Shughuli za mazishi hufanywa kwa makini kuepuka maambukizi ya Ebola
Maafisa
wa Afya nchini Sierra Leone wamegundua miili kadhaa katika maeneo ya
mgodi wa Almasi, na kusababisha hofu kuwa pengine ugonjwa wa Ebola
haujaripotiwa ipasavyo.
Shirika
la afya duniani,WHO limesema limebaini kisa hiki kipya mashariki mwa mji
wa Kono, timu ya Wataalamu imepelekwa Kono kufanya uchunguzi kuhusu
uwepo wa ugonjwa wa Ebola.
Watu 6,346 wamepoteza maish akutokana na ugonjwa huo na zaidi ya 17,800 wameathirika na Ebola.BBC
No comments:
Post a Comment