akipelekwa chumba cha kusikilizia kesi yake |
Mtuhumiwa wa mauaji hayo Pacificus Cleophace Simon akiwasili mahakamani |
akielekea mahabusu ya mahakama ya mkoa wa Iringa |
akielekea katika chumba hicho |
Katika pozi zake tofauti huku akisindikizwa na askari huyu |
bado hataki sura yake itambuliwe kirahisi |
Akitolewa mahakamani |
akirudi mahabusu |
mwili wa marehemu Mwangosi ukikanywagwa na askari waliokuwa wakimsaidia mwenzao aliyejeruhiwa kwa bomu lililomuua Mwangosi
ASKARI kikosi cha kituliza ghasia (FFU )mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi kupandishwa tena kizimbani leo katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa.
ASKARI kikosi cha kituliza ghasia (FFU )mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) anayetuhumiwa kumuua aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi kupandishwa tena kizimbani leo katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa.
Mtuhumiwa huyo leo anatarajia kufikishwa tena mahakamani huku tayari mahakama hiyo chini ya hakimu
Dyness Lyimo ikiwa imetoa onyo kwa askari waliomfikisha mahakamani
hapo mara ya mwisho kutokana na kitendo cha kuidharau mahakamani hiyo
kwa kumtoa mtuhumiwa huyo ndani ya chumba cha mahakama kabla ya shughuli
za mahakama kuhitimishwa .
Askari
hao na mtuhumiwa walionyesha kuidharau mahakamani hiyo kwa kumtoa
mtuhumiwa huku mahakama ikiwa inaendelea na kupelekea hakimu kumwagiza
wakili wa serikali kuwafuata askari hao na mtuhumiwa ili kurudi ndani ya
chumba hicho na kuwahoji askari hao kwa kitendo walichokifanya kabla ya
kuomba msamaha .
Kesi hiyo namba namba 1 ya mwaka 2012 ya mauwaji hadi sasa mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo zaidi ya mara nne na kesi hiyo ikiendelea kutajwa .
Kesi hiyo namba namba 1 ya mwaka 2012 ya mauwaji hadi sasa mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo zaidi ya mara nne na kesi hiyo ikiendelea kutajwa .
Mtuhumiwa
huyo anatuhumiwa kumuua kwa kwa bomu aliyekuwa
mwandishi wa habari wa Chanel Tena mkoa wa Iringa
marehemu Mwangosi septemba 2 Septemba mwaka jana katika kijiji cha
Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa wakati wa vurugu kati
ya polisi na wafuasi wa Chadema .kinyume na kifungu cha sheria
namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai,
sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,
- Iringa
ccm na gesi ya mtwara
1. Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea maelezo ya Serikali kuhusu maandamano na vurugu zilizotokea Mkoani Mtwara tarehe 27 Desemba, 2012 tarehe 25 Januari, 2013 na tarehe 26 Januari, 2013. Maandamano na vurugu hizo zilizodaiwa kuwa na lengo la kupinga mradi wa bomba la Gesi kujengwa na kupeleka Gesi Dar es Salaam.
2. Baada ya kupokea maelezo haya ya Serikali, Halmashauri Kuu ya Taifa imebaini kuwa: -
(a) Kwa sehemu kubwa Wananchi wa Mkoa wa Mtwara hawakuwa wamepewa elimu ya kutosha juu ya uendelezaji wa Gesi na jinsi watakavyonufaika.
(b) Baadhi ya Wanasiasa na baadhi ya Viongozi wa Makundi mbalimbali waliamua kutomia suala la Gesi kupandikiza lugha za chuki, uchochezi na upotoshaji wa maendeleo ya Mradi wa Gesi kwa lengo la kujitafutia umaarufu.
(c) Suala la Gesi limetumika kama kisingizio tu cha kufanya vitendo vya rurugu na uvunjifu wa amani.
3. Kutokana na ukweli huu, Halmashauri Kuu ya Taifa inaelekeza ifuatavyo:-
(i) Imesikitishwa na vurugu zilizotokea na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha na uharibifu mkubwa wa mali na majengo ya CCM, Serikali, Wabunge na watu binafsi. Halmashauri Kuu ya Taifa inawapa pole wafiwa na waliopoteza mali zao.
(ii) Inaiagiza Serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu waliofanya vurugu na uharibifu mbalimbali na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria. Pia, kuwa makini na kuhakikisha matukio kama haya hayajitokezi tena.
(iii) Inaiagiza Serikali kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi wa maeneo husika kuhusishwa na kuelimishwa juu ya miradi mbalimbali kwenye maeneo yao.
(iv) Halmashauri Kuu ya Taifa inawataka Wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kuishi kwa amani na utulivu kama ilivyo desturi yao, maana vurugu pamoja na kuharibu mali na kugharimu maisha vinaweza kuwakimbiza wawekezaji waliojitokeza na ambao shughuli zao zitawafaidisha wananchi wa Mkoa huu na Watanzania kwa ujumla .
HALMASHAURI KUU YA TAIFA
Dodoma 10 – 11 Februari,2013
Dhahabu Ikiisha Tutawapeleka Wapi Wafanyakazi Wetu?
Mikataba ya kuchimba dhahabu hapa nchini ilianza kusainiwa na serikali ya awamu ya tatu ya Mzee Benjamen William Mkapa; mikataba hii imesainiwa katika taratibu na mazingira ya kifisadi kwa vile kwanza muda wa mikataba ni miaka 99 na murahaba wa asilimia tatu (3%), mikataba ya aina hii haipo popote pale duniani zaidi ya hapa kwetu Tanzania! Sasa mimi najiuliza kwamba hivi Mkapa alikuwa anafikiria nini kusaini mikataba ya asilimia tatu tena kwa kipindi cha miaka 99 wakati alikuwa anajua kwamba yeye amechaguliwa kwa kipindi cha...
miaka 10 tu! Je, alijiona kwamba amepata wawekezaji wajinga sana kiasi kwamba wamekubali
kutoa asilimia tatu hivyo aliona akiwaachia hawawezi kupatikana tena!? Na ndiyo maana akaona
madhali wamekubali kusaini mikataba basi asiwape nafasi bali awagandamize kwa kuwapa
mikataba ya miaka 99! Mimi ninavyooona hata hiyo asilimia tatu hatuipati kulingana na hali
halisi ya ufisadi uliopo hapa nchini, kama kuna kitu tunachopata kutoka katika mikataba hii
ya kifisadi ya dhahabu haiwezi kuzidi nusu asilimia kwa mwaka (0.5%)! Ni kwanini Mkapa
asingelisaini mikataba hata ya zero point one percent (0.1%) lakini iwe mkataba wa miaka 10 tu!
Tukiachana na mambo ya asilimia (murahaba) ambayo nitayachambua baadae katika makala
hii, ningependa nijaribu kuzungumzia hujuma zinazofanywa katika migodi yetu; migodi yetu
ya dhahabu inafanyiwa hujuma ambazo huwezi kuamini kama nchi hii kweli ina wenyewe, na
hata kama wapo wenyewe lakini hawapo hai bali watakuwa wameshakufa! Nasema hivyo kwa
vile kulingana na taratibu za uchumbaji wa madini duniani, hasa tukijifunza kutoka kwa nchi
kiongozi wa uchumbaji wa madini duniani ya Afrika ya Kusini; mgodi wa madini ya aina yoyote
ile ni lazima uwe umeajiri wafanyikazi ambao hutekeleza majukumu mbali mbali katika mgodi
huo kulingana elimu au ujuzi waliokuwa nao, hawa wote ni wafanyikazi ambao wanautegemea
mgodi huo kwa ajili ya kupata mishahara na kutunza familia zao; baadhi ya wafanyikazi ni
vijana ambao hawana familia na wengine ni watu wazima ambao wana familia zinazowategemea
ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto, matibabu, kuwalisha na kuwavalisha, hivyo jinsi
shughuli za mgodi zinavyodumu kwa muda mrefu ndiyo ambavyo wafanyikazi wanavyoishi
maisha mazuri ikiwa ni pamoja na kuzimudu familia zao. Kwa serikali yoyote ile makini lazima
ihakikishe kwamba inalinda ajira za wananchi wake kwa kuhakikisha kwamba umri wa mgodi
unadumu kwa muda mrefu kadri inavyowezekana ili kuendelea kutoa ajira kwa wafanyikazi
MAHAKAMA KUU INAYOENDELEA NA KIKAO CHAKE MBOZI YAMHUKUMU KUNYONGWA HADI KUFA MSHTAKIWA
Mahakama kuu kanda ya Mbeya
imemhukumu PETER MWAFRIKA mkazi wa Ndolezi wilayani Mbozi kunyongwa
hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuua kwa kukusudia.
Akisoma hukumu hiyo iliyochukua saa
1.30 Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya mbeya NOEL CHOCHA amesema
licha ya mikono ya mahakama kufungwa kutoa adhabu ndogo kwa kosa la maauaji ya
kukusudia, pia adhabu hiyo ni hatua ya kukomesha watu wenye tabia kama za
mtuhumiwa kujichukulia hatua mikononi mwao.
Akirejea mazingira ya kesi hiyo jaji
Chocha amesema mnamo Februaly 11,2010 mshatakiwa na wenzake watatu walifanya
kosa la mauaji ya kukudia chini ya kifungu 196 chasheria ya mwenendo wa makosa
ya jinai kwa kumuua KOSAM MWAFRIKA ambaye ni kaka wa marehemu
katika kijiji cha Shaji kwa kumkata koromeo na kulitenganisha vipande viwili.
Jaji Chocha katika maelezo yake
alisema mshtakiwa akiwa na wenzake ambao walitoweka baada ya mauaji hayo
walimvamia Kosam akiwa na mkewe shambani kwake eneo la Zanzule, Ndolezi na
kisha kumkamata marehemu kwa maelezo kuwa walikuwa wametumwa kumkamata ili
wampeleke polisi kwa kosa la wizi wa Ng'ombe.
Hata hivyo katika mabishano shambani
hapo, marehemu na wenzake walitamka wazi kuwa walikuwa wametumwa kumuua
marehemu hivyo kuongeza nguvu za ushahidi wa kumtia hatiani.
sababu za mauaji hayo ni ugomvi wa
muda mrefu uliokuwepo kati ya marehemu na mama yake mzazi wa mshtakiwa ambao
walikuwa wakigombea ardhi,(wote ni ndugu) na kwamba siku moja kabla ya tukio
hilo kulikuwa na kesi katika mahakama ya mwanzo Mlowo iliyokuwa imefunguliwa na
Mama mzazi wa mshatakiwa.
Inaelezwa pia kuwa wakiwa njiani
kumpeleka polisi, baada ya kubaini kuwa kuna watu wanawafuatilia ghafla
mtuhumiwa mwingine (ambaye hakuwepo mahakamani) alimkata marehemu panga la
shingo na kumfanya marehemu akose nguvu na kuanguka, hata hivyo kwa kuonyesha
kutoridhika na hali hiyo mtuhumiwa aliongezea kwa kumkata marehemu na panga
kwenye koromeo na kulitenganisha kabisa.
Jaji kabla ya kutoa hukumu alirejea
mazingira ya tukio hilo na kujiridhisha na miongozo, viini vya shauri la mauaji
na hoja zilizotolewa na washauri wa mahakama ambapo ilithitika kuwa kulikuwa na
dhamira ya mauaji na tendo la mauaji lilifanyika
Katika ushahidi wa shauri hilo jumla
ya mashahidi watatu waliletwa mahakamani akiwemo kaka wa mshtakiwa ambao wawili
kati yao walithibitisha pasipo shaka kwamba mshtakiwa Peter kuhusika na
tukio la kumuua kwakukusudia Kosam .
Katika utetezi wake wakili wa
mshtakiwa ZAKIA SULEIMAN aliiomba mahakama impe adhabu nafuu mshtakiwa kutokana
na umri wake mdogo hivyo mchango wake kuhitajika katika ujenzi wa taifa, pamoja
na kuwa na wategemezi wakiwemo wake wawili na watoto wane.
Serikali iliwakilishwa na Wakili
Rogers Francis
katika hatua nyingine jaji Chocha
aliamua kufanya kazi ya kutoa elimu mahakamani humo, akirejea matukio
yaliyojitokeza hivi karibuni wilayani Momba na Mbozi aliyoyaita ni yanafanywa
na watu wasiopenda ama hawana habari na Utawala wa sheria yakiwemo kuwazika
watu wakiwa hai, ambapo amesisitiza hali hii inaonyesha kuwepo kwa watu
waliovuka kiwango cha ukatiri katika jamii.
amesema hali ya kushamiri mauaji wilaya za Mbozi na
Momba kuhaonyesha namna jamii na watu wenye tabia kama za mshitakiwa
wasivyopaswa kuvumilika mbele ya sheria na kwamba adhabu hiyo itasaidia
kuwaelimisha wengine wenye mitazamo kama ya mshtakiwa Peter Mwafrika.
Habari kwa hisani ya Danny Tweve Mbozi
Finland yataka nchi ilinde matumizi ya maliasili
BALOZI wa
Finland nchini, Sinikka Antila, amewetaka viongozi wa Tanzania kusimamia
vizuri matumizi ya maliasili kutokana na maliasili hizo, kuwa ndiyo
ufunguo wa ukuaji wa maendeleo ya nchi.
Antila
alitoa kauli hiyo, jijini Dar es Salaam jana, wakati wa mkutano
uliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi, kwa ajili ya uzinduzi wa Jukwaa la
Uchumi wa Kijani, uliowakutanisha viongozi wa taasisi mbalimbali
kujadili ushirikishwaji wa jamii katika kusimamia ukuaji wa uchumi.
LOWASSA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUREJESHA AMANI KATI YA WAISLAMU NA WAKRISTOWAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, amewataka viongozi wa dini nchini kusaidia kurejesha hali ya amani kati ya Waislamu na Wakristo ambayo inaonekana inaanza kupotea. Akizungumza nyumbani kwake Monduli, wakati akipokea ujumbe kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa alisema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buseresere mkoni Geita yanasikitisha sana na kuongeza kuwa ni dalili mbaya ya kutoweka kwa amani ya Tanzania. ``Rais ameelezea masikitiko yake, kwa kweli inasikitisha sana, mimi nawaomba viongozi wa dini na madhehebu yote wasimamie kuzuia mambo haya, nawaomba Watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu isipotee,” alisema. Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, aliongeza kuwa Watanzania wameoleana, wamekuwa wakiishi pamoja kwa miaka yote bila kubaguana kwa misingi ya dini, rangi wala kabila, na kuhoji haya mambo yanatoka wapi. Alisema kuwa Tanzania imekuwa ni mfano wa kuigwa kote dunia kutokana na amani iliyopo, ambayo ni matunda ya uongozi wa waasisi wa taifa hili hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Aman Karume. Katika fujo hizo za Buseresere, mchungaji mmoja wa kanisa aliuawa baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya Waislamu na Wakristo, chanzo kikiwa ni Wakristo kuamua kuchinja ng’ombe na kuuza kwenye bucha yao, hatua iliyopingwa na Waislamu. Ujumbe huo uliofika nyumbani kwa Lowassa uliongozwa na msaidizi wa askofu mteule wa KKKT dayosisi hiyo, ulimshukuru kutokana na kusimamia na kuendesha harambee ya ujenzi wa kanisa kuu la Shinyanga Januari mwaka jana ambapo zaidi ya sh milioni 200 zikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi zilipatikana. KATA, TARAFA, JIMBO BORA KWA USALAMA 2012 ZAPEWA TUZO
Na. Christina Mponji-Jeshi la Polisi, Dodoma.
………………………………………………………
Wito umetolewa kwa Majimbo,
Tarafa na Kata zote nchini kuimarisha dhana ya Polisi jamii na ulinzi
shirikishi katika maeneo yao, ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu
kuanzia ngazi ya familia ambako ndiko hasa chimbiko la uhalifu.
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini IJP Said Mwema, wakati akitoa tunuku ya hati ya
utendaji bora kwa Kata/Shehia, Tarafa, na Jimbo zilizofanya vizuri
katika mapambano dhidi ya uhalifu nchini kwa mwaka 2012.
Tuzo hizo zimetolewa katika
Mkutano Mkuu wa Maofisa wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaoendelea
mjini Dodoma katika ukumbi wa Pius Msekwa, ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa mpango wa maboresho ndani ya jeshi hilo.
Kata zilizofanya vizuri ni
pamoja na kata ya Bukwe Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, Kizwite ya
mkoani Rukwa, Isansa ya mkoani Mbeya, pamoja na shehia ya Ng’omeni
kutoka mkoa wa Kaskazini Pemba.
Tarafa zilizofanya vizuri ni
tarafa ya Girango ya mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, Lwiche ya mkoani
Rukwa, Igamba ya mkoani Mbeya pamoja na Jimbo la Mji Mkongwe la Mkoa wa
Mjini Magharibi visiwani Zanzibar ambapo tuzo hizo zimepokelewa na
makamanda wa mikoa hiyo kwa niaba ya kata/shehia na tarafa/majimbo yao.
IJP Mwema amesema, endapo kata
na tarafa zote nchini zitaimarisha dhana ya ulinzi shirikishi na polisi
jamii, ni wazi kuwa matukio ya uhalifu yatapungua kwa kiasi kikubwa na
hatimaye kuwa historia.
Akiongea katika hafla hiyo Mkuu
wa Huduma za Polisi Jamii, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Lazaro Mambosasa
alisema kuwa kata na tarafa zilizofanya vizuri, zilikuwa na kiwango
kikubwa cha matukio ya kihalifu lakini kupitia dhana ya ulinzi
shirikishi na polisi jamii wamefanikiwa kudhibiti vitendo hivyo huku
akitolea mfano kata ya Bukwe ambako kulikuwa na migogoro ya kikabila, na
hivi sasa migogoro hiyo imekoma kabisa.
Akiongea kwa niaba ya wenzake,
kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishna Msaidizi Diwani Athumani,
amesema jamii sasa imeanza kuelewa umuhimu wa kushirikiana na jeshi la
polisi katika mapambano dhidi ya uhalifu na kwamba wamekuwa mstari wa
mbele katika kuhamasishana juu ya uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi
shirikishi.
Jeshi la polisi limekuwa
likifanya jitihada mbalimbali za kuimarisha hali ya ulinzi na usalama
kuanzia ngazi ya kata/shehia, ambapo hivi karibuni wametoa pikipiki kwa
wakaguzi tarafa ili kuwarahisishia utendaji katika tarafa zao.
UKIFIKA MBEYA TU? KARIBUNI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA MJIONEE MAAJABU YA MUNGU
MUONEKANO WA MLIMA RUNGWE
|
No comments:
Post a Comment