|
NILIPOFIKA
KATIKA KITUO CHA WAGONJWA WA UKOMA KILICHOFUNGULIWA MWAKA 1895 NA
KUJENGWA NA JUMUIYA YA MADOLA KWA USHIRIKIANO WA WAKOLONI NA KITUO
KUFUNGWA MWAKA 1950 NA UGONJWA WA UKOMA UKATANGAZWA KUISHA TANGANYIKA
LEO NIMEKUTANA NA TANGAZO HILI
|
|
MUONEKANO WA MAKETE WILAYANI RUNGWE KIJIJI WANAPOISHI WAGONJWA WA UKOMA. UGONJWA WA UKOMA KWA KIRUGHA CHA KINYAKYUSA UNATAMBULIKA KUWA NI MAKETE HIVYO ENEO HILI LIMETAMBULIKA KUWA MAKETE KWAKUWA WAGONJWA WA UKOMA WANAISHI HAPA NA MAENEO HAYA ILIKUWA NI MAPORI YA KUTISHA MAANA WAGONJWA ZAMANI WALIKUWA WANATENGWA NA JAMII KWA HOFU YA KUAMBUKIZA WENGINE |
|
MUONEKANO WA MAJENGO YALIYOKUWA KITUO CHA WAGONJWA WA UKOMA MAKETE WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA |
|
MOJA YA MAKANISA YALIYOPO KITUONI HAPO YAKIWA YAMEFUNGWA |
|
WANANCHI WA KIJIJI CHA KISONDELA WAKIWA WANAPITA KITUONI HAPO HUKU WAKIELEZEA KUWA KITUO KIMETELEKEZWA NA SERIKALI NA HAKUNA MATUMIZI MMBADALA YALIYOLENGA KUTUMIA KITUO HICHO HIVYO VITU VINGI VIMEIBWA NA KUBAKI MAJENGO JAPO KWA SASA NI IMARA LAKINIYANAHITAJI USIMAMIZI |
|
KATIKA KITUO HICHO JENGO MOJA NDILO LINATUMIKA KAMA OFISI YA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA KISONDELA |
|
KWAKWELI KWAKUWA ILIKUWA MALA YANGU YA KWANZA SIJAELEWA KINACHOENDELEA KATIKA KITUO HIKI NAJIULIZA KWANINI PASIENDELEZWE? TUNAHITAJI VYUO VYA VETA, HIGH SCHOOL, HOSPT, KWANINI HAPA TANGU KITUO KIFUNGWE MWAKA 1950 NA WAGONJWA WENGI WAMEFIA HAPO NA WENGINE KUPEWA MAKAZI AMBAO HADI SASA WATOTO WAO WAPO KATIKA KIJIJI HICHO SASA KWANINI PASIENDELEZWE ILI WANANCHI WAKAFAIDIKA NA KITUO HIKI KULIKO SASA KILIVYO? |
|
NIKAAMUA KUJURUDIA KANISANI AMBAKO AKINA MAMA WA JUMUIYA YA KIKRISTO WILAYANI RUNGWE WAMETEMBELEA WAATHIRIKA WA UGONJWA WA UKOMA WANAOISHI KIJIJI CHA KISONDELA WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA |
|
IBADA IMEFANYIKA KANISA LA MORAVIANI MAKETE WILAYANI RUNGWE |
|
NIA NA MADHUMUNI ILIKUWA NI IBADA YA MAOMBEZI NA KUMSHUKURU MUNGU |
|
IBADA IKIENDELEA KWA AMANI NA FURAHA MAANA HAYAYOTE HAYATAFANYIKA KAMA TANZANIA IKIINGIA MACHAFUKONI KAMA AMANI ILIYOPO ITACHAFULIWA KILA MTU YAMPASA KUILINDA AMANI ILIYOPO |
|
KATIBU WA UMOJA WA WANAWAKE WA CCT WILAYANI RUNGWE ROSTA MWAMBENJA AKIONGEA NA WAUMINI NA WAGONJWA WA UKOMA JINSI MUNGU ANAVYO WAPENDA KWA KUPITIA WATU MBALIMBALI KUJITOLEA VITU KAMA NGUO, PESA, NA VYAKULA VITAKAVYOGAWIWA KWA UPENDO WA KUWAJARI WAGONJWA WASIO JIWEZA KWA KUWA MAANDIKO YAMESEMA IBADA YA KWELI NI KUWAJARI WASIOJIWEZA |
|
WAKIWA NJE YA KANISA TAYARI KWA KUPEWA MISAADA |
|
MZEE ALBETO MWALUANDA AKIONGEA KWA UCHUNGU JINSI WASIVYOPATA HUDUMA ZA MSINGI HUKU TATIZO LA UKOMA LIKIONGEZEKA KIJIJINI HAPO NA SERIKALI KUWATELEKEZA HATA KUWATEMBELEA IMEKUWA SHIDA. PIA AMESEMA KUWA SERIKALI ISIMAMIE AMANI YA TANZANIA MAANA KAMA NCHI IKIINGIA MACHAFUKONI JE WAO KAMA WAKOMA WATAKIMBILIA WAPI? |
|
MZEE WA KANISA LA MORAVIANI MAKETE AKISHUKURU WAGENI WA CCT KWA KUTEMBELEA WAKOMA JAPO ALIKUWA NA WITO KWA SERIKALI KUFUFUA HUDUMA TENA MAANA WAGONJWA WANAZIDI KUONGEZEKA KIJIJINI HAPO |
|
BAADHI YA WAGONJWA WA UKOMA |
|
MUDA WA MAOMBEZI KWA WAGONJWA NA KUOMBEA AMANI YA NCHI YA TANZANIA |
|
KIONGOZI WA WAGONJWA WA UKOMA AKIPOKEA ZAWADI KWA NIABA YA WENZAKE |
|
ZAWADI ZIKATOLEWA NA WANAWAKE WA CCT WILAYANI RUNGWE KWA WAATHIRIKA WA UKOMA MAKETE KIJIJI CHA KISONDELA |
|
HUWEZI AMINI KUWA BIBI HUYU HAWEZI KUTEMBEA VYEMA LAKINI HAPO ANASHUKURU KWA CCT KWA KUWAKUMBUKA NA KUWAPA MSAADA WA NGUO, CHAKULA, NA FEDHA IKIWA NI ALAMA YA UPENDO KWAO |
|
BIBI KWA MSAADA WA MJUKUU WAKE WAKIFUNGA ZAWADI ZAO ILI WARUDI MAKWAO |
|
MAMA AKIFUNGA ZAWADI ZAKE |
|
BALOZI WENU NIKIONGEA NA MZEE SWILLA MMOJA WA WAATHIRIKA WA UKOMA AMBAPO NILIPATA MENGI SANA KWAKE NA KWANINI SERIKALI NA JAMII IMEWATENGA KWA KIASI KIKUBWA KWA KUTOWAKUMBUKA KWA KUPEWA HUDUMA ZA MSINGI KAMA DAWA, MAVAZI NA MALAZI, LAKINI SWILLA ANASEMA WAGONJWA WA UKOMA BADO WAPO NA WANATESEKA SANA HIVYO AMEIOMBA JAMII NA SERIKALI KUWATEMBELEA ILI KUJUA MAHITAJI YAO YA MSINGI. PIA AMESEMA UGONJWA WA UKOMA UMEKUWA TISHIO MAENEO HAYO KWAKUWA SERIKALI HAIJAWEKA MIKAKATI YA KUTOKOMEZA UGONJWA HUO HIVYO WATU WENGI WATAENDELEA KUATHIRIKA ( KINGOTANZANIA INATOA WAZO KWA WADAU WA HUMU NDANI KUWASAIDIA WENZETU WANAOUMWA UKOMA ILI TUWE NA WAZO LA PAMOJA NI JINSI GANI TUTAKAVYOWAFIKIWA WENZETU WENYE UHITAJI HUU WA MATIBABU, MALAZI, MAVAZI NA ZAIDI CHAKULA) ASANTE NDIMI BALOZI WENU KINGO | |
|
|
ASKOFU DR ESRAEL PETER MWAKYOLILE AONGOZA MAZISHI YA MCHUNGAJI YOHANA MWASAMPETA KKKT USHARIKA WA MASEBE WILAYANI RUNGWE MKOA WA MBEYA
|
ASKOFU DR ESRAEL MWAKYOLILE KKKT DAYOSISI YA KONDE |
|
USHARIKA WA MASEBE MAZIKO YALIPOFANYIKA |
|
MFIWA MCH MWASAMPETA MDOGO WA MAREHEM AKIWA NA WACHUNGAJI WENZAKE KABLA YA IBADA KUANZA |
|
WACHUNGAJI WA KKKT DAYOSISI YA KONDE WAKIWA WAMEBEBA JENEZA KUELEKEA MAKABURINI |
|
JENEZA LIKISHUSHWA KABURINI |
|
YOHANA MWASAMPETA , ULIKUJA KWA UDONGO, NA UTARUDI KWA UDONGO, SIKU YA MWISHO UTAFUFULIWA,. NIMANENO YA MWISHO BABA ASKOFU MWAKYOLILE AKIHITIMISHA MAZIKO YA MCHUNGAJI YOHANA MWASAMPETA |
|
MKE WA MAREHEM NA WAFIWA WENGINE |
|
MCH MWASAMPETA MDOGO WA MAREHEM MWENYE SUTI NYEUPE AKIWA ANARUDISHIWA UDONGO KATIKA KABURI LA KAKA YAKE |
ZAIDI YA ABIRIA 50 WA
BASI LA SUMRY LITOKALO SUMBAWANGA KUJA MBEYA WANUSURIKA KUFA KWENYE
AJALI ILIOTOKEA MPAKANI MWA SONGWE NA MBOZI MBEYA
*Azindua tume ya watu 15, aipa wiki sita kukamilisha kazi
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda
amezindua Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya
mtihani wa kidato cha nne yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na
kuwataka wajumbe wa Tume hiyo watafute kiini cha mserereko wa kushuka
kwa ufaulu kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi
(Jumamosi, Machi 2, 2013) wakati akizungumza na wajumbe wa Tume hiyo
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Dk. Shukuru Kawambwa.
“Nimetafuta takwimu za tangu
mwaka 2005, Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani na kubaini
kuwa tangu wakati huo hadi mwaka 2009 tulikuwa tukifanya vizuri, lakini
kuanzia mwaka 2010 hadi 2012 matokeo yamekuwa yakishuka sana,”
aliwaambia wajumbe wa Tume hiyo na waandishi wa habari waliohudhuria
uzinduzi huo.
Alisema hali hiyo haikuwa kwenye
shule za sekondari za umma (kata) peke yake bali hata kwa shule za
Serikali, za watu binafsi na kwenye seminari ambazo kwa miaka mingi
zimekuwa na sifa ya kufanya vizuri kuliko shule za kawaida.
Akitoa mfano, Waziri Mkuu
alisema: “Mwaka 2005 kiwango cha ufaulu kilikuwa asilimia 89.3; mwaka
2006 asilimia 89.12; mwaka 2007 asilimia 90.6; mwaka 2008 asilimia 83.6
na mwaka 2009 asimilia 72.5, hapa napo tulikuwa bado tuko vizuri japo si
sana ikilinganishwa na miaka mine iliyotangulia.”
“Lakini mwaka 2010, kiwango cha
ufaulu kilishuka na kufikia asilimia 50.4, mwaka 2011 kilipanda kidogo
na kufikia asilimia 53.6 na kilishuka zaidi mwaka jana ambapo kilifikia
asilimia 34.5. Hapa ni lazima mtu utapata maswali ya msingi na kujiuliza
nini kimetokea katika miaka ya hivi karibuni,” alisema.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwaonesha ng’ombe wafugaji wa Kabila la
Wamasai waliomtembelea katika shamba lake la mifugo kijijini Kwake
Msoga,Kata ya Chalinze,wilayani Bagamoyo jana(Jumapili)(picha na Freddy
Maro).
……………………………………………………………..
Na Freddy Maro Msoga,Bagamoyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
ametoa wito kwa wafugaji nchini kupima na kupanga ardhi kwaajili ya
ufugaji wa bora wenye tija na kuepusha migogoro kati ya wakulima na
wafugaji inayotokana na ufugaji wa kuhamahama kutafuta malisho.
Rais Kikwete alitoa rai hiyo
wakati alipokuwa akizungumza na wafugaji wakabila la wamasai kutoka mkoa
wa Pwani na Morogoro waliomtembelea nyumbani kwake kijijini Msoga kata
ya Chalinze, wilayani Bagamoyo jana(Jumapili).
“Ni lazima mtambue kwamba ufugaji
wa kuhamahama hauna tija kwakuwa watu wengi sasa wametambua thamani ya
ardhi wanaipima na kuimiliki na hivyo maeneo ya kuchunga mifugo
yanapungua.Huu ni wakati muafaka wa kupima ardhi na kuimiliki kwaajili
ya ufugaji wa kisasa,” alisema Rais Kikwete.
Sambamba na kutenga maeneo maalumu
kwaajili ya ufugaji Rais Kikwete amewahimiza wafugaji hao kuotesha
majani kwaajili ya malisho ya mifugo ili kuepuka upungufu wa lishe ya
wanyama wakati wa kiangazi na kuhakikisha mifugo hiyo inabakia na afya
njema kwa faida ya wafugaji.
Wakizungumza awali,wafugaji hao
waliiongozwa na kiongozi wao Mkuu Laiboni Tikwa Moreto walimshukuru Rais
Kikwete kwa kuwajengea Shule ya Sekondari kwaajili ya Watoto wa
wafugaji ambayo sasa hivi ina jumla ya wanafunzi 146.
“ Tunakushukuru sana kwa
kutujengea shule ya Sekondari Moreto na watoto wetu sasa wamepata fursa
ya kusoma na tuna kuomba utusaidie ili tuweze kuongeza madarasa,mabweni
na maji ya kutosha ili wanafunzi waliopo waweze kusoma kwa
ufanisi,”walisema katika risala yao kwa Rais Kikwete.
Akijibu Rais Kikwete aliwapongeza
kwa kuitunza shule hiyo na kusema kuwa maisha ya kuhamahama kwa
wafugaji yanawakosesha watoto wao fursa ya kupata elimu na kuahidi
kuendelea kuisadia shule hiyo ili watoto wengi zaidi waweze kunufaika na
elimu ya sekondari.
Baadaye wafugaji hao walipata
fursa ya kutembelea shamba la mifugo la Rais Kikwete kijijini Msoga na
kujionea ufugaji wa kisasa unaozingatia kanuni bora za kitaalamu ambapo
ngo’mbe mmoja anaweza kufikia uzito wa kilo miasaba.
No comments:
Post a Comment