Thursday, February 28, 2013

SHOTI YA TSH 1,700,000/= YASABABISHA KUJINYONGA VANESA STEVIN KYANDO (30) TUKUYU MJINI

HOTUBA YA RAIS WA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 2013

Kikwete-707591

Utangulizi
Ndugu wananchi;
Namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujalia uzima na kutuwezesha  kuwasiliana kupitia utaratibu wetu mzuri tuliojiwekea wa kufanya hivyo kila mwisho  wa mwezi. Leo nimepanga kuzungumza nanyi mambo matatu; yaani Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Uhusiano wa Waislamu na Wakristo na Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne.


Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo
Ndugu Wananchi;
Tarehe 8 Februari, 2013 kule Addis Ababa, Ethiopia niliungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban Ki-Moon, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Nkosozana Dlamini Zuma na viongozi wa nchi 12 za Afrika Mashariki, Kati na Kusini kutia saini Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na jirani zake.  Pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zilikuwepo nchi za Burundi, Rwanda, Uganda, Sudani Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Angola, Zambia na Tanzania ambazo ni jirani ya Kongo.  Nchi za Ethiopia, Msumbiji na Afrika ya Kusini pamoja na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zilitia saini kama wadhamini.  Ethiopia kwa nafasi yake ya kuwa Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika na Msumbiji kwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).  Nchi wanachama wa Mkutano wa Ukanda wa Maziwa Makuu ziliwakilishwa na Uganda ambayo ni Mwenyekiti wake wa sasa.  Afrika ya Kusini ilishirikishwa kwa kuwa taifa kubwa na linalotegemewa katika ukanda wetu.
Mpango huu ni jitihada nyingine ya kusaidia Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ipate amani ya kudumu.  Kama tujuavyo, tangu mwaka 1997 wakati wa vita vilivyosababisha kuondolewa kwa Rais Mobutu Seseseko mpaka sasa nchi hiyo rafiki na jirani haijapata amani na utulivu wa kudumu.  Kumekuwepo jitihada na mipango kadhaa ya kuleta amani ambayo hata hivyo baada ya muda fulani machafuko hutokea tena na mipango hiyo kuvurugika.  Inakadiriwa kuwa takriban watu milioni 5.4 wamepoteza maisha na watu wengi kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi yao.  Pia kumekuwepo na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na mali nyingi kuharibiwa au kuporwa.
Ndugu Wananchi;
Machafuko yaliyoanzishwa na waasi wa Kundi la M23 mapema mwaka wa jana ndiyo sababu ya kuwepo kwa Mpango huu wa sasa tuliotia saini kule Addis Ababa, Ethiopia tarehe 8 Februari, 2013.  Katika Mpango huo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na jirani zake, Tanzania ikiwemo, tumekubaliana kutokufanyiana vitendo vinavyohatarisha amani na usalama wa nchi zetu.  Tumeazimia tusifanye hivyo ama moja kwa moja kama nchi au kwa kutumia watu wengine.  Aidha, tumekubaliana tusiruhusu watu au vikundi vya watu kutumia nchi zetu kuhatarisha usalama wa nchi nyingine.  Kimsingi tumekubaliana kuwa majirani wema.  Katika Mkataba huo, majukumu ya kila nchi yameainishwa vizuri pamoja na yale ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Mashirika ya Kikanda hususan SADC na ICGLR.
Ndugu Wananchi;
Niliamua kukubali kushiriki na kutia saini Mpango ule kwa kutambua ukweli kwamba sisi majirani wa nchi ya Kongo tunao wajibu wa kusaidia kwa kile tunachoweza.  Wananchi wa Kongo wameteseka kwa muda mrefu mno hivyo kama Mpango huu utawasaidia kupata amani na usalama hatuna budi kuunga mkono.  Ni kwa misingi hiyo hiyo, tulikubali kuchangia kikosi kimoja katika Jeshi la Kimataifa la kulinda amani huko Mashariki ya Kongo kama ilivyoamuliwa na Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu mwezi Julai, 2012.  Uamuzi huo umeungwa mkono na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.  Umoja wa Mataifa umeamua Jeshi hilo liwe sehemu ya Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda Amani nchini Kongo (MONUSCO) jambo ambalo sote tumeliafiki.  Tumepeleka walinzi wa amani Darfur, Sudan na Lebanon, kwa nini tusipeleke Kingo.  Miaka ya nyuma tulishapeleka walinzi wa amani Liberia, Siera Leon na Eritrea.
Ni matumaini yetu kuwa Mpango huu mpya utatekelezwa kwa ukamilifu na kuzaa matunda yaliyokusudiwa.  Kama nchi jirani, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo yenye amani, usalama na utulivu ni jambo lenye maslahi makubwa kwetu.  Ina maana ya kutokuwa na wakimbizi kutoka nchi hiyo, uharamia katika Ziwa Tanganyika kutokuwepo na ustawi wa shughuli za kiuchumi na kibiashara kwa upande wetu na wao.  Ni chachu muhimu ya maendeleo ya Mikoa ya pembeni mwa Ziwa Tanganyika na Tanzania kwa jumla.

Uhusiano wa Waislamu na Wakristo
Ndugu wananchi;
          Jambo la pili ninalopanga kulizungumzia siku ya leo ni uhusiano wa Wakristo na Waislamu hapa nchini.  Kwa miezi kadhaa sasa tangu mwaka wa jana kumekuwepo na matukio kadhaa yanayosababisha mifarakano na kupandikiza chuki baina ya waumini wa dini ya Kikristo na Kiislamu.  Matukio ya kauli na vitendo vya kudharau dini za wengine, kunajisi vitabu vitakatifu vya dini hizo, kuchoma moto nyumba za ibada na mzozo kuhusu nani achinje.   Kumekuwepo  na matumizi mabaya ya radio na simu za mkononi na mifumo  mingine ya mawasiliano iliyoeneza maneno na ujumbe wa chuki na vitisho kwa waumini na viongozi wa dini zetu hizi kubwa hapa nchini.  Kauli na matendo hayo, katika baadhi ya maeneo yamekuwa chanzo cha uhasama na magomvi baina ya waumini na hatimaye kusababisha vifo kama ilivyotokea Buseresere Mkoani Geita na Beit-el-Ras, Zanzibar. 

Ndugu zangu; 
Watanzania hatujawahi kuwa hivi, kumetokea nini? Miaka yote Watanzania ni watu tunaotambua na kuheshimu tofauti za dini zetu mbalimbali tunazoabudu.  Watanzania ni waelewa na kwa ajili hiyo tumekuwa tunavumiliana kwa tofauti zetu na ndiyo maana tumekuwa tunaishi pamoja kidugu, kwa umoja na kushirikiana kwa mambo yote yanayotuhusu maishani isipokuwa wakati kila mmoja anapoingia kwenye nyumba ya ibada kumuomba Mola kwa misingi na taratibu ya dini yake.
Watanzania wa dini zote na makabila tofauti wanaishi nyumba moja, wanasoma pamoja, wanafanya kazi pamoja kwa udugu, upendo, umoja na ushirikiano.  Kuna koo na familia zenye watu wa dini tofauti, wengine Waislamu na wengine Wakristo.  Wapo Waislamu na Wakristo wameoana, wamezaa na wamejukuu na kila mmoja amebakia kuwa mfuasi wa dini yake.  Wapo pia ambao hawakuoa lakini wamezaa watoto na wanashirikiana kulea watoto wao.  Hayo ndiyo maisha ya Watanzania na hiyo ndiyo Tanzania yenye amani na utulivu tuliyozaliwa, kukua na kuishi.  Nawasihi sana Watanzania wenzangu, tuienzi na kuidumisha tunu hii waliyotujengea mababu zetu.
Ndugu Wananchi;
Kuna wenzetu kwa sababu wanazozijua wao na kwa manufaa wanayoyajua wao wanataka kutuvurugia nchi yetu hii nzuri.  Tusiwape nafasi wachochezi hawa kwani hawatutakii mema na wala hawazitakii mema dini zetu na nchi yetu.  Sisi katika Serikali hatutasita kuwachukulia hatua wale wote wanaochochea chuki za kidini, wanaodharau vitabu vitakatifu vya dini nyingine na wanaokejeli dini nyingine.
Nimewakumbusha Polisi na mamlaka husika kote nchini wasifanye ajizi kwenye matukio ya namna hiyo.  Wawachukulie hatua stahiki wale wote wanaohusika.  Nimewataka wazingatie msemo wa Kiswahili usemao “ajizi nyumba ya njaa”.  Wachochezi wa mifarakano  na chuki za kidini wasipodhibitiwa ipasavyo wataleta maafa kwa Watanzania wasiokuwa na hatia.  Nimewakumbusha Wakuu wa Wilaya na Mikoa kama walinzi wa amani wa maeneo yao ya uongozi, watimize ipasavyo wajibu wao.  Pia nimewataka Polisi wakamilishe mapema upelelezi wa makosa ya vurugu za kidini na wahusika wafikishwe haraka kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine.
Ndugu Wananchi;
Naendelea kuwasiliana na viongozi wa dini kuzungumza nao juu ya wajibu wao maalum wa kuhakikisha kuwa wafuasi wao hawawi chanzo au sehemu ya tatizo na mifarakano miongoni mwa waumini wa dini mbalimbali nchini.  Hali kadhalika naitumia nafasi hiyo kuwakumbusha umuhimu wa kuzungumza na wenzao wa upande mwingine kutatua tofauti au matatizo yanayoathiri uhusiano mwema baina yao.
Ndugu Wananchi;
Kuna msemo maarufu usemao “mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi”.  Naomba tuwe wajenga nchi na kamwe tusikubali kuwa wabomoa nchi.  Hivi tukiibomoa nchi yetu tutakwenda wapi? Tutaishi wapi?  Tusikubali kugeuka wakimbizi ndani ya nchi au nje ya nchi yetu.
Kwa mara nyingine tena, napenda kutumia nafasi hii kuwapa mkono wa pole makanisa, familia, ndugu na jamaa wote wa Mchungaji Kachila na Padri Mushi.  Sote tunafahamu machungu waliyonayo kwa kuondokewa na wapendwa wao.  Serikali na wapenda amani wote nchini wapo pamoja nanyi katika kipindi hiki kugumu.  Vile vile natoa rambirambi zangu nyingi kwa waumini wote wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God na Kanisa Katoliki Tanzania kwa kuondolewa ghafla na viongozi wao. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azipumzishe kwa amani roho za viongozi wetu.  Amin.
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012
Ndugu wananchi;
Tarehe 18 Februari, 2013 Baraza la Mitihani la Taifa lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne ya mwaka 2012.  Wanafunzi 397,132 walifanya mtihani huo na kati ya hao, waliofaulu ni 126,851 yaani sawa na asilimia 34.5.  Wanafunzi 240,903 ambao ni sawa na asilimia 65.5 hawakufaulu mtihani huo.  Kwa ulinganifu, matokeo hayo ni mabaya kuliko matokeo mengine ya mtihani huo ya miaka ya hivi karibuni.
Mwaka 2011, jumla ya wanafunzi 336,782 walifanya mtihani huo na waliofaulu walikuwa asilimia 53.6 na ambao hawakufaulu kabisa walikuwa asilimia 46.4.  Mwaka 2010 jumla ya wanafunzi 352,045 walifanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne, asilimia 50.4 ya wanafunzi hao walifaulu  na asilimia 49.6 ya wanafunzi hawakufaulu. 
Ndugu Wananchi;
Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012, yameshtua na kufadhaisha watu wengi nchini na kwa sababu stahiki kabisa.  Kwanza, kwamba kiwango cha kufaulu kimeporomoka sana, tena ghafla, kutoka asilimia 53.6 mwaka 2011 hadi asilimia 34.5 mwaka 2012.  Hili ni anguko la asilimia 19.1 ambalo, kwa kila hali, ni kubwa sana.  Pili, kwamba hata shule zinazofahamika kuwa na historia ya kufaulisha vizuri kama vile seminari, shule za watu binafsi, za mashirika ya dini na sekondari kongwe za Serikali ambazo hazina matatizo kama ilivyo kwa zile sekondari za Kata, nazo safari hii hazikupata mafanikio kama ilivyo kawaida yao.  Nazo zimejikuta zikiwa na idadi ya vijana waliopata daraja la kwanza, la pili na la tatu ikipungua wakati waliopata daraja la nne na waliofeli wakiongezeka. 
Isitoshe na kiwango cha ufaulu wa vijana umepungua pia.  Mwaka 2010 wanafunzi 10 bora wote walikuwa wamefaulu daraja la kwanza la alama  au pointi 7.  Mwaka 2011 katika wanafunzi 10 bora wanane walipata daraja la kwanza kwa alama  7 na wawili alama 8.  Mwaka 2012 katika wanafunzi 10 bora, watatu walipata daraja la kwanza kwa alama 9, watatu alama 10  na wawili alama 11.   
Ndugu Wananchi;
Haya ndiyo mambo yanayozua maswali kwa watu wengi yanayohitaji kupatiwa majawabu ya uhakika.  Kulikoni mwaka 2012?  Ndiyo msingi wa uamuzi wa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda, kuamua kuunda Tume ya kuliangalia suala zima la mitihani ya mwaka 2012 na matokeo yake.  Hali hii haijawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.  Ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu, hivyo lazima ukweli wake ujulikane kwa uhakika.  Hii itawezesha Serikali na wadau wengine kuchukua hatua stahiki kurekebisha mambo mapema iwezekanavyo ili hatimaye mambo yawe mazuri siku za usoni.  Tusipofanya hivyo mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi na lawama zinaweza kuwa kubwa zaidi kwa Serikali.
Ndugu Wananchi;
Hivi sasa kunatolewa mawazo lukuki kuhusu sababu za kwa nini matokeo yamekuwa mabaya.  Wapo wanaodhani kuwa lipo tatizo katika utungaji wa mitihani, usahihishaji wake au kutoa maksi kwa watahiniwa.  Wapo wanaodhani walimu hawawajibiki ipasavyo au baadhi yao kutokumudu masomo wanayofundisha.  Wapo wanaofikiria kuwa wanafunzi hawako makini katika kufuatilia masomo na wazazi hawajali kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni.  Wapo wanaoinyooshea kidole Serikali kwa sera, mitaala na uwekezaji usiokidhi mahitaji ya maendeleo  ya elimu.  Wapo wanaofikiria kuwa Serikali kushindwa kuongeza mishahara ya walimu kwa asilimia 100 kama walivyotaka imechangia.  Orodha ni ndefu, ali mradi kila mtu ana mawazo yake.  Na sisi katika Serikali hatuwezi kuwa tunadhani kwa sababu tunayo dhamana maalum.  Lazima tujue ukweli kwa uhakika na ndiyo maana kuna umuhimu wa Tume.  Naomba kila mtu mwenye mawazo yake ayafikishe kwenye Tume hiyo hapo itakapoundwa ili tupate jawabu muafaka la tatizo hili.
Ndugu Wananchi;
Napenda kuwahakikishia kuwa sisi katika Serikali tumetoa kipaumbele cha juu sana kwa elimu na kwamba hakuna upungufu wa utashi kwa upande wangu na wenzangu wote Serikalini.  Ndiyo maana tumeguswa sana na matokeo haya.  Bajeti ya elimu ya shilingi trilioni 3.6 ambayo ni sawa na asilimia 24 ya bajeti yote ya Serikali ndiyo kubwa kuliko zote.  Kwa ajili hiyo imetuwezesha kuendelea kukabili mahitaji na changamoto za upanuzi mkubwa wa elimu ya sekondari na elimu ya juu.  Bado hatujazimaliza changamoto zote na kwamba bado tuna kazi kubwa mbele yetu, lakini mafanikio yanaendelea kupatikana.  Tutaendelea kutoa kipaumbele cha juu kwa elimu mpaka hapo itakapofikia mahali kwamba matatizo makubwa yatakapokuwa yamepungua sana. 
Hitimisho
Ndugu Wananchi;
 Mungu Ibariki Tanzania!
Mungu Ibariki Afrika!
Nashukuru kwa kunisikiliza!


 SHOTI YA TSH 1,700,000/= YASABABISHA KUJINYONGA VANESA STEVIN KYANDO (30) TUKUYU MJINI

MWILI WA MAREHEM VANESA STEVIN KYANDO UKIWA BADO KUSHUSHWA AKIWA AMEJINYONGEA KANGA
KWA MAELEZO YA VYANZO MAREHEM ASUBUHI KABLA YA KUFIKIA HATUA YA KUJINYONGA ALIPIGIWA SIMU NA SHEMEJI YAKE MAALUFU KWA JINA LA LUMAGE IKIMTAKA KURUDISHA PESA ALIZOINGIZA SHOT DUKANI KWAKE TSH 1,700,000/= MILION MOJA NA LAKI SABA AU AMKUTE MAITI.

WATU WENGI WAMESHTUSHWA NA TUKIO HILI KWA KUWA VANESA NI BINTI ANAYEFAHAMIKA SANA KWA UPOLE WAKE NA UCHA MUNGU MAANA HAKUNA ANAYEAMINI TUKIO HILI KUWA NI LA KWELI LAKINI TAYARI BINTI VANESA AMEFARIKI NA AMEZIKWA NYUMBANI KWAO TUKUYU MJINI KATA YA KAWETELE MITAA YA MACHINJIONI



ASUBUHI HII HAKUNA MTU ANAYEAMINI KILICHOTOKEA

POLICE ADAM AKIWA ANAJIANDAA KUFANYA KAZI YA KUSHUSHA MWILI WA MAREHEM

WAKAZI WA TUKUYU WAKISHANGAA NA WENGI WAKIWA NA MAJONZI BAADA YA KUSHUHUDIA VANESA AKIWA AMEJINYONGA


MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAKULIMA WA CHAI WILAYANI RUNGWE WAFANYIKA NA BEI ELEKEZI YA TAIFA KUWA TSH 206 LAKINI KWA KUJALI WAKULIMA WATCO KATUMBA ITAWALIPA WAKULIMA WA CHAI RUNGWE SH 231 KWA KILO MOJA YA MAJANI MABICHI YA CHAI

KITUO CHA MAFUNZO NA OFISI YA RSTGA WILAYANI RUNGWE NDIPO NA MKUTANO MKUU UMEFANYIKA
LEBI B. MWAKATOBE MTENDAJI MKUU WA RSTGA RUNGWE AKIWA OFISIN KWAKE AKIJIANDAA NA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAKULIMA WA CHAI

BAADHI YA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA RSTGA

SEHEMU YA MASHAMBA MAPYA YA CHAI AMBAPO NI MKAKATI MPYA WA WATCO KUPANDA CHAI MPYA ILI KUONGEZA UZARISHAJI WA CHAI KWAKUWA ZAO LA CHAO LIMEKUWA NI ZAO PEKEE WILAYANI RUNGWE KWA KUINUA YA UCHUMI WA WAKULIMA NA JAMII

CHANGAMOTO ILIYOJITOKEZA KATIKA MKUTANO HUU NI ZAO LA CHAI KUWA NI ZAO LINALOLIMWA NA WAZEE WALIOWENGI NA SIO VIJANA HIVYO VIJANA WAMETAKIWA KUJITOKEZA KULIMA CHAI KWAKUWA NDILO ZAO LENYE UHAKIKA WA AJIRA NA KIPATO

MWENYEKITI WA BODI RSTGA JOHNSON MWAKASEGE AKIONGEA NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA MWAKA AKIWAELEZA JINSI MIPANGO ILIVYOTEKELEZWA NA CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO KATIKA KUUENDESHA UMOJA WAO WA CHAI RUNGWE

MTENDAJI MKUU WA RSTGA LEBI MWAKATOBE AKIONGEA NA WAJUMBE WA MKUTANO AKIWAELEKEZA BAADHI YA MAMBO YALIYOFANIKIWA LA ZAIDI KUKAMILIKA KWA UFUNGAJI WA MITAMBO YA REDIO AMBAYO INATARAJIWA KUANZA MATANGAZO HIVI KARIBUNI NA AMESEMA KUWEPO KWA KITUO CHA REDIO NI HATUA KUBWA KATIKA KUWAFIKIA WANANCHI NA UFIKISHWAJI WA ELIMU HATA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KILIMO KWANZA

MGENI RASM MHE, MECKSON MWAKIPUNGA AMEWATAKA WAKULIMA KUONGEZA UBORA WA CHAI WANAYOZARISHA KWA KUWA NDIO ZAO PEKEE WILAYANI RUNGWE LINALOTEGEMEWA KWA UCHUMI WA WATU WA RUNGWE ZAIDI AMEKEMEA TABIA ILIYOJITOKEZA YA HAPA TANZANIA YA KUSHABIKIA UDINI AMEWATAKA WANANCHI KULINDA AMANI ILIYOPO KWAKUWA IKIPOTEA KUIREJESHA ITAKUWA GHARAMA SANA

JUMA LIGANJA MHASIBU WA RSTGA AKISOMA MAPATO NA MATUMIZI NA AMBAPO WAJUMBE WALIFURAHIA JINSI MAMBO YANAVYOKWENDA SAWA KATIKA KUSIMAMIA FEDHA ZA WAKULIMA NA KULIPA WAKULIMA KWA WAKATI
MR MHAGAMA AKIONGEA KWA NIABA YA MKURUGENZI WA WATCO

MKUTANO ULIKWISHA NA WAJUMBE WAKARUDI MAKWAO MWAKALELI, SUMA ,NDITU, LWANGWA, MASEBE, MANOW, KIKOTA, MBAMBO, MASOKO, RUNGWE, BUSISYA, KATUMBA , KYIMBILA, KAPUGI, MMMM NASEMEMU ZINGINE NIMESAHAU

MR BAKARI DEREVA WA RSTGA
HII NI SEHEM YA CHUMBA CHA REDIO YA WALIMA WA CHAI AMBAYO IKO MBIONI KUFUNGULIWA

 

bosi tazara afurumushwa

article_thumbs.php
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Bw. Akashambatwa Mbikusita-Lewanika, hatimaye ameachia ngazi baada ya kuendesha kampeni kali ya miezi kadhaa kutaka aendelee kuongoza Mamlaka hiyo kwa miaka mingine mitatu.


Hatua hiyo ya kuachia ngazi imekuja baada ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri la Mamlaka hiyo kuonyesha dhahiri kutotaka Mzambia huyo aendelee na uongozi wa TAZARA kutokana na utendaji wake mbovu na uongozi mbaya uliowabagua wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa misingi ya utaifa wao.

Habari za ndani za Mamlaka hiyo zimesema Bw. Akashambatwa ambaye kipindi chake cha uongozi kiliisha tarehe 22 Januari, 2013 kiliongezwa kwa maombi maalum ya Serikali ya Zambia kwamba Serikali hiyo ilihitaji muda mrefu kidogo kumpata mbadala wake, licha ya Serikali ya  Tanzania kutoridhishwa na utendaji wake.
Katika kikao chake cha tarehe 20 Februari, 2013 jijini Lusaka, Zambia, Baraza la Mawaziri lilijadili kwa siri na kwa kirefu suala la mtendaji Mkuu huyo ambaye inasemekana aliombewa tena na Serikali ya Zambia kipindi cha nyongeza, ombi ambalo inadaiwa lilipingwa vikali na ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.
Taarifa za uhakika ndani ya Wizara ya Uchukuzi zinasema Serikali ya Tanzania haikumtaka Mtendaji Mkuu huyo kwa sababu kadhaa zikiwemo :uwezo mdogo, ubadhirifu, kuchochea ubaguzi kati ya Watanzania na Wazambia, ukaidi na uchochezi. Inadaiwa kuwa Mtendaji Mkuu huyo alizuia kuanzishwa kwa mradi wa usafiri jijini Dar es Salaam bila sababu yoyote ya msngi na kuishia kusambaza taarifa za uongo na uchochezi Zambia na magazeti mbalimbali nchini.
Tarehe 25 Februari, 2013 Gazeti la kila siku la Zambia, Zambia Daily Mail, liliripoti tukio hilo la kuachia ngazi kwa kiongozi huyo ambaye anajulikana sana nchini Zambia kama mfanyabiashara na kiongozi wa kimila (chief),                                             
Gazeti hilo lilinukuu barua ya Bw. Akashambatwa ya tarehe  22 Februari, 2013 kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Ujenzi, Ugavi na Mawasiliano ya Zambia, akielezea kuwa hakuna faida ya kuomba kurefushwa kwa mkataba wake wakati vyombo vikuu vya uongozi vya TAZARA, Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Mawaziri, havionyeshi kumkubali.

Kuondoka kwa Bw. Akashambatwa kwenye uongozi wa TAZARA kunatarajiwa kupokewa na wafanyakazi wa TAZARA kwa nderemo na vifijo.

WAZIRI MKUU KESHO ATAKUTANA NA TUME KUCHUNGUZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

IMG_9964 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda kesho (Jumamosi, Machi 2, 2013) atakutana na Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa Februari 18, mwaka huu. 
Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi.
 
Tume hiyo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
 
Wadau wengine wanatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
 
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.

last papal audience of his holiness benedict xvI

pope 7410c

Venerable Brothers in the Episcopate and in the Priesthood!
Distinguished Authorities!
Dear brothers and sisters!

Thank you for coming in such large numbers to this last General Audience of my pontificate.
Like the Apostle Paul in the biblical text that we have heard, I feel in my heart the paramount duty to thank God, who guides the Church and makes her grow: who sows His Word and thus nourishes the faith in His people. At this moment my spirit reaches out to embrace the whole Church throughout the world, and I thank God for the “news” that in these years of Petrine ministry I have been able to receive regarding the faith in the Lord Jesus Christ, and the charity that circulates in the body of the Church – charity that makes the Church to live in love – and of the hope that opens for us the way towards the fullness of life, and directs us towards the heavenly homeland.


I feel I [ought to] carry everyone in prayer, in a present that is God’s, where I recall every meeting, every voyage, every pastoral visit. I gather everyone and every thing in prayerful recollection, in order to entrust them to the Lord: in order that we might have full knowledge of His will, with every wisdom and spiritual understanding, and in order that we might comport ourselves in a manner that is worthy of Him, of His, bearing fruit in every good work (cf. Col 1:9-10).

At this time, I have within myself a great trust [in God], because I know – all of us know – that the Gospel’s word of truth is the strength of the Church: it is her life. The Gospel purifies and renews: it bears fruit wherever the community of believers hears and welcomes the grace of God in truth and lives in charity. This is my faith, this is my joy.

When, almost eight years ago, on April 19th, [2005], I agreed to take on the Petrine ministry, I held steadfast in this certainty, which has always accompanied me. In that moment, as I have already stated several times, the words that resounded in my heart were: “Lord, what do you ask of me? It a great weight that You place on my shoulders, but, if You ask me, at your word I will throw out the nets, sure that you will guide me” – and the Lord really has guided me. He has been close to me: daily could I feel His presence. [These years] have been a stretch of the Church’s pilgrim way, which has seen moments joy and light, but also difficult moments. I have felt like St. Peter with the Apostles in the boat on the Sea of Galilee: the Lord has given us many days of sunshine and gentle breeze, days in which the catch has been abundant; [then] there have been times when the seas were rough and the wind against us, as in the whole history of the Church it has ever been - and the Lord seemed to sleep. Nevertheless, I always knew that the Lord is in the barque, that the barque of the Church is not mine, not ours, but His - and He shall not let her sink. It is He, who steers her: to be sure, he does so also through men of His choosing, for He desired that it be so. This was and is a certainty that nothing can tarnish. It is for this reason, that today my heart is filled with gratitude to God, for never did He leave me or the Church without His consolation, His light, His love.

We are in the Year of Faith, which I desired in order to strengthen our own faith in God in a context that seems to push faith more and more toward the margins of life. I would like to invite everyone to renew firm trust in the Lord. I would like that we all, entrust ourselves as children to the arms of God, and rest assured that those arms support us and us to walk every day, even in times of struggle. I would like everyone to feel loved by the God who gave His Son for us and showed us His boundless love. I want everyone to feel the joy of being Christian. In a beautiful prayer to be recited daily in the morning says, “I adore you, my God, I love you with all my heart. I thank You for having created me, for having made me a Christian.” Yes, we are happy for the gift of faith: it is the most precious good, that no one can take from us! Let us thank God for this every day, with prayer and with a coherent Christian life. God loves us, but He also expects that we love Him!

At this time, however, it is not only God, whom I desire to thank. A Pope is not alone in guiding St. Peter’s barque, even if it is his first responsibility – and I have not ever felt myself alone in bearing either the joys or the weight of the Petrine ministry. The Lord has placed next to me many people, who, with generosity and love for God and the Church, have helped me and been close to me. First of all you, dear Brother Cardinals: your wisdom, your counsels, your friendship, were all precious to me. My collaborators, starting with my Secretary of State, who accompanied me faithfully over the years, the Secretariat of State and the whole Roman Curia, as well as all those who, in various areas, give their service to the Holy See: the many faces which never emerge, but remain in the background, in silence, in their daily commitment, with a spirit of faith and humility. They have been for me a sure and reliable support. A special thought [goes] to the Church of Rome, my diocese! I can not forget the Brothers in the Episcopate and in the Priesthood, the consecrated persons and the entire People of God: in pastoral visits, in public encounters, at Audiences, in traveling, I have always received great care and deep affection; I also loved each and every one, without exception, with that pastoral charity which is the heart of every shepherd, especially the Bishop of Rome, the Successor of the Apostle Peter. Every day I carried each of you in my prayers, with the father's heart.

I wish my greetings and my thanks to reach everyone: the heart of a Pope expands to [embrace] the whole world. I would like to express my gratitude to the Diplomatic Corps accredited to the Holy See, which makes present the great family of nations. Here I also think of all those who work for good communication, whom I thank for their important service.

At this point I would like to offer heartfelt thanks to all the many people throughout the whole world, who, in recent weeks have sent me moving tokens of concern, friendship and prayer. Yes, the Pope is never alone: now I experience this [truth] again in a way so great as to touch my very heart. The Pope belongs to everyone, and so many people feel very close to him. It’s true that I receive letters from the world's greatest figures - from the Heads of State, religious leaders, representatives of the world of culture and so on. I also receive many letters from ordinary people who write to me simply from their heart and let me feel their affection, which is born of our being together in Christ Jesus, in the Church. These people do not write me as one might write, for example, to a prince or a great figure one does not know. They write as brothers and sisters, sons and daughters, with the sense of very affectionate family ties. Here, one can touch what the Church is – not an organization, not an association for religious or humanitarian purposes, but a living body, a community of brothers and sisters in the Body of Jesus Christ, who unites us all. To experience the Church in this way and almost be able to touch with one’s hands the power of His truth and His love, is a source of joy, in a time in which many speak of its decline.

In recent months, I felt that my strength had decreased, and I asked God with insistence in prayer to enlighten me with His light to make me take the right decision – not for my sake, but for the good of the Church. I have taken this step in full awareness of its severity and also its novelty, but with a deep peace of mind. Loving the Church also means having the courage to make difficult, trying choices, having ever before oneself the good of the Church and not one’s own.

Here allow me to return once again to April 19, 2005. The gravity of the decision was precisely in the fact that from that moment on I was committed always and forever by the Lord. Always – he, who assumes the Petrine ministry no longer has any privacy. He belongs always and totally to everyone, to the whole Church. His life is, so to speak, totally deprived of the private sphere. I have felt, and I feel even in this very moment, that one receives one’s life precisely when he offers it as a gift. I said before that many people who love the Lord also love the Successor of Saint Peter and are fond of him, that the Pope has truly brothers and sisters, sons and daughters all over the world, and that he feels safe in the embrace of their communion, because he no longer belongs to himself, but he belongs to all and all are truly his own.

The “always” is also a “forever” - there is no returning to private life. My decision to forgo the exercise of active ministry, does not revoke this. I do not return to private life, to a life of travel, meetings, receptions, conferences and so on. I do not abandon the cross, but remain in a new way near to the Crucified Lord. I no longer wield the power of the office for the government of the Church, but in the service of prayer I remain, so to speak, within St. Peter’s bounds. St. Benedict, whose name I bear as Pope, shall be a great example in this for me. He showed us the way to a life which, active or passive, belongs wholly to the work of God.

I thank each and every one of you for the respect and understanding with which you have welcomed this important decision. I continue to accompany the Church on her way through prayer and reflection, with the dedication to the Lord and to His Bride, which I have hitherto tried to live daily and that I would live forever. I ask you to remember me before God, and above all to pray for the Cardinals, who are called to so important a task, and for the new Successor of Peter, that the Lord might accompany him with the light and the power of His Spirit.

Let us invoke the maternal intercession of Mary, Mother of God and of the Church, that she might accompany each of us and the whole ecclesial community: to her we entrust ourselves, with deep trust.
Dear friends! God guides His Church, maintains her always, and especially in difficult times. Let us never lose this vision of faith, which is the only true vision of the way of the Church and the world. In our heart, in the heart of each of you, let there be always the joyous certainty that the Lord is near, that He does not abandon us, that He is near to us and that He surrounds us with His love. 

Thank you!

ACHENI KULALAMIKA JUU YA MATOKEO SHIRIKIANENI NA WALIMU MJUE CHANZO NI KIPI-WASIKE

images  
Na Gladness Mushi wa KingoTanzania
……………………………………………………
WAZAZI  wametakiwa kuacha tabia ya kulalamika hasa wanapoona matokeo
ya mithiani ya kitaifa yamekuwa mabaya na badala yake wanatakiwa
kutafuta mbinu ambazo watashirikiana na walimu ili kuweza kuokoa wimbi
kubwa la watoto ambao wanashindwa kufanya vema katika mithiani ya
mwisho
Asilimia kubwa ya wazazi wao wanapenda kutoa lawama kwa walimu  na
hata wakati mwingine kwa Serikali bila kujua kuwa wao wana nafasi
kubwa sana ya kuweza kuwasaidia watoto wao pindi wanapokuwa mashuleni
na hata kabla hawajafanya mithiani yao ya mwisho
Hayo yalielezwa jana Jijini hapa na Mkuu wa shule ya Sekondari ya
Arusha Modern,Philiph Wasike wakati akiongea na wanafunzi pamoja na
wazazi katika maafali ya Saba ya kidato cha sita shuleni hapo.
Wasike alisema kuwa lawama ambazo wanatoa wazazi hasa wanapoona
matokeo ya mwisho   ni mabaya kamwe hayataweza kuwasadia na badala
yake ndio yanazidi kuangamiza watoto,hivyo basi wanatakiwa kuhakikisha
kuwa wanabuni mbinu ambazo zinaweza kuwasaidia wanafunzi wao
Aliongeza kwa kutolea mfano kuwa kwa sasa asilimia kubwa sana ya
wazazi wanawaza jinsi ya kulipa ada lakini hawawazi jinsi ya
kuwasaidia wanafunzi  hasa wale wenye uelewa mdogo hivyo mzigo huo
unaachiwa kwa walimu  pamoja na uongozi wa shule ambao wakati mwingine
nao unalemewa kwa kuwa hakuna msaada kuutoka kwa wazazi
“matokeo ya kidato cha nne yaliyoytangazwa wiki iliyopita watoto
wamefeli sana lakini kila mzazi analaumu bila ya kujua kuwa nao wao ni
chanzo kikubwa sana kwa kuwa wazazi wengi sana wanawaza jinsi ya
kupata ada hawawazi jinsi ya kuwasaidia na kuwapa moyo wanafunzi sasa
ni vema kila mzazi kabla hajatanguliza lawama mbele kwanza wanatakiwa
kuhakikisha kuwa wanafuatilia maendeleo ya wanafunzi wao kwa ukaribu
sana”aliongeza Wasike
Katika Hatua nyingine alisema kuwa nayo Serikali inatakiwa kuhakikisha
kuwa inajiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa wanaboresha zadii sekta
ya elimu kwa kuhakikisha kuwa walimun wanakuwa na maslahi mazuri ili
walimu nao waweze kuwa na moyo pindi wanapowafundisha wanafunzi
Pia alisema kuwa hata walimu wanapokosa maslahi mazuri kuna changia
kwa kiwango cha hali ya juu sana washinde kufundisha kwa Moyo hali
ambayo kwa wakati mwingine inasababisha wanafunzi wafanye vibaya
katika mithiani yao ya mwisho hali ambayo wakati mwingine inaongeza
Mbumbumbu kwenye taifa
‘sekta ya elimu ni moja ya sekta ambazo zinatakiwa kupewa kipaumbele
kikubwa sana ikiwa ni pamoja na kuangalia hata mazingira ya
kufundishia kwa kuwa hata wakati mwingine mazingira nayo yanakuwa ni
magumu sana sasa tunapolalamika kuwa matokeo ni mabaya ni lazima
tuangalie vyanzo ni nini na wala sio kumtafuta mchawi wa matokeo ni
nani”alibainisha Wasik
imani2
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Mark Wiessing,( kulia) na  Afisa Mkuu wa Biashara- M-Pesa- Jacques Voogt wakitia sahihi katika mkataba kam ishara ya ushikiano na makubaliano ya kumwezesha mteja wa NMB kufanya muamala wowote kwenye akaunti yake kwa kutumia huduma ya M-Pesa wakati maofisa wa NMB na Vodacom wakishuhudia.



No comments: