


 Mume wa Mtuhumiwa huyo Sulemani Rubea(49) amekataa mke wake kutuhumiwa kwa ushirikina ambapo aliwatupia lawama wanakijiji kwa madai kuwa wanaendekeza udini na kutopenda maendeleo na ndiyo maana hawawataki mtaani hapo.

Moja ya askari akipata maelezo kwa mama aliyepotelewa na mtoto wake katika mazingira ya kutatanisha wiki mbili zilizopita mpaka sasa hajapatikana mtoto huyo





Wananchi hao kwa pamoja waliazimia kumhamisha Mwanamke huyo Mtaani hapo katika mkutano ulihudhuriwa na wakazi zaidi ya 200 ambao walidai kuchoshwa na hali hiyo.


Hii ndiyo nyumba anayoishi anaetuhumiwa kwa uchawi ilolo Mbeya


 Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Kulaba Ngambi amesema wananchi walikuwa wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo ili aendelee kuishi mtaani pale ili hali wao hawamtaki mtaani hapo.

Wananchi wa Mtaa wa Ilolo Kata ya Manga Jijini humo kumfukuza mtaani hapo Mwanamke anaye fahamika kwa jina la Zainabu Zuberi akituhumiwa kuhusika na ushirikina.

Wananchi hao ambao awali walitaka kujichukulia hatua mkononi kwa kumpiga na kumchomea moto nyumba yake mtuhumiwa huyo walidai kuchoshwa na maovu yanayofanywa na mwanamke huyo.
Baadhi ya matendo ya kishirikina wanayomtuhumu mwanamke huyo kuhusika nayo ni pamoja na kujigamba kuwamaliza wanakijiji hao kwa kuwaloga ikiwa ni pamoja na kuwaloga watoto wao kitu ambacho wanasema kimeshatokea.
Wamedai kuwa mwanamke huyo amekuwa akiwagusa wanawake wajawazito na mimba zao huharibika ambapo pia wanafunzi wanaotoka katika mtaa huo wakifika Shule hushindwa kuona kabisa matukio ambayo mwanamke huyo anahusishwa. 
Walisema mwanamke huyo anatuhumiwa kujihusisha na matukio ya kishirikina tangu ahamie mtaani hapo takribani miaka mitatu ambapo walisema wakazi hao walimwonya mapema kuhusu tabia hiyo baada ya kufuatilia historia ya maeneo aliyowahi kuishi.  
Kwa upande wake Mume wa Mtuhumiwa huyo Sulemani Rubea(49) amekataa mke wake kutuhumiwa kwa ushirikina ambapo aliwatupia lawama wanakijiji kwa madai kuwa wanaendekeza udini na kutopenda maendeleo na ndiyo maana hawawataki mtaani hapo.
Rubea ameongeza kuwa mtaani hapo hawapendi mtu wa dini ya nyingine kujenga eneo hilo jambo ambalo lilipingwa vikali na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kumjadili mtuhumiwa huyo.
Awali mume wa mtuhumiwa huyo alikiri kuhama nyumba na mitaa zaidi ya kumi ambapo lisema maeneo mengine alikuwa amejenga lakini sehemunyingine alikuwa amepanga tu ingawa aligoma kusema sabbu inayomfanya ahame maeneo hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Kulaba Ngambi amesema wananchi walikuwa wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo ili aendelee kuishi mtaani pale ili hali wao hawamtaki mtaani hapo.
Amesema baada ya kuona wanachi wamepagawa na kutaka kujichukulia hatua mkononi ili mlazimu kuitisha mkutano wa hadhara ikiwa na kuitaarifu jeshi la polisi ambalo lilifika mapema eneo la Mkutano na kwatuliza wananchi wasifanye lolote ambapo Askari hao waliondoka na mtuhumiwa.
Aidha katika mkutano huo wananchi hao kwa pamoja waliazimia kumhamisha Mwanamke huyo Mtaani hapo katika mkutano ulihudhuriwa na wakazi zaidi ya 200 ambao walidai kuchoshwa na hali hiyo.
Matukio kama hayo yanayoashiria vitendo vya kishirikina ni pamoja na tukio la hivi karibuni la watu wawili kuzikwa wakiwa hai wakituhumiwa kuhusika na vitendo hivyo viovu ndani ya jamii.
 Na Mbeya yetu

Inasikitisha sana! Mwanafunzi auawa,anyofolewa viungo Wwilayani Kyela mkoani Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Abbas Kandoro.
MWANAFUNZI wa darasa la sita Shule ya Msingi Kasumulu, Kata ya Ngana, wilayani Kyela, Kaselema Mpale (14)  ameuawa kikatili kwa kuchinjwa na kitu chenye ncha kali, kisha kunyofolewa baadhi ya viungo vyake sehemu ya mwili.
Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Lucia Kamnyonge alisema tukio hilo lilitokea     Februari 8, mwaka huu saa 1:30 usiku, alipotumwa na baba yake kwenda nyumba ya jirani kuchukua mpunga ambao ungetumika kwa chakula usiku.
Kamnyonge alisema mtoto wake hakupatikanika hadi alipokutwa siku ya pili yake, akiwa amechinjwa na kunyofolewa baadhi ya sehemu zake za mwili ambazo ni pua, mdomo, jicho, kuondolewa sehemu zake za siri na kuchunwa ngozi ya kichwa karibu na utosi na mwili wake kutundikwa juu ya mti.
Aliendelea kuwa baada ya hali hiyo taarifa ilipelekwa ofisi ya serikali ya kijiji, uliitishwa mkutano wa wananchi wote na walitawanyika kuanza  kumtafuta mtoto huyo bila ya mafanikio.
Baadaye, baba yake alimkuta juu ya mti akiwa ametundikwa kichwa chini miguu juu na viungo vyake hivyo vikiwa vimenyofolewa.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ibungumbati lilipotokea tukio hilo, Adam Mkese alidai tukio hilo limewashtua na kwamba, mkutano wa kijiji ulioitishwa kwa dharura wananchi walimhusisha baba mzazi wa mtoto huyo na mauaji hayo.
Mkese alidai watu wa kijiji hicho walimhusisha kutokana na mazingira tata ya kifo chenyewe na maelezo ya kujichanganya aliyoyatoa.
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Naomi  Charles alidai kuna dalili za mzazi huyo kuhusishwa na mauaji hayo na kwamba, polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho,  Baruti Mwakasala alidai kuwa hali katika kijiji hicho siyo nzuri na kushukuru polisi kwa hatua za haraka walizochukua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kukiri kumshikilia baba mzazi wa mtoto huyo kwa uchunguzi zaidi. 
Mwananchi
 

JK.awatambulisha WajuMBe wa Kamati Kuu Dodoma

8E9U8863 a62b3
Mwenyekiti wa CCm Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM nje ya ukumbi wa White House,Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo
 

Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya Serengeti- nI MAAJABU SABA YA ASILI


 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders Bw. Philip Imler. 
Tanzania imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti, hafla hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabalozi, Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika picha kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na Lynn Imler mmja wa wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates  muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu saba ya
asili ya Afrika iliyofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha.
Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kama vinavyoonekana.
Wadau kutoka TTB ambao pia walikuwa ni miongoni mwa wanakamati ya maandalizi wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Dk. Aloyce Nzuki akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini Mchungaji Msigwa, Kushoto ni Mh Shah kutoka Mafia na mmoja wa wajumbe wa bodi ya Utalii TTB.
Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakiwa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria pia.
Mbunge Mh. James Lembeli akisalimiana na Bw. Mike Teyrol walipokutana katika hafla hiyo.
Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bi Devitha Mdachi akiwa pamoja na maafisa wengine wa bodi hiyo wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi katikati ni msaidizi wake Bw. Miskanji.

Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Mkurugenzi wa Hifadhi za taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiwasikiliza wabunge waliohudhuria katika hafla hiyo kulia ni Deo Filikunjombe na kushoto ni David Kafulila.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Dk. Aloyce Nzuki wakati alipowasili kwenye hoteli ya Maount Meru kwa ajili ya utoaji tuzo hizo.
Mama Tunu Pinda wa pili kutoka kushoto akiwa katika hafla hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk Aloyce Nzuki na katikati ni Lynn Imler kutoka Seven Natural Wonders.
Mabalozi mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo wa kwanza kutoka kulia ni Balozi Mutinda Mutiso Balozi wa Kenya Nchini Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Bw. Godbless Lema  kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB)  Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla hiyo.
Bw Allan Kijazi kushpto akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi tuzo ya Hifadhi ya Ngorongoro Crates Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi  katika hafla hiyo, kushoto ni Philip Imler wa Seven Natural Wonders.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea katika hafla hiyo.
Muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.
 

UKIFIKA MBEYA TU? KARIBUNI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA MJIONEE MAAJABU YA MUNGU

ZIWA KISIBA (MASOKO) WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA
ZIWA NGOSI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA. KATI YA MAAJABU KUMI NA TISA YANAYOPATIKANA WILAYANI RUNGWE MAYA MAZIWA NI SEHEMU YA MAAJABU YALIYOAINISHWA KAMA SEHEMU KUU YA UTALII. MAZIWA HAYA YAPO JUU YA MILIMA NA HAYANA SEHEMU YA KUINGILIA MAJI WALA MAJI KUTOKA HATA KUPUNGUA KWA KINA CHA MAJI WALA KUONGEZEKA
 
MUONEKANO WA MLIMA RUNGWE

No comments: