Wednesday, February 13, 2013

MBEYA TENA. MFANYABIASHARA AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA WA BINADAMU ILOLO MBEYA


BARAKA KIBONA, MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIRI KUKUTWA NA KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU HAPA AKIWA NDANI YA GARI YA POLISI
MTUHUMIWA AKIPAKIWA NDANI YA GARI YA POLISI
HAYA MABOKSI INNASADIKIWA YALITAKIWA YAJAE HELA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA
BAADHI YA WANANCHI WA MTAA WA ILOLO WAKISHANGAA TUKIO HILO NYUMBANI ALIKOPANGA MTUHUMIWA HUYO


MNAMO TAREHE 12.02.2013 MAJIRA YA SAA 11:00HRS HUKO ENEO LA ILOLO JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WALIMKAMATA BARAKA S/O KIBONA,MIAKA 30,MNDALI,MFANYABIASHARA, MKAZI WA ILOLO AKIWA NA KIUNGO CHA BINADAMU SEHEMU YA KIGANJA CHA MKONO WA KULIA  NDANI YA NYUMBA YAKE .
MBINU ILIYOTUMIKA NI KUFICHA KIUNGO HICHO CHUMBANI NDANI YA BOX KWA KUZUNGUSHIWA KAMBA . MTUHUMIWA  ANAKIRI KUMILIKI  KIUNGO HICHO AMBACHO  ANADAI ALIPEWA NA MGANGA WAKE WA KIENYEJI KWA MADHUMUNI YA KUKITUMIA KIUNGO HICHO KWA AJILI YA  KUJIKINGA/KUJILINDA KATIKA BIASHARA ZAKE ZA KIMACHINGA ZISICHUKULIWE  KWA NJIA YA KISHIRIKINA IKIWA NI PAMOJA NA FEDHA ZAKE. 
TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUSADIKI IMANI ZA KISHIRIKINA  KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAFANYE KAZI ZAO KWA BIDII KWA KUMCHA MWENYEZI MUNGU KUPITIA IMANI ZA DINI ZAO. 
AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII KUENDELEA KUUCHUKIA UHALIFU KWA KUWAFICHUA WAHALIFU NA UHALIFU KATIKA MAMLAKA HUSIKA UNAOJITOKEZA KATIKA  MAENEO YAO.
      Signed by
[B.N.MASAKI -SSP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MBEYA

Aliyemuua Osama aibuka

Osama bin Laden  

RISASI tatu zilimmaliza Osama bin Laden na kuandika historia.Karibu miaka miwili sasa, baada ya kimya na siri ya namna mauaji hayo yalivyofanyika, siri iliyofichwa imewekwa wazi kuhusu namna Osama alivyowapa kiwewe askari waliomvamia nyumbani kwake ambao walishindwa kumkamata akiwa hai tofauti na dhamira ya awali.
Askari aliyetekeleza mauaji hayo, tayari amefunguka na kueleza kwamba mshtuko alioupata alipokutana uso kwa uso na kiongozi huyo ulimsukuma kutekeleza mauaji yake.

“Nilimpiga risasi tatu. Nilimshuhudia akiwa amekufa ulimi nje. Nilimwona namna alivyokuwa akikata pumzi yake ya mwisho. Niliuliza akilini: Hivi hili ni jambo jema au ni jambo baya kabisa kuwahi kulifanya katika maisha yangu?”anaeleza askari huyo.

Askari huyo ambaye alipewa jina la the Shooter “mdunguaji” amesema hawakuwa na uhakika wa kumshinda, hadi walipofanikiwa kumtia nguvuni akiwa chumbani kwake katika uvamizi uliofanyika usiku wa manane.

Operesheni hiyo ilifanyika Mei 2, 2011 baada ya maandalizi yaliyowawezesha askari sita wa Marekani kumvamia kiongozi huyo wa kikundi la Al Qaeda aliyekuwa akisakwa kwa gharama zote na Marekani akiwa katika makazi yake huko Jalallabbad, Pakistan.



BEYA CITY YAICHABANGA POLISI IRINGA 2-0





Waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakiwa makini kuangalia mechi hiyo


mashabiki wa timu ya Mbeya city wakishangilia ushindi wa mabao mawili dhidi ya polisi Iringa

Mkuu wa Wilaya Rungwe ndugu Crispin Meela. akiongea na waandishi wa habari mara baada ya mpira kwisha
Timu ya Mbeya City inayocheza Ligi daraja la kwanza Tanzania bara, imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kupanda daraja kwa kushiriki ligi kuu msimu ujao baada ya kuichapa timu ya Polisi Iringa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Katika msimamo wa ligi daraja la Kwanza timu ya Mbeya City ina Pointi 22 na ndiyo inayoongoza kundi A ikifuatiwa na Polisi Iringa iliyo na Pointi 14, hivyo Mbeya City ikishinda mechi mbili kati ya nne zilizobaki itashiriki ligi kuu msimu ujao
Na mbeya yetu.
 
 

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NGUVU ZA ATOMIKI DUNIANI (IAEA) YUKIYA AMANO WAZINDUA JENGO JIPYA LENYE VIFAA VYA KISASA KUSHUGHULIKIA MAGONJWA YA KANSA NCHINI

Picha na 1 
Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akikata utepe kwa kushirikiana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki  Duniani Yukiya Amano (wa pili kutoka kushoto) kuashiria uzinduzi rasmi wa  jengo jipya lenye  vifaa vya kisasa kwa ajili ya  kuwahudumia wagonjwa wa kansa katika Taasisi ya Kansa leo Ocean Road jijini Dar es salaam. Wengine ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kansa Ocen Road Prof. Twalib Ngoma (wa tatu kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid.
Picha na 2 
Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwaonyesha wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo jipya la kuwahudumia wagonjwa wa kansa  katika Hospitali ya Kansa Ocean Road  kitabu cha Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti na kupambana na Kansa nchini.
Picha na 3 
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania lenye uwezo wa kuhudumia wa 257 kwa gharama ya shilingi bilioni 7.2 huku Shirika la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) likichangia mashine 2 za kutambua sehemu zilizoathiriwa na ugonjwa wa kansa katika mwili wa binadamu zenye uwezo wa kuhudumia wagonjwa 1600 kila moja kwa mwaka.
Picha na 5 
Baadhi ya wataalam wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road  wakiwa ndani ya moja ya chumba cha  jengo jipya lililozinduliwa jijini Dar es salaam chenye moja ya mashine yenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa 1600 kwa mwaka. Mashine hiyo imetolewa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA).
Picha na 6Sehemu ya nje ya jengo jipya la Taasisi ya Kansa ya Ocean Road lenye vifaa vya kisasa lilozinduliwa leo jijini  Dar es salaam.
Picha no 4Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki  Duniani Yukiya Amano akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  jijini Dar es salaam mara baada ya kuzinduliwa kwa jengo jipya la Taasisi ya Kansa Ocean Road lililojengwa na serikali ya Tanzania huku  shirika hilo likitoa msaada wa mashine mbili kwa za kutambua athari za ugonjwa wa kansa kwenye mwili wa binadamu.

No comments: