Tuesday, February 26, 2013

WATU WANNE WAMESHIKILIWA NA JESHI LA POLISI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA KWA KUKUTWA KATIKA MASHINE YA KUTOLEA PESA BENKI YA NMB TUKUYU MJINI NA KUKUTWA NA ATM CARD 150, NA TSH 20,543,200/=

WATU WALIO HUSIKA NA KUKUTWA NA KIASI CHA PESA TSH 20,543,200 NA ATM CARD 150 USIKU WASAA TATU KATIKA ATM YA BENKI YA NMB TAWI LA TUKUYU MKINI NI MILAJI KITALE (34) MKAZI WA MSASANI TUKUYU, JOSEPH PETER 20 TUKUYU, JUMANNE MGERE 29 MKAZI WA MBOZI MBEYA  NA JUMA KABELO 20 MKAZI WA TUKUYU

BADO UCHUNGUZI UNAENDELEA HUKU JESHI LA POLISI LIKITOA WITO KWA WATU KUTOA USHIRIKIANO  KWA KUTOA TAARIFA ZAIDI ILI KUBAINI TATIZO PIA JESHI LA POLISI LIMEWATAKA WANANCHI KWA PAMOJA KUSHIRIKI ULINZI SHIRIKISHI KWA KUWABAINI WAHARIFUNA SHERIA KUCHUKUA MKONDO WAKE

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AKIONGEA NA WANAHABARI NA WAJUMBE WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA JINSI YA KUKABIRIANA NA WATU KUWEKA DHAMANA ATM CARD KATIKA MIKOPO ISIYO RASM ZAIDI SERIKALI IMEPIGA MALUFUKU WATUMIAJI WA ATM KUWAKABIDHI WATU WENGINE KADI ZAO KWA MINAJIRI YA KUKOPESHWA VITU HIVYO ATAKAE PATIKANA ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAKIWA KATIKA KIKAO CHA DHARULA ILI KULITOLEA MAAMUZI SUALA LILILOJITOKEZA LA WATU KUKUTWA NA ATM 150

WAJUMBE WAKISIKILIZA KWA MAKINI


MKUU WA WILAYA YA RUNGWE CHRISPIN MEELA AFANYA ZIARA KIWANDA CHA CHAI NA  MASHAMBA YA WATCO  NA KUJIONEA JINSI MWEKEZAJI KWA KUSHIRIKIANA NA RSTGA WANAVYO FANYA KAZI YA UZARISHAJI WA CHAI WILAYANI RUNGWE.
MKUU WA WILAYA AKIWASIRI KATIKA OFISI ZA WATCO ILIYOMO KATIKA MASHAMBA YA KYIMBILA TUKUYU

JUU MKUU WA WILAYA AKIPATA MAELEKEZO YA JINSI CHAI INAVYOZARISHWA KATIKA VITALU TAYARI KWA KUPANDWA SHAMBANI

IKIWA NI MKAKATI WA WATCO KUONGEZA UZARISHAJI WA CHAI HILI NI SHAMBA JIPYA LA CHAI AMBALO LIMEPANDWA MWAKA JANA SASA LINA MWAKA MMOJA TANGU MBEGU MPYA IPANDWE


HILI NI SHAMBA LA ZAMANI AMBALO SASA CHAI HII HUONDOLEWA NA KUPANDWA CHAI NYINGINE ILI KUONGEZA UZARISHAJI WA CHAI

MICHE MIPYA YA CHAI  IKIPANDWA

CHAI ILIYO TAYARI KWA KUCHUMWA NA KUPELEKWA KIWANDANI

BAADA YA ZIARA YA MASHAMBANI UKAWADIA MUDA WA KUJIONEA JINSI KIWANDA KINAVYOFANYA KAZI YA KUZARISHA CHAI

GARI LILIOTOKA KUCHUKUA CHAI SHAMBANI LIKIPAKUA CHAI KIWANDANI TAYARI KWA HATUA ZINAZOFUATA

CHAI KATIKA HATUA YA KUNYAUSHA

MKUU WA WILAYA NA MSAFARA WAKE WAKIJIONEA CHAI IKIWA KATIKA HATUA YA KWANZA KATIKA MASHINE
SEHEM YA MTAMBO UKISAGA CHAI

BAADA YA USAGAJI WA CHAI HAPA NDIPO SEHEMU CHAI INAPANGWA KATIKA MAGREDI

MR KAMBASILA AKIMUELEZA MKUU WA WILAYA JINSI MITAMBO INAVYOFANYA KAZIMKURUGENZI WA WATCO PETER ROWLAND AKIELEZA JINSI KIWANDA KINAVYOZARISHA CHAI NA JINSI WATCO INAVYOSHIRIKI HUDUMA ZA KIJAMII WILAYANI RUNGWE KWA KUJENGA MASHULE MIENDOMBINU YA MAJI NA NA VINGINE KWA KUSHIRIKIANA NA WAKULIMA WADOGO WILAYANI RUNGWE RSTGA
JOHNSOM MWAKASEGE MWENYEKITI WA BODI WA WAKULIMA WADOGO WILAYANI RUNGWE RSTGA AMESEMA KUWA HADI SASA WAKULIMA WADOGO WA CHAI WILAYANI RUNGWE WANAMIRIKI 30% YA HISA KATIKA KIWANDA CHA WATCO NA WANATARAJIA KUFIKA MWAKANI KUWA NA UBIA WA HISA 49%

O
PETER ROWLAND MKURUGENZI WA WATCO

MKUU WA WILAYA YA RUNGWE  CHRISPIN MEELA. BAADA YA ZIARA YA MASHAMBANI NA KIWANDANI AKAPATA WASAA WA KUONGEA NA WATENDAJI WA WATCO, KANZA AMEWAPONGEZA SANA WATCO KWA KUWEKEZA RUNGWE NA KUWA NA MIKAKATI MIPYA YA KUBORESHA MASHAMBA KWA KUPANDA CHAI KATIKA MASHAMBA YAO PIA AMEWAPONGEZA WATCO KWA KUJALI MAZINGIRA KWA KUWA NA MIKAKATI YA KUPANDA MITI  ILI KUTUNZA MAZINGIRA


14.OCTOBER 1999  MWEKEZAJI WA TATEPA PPETER ROWLAND KUSHOTO AKIWEKA SAIN YA UNUNUZI WA KIWANDA KWA UBIA NA WAKULIMA WADOGO WILAYANI RUNGWE MWENYE SUTI NYEUPE NI MAREHEM MZEE MWAKANGALE AKIWEKA SAIN KWA UBIA WA 25% NA TATEPA 75%

KARINUNI RUNGWE MJINI TUKUYU KATIKA MKOA WA MBEYA


JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu 13, wakiwemo askari wawili wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na polisi mmoja kwa matukio ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman amesema watuhumiwa hao wamewagawanya katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni la watuhumiwa 9 wakiwemo askari hao wawili wakidaiwa kuhusika na tukio la kuwaua kikatili na kisha kuwazika dereva na utingo wake
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman akiwa na viongozi wenzake wa jeshi hilo la polisi wakati wa kuongea na waandishi wa habari wa Mbeya
Siraha zilizokamatwa na na jeshi hilo la polisi ndizo zilikokuwa zinatumika na majambazi hayo 
Moja ya bastora iliyotengenezwa kienyeji kwa kutumia vipande vya bomba lakini inatumia risasi za kawaida na nihatari sana siraha hii
Hizi ni vifaa vilivyokamatwa katika matukio mbalimbali yaliotokea mkoani hapa kamanda amewaomba wananchi wa mbeya kuja kuvitambua ofisini kwakwe 
Hizi ni siraha na sare za jeshi ambazo walikuwa wanatumia majambazi hao waliokamatwa kwa tuhuma za mauaji
Waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
Mfanyabiashara maarufu wa eneo la Mwanjelwa, Gath Mbilinyi (32), anaetuhumiwa kuteka na kuua
Hawa ndiyo wanaotuhumiwa  kuwaua  dereva na utingo wake na kisha kwenda kuwazika porini  
Samahani kwa picha hizi zinasikitisha haya niamabaki ya miili ya tingo na dereva wake waliouwawa na watuhumiwa hapo juuJESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu 13, wakiwemo askari wawili wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na polisi mmoja  kwa matukio ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.

Akizungumza na waandishi habari jijini Mbeya Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman amesema watuhumiwa hao wamewagawanya katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni la watuhumiwa 9 wakiwemo askari hao wawili wakidaiwa kuhusika na tukio la kuwaua kikatili na kisha kuwazika dereva na utingo wake.

kundi la pili ni la watuhumiwa wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya dereva wa polisi lililotokea Wilayani Chunya mkoani hapa baada ya kufanyika uporaji wa shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha mafuta eneo la Matundasi wilayani chunya.

Akitoa ufafanuzi zaidi Kamanda Diwani amesema, katika tukio la kwanza ni lile lililotokea Februari 2 katika eneo la Mafinga,Mkoani Mbeya, ambapo watuhumiwa wa kundi la kwanza waliwateka dereva na utingo wake, Festo Kyando (45) na Jafari lililotokea na kuwaua kisha kwenda kuwazika porini.

Amesema dereva huyo alikuwa ametoka Jijini Dar es salaam kubeba mzigo wa wafanyabiashara kwa lengo la kuleta mkoani Mbeya, lakini kumbe walikuwa wakiwindwa na walipofika mkoani Iringa walitekwa na kufanyiwa mauaji hayo ya kinyama.

Kamanda Diwani amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi lilianza uchunguzi mkali na hatimaye kunasa mtandao huo wa watu 9 wakiwemo askari hao wawili wa jeshi la polisi na JWTZ,ambao uchunguzi umebaini kuwa hutoa mavazi ya majeshi hayo na silaha.

Kamanda Diwani amewataja watuhumiwa hao kuwa MT.85393 Samwel Charles  Balumwina(31) wajiriwa wa jeshi la wananchi kikosi 844 kikosi cha Itende Mbeya na G.1901PC Samwel Kigunye (27) askari wa jeshi la polisi Jijini Mbeya.

Wengine ni mfanyabiashara maarufu wa eneo la Mwanjelwa, Gath Mbilinyi (32), Rajabu Mbilinyi(25), Gregory Mtega(25,Francis Sanga(30) pamoja na ndugu ambao ni wafanyabiashara maarufu katika mji wa Makambako mkoani Njombe ambao ni Japhet Ng'ang'ana(24), Claud Ng'ang'ana(36), Hilally Ng'ang'ana(30)

Hata hivyo amesema walifanikiwa kukamata bidhaa hizo katika eneo la Tunduma ambako tayari zilikuwa zimekamatwa na kwamba miongoni mwa watuhumiwa ndiye aliyeuziwa mzigo huo.

Amesema mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina tofauti pamoja na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo vinashikiliwa na jeshi la Polisi Tunduma Wilani Mbozi Mkoani hapa.

Katika tukio la pili ni lile linalohusisha vifo vya watu wawili wilayani Chunya, ambao ni dereva wa polisi na dereva wa gari la majambazi baada ya kutokea kurushiana risasi.
Amesema tukio hilo lilitokea Februari 6 baada ya watuhumiwa wanne ambao wanashikiliwa na jeshi hilo kufanya uporaji wa shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha matundasi wilayani humo.
Amewataja madereva hao waliouwawa katika tukio hilo kuwa ni dereva wa polisi aliyefahamika kwa jina moja la Jafari, ambapo yule wa majambazi akitajwa kwa jina la  Shabani John.
Diwani amewataja watuhumiwa wanashikiliwa kwa tukio hilo kuwa ni Manase Kibona (37).Emmanuel Mndendemi na Masai Hongole, Mashaka George, John Mahenge, Narasco Mabiki.

Kamanda huyo amezitaja mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina tofauti pamoja na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo vinashikiliwa na jeshi la Polisi Tunduma Wilani Momba  Mkoani Mbeya.

Aidha,kamanda Diwani  amevitaja baadhi ya vielelezo vilivyokamatwa  kuwa ni Bunduki aina ya Shot Gun moja ambayo namba zake zilifutika, Gobore moja ambalo pia namba zake zilifutika, Bastora tatu zilizotengenezwa kienyeji zisizo na namba na zinazotumia risasi za s/Gun.

Vingine ni Risasi 31 za Silaha ya SMG/SAR, Sare za Jeshi (JWTZ), suruali 4, mashati 4 kofia 3 na Viatu jozi mbili , Risasi 99 za S/GUN, Risasi 25 za Bastola na magari yenye namba T 464BLX TOYOTA COROLA,T381 BDR VITZ, T 251 AKU Toyota Pick Up ,T 193 BDY  Toyota Premio na T 214 ASV  Toyot Mark II.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi anawashukuru wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliojitokeza katika kutoa ushirikiano wa kuwasaka majambazi hayo ambapo pia anaendelea kutoa wito kwa watu wenye taarifa za watu ambao haeajakamatwa.
Ameongeza kuwa taratibu za upelelezi zimekamilika ambapo taratibu za kuwafikisha mahamakamani zinaendelea.
   

picha Mbeya yetu na jeshi la polisi 

 

Rais Kikwete akagua Ukumbi Wa Mikutano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam

8E9U3337 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali(picha na Freddy Maro)
8E9U3420 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali                         (picha na Freddy Maro)

 

Redio mbili zafungiwa kwa kosa la uchochezi na kuvunja maadiri ya utangazaji

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/u/0/?ui=2&ik=39b87d7912&view=att&th=13d166efe6f185d0&attid=0.2&disp=inline&realattid=f_hdnlumav1&safe=1&zw&saduie=AG9B_P95l94oWwHpN5qv9zVT7G9B&sadet=1361881866782&sads=ZAWE8-e7ioW2c2mwT4JrX6d6q2M
Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo.

Na Thehabari.com
KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na  Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.

Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa

uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa

kufanya.
Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa
wakiviamini vituo hivyo.
Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.
 

Mizengo Pinda awataka watanzania kutoibeza tume yake kuchunguza matokeo

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda 
“Wengine wanasema tume zipo nyingi, si kweli kwamba zipo nyingi na hazifanyi kazi, kila mtu ana mawazo yake, jambo hili ni kubwa na lazima lishughulikiwe kwa ukubwa wake chansingi hapa lazima tupate majibu ya kina na kila mtu aelewe nini kimesababisha tatizo hili,”alisema Pinda.
Post a Comment