USAFIRI LEO ASUBUHI KATIKA BARABARA YA KYELA , TUKUYU HADI MBEYA KULIKUWA WA SHIDA HADI KUFIKIA WATU KUSAFIRI KWA SHIDA |
HAKUNA KAZI HAPA NI KUUCHAPA USINGIZI TU |
NIKIWA SAFARI NIKAKUMBANA NA MGOMO WA WASAFIRISHAJI NA SASA IMEKUWA SHIDA SANA KILA KUKICHA MADEREVA NI KUGOMA NA HUU MGOMO NI WA TATU KWA MWAKA HUU |
NIMEFIKA SALAMA HOME NA KWAKUWA KAZI NYINGI HAKUNA KUPUMZIKA NIPO OFISIN NAPIGA KAZI KARIBUNI SANA OFISIN KWA MDAU WENU KINGO |
MHANGA WA UMEME IRINGA AENDELEA NA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA
Ndg.
Selemani Mbuma aliepata ajali mbaya ya Umeme hiv ikaribuni bado yuhai
akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Iringa word namba 9
Pichani mkewe Bi Haule akishirikiana na wauguzi kumuhudumia mume wake
Ndugu huyu anahitaji msaada zaidi wamtibabu kulingana na hali alionayo
baadaya ajali. PICHA NA SAID NG'AMILO
OFISIN KWA MKUU WA MKOA WA MBEYA MAZUNGUMZO YAKIENDELEA KATI YA SERIKALI NA BARAZA LA MAASKOFU MBEYAPolisi yatangaza dau aliyemuua Padri Mushi
Padri Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili
iliyopita wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu
Teresia lililopo Beit el Ras nje kidogo ya mji wa Zanzibar, ambapo
inadaiwa kuwa waliomuua walikuwa wamepanda pikipiki aina ya Vespa na
walimfyatulia padri huyo risasi tatu akiwa ndani la gari yake.
WAKATI kukiwa na taarifa kwamba maofisa wa
Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) wametua nchini kwa ajili ya
kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, Jeshi la Polisi
limetangaza dau la Sh10 milioni kwa atakayefichua aliyemuua padri huyo.
Padri Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi Jumapili
iliyopita wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu
Teresia lililopo Beit el Ras nje kidogo ya mji wa Zanzibar, ambapo
inadaiwa kuwa waliomuua walikuwa wamepanda pikipiki aina ya Vespa na
walimfyatulia padri huyo risasi tatu akiwa ndani la gari yake.
Wakati polisi wakitangaza dau hilo, Sheikh Ali
Khamis Ali (65) mkazi wa Kitope Kaskazini Unguja, aliuawa jana kwa
kukatwa mapanga mjini Zanzibar, baada ya wezi kuvamia shambani kwake.
Habari za kuaminika zilizopatikana juzi zinaeleza
kuwa maofisa hao wa FBI, wako nchini na tayari na wamekutana na baadhi
ya viongozi wa Serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo.
Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa maofisa hao
walikutana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi kwa
ajili ya kuangalia ni namna gani watafanya shughuli zao katika
upelelezi huo.
Pamoja na ushiriki FBI, taarifa zinaeleza kuwa
maofisa wa Serikali ya Tanzania wamezungumza na taasisi za upelelezi za
nchi tano, ili kuongeza nguvu katika upelelezi huo.
Taasisi nyingine inayotajwa kuwa huenda ikashiriki
katika uchunguzi huo ni Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ya
Uingereza (Scotland Yard).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima
alilithibitishia gazeti hili kwamba Serikali imeanza kufanya mazungumzo
na mashirika mbalimbali ya upelelezi duniani kwa ajili ya kushirikiana
nayo kuchunguza mauaji ya Padri Mushi, lakini akasema kuwa ni mapema mno
kuyataja.
“Tumefuata maagizo aliyotoa Rais Kikwete kwamba
tushirikishe mataifa mbalimbali kuchunguza mauaji yaliyotokea Zanzibar,
siwezi kutaja kwa majina, ila tayari tumeanza kuzungumza na nchi
mbalimbali,” alisema Silima.
Akizungumza mjini Zanzibar jana, Kamishna wa
Polisi visiwani humo, Mussa Ali Mussa alisema kuwa hadi sasa hakuna mtu
aliyefikishwa mahakamani kuhusiana na tukio hilo la mauaji.
“Hakuna aliyefikishwa mahakamani, lakini wapo watu
ambao wamekamatwa wakihusishwa na tukio hili na tunaendelea kuwahoji,
wengine tunawaachia,” alisema na kuongeza:
“Tumeahidi kutoa Sh10 milioni kwa mtu yeyote, atakayetoa taarifa za mauaji ya Padri Mushi, hii itakuwa kama zawadi tu.”
WAZIRI MKUU AUNDA TUME KUCHUNGUZA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameunda Tume
maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne
ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru
Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
Katika matokeo hayo
yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya
mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi
wakati wowote wiki ijayo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa
Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of
Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa
huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za
Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
Wadau wengine watatoka Chama cha
Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa
Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Amesema Serikali inawaomba wadau
wa elimu, wazazi, walezi na wananchi wote kwa ujumla watoe ushirikiano
kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.
KIMENUKA:TFF YATAKIWA KUFUTA MATUMIZI YA KATIBA YA MWAKA 2012
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
SERIKALI imeliagiza Shirikisho la
Mchezo wa Mpira wa Miguu nchini (TFF) kufuta matumizi ya Katiba ya
Shirikisho hilo ya mwaka 2012 badala yake watumie Katiba ya mwaka 2006
kwa kuwa Katiba ya mwaka 2012 imekiuka kanuni za Sheria ya Baraza la
Michezo la Taifa ( BMT) Na.11 (1).
Agizo hilo limetolewa leo na
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella
Mukangara alipokuwa akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam
kuhusu mgogoro wa uchaguzi wa Viongozi wa TFF.
Dkt. Mukangara pia ameiagiza TFF
kufuata utaratibu wa kurekebisha Katiba za vyama vya michezo, kwa mujibu
wa Sheria ya BMT iliyotungwa na Bunge pamoja na kanuni zake ambazo ziko
wazi na rahisi kuzifuata.
Alifafanua kuwa TFF walikiuka
Sheria Na. 12 ya Baraza la Michezo la Taifa na marekebisho yake Na.6 ya
mwaka 1971 pamoja na kanuni za usajili Na. 442 za mwaka 1999.
“Kanuni ya BMT Na. 11(1) inaeleza
wazi utaratibu wa marekebisho ya Katiba ambapo walitakiwa wajaze Fomu
Na. 6,7,8 na 9 kisha baada ya siku 14 Msajili wa vyama vya michezo
anatakiwa kuwajibu, kama anakubali anatumia Fomu Na. 11 na kama anakataa
anatumia Fomu Na. 10 lakini TFF walikiuka yote haya.” Ameeleza Dkt.
Mukangara
Aidha, Dkt Mukangara ameiagiza TFF
kufanya uchaguzi wa Viongozi kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 2006 kwa
kuzingatia Sheria na Kanuni za BMT na kama kuna umuhimu wa kurekebisha
Katiba waitishe mkutano Mkuu kwa kufuata misingi ya Katiba yao ya
mwaka 2006 na kanuni za BMT kwa ajili ya kufanya maboresho hayo.
Akizungumzia taarifa zilizotolewa
na vyombo vya habari kuwa FIFA watakuja nchini kufuatilia mgogoro wa
TFF, Waziri amemwagiza Msajili wa Vyama vya michezo pamoja na TFF
kuwataarifu FIFA kuhusu maelekezo yake ya kutumia Katiba ya mwaka 2006
na wawaeleze hali halisi iliyojitokeza.
Amesema kuwa hakuna chama chochote
cha michezo nchini kilicho juu ya BMT, hivyo vyama vyote na vilabu
vyote vya michezo viendelee na shughuli zao za kuendeleza michezo kwa
kuzingatia Sheria na Kanuni za BMT pamoja na Katiba zao.
Kumekuwepo na mgogoro katika
mchakato mzima wa uchaguzi wa Viongozi wa TFF ikiwemo baadhi ya wagombea
kulalamika kuenguliwa na wadau mbalimbali kulalamika kuwa haki
haikutendeka na wengine kuonyesha wazi kutofuatwa kwa utaratibu wa
kurekebisha Katiba hali iliyopelekea Wizara yenye dhamana ya michezo kwa
kushirikiana na BMT kuingilia kati hasa katika suala la ukiukwaji wa
marekebisho ya Katiba.
|
No comments:
Post a Comment