Katika hali isiyokuwa ya kawaida
halmashauri ya wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imeingia lawamani baada ya
kuwalipa walimu wapya viwango tofauti vya malipo ya kujikimu tofauti na
ilivyoagizwa na serikali.
Hatua hiyo imekuja baada ya
walimu hao kuripoti katika halmashauri hiyo na kutakiwa kulipwa fedha zao kwa
mujibu wa mchanganuo wa serikali.
Walimu wapya wenye shahada
walitakiwa kulipwa kiasi cha sh.315,000/=, badala yake wamelipwa sh.240,000/=
na walimu wa stashahada walitakiwa kulipwa 240,000 na badala yake wamelipwa
190,000/= .
Hali hiyo imesababisha walimu
hao kuhoji kwa nini wao wapewe hivyo ili hali wenzao wa mikoa na halmashauri
zingine wakipewa pesa kamili?
Vuta ni kuvute hiyo
iliyochukua takribani siku mbili haikuzaa matunda baada ya maofisa wa
halmashauri hiyo kudai kuwa pesa hizo zinalipwa kutokana na umbali wa kituo cha
kazi cha mwalimu husika.
Hata hivyo majibu hayo
hayakuwaridhisha walimu hao na kuendelea kutafuta haki yao na kuamua kwenda kwa
Mkurugenzi wa halmashauri yao lakini haki yao haikupatikana kutokana na mkurugenzi
huyo kutotaka kuonana na mtu yeyote hivyo kuwaambia katibu muhtasi kuwa hayuko
tayari kuonana na mtu yeyote.
Baada ya kuona haki yao
haipatikani waliamua kumpigia simu na aliwajibu kuwa wapeleke suala hilo kwa
maandishi ili alishugulikie, ndipo siku iliyofuata mkuu wa wilaya hiyo ya Rungwe
alikutana na walimu hao na maafisa wa halmashauri na kuanza kufanya nao
mazungumzo.
Lakini katika hali ya
kushangaza mkuu huyo wa wilaya alifanya kikao cha faragha kwanza na maafisa wa
halmashauri na baadae ndipo akaja kutoa maamuzi na kuwaambia kuwa wao wamepewa
fedha kidogo kutoka serikali kuu na ndio maana wameamua kuwapa hizo, lakini
majibu hayo yalikuwa yakitofautiana na majibu ya siku zingine yaliyo sema fedha
zinatolewa kwa kuangalia umbali wa eneo la kituo cha kazi.
Baada ya majibu hayo walimu
hao walionekana wakiwa na nyuso za huzuni mithili ya mtu aliye achwa nyikani.
“Haiwezekani wenzetu wa
wilaya zingine wapewe stahiki zao zote halafu sisi tunapewa nusu, hakika huu ni
ufisadi wa machomacho tukienda kufundisha madudu tusilaumiwe maana watu
tumefika tangu wiki iliyopita halafu hatuna nyumba tuna lala gesti leo
tunalipwa fedha kidogo hakika tutafika tu.” Alisikika mwalimu mmoja akihamaki.
Hii ni mara ya pili halmashauri
hiyo kuingia lawamani baada ya mwaka jana 2012 kufanya hivyo hivyo hadi walimu
waliamua kuwafungia ofisini maofisa wa halmashauri hiyo na ndipo wakaamua
kuwalipa na hii inaonekana wazi kwa halmashauri hiyo kufanya mtindo huu kila
mwaka.
"Tunaiomba serikali na hasa
TAMISEMI kuingilia kati suala hili na kuwachukulia hatua watumishi wa serikali
wa halmashauri hii ili hali hiyo isijitokeze tena na walimu tupewe haki yetu"
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI ITALAZYA WILAYANI MBEYA VIJIJINI WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKANA NA UKOSEFU WA VYOO
HIVI NI VYOO VYA WAALIMU WA SHULE HIYO |
WANAFUNZI SASA HUJISAIDIA KATIKA VICHAKA HIVI KWAKWELI HATARI SANA KUKUTANA NA NYOKA NA WADUDU WENYE SUMU KALI picha na kamanga wa mbeyayetu |
KIBANDA ASAFIRISHWA KWENDA KUTIBIWA AFRIKA YA KUSINI
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, akiwa ndani ya Ndege ya Flightlink.
Absalom
Kibanda akiwa na mkewe ndani ya Ndege, Anjella Semaya, tayari kuanza
safari ya kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa matibabu.(Picha na Amanitanzania)
Baadhi ya waandishi na viongozi wa jukwaa la wahariri wakiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi kwa ajili ya kumjulia hali.
Absalom Kibanda akiwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kabla ya kusafirishwa kwenda Afrika ya kusini.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege ya Flightlink wakimpandisha Absalom Kibanda ndani ya Ndege.
akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimili
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Hussein Bashe akizungfumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kutekwa kwa, Absalom Kibanda
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freema Mbowe akimjulia hali Absalom Kipanda katika Hospitali ya Taifa ya Mhumbili Dar es Salaam. Picha na Amanitanzania
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMJULIA HALI MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI ABSOLOM KIBANDA MUHIMBILI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, ambaye pia ni
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absolom
Kibanda, aliyelazwa katika Wodi ya Moi katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, baada ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia
leo wakati akiingia nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es
Salaam. Picha na OMR
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya New Habari 2006 Ltd, Absolom Kibanda, akionekana
jinsi alivyojeruhiwa.
SEHEMU YA CAVA YA ALBAM YA UMENIINUA |
MAANDALIZI YA ALBAM YA VIDEO YA UMENIINUA |
ALBAM INA NYIMBO 8 NA WIMBO MKUU UKIWA NI (UMENIUA) IKO TAYARI KUINGIA SOKONI. MUIMBAJI WA NYIMBO ZA INJIRI BETRICE KITALI AMESEMA KUWA WATU WASUBIRI KUBARIKIWA KUTOKANA NA UJUMBE WA MUNGU ALIYE HAI ULIOMO KATIKA NYIMBO HIZI ZAIDI ANAWATAKIA AMANI WATANZANIA KWAKUWA AMANI NA UPENDO NDIO SIRAHA YA MAISHA YA WACHA MUNGU |
No comments:
Post a Comment