Simon
Mwakifwamba (kushoto) na wadau wengine wakimsaidia Sajuki (katikati)
kutoka jukwaani baada ya kudondoka katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid,
jijini Arusha mwishoni mwa mwaka jana.
STAA wa
filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo alfajiri
katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu. Kwa
mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu
Amiri ni kwamba hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la
upungufu wa damu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Amen!
Leo Jumatano
MICHEZO
MFARANSA WA SIMBA AAHIDI KUVUNJA REKODI YA SIANG'A 2003 SIMBA SC
Liewig kushoto akisaini mkataba jana. Kulia Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange 'Kaburu' |
Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA mpya
wa Simba SC, Mfaransa Patrick Liewig amesema kwamba lengo lake ni kuifikisha
klabu hiyo katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu na
anaamini hilo linawezekana kwa kuwa timu ina wachezaji wazuri.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY jana, Liewig alisema kwamba ana imani Simba ni timu nzuri, kwa
sababu katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoifunga
1-0 Zambia, kulikuwa kuna wachezaji wengi wa Simba SC.
“Zambia ni
timu nzuri, ni mabingwa wa Afrika, kama Tanzania iliifunga Zambia ikiwa na
wachezaji wengi wa Simba, sioni kwa nini tusifike Robo Fainali ya Ligi ya
Mabingwa,”alisema Liewig.
Liewig
alisema leo anakwenda Zanzibar kuungana na kikosi cha timu hiyo ambacho
kitakuwa kikishiriki Kombe la Mapinduzi.
“Nitakutana
na wenzangu katika benchi la ufundi huko, Julio (Jamhuri Kihwelo) na Moses
(Basena), tutashirikiana kufanya kazi, baada ya hapo tutakwenda Oman, tukirudi
tutaanza Ligi (Kuu) na Ligi ya Mabingwa.
Nimeambiwa
pia kuna Kombe la Kagame (Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati) Rwanda,
tutakwenda, pamoja na yote, nitashughulikia pia na program ya vijana, lazima
tuibue vipaji kutoka chini,”alisema.
Simba SC itaanza na Recreativo de Libolo ya Angola, katika
Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Februari 17 hadi 19 na
kurudiana nayo kati ya Machi 2 na 4, mwakani.
Mara
ya mwisho Simba SC kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo ilikuwa
mwaka 2003, wakati huo ikiwa chini ya kocha Mkenya, James Aggrey
Siang'a.
Liewig jana
alisaini mkataba wa miezi 18 kuifundisha Simba, akimpokea Mserbia Milovan
Cirkovick aliyetupiwa virago baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya
Bara.
Liewig ni
kocha wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC
Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, ambaye ana Stashahada ya
Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa na
Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller, anatarajiwa kwenda Zanzibar
kesho.
Liewig pia
amehudhuria kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo
Kikuu cha Dijon.
Kwa upande
wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha
Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za
timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha
kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia
mwaka 1989 hadi 1990: alikuwa Meneja
Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi
1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez,
1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa
Msaidizi wa Alain Giresse.
Liewig pia
alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa
ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari
mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za
U20 nchini Burkina Faso.
Kuanzia
mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa
mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super
Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya
makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa
Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba
mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya TunisiaJK.Azindua Matokeo Ya Sensa Ya Watu Na Makazi 2012.
Rais
Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuzindua matokeo ya
Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2012 jana jijini Dar es salaam ambapo
idadi ya watu Tanzania imefikia milioni 44 929 002. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO
Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali na vyama vya siasa.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja kwenye bango linaloonyesha
idadi ya watu Tanzania na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya sensa ya watu na makazi
ya mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment