Saturday, December 22, 2012

TAIFA STARS YAIPA HESHIMA TANZANIA NA KUPUNGUZA MACHUNGU YA UGANDA

TAIFA STARS YAIFUNGA CHIPOLOPOLO 1-0 UWANJA WA TAIFA

Mchezaji wa timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo James Chamanga akiruka juu kuwania mpira huku mchezaji wa timu ya Tanzania Taifa Stars Mrisho Ngasa akiuvizia, katika mchezo wa FIFA wa kirafiki unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Timu ya Tanzania Taifa Stars imeifunga Chipolopolo ya Zambia goli 1-0 na kutoka kifua mbelea uwanjani , mfungaji wa goli hilo akiwa Mrisho Ngasa katika dakika ya 45 ya mchezo huo.
Mchezaji wa Taifa Stars Mrisho Ngasa akishangilia na kupongezwa na wenzake mara baada ya kufunga goli la mkwanza katika mchezo huo.
  Wachezaji wa Taifa Stars wakitoka nje ya uwanja kwa mapumziko baada ya kipindi cha kwanza kuisha kwenye uwanja wa Taifa.
Mashabiki wa timu ya Taifa Stars wakishagilia mara baada ya Mrisho Ngasa kufungo goli la kwanza dhidi ya Chipolopolo katika mchezo huo
 
Kikosi cha timu ya Zambia kikiwa katika picha ya pamoja.
 
Mnazi Mkubwa wa Timu ya Yanga na Taifa Stars Heavy D. akinyanyua skafu yake yenye bendera na maneno ya Tanzania wakati wimbo wa taifa ukiimbwa kabla ya mchezo huo.
 
Kulia ni Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Zambia Kalusha Bwalya na mabalozi wa Zambia nchini Judith Kangoma-Kapijimpanga na Balozi Tanzania nchini Zambia Bi. Grace Mujumi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo.
 
Mashabiki wa timu ya taifa ya Zambia wakishangilia timu yao katika mchezo huo.

Jocelyine Alipoibuka Mshindi Miss East Africa Tanzania

Jocelyne Maro Mii East Africa Tanzania akipunga mkono kwa mashabiki wake mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam akiwashinda warembo wenzake kutoka mataifa mbalimbali ya Ukanda wa Afrika Mashariki na nchi Jirani na Ukanda huo.

Jocelyne Maro Mtanzania wa kwanza kushinda taji hilo toka lililpoanzishwa amejinyakulia zawadi zenye tmamani ya dola za kimarekani 30,000 likiwemo Gari aina ya Toyota Verossa, mara baada ya majaji kumtangaza mrembo huyo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe huku watu mbalimbali wakimpongeza kwa ushindi wake PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na Miss Uganda Ayisha Nagudi mshindi wa pili katika shindano hilo kushoto na Miss Burundi Ariela Kwizera ambaye alipata nafasi ya tatu katika shindano hilo.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipiga picha ya pamoja na warembo wenzake alioingia nao kwenye tano bora ya shindano hilo.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akiwa amepigwa na butwaa mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo jana usiku.
Miss Eats Africa Jocelyne Maro akipongezwa na wenzake mara baada ya kushinda katika shindano hilo.
 
Warembo wakipita jukwaani na vazi la ufukweni.


 
Warembo wakipita na vazi la Ubunifu.
Mkurugenzi wa Rena Event Bw. Rena Calist wa pili kutoka kulia akifuatilia kwa karibu jinsi shindano lilivyokuwa likiendeshwa kulia ni mmoja wa maofisa wa Miss East Afrca John Momadi
 
Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.
Mwanamuziki Mad Ice akifunikwa kwa wimbo wake katika shindano hilo kama anavyoonekana akishangiliwa na mashabiki wake
 
The Voice Wonder nao wakifunika mbaya.
 
Mzungu Kichaa akaleta kichaa chake jukwaani na kuwaburudisha vya kutosha watu mbalimbali waliohudhuria katika shindano hilo.
 
Enjoying with some EA students from Netherlands and Germany . It's real a funny day
GAZETI LA LEO

No comments: