Wednesday, February 20, 2013

DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AMETOA ZAIDI YA TANI MOJA YA MIFUKO YA SARUJI NA KUHAMASISISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KATA YA ITAGANO JIJINI MBEYA



DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA AKIWEKA TOFARI KUHAMASISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI ITAGANO 
HAPA MWESHIMIWA DR. MARYA MWANJELWA AKIENDELEA NA UJENZI WA KUPANDISHA UKUTA WA DARASA MOJA

DR.MARY MWANJELWA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA AMBAYE PIA NI M-NEC TAIFA  AKIMKABIDHI MIFUKO YA SARUJI ZAIDI YA TANI MOJA MWESHIMIWA DIWANI KATA YA ITAGANO MBWIGA NDALAMA KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI ITAGANO
NAE MWESHIMIWA DIWANI WA KATA YA ITAGANO MBWIGA NDALAMA AKIMSHUKURU MWESHIMIWA MBUNGE DR.MARY MWANJELWA KWA KUTOA MSAADA HUO NA PIA KUWAHAMASISHA KATIKA UJENZI WA SHULE HIYO YA SEKONDARI ITAGANO DIWANI HUYO AMESEMA KUWA SHULE HIYO ITAKAPOKAMILIKA ITASAIDIA HATA WATOTO WA VIJIJI JIRANI NA KATA HIYO KUAPATA ELIMU YA SEKONDARI  PIA WAMEMWAHIDI MWESHIMIWA MBUGE KUWA MADARASA MATATU MPAKA KUFIKIA MWEZI WA SITA YATAKUWA YAMEKAMILIKA NA TAYARI KWA KUTUMIWA
HAPA MWESHIMIWA MBUNGE AKIPATA MAELEZO TOKA KWA MWESHIMIWA DIWANI WA KATA YA ITAGANO JINSI UJENZI WA MADARASA HAYO UTAKAVYOKAMILIKA MAPEMA MARA BAADA YA KUKABIDHIWA SARUJI
MWESHIMIWA MBUNGE AKIONGEA NA WAKAZI WA KATA YA ITAGANO MARA BAADA YA KUKABIDI MSAADA HUO WA MIFUKO YA SARUJI
HII NDIYO SHULE YA SEKONDARI ITAGANO AMBAYO MWESHIMIWA DR MARY MWANJELWA AMETOA MSAADA  WA MIFUKO YA SARUJI
MARA TU BAADA YA KUMALIZA UTOAJI WA MSAADA PAMOJA NA UHAMASISHAJI WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI ITAGANO MWESHIMIWA MBUNGE ALIPATA NAFASI YA KUONGEA NA KINA MAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA ITAGANO

 

misa ya buriani pd.mushi


RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE!!! PADRI EVARIST MUSHI APUMZIKE KWA AMANI. . . .UKIFA KATIKA KRISTU UTAFUFUKA NAE SIKU YA MWISHO. UMEVIKWA TAJI YA USHINDI.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WA MILELE UMUANGAZIE!!! PADRI EVARIST MUSHI APUMZIKE KWA AMANI. . . .UKIFA KATIKA KRISTU UTAFUFUKA NAE SIKU YA MWISHO. UMEVIKWA TAJI YA USHINDI.


KANISA LACHOMWA MOTO ZANZIBAR

images 
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
……………………………………………………
 WAKATI Watanzania wakiendelea kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la Walokole la Shaloom lililoko eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, alisema jana kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku.
Amesema moto huo ulizuka mara baada ya kikundi cha watu watatu kuonekana wakipita njia karibu na kanisa hilo na baada ya muda mlinzi wa kanisa hilo alisikia kanisa likishambuliwa kwa mawe juu ya maapaa.
Amesema baada ya mlinzi huyo kubaini kuwepo kwa hatari, alilazimika kukimbia kwenda kujificha lakini huku akiangalia kwa mbali kinachoendelea.
Kamanda Olomi amesema kuwa wakati mlinzi huyo akiwa amejibanza mafichoni huku akiangalia kinachotokea, mara aliona moto ukiwaka ndani ya kanisa na ndipo alipopiga simu kwa kiongozi wa kanisa hilo naye kuwajulisha Polisi.
Amesema Polisi walipofika hapo walisaidiana na wananchi kuuzima moto huo lakini wakati huo tayari ulishateketeza thamani za kanisa hilo na vitu vingine vilivyokuwa kanisani hapo.
Kamanda Olomi amesema moto huo ungeweza kusababisha athali kubwa kama usingedhibitiwa mapema.
Hata hivyo amesema uimara wa dali lililotengenezwa kwa Gibsam kumesaidia kuunusuru moto huo kuunguza mapaa na kuliteketeza kabisa kanisa hilo.
Amesema wakati uongozi wa kanisa hilo ukifanya tathimini ya harasa iliyopatikana kutokana na moto huo, Jeshi la Polisi limeanza kuwasaka washukiwa kwa kutafuta taarifa kwa raia wema na bado hakuna mtu ama watu waliokamatwa kuhusika na tukio hilo.
Hata hivyo Kamanda Olomi amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii, wataanza utaratibu wa kuyalinda makanisa yote ili kuzuia matishio mengine kama hayo.

MIAKA MITATU JELA KWA KUJIFANYA AFISA USALAMA WA TAIFA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi, imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela, Shaban Juma, maarufu kwa jina la Mzigaba (31), baada ya kupatikana na hatia ya kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa.


Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga Tengwa, alitoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa mashitaka katika kesi hiyo.

Alisema ametoa adhabu hiyo, ili iwe fundusho kwa mshitakiwa na watu wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

Akitoa utetezi wake kabla ya hukumu hiyo, Juma ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa Kichangani, mjini hapa, aliiomba mahakama imwachie huru kwa madai kuwa ushahidi uliotolewa dhidi yake haukuwa wa ukweli.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi, Lazaro Masembo, alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo tarehe tofauti Aprili mwaka jana.

Alidai Juma katika kipindi hicho alijipatia sh 315,000 baada ya kuwadanganya watu kuwa ni Ofisa Usalama wa Taifa na kwamba alitumwa na idara hiyo kuorodhesha majina ya watu wanaotaka ajira ya utumishi katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Idara ya Usalama wa Taifa.

Alieleza kuwa mshitakiwa alikamatwa baada ya watu waliompa pesa kuona muda unapita huku wakiwa hawaoni kinachoendelea kuhusiana na ajira zao kwenda kutoa taarifa Polisi.

MBOZI YAKABIDHI MAABARA ZINAZOHAMISHIKA NNE KWA SHULE ZA SEKONDARI

 MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA MBOZI LEVISON CHILLEWA AKIMKABIDHI DIWANI WA MSIA MH MAKUNGANYA MOJA YA MEZA ZILIZOTOLEWA KUFUATIA MSAADA WASERIKALI WA KIASI CHA SHILINGI MILION 24 KWA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KWAAJILI YA KUBORESHA MAABARA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI 
 MMOJA WA WATAALAMU WA MAABARA AKIONYESHA NAMNA ZANA HIZO ZINAVYOFANYA KAZI KABLA YA KUKABIDHIWA KWA WAKUU WA SHULE ZA KATA WALIOONGOZANA NA MADIWANI WAO
 MIONGONI MWA SHULE ZA KATA ZENYE UHITAJI WA VIFAA NA MAABARA AMBAPO KWA MIAKA TAKRIBANI SITA WATOTO WAMEKUWA WAKISOMA BILA KUFANYA MAZOEZI YA VITENDO 
 AFISA ELIMU SEKONDARI WILAYA YA MBOZI BWANA ISAACK MGAYA AKIPEWA MKONO WA SHUKRANI NA BAADHI YA WALIMU NA DIWANI WA KATA YA RUANDA BAADA YA SHULE YA LUMBILA KUPEWA MEZA YA MAABARA INAYPOTEMBEA
 MIONGONI  MWA ZANA ZITAKAZOGAWIWA MASHULENI KWAAJILI YA KUIMARISHA MAFUNZO KWA VITENDO
OFISA KATIKA IDARA YA ELIMU SEKONDARI AKIONYESHA NAMNA YA KUUNGANISHA  MFUMO WA MAJI KWENYE MEZA YA MAABARA

HALMASHAURI ya wilaya Mbozi imekabidhi meza nne za maabara inayotembea kwaajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya Baiolojia, Kemia , Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa ni sehemu ya hatua za kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule za sekondari katika masomo ya sayansi.
Afisa Elimu sekondari wilayani Mbozi bwana Isaack Mgaya, amesema meza hizo zenye thamani ya shilingi Milion 24 zinatokana na msaada uliotolewa na serikali mwezi juni wa kiasi hicho cha fedha kwaajili ya kuziwezesha shule za sekondari kuwa na Maabara zinazohamishika.
Amesema hatua hiyo inaziwezesha shule Mbili za sekondari kwa wilaya mpya ya Momba za Mkulwe na Nkangamo kuwa na maabara wakati kwa upande wa wilaya ya Mbozi shule za sekondari za Msia na Lumbila pia zimenufaika.
Bwana Mgaya amesema Mobile Laboratory kama zinavyofahamika zimebuniwa ili kuwezesha kukidhi mafunzo ya masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari na Vyuo.
Aidha alifafanua kuwa matumizi yake yanawezesha madarasa hayo kuhama hama kulingana na mahitaji na kwamba pia zinaweza kutumika chini ya miti, ama maeneo yasiyo na mifumo ya umeme ama maji hivyo kurahisisha uelewa wa wanafunzi kulingana na mazingira waliyopo
kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Mbozi bwana Levison Chilewa ambaye aliambatana na Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Momba Bwana Juma Kitabuge ameeleza kuwa kutokana na muundo wa maabara hizo, madiwani wa kata zilizonufaika na mpango huo wanapaswa kujenga hoja za kushawishi madiwani wenzao ili kutenga kiwango kikubwa cha fedha za mapato ya ndani ya halmashauri hizo mbili kwaajili ya ununuzi wa meza hizo ambazo zitakuwa mkombozi kwa watoto katika masomo ya sayansi.
Alisema hivi sasa wanafunzi wamekuwa waoga wa masomo hayo kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya kusambazwa kwa teknolojia hiyo rahisi kunawawezesha wanafunzi sasa kujifunza katika hali iliyobora zaidi kwa vitendo.
Alisema ni vyema pia kwa shule zilizo karibu kuona namna ambavyo zinaweza kushirikiana kutumia maabara moja kwa kutembeleana hatua ambayo itarahisisha katika ufundishaji na hata kuleta tija katika matumizi ya maktaba hizo badala ya kuazimisha meza hizo kutoka shule moja kwenda shule nyingine hali ambayo inaweza kusababisha uharibifu.
Akizungumzia msaada huo, diwani wa kata ya Ruanda bwana Keneth Mgala amesema, kimsingi hatua hiyo itasaidia kupunguza hali ya matokeo mabaya kwenye masomo ya sayansi ambapo wanafunzi wakti mwingine wanalaumiwa kwa kuonewa kutokana na mazingira yenyewe ya shule kukosa vitu muhimu kama maabara hivyo kushindwa kuhamisha nadharia katika vitendo ama kuoanisha vyote viwili.
Kwa kipindi kirefu,Shule pekee yenye maabara ya kubuniwa na utundu wa mwalimu mmoja wilaya ya Mbozi ipo katika shule ya sekondari ya Vwawa ambapo maaabara hiyo imekuwa  shule kadhaa zimekuwa zikitembelea na  kujifunza ubunifu huo kwa lengo la kwenda kutengeneza katika shule zingine ili kuongeza hamasa ya  wanafunzi kupenda masomo ya sayansi

Kwa hisani ya Danny Tweve wa Indaba blog.


No comments: