Saturday, March 2, 2013

IBADA YA MAOMBEZI DUNIANI JUMUIYA YA KIKRISTO CCT WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA YAFANYIKA KWA AMANI NA KESHO IBADA ITAENDELEA AKINA MAMA WA RUNGWE KUTEMBELEA WAGONJWA WA UKOMA NA WALEMAVU WALIOPO WILAYANI MAKETE MKOANI IRINGA NA KUTOA VITU MBALIMBALI VILIVYOCHANGWA NA WANAICHI WA RUNGWE

KABLA YA IBADA YA MAOMBEZI YALIANZA MAANDAMANO YALIFANYIKA KUTOKA KANISA LA KATUMBA LUTHERANI HADI KANISANI KATUMBA MORAVIANI
MWENYEKITI WA CCT WILAYA YA RUNGWE  ANNA CHARLES AKIONGOZA MAANDAMANO YA SIKU YA MAOMBEZI DUNIANI WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA


IBADA YA MAOMBEZI WILAYANI RUNGWE KWA  CCT ILIONGOZWA NA                  ROSTA MWANKENJA KATIBU WA CCT WILAYA YA RUNGWE
KWAYA YA KATUMBA MORAVIANI WAKIMWABUDU MUNGU ALIYE HAI  ILI ASIKIE MAOMBI YA WATU WAKE
MCH ANGETILE KILINDU AKIHUBIRI LEO SIKU YA MAOMBEZI DUNIANI, KATIKA MAHUBIRI YAKE AMESISITIZA WAJIBU WA MWANAMKE KATIKA JAMII ILI TAIFA ILIPATE KUFANIKIWA, YAPASWA MWANAMKE KUOMBEA SANA KWA MUNGU FAMILIA NA JAMII ILI KUWA NA MSHIKAMANO NA AMANI KATIKA TAIFA LETU.                   (MATHAYO 25; 31 - 40 ASIKIAYE NA AFAHAMU)
MUDA WA MAOMBI UKAFIKA
MAOMBI YALIHUSU MAMBO MAWILI MOJA NI KUOMBA KILA MTU KWA HITAJI LAKE KWA MUNGU WAKE NA SUALA LA PILI NI KILA MTU KUOMBEA AMANI TAIFA LETU LA TANZANIA NA ULIMWENGU WOTE
MWENYEKITI WA CCT WILAYANI RUNGWE ALIPATA NAFASI YA KUSOMA RISALA KWA MGENI RASM

MCH MWAISANGO AMBAYE NI KATIBU MSTAFU WA KANISA LA MORAVIANI
MKUU WA WILAYA YA RUNGWE  CHRISPIN MEELA AKIONGEA NA AKINA MAMA NA WATU MBALIMBALI KUHUSU UMUHIMU WA SIKU YA MAOMBI DUNIANI.AMESEMA KUWA AKINA MAMA NDIO NGUZO KUU YA AMANI NA UPENDO KATIKA JAMII, PIA AMESEMA KUWA KUPOROMOKA KWA MAADIRI NI KWASABABU WAZAZI HASA AKINA MAMA WAMEPUNGUZA WAJIBU WA KULIOMBEA TAIFA ZAIDI AMEWATAKA WANANCHI HASA WA RUNGWE NA TAIFA KWAUJUMLA KUIFANYA WILAYA YA RUNGWE KUWA SEHEM YA AMANI HIVYO YEYOTE ANAYELETA UCHOCHEZI AKAFANYIE KWAO NA SI WILAYANI RUNGWE ZAIDI AMEWATAKA WANA RUNGWE KUWA NA UTARATIBU WA KUKAA MEZANI KUJADIRI CHANGAMOTO NA MAENDELEO YA WILAYA YA WILAYA
BAADA YA IBADA YA MAOMBEZI LEO IBADA ITAENDELEA KESHO KWA JUMUIYA YA CCT WILAYA YA RUNGWE MWAKA KUSAFIRI KWENDA WILAYA YA MAKETE KATIKA KITUO CHA WALEMAVU NA WAGONJWA WA UKOMA ILI KUTOA SALAM NA VITU MBALIMBALI AMBAVYO WANAWAKE NA JAMII YA WATU WA RUNGWE WAMEJITOLEA WA WATU WA MAKETE AMBAO KWA MAKUSUDI YA MUNGU WANA ULEMAVU NA WENGINE KUPATWA NA TATIZO LA UKOMA

 

AKWIMU ZA WIZI WA WATOTO MKOA WA MBEYA

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAWATAHADHARISHA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MBEYA KUWA  MAKINI NA MIENENDO YA WATOTO WAO WAENDAPO NA WARUDIPO SHULENI NA WAWAPO MICHEZONI. HAKIKISHENI WANARUDI NYUMBANI MAPEMA, WAFUNDISHENI KUTOPOKEA ZAWADI AU LIFTI KUTOKA KWA WATU WASIOWAFAHAMU, KWA KUFANYA HIVYO ITASAIDIA KUWAEPUSHA WATOTO WETU NA VITENDO VYA WIZI WA  WATOTO UNAOWEZA KUJITOKEZA . TAHADHARI HII INATOKANA NA KUIBUKA KWA WIMBI LA MATUKIO YA WIZI WA WATOTO WADOGO.

TAKWIMU ZA WIZI WA WATOTO MKOA WA MBEYA

JANUARI – FEBRUARI 2013 WIZI WA WATOTO

MBEYA             Matukio 2
-       Watoto walioibwa 2, Me 1,Ke 1
-       Watuhumiwa      Me 1,Ke 1
[Wamepatikana]
MOMBA            -     Tukio 1
-       Watoto walioibwa       Ke 1
-       Watuhumiwa  -Nil
Amepatikana
KYELA                        -     Tukio 1
-       Watoto walioibwa Ke 1
Amepatikana
 JANUARI – DESEMBA 2012 WIZI WA WATOTO

MBEYA             Matukio 4
-       Watoto walioibwa  Me 3, Ke 1
-       Wamepatikana wote wazima
-       Watuhumiwa      Me 3, Ke 1
RUNGWE            -     Kesi 2
-       Watoto walioibwa 2, Me 1,Ke 1
-       Wamepatikana
-       Watuhumiwa      Me 1,Ke 1
MBARALI             -     Kesi 1
-       Mtoto 1
-       Amepatikana
Uchunguzi wa mashauri hayo bado unaendelea ili kubaini chanzo cha matukio hayo, yeyote mwenye taarifa kuhusiana na matukio haya azitoe kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.
 
 


Post a Comment