VIONGOZI WA JUKWAA
LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA WAKITOA TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI MBEYA
|
HATIMAYE YAMETIMIA, MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha Wilvina Mkandara(24) kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya kumtesa hadi kumsababishia
Wilvina Mkandala (24) akitolewa mahakamani mara tu baada ya kusomewa hukumu ya kifungo cha maisha huku watu walio hudhuria Mahakamani hapo wakipunga mikono ishara ya kwaheri na huku Askali akicheka |
Baadhi ya wakazi wa majengo alikokuwa anaishi mtuhumiwa wakimsifu hakimu kwa hukumu aliyotoa kwa mtuhumiwa huyo |
kila aliyepita mbele ya kamela yetu alikuwa anatabasam kwa furaha bada ya kutolewa kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa |
Mtoto Aneth kabla ya kukatwa kwa mkono wake wa kushoto hapo ni siku alipokuwa na wasamalia wema akiwa katika hali mbaya na huku ameshika kinyesi kwa ajili ya kula ikiwa ni adhabu |
Mtoto Aneth mara baada ya kukatwa mkono wa kushoto kwa ujumla mtoto huyu anaendelea vizuri na alishatoka hospitalini
MAHAKAMA ya Wilaya ya
Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha Wilvina Mkandara(24) kutokana na kesi
iliyokuwa inamkabili ya kumtesa hadi kumsababishia ulemavu mtoto wa shemeji
yake.
Akisoma hukumu hiyo
Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo alisema mshakiwa amehukumiwa
kutokana na kifungu cha 235 cha mwenendo wa makosa ya jinai cha mwaka 1985.
Amesema Mahakama
inaweza kumtia hatiani mtuhumiwa kutokana na ushahidi wa mazingira au ushahidi
wa moja kwa moja ambapo alisema mshtakiwa anahukumiwa kutokana na ushahidi wa
mazingira kwa sababu mhangwa wa tukio hilo alishindwa kutoa ushahidi wa moja
kwa moja.
Ameongeza kuwa
mahakama hiyo imeona mshtakiwa anastahili adhabu kutokana na mtuhumiwa huyo
kama mzazi kushindwa kujali afya ya mtoto ili hali alikuwa mama mlezi ikiwa ni
pamoja na kumpeleka Hospitali kwa wakati ili apatiwe matibabu.
Ndeuruo amesema pia
mahakama hiyo haikuridhishwa na na ushahidi wa mtuhumiwa alioutoa mahakamani
kuwa majeraha yaliyokutwa mwilini mwa mhanga wa tukio hilo yalitokana na kuugua
kwa tetekuwanga jambo ambalo alisema si la kweli.
Amesema kuwa mshtakiwa
ametoa maelezo wakati wa utetezi wake yanayopingana na na maelezoya daktari
aliyemtibu mgonjwa alipofikishwa hospitali wakati akitoa ushahidi mahakamani
hapo.
Hata hivyo kabla ya
kutoa hukumu hiyo Hakimu huyo alisema kutokana na ibara ya 16 ya sheria ya African
Charter inayotaka Nchi itunge sheria ya kulinda haki za watoto ambapo Tanzania
haina sheria hiyo hivyo kusababisha watu kuwanyanyasa watoto.
Hakimu huyo ametoa
wito kwa taasisi zinazohusika kutunga sheria hiyo mara moja ili kulinda haki za
watoto ambayo itatamka wazi adhabu kwa wale watakaobainika kuwatesa na
kuwanyanyasa watoto.
Kwa upande wake
mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa ameiiambia mahakama hiyo kumpa
adhabu kali mtuhumiwa huyo ili liwe fundisho kwa wazazi wengine wenye tabia
kama hizo ambao hajakamatwa.
Amesema kitendo
kilichofanya na mshtakiwa huyo ni kitendo chakinyama ambacho kinatakiwa
kulaaniwa vikali hivyo kupitia adhabu atakayopewa mtuhumiwa inaweza kupunguza
unyasasaji kama huyo katika jamii.
Aidha mshtakiwa Wilvina
alipotakiwa kujitetea ili apunguziwe adhabu kabla ya kusomewa aliomba mahakama
hiyo impunguzie adhabu kwa kile alichodai kuwa ni mjamzito, pia hajui mtoto
wake aliyemzaa alipo pamoja na mawasiliano na familia yake.
Akitoa hukumu hiyo
hakimu Ndauruo amesema amesikitishwa na kitendo cha mtuhumiwa cha kuomba
kupunguziwa adhabu kutokana nakutomwona mtoto wake hali inayoonesha kutomjali
mtoto aliyemtendea kosa.
Ameongeza kuwa
Mahakama imefuatilia historia ya nyuma ya mtuhumiwa ambayo haioneshi kama
anamatukio kama hayo ambayo aliwahi kuyafanya lakini mtuhumiwa anastahili
adhabu kali kama upande wa mashtaka ulivyo sahauri na kutokana na mhanga kuwa
na ulemavu wa kudumu.
Amesema mahakama
inamhukumu kifungo cha maisha kifungo kitakachothibitishwa na mahakama kuu
kutokana na mtuhumiwa kuwa na haki ya kukata rufaa kama ameona ameonewa katika
kesi hiyo.
Mwanamke huyo
alipandishwa kizimbani Novemba 16, Mwaka chini ya Mwendesha mashtaka wa
Serikali, Achiles Mulisa aliiambia Mahakama kuwa Mtuhumiwa Wilvina Mkandala
(24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo
imemsababishia ulemavu mtoto Aneth.
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 HAYA HAPA
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.
TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)
ILIYOFANYIKA OKTOBA 2012
1.0 UTANGULIZI
Mitihani ya Kidato cha Nne
(CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia
tarehe 8-25 Oktoba 2012. Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi
matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :
2.0 MTIHANI WA MAARIFA (QT)
2.1 Usajili na Mahudhurio
Katika Mtihani wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176.
Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42 ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani.
2.2 Matokeo ya Mtihani wa Maarifa (QT)
Watahiniwa 5,984 kati ya 17,137 waliofanya mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).
3.0 MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012
Jumla ya vituo 5,058 vilitumika
katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155
vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa
wa kujitegemea.
ENDELEO KWA KUBOFYA HAPO CHINI
Ali Hassani Mwinyi amewataka viongozi wa kidini nchini kuihami amani na utulivu inaotishiwa kuvurugwa
RAIS
mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassani Mwinyi amewataka viongozi
wa kidini nchini kuihami amani na utulivu inaotishiwa kuvurugwa na
misukosuko ya kidini, kisiasa na kijamii inayojitokeza katika maeneo mbalimbali yanchi.
Alhaj Mwinyi alisema hayo wakati
maadhimisho ya sherehe za siku ya uzawa wa Mtume Mohamma (SWA),
yalioandaliwa na Jumuiya ya Khoja Shia Ithnaasheri, kufanyika jijini Dar
es Salaam leo.
Alisema nchi hivi sasa inapita
kwenye misukosuko inayokana na vitendo hivyo na endapo viongozi wa
kidini hawatakuwa makini katika kukemea waumini wao basi huenda nchi
ikaingia kwenye matatizo ambayo hayana slahi kwa nchi.
Alhaj Mwinyi alisema mkiwa
viongozi wadini mnalo jukumu la kila mmoja wenu kutumia elimu na fursa
zilizopo kwa kuwatuliza vijana kutoingia katika vitendo vya uvunjifu wa
amani kwa kisingizio cha dini.
“Tanzania inaongoza kwa
kudumisha amani, utulivu na ustaarabu kwa miaka mingi kama ingekuwa
wachezaji mpira tungesema sisi ni machampioni wa amani katika Bara la
Afrika”alisema Alhaj Mwinyi.
Alisema ni wajibu wa Masheikh
hao kusimamia na kulinda amani na utulivu uendelee kuwepo ili kila
muumini aweze kufanya ibada, kwenda msikitini na kufanya shughuli
nyingine za maendeleo kwa maslahi ya nchi.
Aliongeza kuwa hakuna haja ya
kufikishana mahala kuwa kila mmoja anakuwa na wasiwasi wa maisha yake
kitendo ambacho kinaenda kinyume na mafundisho ya Mtume Mohamad (SWA).
“Tanzania ni nchi kongwe na
haikuanza leo pia ni sawa na gunia ambalo limekusanya watu wengi wa dini
mbalimbali na wasio na dini hivyo ni vema watu wakajenga ustaarabu wa
kuvumiliana”alisema Alhaj Mwinyi.
Alhaj Mwinyi alisema wajibu wa
Waislam ni kuhakikisha wanaishi kwa amani na watu wengine ambao
hawajawaingilia na kutaka kuwafuta katika nchi hii.
Vilevile ieleweke wazi kuwa
hakuna anaweza kumfuta mwenzake katika kile anachokiamini hivyo ni vema
kila mtu akajifunza kumvumilia mwingine.
Alisema kubwa ni kla mmoja
kujizuia kumuingilia mwingine kwenye dini yake, kazi hiyo hakuna
mwingine wa kuifanya bali ni Masheikh hao.
Aliwaasa Masheikh hao kuacha kushabikia mambo madogo ambako ushabibiki ukiendekezwa iko siku unaweza kuvuruga amani ya nchi hii.
UKIFIKA MBEYA TU? KARIBUNI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA MJIONEE MAAJABU YA MUNGU
MUONEKANO WA MLIMA RUNGWE
RAIS KIKWETE AZIFARIJI FAMILIA ZA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA GARI UBENA ZOMOZI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifariji ndugu, jamaa na marafiki wa
familia zilizoondokewa na watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani
maeneo ya kijiji cha Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani Februari
11, 2013 iliyoua hapohapo watu wanane wakiwemo wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II
lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi hii ya Februari 16, 2015 amekwenda
kuhani na kufariji ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizoondokewa na
watoto na wazazi kufuatia ajali ya barabarani maeneo ya kijiji cha
Kibiki, Ubena Zomozi katika mkoa wa Pwani iliyotokea Februari 11, 2013
na kupoteza hapohapo maisha ya watu tisa wakiwemo wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Chalinze baada ya gari dogo aina ya Toyota Mark II
lililokuwa limebeba abiria wanane kugongana uso kwa uso na roli la
mizigo
Familia alizokwenda kuhani na kuzifariji ni pamoja na za
marehemu Hassan Erasto Kurunge (57), Maria Sadiki ((52) na mtoto wa
mwaka mmoja Samweli Ismail wa kata ya Ubena.
Wengie ni marehemu Essau Enos Mwamgingo (16) , Stella Isaack Kazimoto (18), Bahati George Mbena (17) na Latifa Maneno (17)
Akiwa ameongozana na Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Mhe Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe.
Ahmed Kipozi, Rais Kikwete alieleza kusikitishwa kwake kwa ajali hiyo,
na kuwataka madereva wawe makini katika kuzingatia sheria za usalama
barabarani
Rais Kikwete alisikitishwa zaidi
kwa taarifa kwamba gari hilo dogo lilikuwa limebeba abiria wanane, na
kuwa dereva wake ambaye pia alipoteza maisha, hakuwa makini katika
kuzingatia sheria za usalama barabarani.
hakuna kulipiza kisasi-kard.pengoAskofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (Pichani) amewataka wakatoliki na watanzania kwa jumla kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo kumetokea kundi la watu wachache kutaka kuvunja amani hapa nchini kwa kutumia udini.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo, Kardinali Pengo amesema moyo wa kisasi
hautasaidia kitu chochote, kinyume chake utaleta maafa yaliyo makubwa
zaidi na kutuingiza katika janga kubwa zaidi.
Ameongeza kuwa siku ya tarehe 20 kutakuwa na ibada katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph itakayoongozwa na Askofu Msaidizi kwa lengo la kumuombea marehemu Padri Evarist Mushi na kuliombea taifa ili watanzania tuendelee kuwa wamoja na tubaki katika amani tuliokwisha kuizoea. Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amezungumza hayo baada ya kusoma waraka uliotolewa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu uliozungumzia mambo mengi ikiwemo kuwataja wakatoliki kama ‘makafiri’ na kuwa bado haijawa mwisho wa mapambano. |
No comments:
Post a Comment