Mkuu wa mkoa Mbeya Abass Kandoro akikata utepe kuzindua chanjo ya mpya ya Rotavitus na Nimonia katika kituo cha afya Ruannda jijini Mbeya |
Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Kandoro akimwekeamatone moja ya watoto waliyofika katika uzinduzi huo |
Mkuu wa mkoa Mbeya akihutubia wananchi waliyofika katika uzinduzi wa chanjo hiyo |
Mratibu wa chanjo mkoa wa Mbeya Japhet Mihanye akisoma risala kwa mgeni rasmi |
Mstahiki meya wa jiji la Mbeya Atanath Kapunga akimshukuru mgeni rasmi kwa uzinduzi wa chanjo hiyo |
Baadhi ya wakina mama waliyobahatika kupata chanjo katika uzinduzi leo |
Waziri Membe atangaza kutogombea ubunge tena
WAZIRI
wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza
kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.Membe ambaye ni
Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa
akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.
kinana akemea chokochoko za kidini
KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana amekerwa na chokochoko za kidini zilizoanza kujipenyeza hivi karibuhi na kutoa wito kwa madhehebu ya dini na taasisi zake hapa nchini,kuendelea kuhubiri amani kwa kuliombea taifa , ili wananchi waendelee kujivunia amani iliyoachwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Kinana alitoa kauli hiyo juzi kwenye maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Imam Husein, yanayoadhimishwa na dhehebu la KhojaShia Ithna Asheri Jamaat Arusha kote duniani na kufanyika kwenye msikiti wa jumuiya hiyo jijini hapa , ambapo watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa madhehemu pamoja na viongozi wa chama na Serikali walihudhuria.
Kinana alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa viongozi wa dini na taasisi zake kuendelea kuienzi amani kwa kuhubiri suala la kudumisha amani na kuonya kwamba Serikali haitasita kuchukua hatua za haraka kwa mtu ama kikundi chochote cha dini kitakachojihusisha na uvunjivu wa amani.
DK. HARRISON MWAKYEMBE ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE SONGWE MBEYA
Mmoja ya wahandisi wa ujenzi wa uwanja huo wa songwe akimwelezea waziri wa uchukuzi Dk Mwakyembe akimwelezea hatuza za mwisho za ujenzi wa maegesho ya ndege kubwa |
Mkuu wa majeshi Tanzani Jenerali Mwamnyange akisalimiana na kuagana na RPC wa Mbeya Diwani katika kiwanja hicho cha songwe kabla ya kuanza kwa ziara ya waziri wa uchukuzi Dk Mwakyembe |
Jenerali Mwamnyange akiondoka uwanjani hapo kurejea Dsm alikuwepo Mbeya kwa mapumziko Mafupi |
Huu ni mnara wa kuongozea ndege katika kiwanja hicho cha Songwe Mbeya |
Mwongoza ndege mwandamizi John Chambo akimwezea waziri Mwakyembe jinsi wananvyofanya kazi ya kuongoza ndege katika mnara huo |
Mkuu wa kitengo cha hali ya hewa Issa Hamad akimwelezea waziri mwakyembe juu ya shughuli zoa za upimaji wa hali ya hewa uwanjani hapo na mkoa kwa ujumla kuwa |
Hili ndilo eneo la maegesho ya ndege kubwa aina ya boing 737 ambalo mwishoni mwamwezi huu wa kwanza litakamilika |
Hili ni eneo la kutua ndege na kurukia barabara hiyo ya ndege inaurefu wa zaidi ya kilometa 3.5 km |
Hii ni sura ya mbele ya uwanja huo wa songwe Mbeya |
Hili ni jengo la kikosi cha zimamoto uwanjani hapo |
Picha na Mbeya yetu |
No comments:
Post a Comment