Wednesday, March 6, 2013

TEMBEA UJIONEE MWENYEWE WATU WAMEJENGA NYUMBA NZURI LAKINI CHOO MMMMMMM

WILAYANI RUNGWE MAENEO YA KATUMBA LEO
BAADA YA KULA NIKAOMBA KWA WENYEJI NIENDE MJENGONI KUFIKA MJENGONI SIKUONA NDOO YA MAJI NIKAKUTA MABUNZI YA MAHINDI NIKAAMUA KUHAIRISHA  NIKAENDA KWA JIRANI MWINGINE
KUFIKA KWA JIRANI MWINGINE MMMMMMMM HATA KUINGIA NIKAOGOPA

NIKAENDA KWA JIRANI WA TATU HAPO NIKAISHIWA NA NGUVU NILICHOKUTANA NACHO NIKAAMUA KUHAIRISHA TU HADI NIRUDI NILIKOZOEA HOME KWANGU MAANA NIKASHITUKIA WENYEJI WALIKUWA WANANIONA KAMA KITUKO SASA

 

CHAMA CHA WAENDESHA BAJAJI MKOA WA MBEYA CHATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA UYOLE MBEYA

Chama cha waendesha bajaji na walezi wao wakikabidhi msaada wa chakula kwa mlezi wa kituo cha Nuru kilichopo Uyole jijini Mbeya
Chama cha waendesha bajaji wakiwa katika picha ya pamoja na watoto hao yatima wa kituo cha Nuru
Mlezi wa madereva wa bajaji Mwaka Mwakisu amewasisitizia madereva bajaji kuwa kile kifaida kidogo wanachopata katika kazi yao ni muhimu kuwakumbuka watoto yatima kwani ni jukumu letu kuwalea watoto hawa maana ni wetu sote pia vijana tuache ngono uzembe alisema Mwakisu
Mlezi watoto hao katika kituo hicho, Rose Kawiche, akiwashukuru chama hicho cha madereva wa bajaji kwa moyo wao huo wa kuwajali watoto hao na amewaomba wasichoke kuwatembelea mara kwa mara watoto hao kujua wanaendeleaje
Mwenyekiti wa waendesha bajaji mkoa wa Mbeya Iddi Ramadhani amewataka vijana wenzie kuacha tabia ya kuwapa mimba mabinti na kicha kuwaacha matokeo yake hao mabinti nao hutupa hao watoto yaani huwezi amini hapa huwenda mmoja wetu anamtoto hapa hivyo basi jamani tuwatunze hawa watoto na kuwasaidia mara kwa mara maana huyu mama mlezi peke yake hawezi alisema Iddi
Katibu wa bajaji mkoa wa Mbeya  Ernest Mwaisango amesema chama chao sasa kimejipanga vizuri kuwasaidia watoto yatima na wanaje mkoa wa mbeya kwani kipato chao kidogo kitatosha kugawana na yatima hao
Mlezi wa chama cha madereva wa bajaji Aneth au mama Somji amewataka wanawake waache kutupa watoto maana sasa tunawapa watu wengine shida ya kuwalea
Wanachama wa bajajiwakiondoka mara baad ya kutoa msaada wa chakula kituoni hapo
  Chama Cha Waendesha Bajaji Jijini Mbeya, kupitia kwa mlezi wao, Mwaka Mwakisu wametembelea  kituo cha kulelea watoto yatima cha Nuru Kilichopo Uyole ambapo wametoa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo ni vyakula vyenye thamani  ya shilingi 320,000.
Mlezi wa chama hicho cha waendesha Bajaji, Mwaka Mwakisu, alitumia fursa hiyo  kuwataka vijana na jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa huruma na kutojihusisha na matukio ya unyama kama hayo ya kutupa watoto wasiokuwa na hatia.
 “Kama tulivyosikiwa wenyewe vijana hapa historia ya watoto hawa kutoka kwa mlezi wao, alivyosema kuwa tangu kuanzishwa kwake kwa kituo hiki walianza na watoto wawili mwaka 2013 lakini leo hii wamefikia idadi ya watoto 17 na kibaya zaidi mama huyu anasema watoto wamekuwa wakiokotwa wakiwa wametupwa majalalani na kutelekezwa”  
“Jamani hali hii inatia uchungu kwa kweli watoto kama hawa  hali waliyonayo ni lazima ifike mahala jamii hususani akina dada kuwa na moyo wa huruma  kuliko kuwa na moyo wa kikatili kama huu” alisema Mwakisu.
Aidha, Mwakisu aliwataka vijana na jamii kwa ujumla kuwa walinzi wa karibu kwa akina mama ambao wanaona wapo katika hali ya ujauzito kuwachunga na kwamba pindi atakapoonekana kutokuwa na ujauzito ni bora akaulizwa  na kama hana mtoto achukuliwe hatua zaidi ili kuweza kupunguza idadi ya watoto yatima.
 Awali Mlezi watoto hao katika kituo hicho, Rose Kawiche, alisema kuwa ongezeko la watoto wanaotupwa limekuwa likiongeza siku hadi siku.
“Kwa kweli idadi ya watoto imekuwa ikongzekeza siku hadi siku kwa mfano kwa mwaka jana pekee tumepokea watoto watano na sasa ninawatoto 17, na hawa wote ni wale wamekuwa wakiokotwa majalalani wakiwa bado kichanga na kwamba kama hawa mnaowaona hapa umri wao hauzidi miezi sita na saba” mpaka  miaka mitano alisema mama huyo huku akionekana kutokwa na machozi.

DOGO AAMBIWA NYIE NDIYO MNAOTULETEA ZIRO TWENDE SHULE HII MBEYA VIJIJINI

MWANAFUNZI EMMANUEL ZAWADI WA SHULE YA MSINGI RUANDA KATA YA ILEMBO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI AKIKAMATWA NA WANAFUNZI KUMPELEKA SHULE SABABU YA UTORO DOGO HUYO HUWA HAENDI SHULE HUSHINDA VICHAKANI LEO KAPATIKANA
NYIE UTORO WENU NDIYO UNASABABISHA SHULE ZETU ZIPATE ZIRO NYINGI WALISIKIKA WANAFUNZI HAO WAKISEMA 


Picha na Ezekiel Kamanga  Mbeya

 

Makubwa haya...!Uchaguzi ukifika itakuwaje?

225067 582517745109073 1148771816 n 8147b
Picha na Jem

 

Absalom Kibanda avamiwa,ajeruhiwa vibaya

 

image
Pichani ni Ndugu Absalom Kibanda akiwa amelazwa kwenye moja ya chumba cha matibabu,hospitali ya Taifa Muhimbili.Get Well soon Absalom Kibanda.Picha kwa hisani ya Mtandao wa Mabadiliko.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri,na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa New Habari Coperations Ltd, Ndugu Absalom Kibanda, amevamiwa usiku  wa kuamikia leo akiwa anashuka nyumbani kwake Mbezi Beach na watu wasiofahamika na kumpiga kichwani. Amepata majeraha Makubwa kichwani na hasa jichoni,aidha taarifa inaeleza kuwa baada tukio hilo Kibanda alikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa Matibabu.
Wadau hii ni taarifa ya kushtua sana,lakini tutazidi kutaarifiana kadiri ya habari zitakavyokuwa zinapatikana,kikubwa tumwombee Mungu amponye haraka mpiganaji mwenzetu.
                   
  

Takukuru yanasa walimu wakitoza rushwa wanafunzi


Na: Godfrey Kahango, Mbeya
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoani Mbeya imewanasa walimu wawili wa Shule ya Sekondari ya Forest kwa tuhuma za kushawishi na kupokea rushwa ya kati ya Sh500 na Sh1,000 kwa wanafunzi wanaochelewa asubuhi. Imeelezwa kwamba kutokana na mtindo huo, walimu hao wamekuwa wakijikusanyia wastani wa Sh150,000 kwa siku. Walimu hao walikamatwa saa 8.30 mchana jana shuleni hapo baada ya baadhi ya wanafunzi kutoa taarifa Takukuru za kuwapo kwa tabia hiyo ya kulazimishwa kutoa fedha wanapokuwa wamechelewa kufika shuleni asubuhi. Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Mbeya, Daniel Mtuka, aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kwamba walimu hao
(majina tunayo), walitiwa mbaroni wakati wakiwatoza wanafunzi hao fedha hizo.
Hadi wanakamatwa, walimu hao walikutwa na kiasi cha Sh64,000 walizokuwa wamezikusanya kutoka kwa wanafunzi hao, huku pembeni kukiwa na rundo la fimbo lililokuwa likitumika kuwachapa.
Mtuka alisema waligundua kuwa walimu hao walikuwa wanatengeneza kiasi cha 150,000 kwa siku kutokana na wastani wa wanafunzi 300 waliokuwa wanawachapa. Shule hiyo ina wanafunzi 900.
“Walimu hao wamekuwa na mradi huo wa kuwalipisha wanafunzi na wanaoshindwa kulipa walikuwa wanachapwa viboko visivyokuwa na idadi,” alisema na kuongeza:
“Kwanza walimu hao walikuwa wanachukua majina ya wanafunzi waliochelewa kutoka kwa walimu walioko zamu na kuanza kuwaita kwenye chumba walichokuwa wanakiita ‘Gwantanamo’ na kutoza fedha hizo.”
Walimu hao walichukua jina hilo kutoka Kambi ya Guantanamo Bay iliyoko karibu na Kisiwa cha Cuba, ambako Marekani imeweka kambi ya kijeshi.
Kambi hiyo ilianzishwa Januari, 2002 wakati Marekani ikiwa chini ya George Bush kwa ajili ya kuhifadhi mateka wa kivita kutoka Afghanistan na Iraq.
Kwa nyakati tofauti, wanafunzi walisimulia vituko vya walimu hao.
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza, (jina tunalihifadhi), alisema kuwa mwanafunzi ambaye alikuwa hana fedha za kuwapatia, alikuwa anaambiwa kuweka kichwa chini, miguu na miguu juu kisha mwalimu huyo anamchapa kwenye makalio hadi sehemu unapopita uti wa mgongo.
“Baada ya kuona vitendo hivyo vinaendelea, huku uongozi wa shule ukiwa umekaa kimya, tukaamua kuwaambia viongozi wa serikali ya wanafunzi na ndiyo waliokwenda Takukuru,” alisema.


 

No comments: