Saturday, February 16, 2013

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE MKOANI MBEYA CHRISPIN MEELA AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA CHAI CHA METL NA KUJIONEA UFANYAJI KAZI WAKE

MASHAMBA YA CHAI YA GD ESTATE WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA YANA UKUBWA WA HEKTA 1,177 ZILIZOPANDWA CHAI JAPO UKUBWA WA SHAMBA LOTE LINALOMILIKIWA NA MWEKEZAJI METL NI HEKTA 3,277

KIWANDA CHA CHAI CHA MSEKELA KILICHO FUNGA TANGU MWAKA 2002 HADI SASA HAKIFANYIKAZI NA MIUNDOMBINU KUFA NA KUBAKI MAGOFU. KATIKA ZIARA HII MWEKEZAJI AMEAHIDI KUFIKA MWEZI MEI MWAKA 2013 MITAMBO MIPYA ITAANZA KUFUNGWA UPYA

KIWANDA CHA CHIVANJA KINACHOENDELEA NA UZALISHAJI KWA SASA WA CHAI



SWALI NI KWANINI MASHAMBA HAYAKO KATIKA HARI NZURI YA UTUNZAJI? MKUU WA WILAYA CHRISPIN MEELA  AKIMUULIZA MWEKEZAJI JIBU.. TUMEJIPANGA VYEMA KUBADIRI HALI HII ILI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAJANI MABICHI MASHAMBANI

MR KAKIKO DARDO WILAYA YA RUNGWE AKISIKILIZA KWA MAKINI MAELEZO YA MENEJA WA MASHAMBA

MR MZARA AFISA KILIMO WILAYA YA RUNGWE AKISIKILIZA MAELEZO YA MENEJA WA MASHAMBA YA CHAI KWA UMAKINI

WANANCHI WAKICHUMA CHAI KATIKA SHAMBA LA GD ESTATE

MAMA FARAJA AKIUZA CHAI YAKE ALIYOCHUMA KATIKA SHAMBA LA GD ESTATE

CHAI IKITOKA SHAMBANI TAYARI KWA KUANZA KUSAGWA

CHAI IKISUBIRIWA KUSAGWA

CHAI ILIYOSAGWA TAYARI

CHAI ILIYOTAYARI KWA KUSAFIRISWA TAYARI KUINGIZWA SOKONI KWA MLAJI

BAADA YA ZIARA YA MASHAMBANI NA KIWANDANI UKAWADIA MUDA WA KUJUA MENGI ZAIDI JINZI KUHUSU UTENDAJI WA KAZI KWA MUWEKEZAJI HUYO

MR GEORGE MWAMAKULA AMBAYE NI GROUP MANAGER - TEA AKITOA UFAFANUZI WA MASWALI YALIYOKUWA YANAULIZWA NA WANDISHI WA HABARI
MKUU WA WILAYA CHRISPIN MEELA AKIKABIDHIWA CIMENT TANI 10 SAWA NA MIFUKO 200  KWA AJILI YA UJENZI WA MADARASA YA SEKONDARI WILAYANI RUNGWE


MECHI YA KIRAFIKI KATI YA TUKUYU STARS BANYAMBALA NA PRISON YA MBEYA INAYOSHIRIKI LIGI KUU TANZANIA BARA
MUONEKANO WA RUNGWE

HEKAHEKA LANGONI MWA PRISON


TUKUYU STARS WAKIWA MAPUMZIKO

TIMU YA PRISON WAKIWA KATIKA MAPUMZIKO

DIWANI KATA YA KAWETELE NDUGU MWASAKILALI CHAMA CHA NCCR AKITOA ZAWADI YA MPILA KWAAJILI YA MAZOEZI KWA TIMU YA TUKUYU STARS

WADAU WA MICHEZO WILAYANI RUNGWE

MPAKA MWISHO WA MECHI PRISON 2 BANYAMBALA 0







MJANE ADHURUMIWA NYUMBA NA SERIKALI YA KIJIJI


Mjane Jerumana Nyinge 50 akiwa ndani ya kibanda chake alichotelekezwa na serikali ya kijiji
Hapo ndipo anapolala mjane huyo
Hivi ndiyo vyombo anavyotumia kupikia mjane huyo
Hiki ndicho kibanda alichopewa na serikali ya kijiji hii ni sura ya mbele ya kibanda hicho
Hii ni sura ya nyuma ya kibanda hicho
Humu ni ndani ya kibanda hicho kuna tundu kubwa kwenye paa la manyasi mvua ikinyesha mjane huyo hawezi kulala maana maji yote huingia ndani
Hakika mjane huyu anaitaji msaada angala nae apate bati choo godoro la kulalia na mahitaji mengine ya kibinadamu tunaomba tusaidiane kumsaidia mjane huyu
Mjane akiwa na jirani yake nnje ya kibada chake

Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Jerumana Nyinge [50] mkazi wa kitongoji cha Usafwani kijiji cha Kongolo Mswiswi Kata ya Mswiswi wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya amedhurumiwa nyumba na serikali ya kijiji hicho.
Hii imekuja baada ya Mwanamke huyo kutelekezwa kwenye kibanda cha nyasi kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu nyumba yake ya bati ibomolewe ili kupisha shughuli za kimaendeleo kijijini hapo kwa ahadi kwamba angeweza kujengewa nyumba nyingine  ya kuweza kuishi.
Mjane huyo ambaye hana watoto amejikuta akiishi kwa dhiki kwa kipindi chote cha masika  ambapo baadhi ya vitu vimeharibika kwa kunyeshewa na mvua kikiwemo chakula pamoja na kukosa mahali pa kulala 
 “Mume wangu alifariki mwaka 2007 na  kuanzia mwaka 2010  serikali ya kijiji imenihamisha  na kunileta hapa bila huduma  za msingi  kama maliwato na bafu ambapo nimekuwa nikijisetiri kwa majirani  na mara kadhaa wamekuwa wakinifukuza “ alisema mjane huyo.
 Kwa upande wake jirani wa mjane huyo  Bwana Mbwiga Mwayila amesema  kuwa mjane huyo amekuwa akiishi maisha hatarishi kutokana na umbali mrefu anaotembea kufuata huduma ya maliwato na hasa nyakati za usiku amekuwa akiwagongea kuomba msaada huo na kuwa  adha kwao kwa kuwakatisha usingizi .
 Bi  Salome Mwampashi ni jarani wa mjane huyo ambaye ameiomba serikali ya kijiji kumsaidia haraka mjane huyo ili kuepuka usumbufu kwa majirani huku akisema  ameshuhudia  mama huyo akipata taabu ya kupika wakati wa mvua kutokana na nyumba anayoishi kuvuja na moto kuzimika 
 Naye  mwenyekiti wa kijiji  hicho ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mswiswi bwa  Fulugence  Mhegele amekiri kubomolewa kwa nyumba ya mjane huyo ilikupisha ujenzi wa maduka na kuleta maendeleo ya kijiji  ambapo amefafanua hapakuwa na mapatano ya kulipa fidia  ingawa diwani huyo hakuonesha mhutasari wowote wa makubaliano hayo .

Na  Ezekiel Kamanga Mbarali

Kwa yeyote yule aliyeguswa kumsaidia mjane huyu  

piga simu namba hizi  Ezekiel Kamanga 0754 49 07 52

                                       joseph Mwaisango 0754 37 44 08

UKIFIKA MBEYA TU? KARIBUNI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA MJIONEE MAAJABU YA MUNGU

ZIWA KISIBA (MASOKO) WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA
ZIWA NGOSI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA. KATI YA MAAJABU KUMI NA TISA YANAYOPATIKANA WILAYANI RUNGWE MAYA MAZIWA NI SEHEMU YA MAAJABU YALIYOAINISHWA KAMA SEHEMU KUU YA UTALII. MAZIWA HAYA YAPO JUU YA MILIMA NA HAYANA SEHEMU YA KUINGILIA MAJI WALA MAJI KUTOKA HATA KUPUNGUA KWA KINA CHA MAJI WALA KUONGEZEKA
 
MUONEKANO WA MLIMA RUNGWE
 Photo
Photo

No comments: