Ndugu zangu,
CAG wetu
mpya alitamka jambo la msingi sana akiwa Arusha hivi karibuni. Kwamba kuna
tatizo la migongano ya kimaslahi kwenye kuyashughulikia matatizo yetu.
Ona leo,
tayari tunayaona mapungufu makubwa kwenye hata ripoti za kichunguzi
zilizowasilishwa Bungeni hivi karibuni. Kwamba kwa baadhi ya waliohusika
kufanya uchunguzi wameonekana kuwa na migongano ya kimaslahi kwenye
walichokichunguza na kukitolea taarifa.
Kama
ilivyomshangaza Jaji Warioba, kuna wengi wanaoshangazwa, kuwa iweje
wahusika wengine kwenye kuhusiana na kashfa ile ya Tegeta Escrow
hawakuainishwa kwenye ripoti na wala hayakutoka maazimio ya hatua za
kuchukuliwa dhidi yao.
Na juzi
tu, tumesikia, kuwa viongozi wa kidini waliotuhumiwa ' wamesafishwa' kwa
dhambi ile ile ambayo viongozi wa kisiasa wametuhumiwa na kuhukumiwa
nayo.
Kauli ya
CAG Assad ilikuwa ni thabiti na ya kuzingatiwa sana. Vinginevyo, kwenye
mashaka, ni heri kumwacha huru mtu kuliko kumtia hatiani.
Maggid,
Iringa.
Iringa.
No comments:
Post a Comment