Gari
 anayoitumia Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip 
Mangula ikitembea katika barabara ya Lami kutoka Sumbawanga kwenda 
Jijini Mbeya. 
Sehemu kubwa ya Barabara hiyo kwa sasa imeshakalika 
hususani miradi miwili ya Tunduma – Ikana na Ikana – Laela, mradi mmoja 
wa Laela-Sumbawanga unaojengwa na Mkandarasi Aasleaff Bam International 
ambao ulikua unasusua sasa unaendelea kwa kiwango cha 
kuridhisha. Maendeleo haya ya barabara na mengine mengi aliyoyaona 
yalikua kivutio kikubwa kwa Mhe. Mangula ambae alitoa ushuhuda kwamba 
tangu afike Mkoani Rukwa mara ya mwisho mwaka 2003 na sasa hali ni 
tofauti kabisa na kwamba kwa kipindi hicho cha Miaka 10 ameioana Rukwa 
Mpya.
KINGOTANZANIA 

No comments:
Post a Comment