Monday, December 8, 2014

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Timu ya mpira wa miguu ya Sunderland (SAFC) zatangaza utalii wa Tanzania Uingereza

Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe na Garry Hutchinson Mkurugenzi wa Biashara wa timu ya mpira  ya Sunderland wakionyesha jezi ya iliyoandikwa Tanzania yenye rangi za timu hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Utalii wa Tanzania yanayotangazwa katika uwanja wa timu hiyo kutoka kulia ni Meneja  wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bw. Geofrey Meena, Teddy Mapunda mjumbe wa Bodi ya wakurugenzi ya (TTB) na kutoka kushoto ni Mdau wa Utalii Bw. Nestor Mapunda na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania  (TTB) Bi. Devotha Mdachi.
 2 
Wachezaji wa timu ya Sunderland wakipasha mwili huku wakiwa wamevalia fulana nyeusi zenye maandishi yanayotangaza na kukaribisha watalii na kutangaza utalii nchini Tanzania. 5Matangazo yakiendelea kuonyeshwa kwenye mbao za matangazo wakati mchezo kati ya Chealsea na Sunderland ukiendelea. 6 
Fulana zinazotangazo utalii wa Tanzania ikiwa zimewekwa kwenye vyumba vya kubadilishia jezi wachezaji wa timu ya Sunderland. 7 
Majarida yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamesambazwa kwenye meza katika mgahawa wa timu ya Sunderland kwenye uwanja wao wa Sunderland 8 
Mabango na yanayotangaza utalii wa Tanzania yakiwa yamewekwa kwenye makumbusho ya timu hiyo. 9 
Haya ni baadhi ya mabango yanayoonyeshwa katika uwanja huo wakati wa michezo ya Ligi k. 10 
Bendera yenye maandishi ya kukaribisha watalii kutembelea Tanzania ikiwa imepandishwa katika miliongoti katika lango kuu la uwanja huo.
………………………………………………………………………………………………
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshirikiana na Timu ya mpira wa miguu ya Sunderland (SAFC) ya nchini Uingereza katika uzinduzi wa utangazaji utalii wa Tanzania pamoja na kuhamasisha uwekezaji kwenye sekta ya michezo (Destination Partner in Tourism and Sports Development). Uzinduzi huo ulifanyika tarehe 29 Novemba, 2014 kwenye kiwanja kinachomilikiwa na timu ya Sunderland “Stadium of Light”
Kwenye tukio hilo ambalo lilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe pamoja na, maafisa kutoka Bodi ya Utalii, Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza pamoja na watanzania waishio nchini Uingereza. Tukio hili lilifanyika wakati timu ya Mpira ya Sunderland ilipoikaribisha timu ya mpira ya Chelasea Football club.
Wakati wa uzinduzi huo matangazo ya Utalii yaliweza kurushwa katika kingo za kuta za uwanja wa timu ya Sunderland na kuonesha vivutio vya vivutio vya utalii wa Tanzania na vile vile yalioneshwa kwenye luniga kubwa iliyokuwepo kwenye uwajani huo. Aidha wachezaji wa timu ya Sunderland walivaa jezi maalum zilizoandikwa ‘Visit Tanzania’ wakati wakifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi kuanza.
Bodi ya Utalii Tanzania ilitumia fursa ya uziduzi huu kuhamasisha wataliii kutoka ndani na nje ya Uingereza pamoja na mashabiki wa timu hizo kutembelea vivutio vya utalii wa Tanzania.

No comments: