MWENYEKITI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA
NORMAN SIGALLA
|
BAADHI YA VIONGOZI WA
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA
|
MWANDISHI WA HABARI FELIX MWAKYEMBE AKIULIZA SWALI KWA KAMATI HIYO |
EMMANUEL LENGWA MWANDISHI AKIULIZA SWALI KWA KAMATI HIYO YA ULINZI YA MKOA WA MBEYA |
MOJA YA WANAKAMATI YA ULINZI MKOA WA MBEYA KAMADA DIWANI AKIJIBU BAADHI YA MASWALI YALIOULIZWA NA WAANDISHI WA HABARI |
TAMKO LA
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MBEYA KUHUSU UCHOCHEZI WA KIDINI
Kwanza kabisa tungependa kutoa pongezi
kwa Viongozi na Waumini wa Dini na Madhehebu mbalimbali hapo Mkoa Mbeya
kuendeleza utamaduni wetu wa kuishi na kushirikiana katika shughuli mbalimbali
za kijamii. Bila kuweka hisia za udini. Tunawashukuru kwa kuendelea
kuvumiliana. Pamoja na kuendelea katika hali hii, kumejitokeza viashiria
mbalimbali vyenye kuonyesha dalili za kumomonyoka kwa maadili, katika Mkoa
wetu.
2.
Kumejitokeza baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa
Wakuzitumia nyumba zetu
takatifu za Ibada kuhubiri mambo
ambayohayahusiani kabisa na mambo yanayohusu Mwenyezi Mungu na
mafundisho yake, kwa kuhubiri mambo ya siasa za chuki kwa dhamira ya
kupandikiza chukidhidi ya Serikali au dini na madhehebumengine. Baadhi yao
wamediriki kuyasema hayo hadharani kwenye miadhara yao au mikusanyiko ya
waumini wao.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaona hali
hii haina
afya njema kwa mustakabali wa amani na utulivu wa Mkoa
wetu na
Nchi kwa ujumla.
3.
Pamoja
na mahubiri hayo pia kumekuwepo nyaraka mbalimbali za kimaandishi za sauti
katika kanda, CD zenye kuhubiri chuki, uchochezi dhidi ya dini au dhehebu lingine.
Kumekuwepo na video katika kanda, CD au DVD zenye kuhubiri chuki, uchochezi,
dharau na kebehi dhidi ya dini nyingine au Serikali na baadhi ya kanda hizo
zimediriki kuhamasisha waumini wake vurugu na hata kuua jambo ambalo Kamti ya
Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya inaamini hakuna dini ya aina yoyote
dunianiinayohimiza waumini wote kutumia kwa jambo lolote lile.
4.
Baada
ya kutafakari, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya imeamua yafuatayo:- inapiga marufuku:
(i)
Kuuza,
kusambaza au kuonyesha, Kanda za sauti CD za sauti, Kanda
za Video, CD, DVD, nyaraka
na maandiko yoyte yenye uchochezi wa aina yoyote ile au kukashifu dini yeyote
katika Mkoa wa Mbeya.
(ii)
Chombo
chochote cha Habari kilichopo Mkoani Mbeya kiepuke
kuandika makala, kunakili au kurusha hewani hotuba, mahubiri au
kuonyesha video zenye kuchochea, kudharau, kuhubiri au kukashifu
dini
yoyote ile
5. Kamati ya
Ulinzi na Usalama Mkoa inawaasa viongozi wa dini
Mbalimbali kutohubiri siasa kwenye majumba ya Ibada kwani
kwa
kufanya hivyo watakuwa wanakiuka sheria za nchi.
Mtawagawa
waumini wenu kwa sababu waumini wanaelewa hayo si maagizo
ya
Mungu, na hayamo kwenye vitabu vitakatifu.
6. Waandishi
wa Habari epukeni kushabikia matamko ya Viongozi wa
Dini au
Siasa yenye kulenga kuleta mgawanyiko katika taifa hili kwa
Misingi ya
kidini au kisiasa kwa kisingizio cha Uhuru wa Habari,
kumbukeni
Amani Umoja na Mshikamano wa Mkoa na Taifa
utategemea
mchango wenu katika kushabikia au kukemea kauli hizo
bila kujali
zimetolewa na kiongozi gain.
Mwisho, Serikali itamchukulia hatua za
kisheria mtu yeyote atakayekwenda kinyume na haya, bila kujali itikadi yake,
dini yake au wadhifa wake. Wananchi wanaaswa kuzikabidhi nyaraka, kanda CD na
DVD kwa ofisi za Serikali ngazi ya Vijiji, kata Wilaya na Mkoa au kituo
chochote cha Polisi. Endapo watakabidhi kwa hiyari hawatachukuliwa hatua.
Imetolewa na:
MWENYEKITI
KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA-MBEYA
VIONGOZI na Watumishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na vyama vya siasa vya upinzani ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Baada ya matokeo yasiyoridhisha msimamizi wa mtandao huu Ally Kingo nimepotelewa na mjomba wangu Atupakisye mwalwega baada ya matokeo sijui aliko huku Vigogowa hapa nchini wakitema cheche
MWANANCHI
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Lowassa alisema matokeo hayo ni aibu kwa
taifa na kuilaumu Serikali kwa kuzitelekeza shule za sekondari za
kata.Alisema taifa kwa sasa linazalisha wabeba kuni na maji na siyo
wasomi ambao wanaweza kushindana kwenye soko la ajira.
WAKATI
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiinyooshea kidole Serikali kwa
kuzitelekeza shule za sekondari za kata, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema hatajiuzulu ng’o kutokana na matokeo
mabaya ya kidato cha nne. Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Bavicha), nalo limetishia kuitisha maandamano ya nchi nzima
kwa kushirikisha wanafunzi wote waliopata sifuri ikiwa waziri huyo
hatajiuzulu. Taifa limeshikwa na mshtuko kutokana na matokeo hayo ambayo
yanaonyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo mwaka
jana, walipata sifuri.
Dk Kawambwa
Akizungumza jana katika uzinduzi wa Mpango Maalumu wa Mafunzo ya Kompyuta katika Shule ya Msingi ya Majengo wilayani Bagamoyo, Dk Kawambwa alisema hawezi kuachia ngazi kwa shinikizo la
wanasiasa.
Alisema yeye si wa kulaumiwa kutokana na wanafunzi hao kufanya vibaya kwenye mtihani wa kidato cha nne na kwamba wanaosema waziri anapaswa kujiuzulu hawana hoja za msingi zaidi ya kutaka kujipatia umaarufu kwa kudandia hoja zinazokuwapo kwa wakati husika. “Unajua katika mfumo wa vyama vingi, kila linapotokea jambo baya basi wanaona dawa ni kiongozi mhusika kung’oka. Unapozungumza waziri kujiuzulu hiyo ni lugha ya kisiasa lakini hata akijiuzulu inakuwa bado tatizo halijaweza kupatiwa ufumbuzi,” alisema. Dk Kawambwa alisema hata Serikali haijafurahishwa na matokeo hayo mabaya na kushauri njia nzuri ni kutafuta dawa ya kukabiliana na tatizo la wanafunzi kufeli huku akiahidi kuwa wizara yake inaangalia tatizo hilo kwa karibu zaidi ili kujua chanzo chake. Alisema amesikitika kuona hata shule ambazo zilikuwa zinategemewa kufanya vizuri zikiwamo za seminari, watu binafsi na kongwe za Serikali, nazo zimefanya vibaya. Aliunga mkono maoni ya kutaka mfumo mzima wa elimu nchini uangaliwe upya kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa elimu.
Lowassa
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Lowassa alisema matokeo hayo ni aibu kwa taifa na kuilaumu Serikali kwa kuzitelekeza shule za sekondari za kata. Alisema taifa kwa sasa linazalisha wabeba kuni na maji na siyo wasomi ambao wanaweza kushindana kwenye soko la ajira. Alisema sekondari za kata ambazo zilianzishwa chini ya usimamizi wake akiwa Waziri Mkuu, zilikuwa ukombozi kwa Watanzania wengi wa kipato cha kawaida na ndiyo sababu waliitikia wito kwa kuchangia ujenzi, hatua ambayo alisema ilimpa faraja kubwa. “Serikali tuliahidi kuzikamilisha shule hizo kwa kuzijengea maabara na kuhakikisha zina walimu. Ni wajibu wake kutimiza. Mimi ndiyo maana hata kwenye Katiba Mpya nilipendekeza uwezekano wa elimu ya sekondari kuwa bure, elimu ni kama mapigo ya moyo ya taifa ukiona hayaendi vyema lazima ujiulize,” alisema. Lowassa, ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008, alisema tangu aondoke madarakani, shule hizo nazo zimetelekezwa. Alimwomba Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua za makusudi, ikiwa ni pamoja na kuunda tume ili ichunguze kwa makini kiini cha matokeo hayo mabaya. “Matokeo hayo ni aibu kwa taifa, walimu, wazazi na wanafunzi wenyewe. Namwomba kwa dhati Rais afanye kitu cha ziada, natambua mchango wa juhudi zake katika sekta nyingine ikiwamo ujenzi wa barabara nchini lakini elimu ndiyo iwe ya kwanza,” alisema. Alitaka ufike wakati nchi iamue kuwekeza katika elimu tofauti na ilivyo sasa kwa Tanzania kuwa nchi inayotenga fedha kidogo zaidi katika sekta hiyo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). TAASISI ya Utawala Bora Tanzania (CEGODETA) yaiomba serikali kukifuta kikundi cha Uamsho
TAASISI ya Utawala Bora Tanzania
(CEGODETA), imeiomba serikali kukipiga marufuku kikundi cha Uamsho na
Jumuiya ya Kimataifa itangaze kuwa Uamsho ni kikundi hatari cha kigaidi
kama ilivyofanya kwa vikundi vya Al-Qaeida, Alshabab na Bokoharam.
Kauli hiyo ilitolewa kupitia
vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, na Mkurugenzi Mtendaji wa
taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya, kuhusu vitendo vya ukabila na udini
vinavyojitokeza kwa watu wachache ambao baadhi yao sio wazawa wa
Zanzibar, kusababisha kuuawa kwa watu wasio na hatia kama vile Mapadre
kwa makusudi wakidhani kwa kufanya hivyo wanachi wataogopa na kuwaachia
watawale kwa misingi ya udini.
Kwa mujibu wa Katiba ya
Tanzania, inakataza uanzishwaji wa taasisi ye yote au chama chochote cha
siasa kuandikishwa nchini kama malengo yake ni ya kidini au kuvunja
Muungano, kutokana tetesi kwamba mauaji yanayotokea Zanzibar
yanahusishwa na kikundi hicho, ni vema kikafutwa.
“Kwa kuzingatia hilo CEGODETA,
tunaunga tamko lililotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwamba uchunguzi wa
kina ufanyike ambao utashirikisha mashirika ya nje na wote wanaohusika
na mauajji hayo pamoja na wanaofadhili watu wao wachukuliwe hatua za
kisheria ili kukata mzizi wa fitina” alisema.
Kongamano la nane la Wanahabari na Wadau wa NHIF lafunguliwa leo Mkoani Mtwara
Mgeni
Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif
Rashid (kulia) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph
Simbakalia (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,Mh. Wilman
Kapenjama Ndile (kushoto) wakiwasili kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa
uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara leo,tayari kwa ufunguzi wa
Kongamano hilo ambalo ni la siku mbili.
Mwenyekiti
wa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya (NHIF),John Bwire akitoa utambuliwa wa Wanahabari waliohudhulia
kongamano hilo toka sehemu mbali mbali hapa nchini,linaloendelea
kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo
cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Mgeni
Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif
Rashid akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika
hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha
Ualimu Mkoani Mtwara.Kauli mbiu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu ni
“Matumizi Sahihi ya Fedha za Uchangiaji Katika Halmashauri ili kuboresha
huduma katika vituo vya matibabu”.
Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha mgeni Rasmi kuhutubia na kufungua Kongamano hilo.
Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh.
Abbas Kandoro akitoa salamu kwa Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF) wanaoshiriki Kongamano hilo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akitoa
taarifa fupi ya Mfuko wa Bima ya Afya kutokana tafiti mbali mbali
zilizofanywa na baadhi ya Wanahabari katika Halmashauri 26 hapa nchini.
Katibu
Mkuu wa Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya Habari hapa nchini,Nevile Meena
akizungumza machache wakati wa Kongamano hilo la nane la Wanahabari na
Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,linaloendelea hivi sasa kwenye
Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Raphael
Mwamotto akitoa muongozo na utambulisho kwa baadhi ya viongozi kutoka
sehemu mbali mbali wanaohudhulia Kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugin Mikongoti akiwasilisha mada yake kwenye Kongamano la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Wadau wakifatilia Mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo.
Baadhi
ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari wakifatilia kwa
makini Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF),linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin
Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara |
No comments:
Post a Comment