Sunday, December 30, 2012

MAGHALA YA KUHIFADHIA BIDHAA ZA WAFANYA BIASHARA WA MWANJELWA YATEKETEA KWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO. SHUHUDIA

MBEYA TENA NA MOTO KWA WAFANYA BIASHARA
Maghala ya kuhifadhia bidhaa mbali mbali za wafanya biashara wa mwanjelwa Mbeya yameteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo maghala hayo yapo maeneo ya uwanja wa ndege wa mwanjelwa
Wanausalama wakiwa makini na vibaka ambao walitaka kuvamia eneo hilo la moto kutaka kupora mali kujifanya wanaokoa mali hizo
Hakika kikosi cha zimamoto cha jiji la mbeya wakishirikiana na kikosi cha zimamoto uwanja wa ndege wa songwe walijitahidi kuuzima moto huo ingawa mara kwa mara waliishiwa maji kutokana na uwezo mdogo wa magari hayo kubeba maji ya kuzimia moto
Moja ya gari ya kampuni ya jambo ikiungua moto katika maghala hayo
Moja ya wafanyabiashara hao ambaye anamizigo yake katika maghala hayo akikatazwa na mwanausalama kwamba asiende kmuokoa mali zake kwani moto ni mkubwa awaachie kikosi cha zimamoto kifanye kazi yake
Mfayabiashara huyo haamini mcho yake huku akilia akiona bidhaa zake zikiteketea kwamoto
Kama kawaida kmufa kmufaana hapa vibaka wakigombea sahani na masufuria kwenye box
Hakika jeshi la polisi linastahili pongezi kwa kazi kubwa ya kuokoa mali za wafanyabiashara ambao bidhaa zao zilikuwa katika maghala hayo hapa polisi wakiwa wamemshika kibaka aliyetaka kuiba mafuta ya kupikia
Kwakweli ilikuwa hatari kwani vibaka walikuwa wanarusha mawe kwa polisi na kwa baadhi ya magari hapa hili gari ikitoka katika ghala hilo likiwa limevunjwa kioo cha mbele
Baadhi ya wananchi wengi wakiwa katika tukio hilo
Haya si maji bali ni mafuta ya kula ambayo yamemwagika baada ya blastiki kuyeyuka kwa moto
Asubuhi hii moto ndiyo unaishia
Hali halisi baada ya kuungua kwa maghala hayo hili si tope mali ni mafuta ya kula yaani mafuta ya kupikia
Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuokota baadhi ya mabaki ya bidhaa zao zilizopona katika moto huo
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani akiongea na waandishi wa habari leo amesema anawapongeza sana wakazi wa Mbeya hasa wale wa maendeo yanayozunguka maghala yalioteketea kwa moto kwa ushirikiano wao kuwezesha kuokoa baadhi ya bidha za wafayabiashara licha ya vijana wachache kutaka kuiba na kutupa mawe askari wake ili wafanye uhalifu wa kupora bidhaa zilizokuwa zinaokolewa hapo mpaka sasa vijana wawili wamekamatwa kwa kutupia askari mawe na kuiba bidhaa zilizokuwa zinaokolewa
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda diwani


PICHA ZOTE NA Jem

Kumekucha: Mbowe Amtangaza Dr Slaa Mgombea Urais 2015

CHANZO: Mtandao wa Wanabidii

Katika Mkutano Mmoja huko Karatu mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amemtangaza Dr W P Slaa kama mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA mwaka 2015 . Mimi Binafsi nashangaa ni Utaratibu gani umetumika kumpitisha Dr Slaa kama mgombea urais wa CHADEMA ,

Najua huwa kuna vikao na michanganuo kadhaa wa kadhaa kwa hapa sijui imekuwaje . Ndugu Tumaini Makene tunaomba utujuze au Mhe Mbowe alikuwa Anapima upepo tu ? Kwa maoni yangu ningependa kumwona Dr Slaa akupumzika amwachie nafasi hiyo mwingine yeye mpaka sasa ameifanyia chadema na taifa hili mengi akiwa mshauri itakuwa hatua nzuri zaidi asiwe kinganganizi kama akikubalia basi apishe utaratibu wa kidemokrasia ufanyike ili kumpata mgombea .

Dr Slaa amegombea mara moja tu mnadai anatakiwa apumzike Vipi kuhusu Pr Lipumba aliyegombea mara zote tangu mfumo wa vyama vingi ulipoanza mnamshaurije? Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network Emmanuel Muganda 01:43 (2 hours ago) to wanabidii Na wengine tunakushangaa wewe unayeshanga. Dr. Slaa is still the flag bearer for Chadema since 2010. Na kazi aliyoifanya kujenga chama tangu wakati huo matunda yake sote tunayaona. Wewe endelea kushangaa wengine wanaendelea kujenga chama chao. Bado tunamhitaji Slaa katika uongozi wa chama kama vile TANU walivyomhitaji Mwalimu Nyerere mwaka 1959 miaka mitano na baadaye, baada ya kuundwa kwa TANU.
KAZI IPO





 

No comments: