Monday, May 6, 2013

MATUKIO YA MACHACE KATIKA SAFAZI ZANGU




MTANZANIA KAWEKEZA HAPA
CHAI MMMM HOTEL NZIMA MTU MMOJA SIJUI IMEKAEEJE HII
MATENGENEZO MAKUBWA YA BARABARA YANAENDELEA
KAMA KAWA KAZI INASONGA
MKONGE UKIKAUSHWA


BAADHI YA MAKAZI YA WAFANYAKAZIWA MASHAMBA YA  MKONGE TANGA


UKIFIKA MAENEO KWA KAWAIDA UNAUONA NLIMA KILIMANJALO VYEMA LAKINI KWAKUWA KIPINDI HIKI CHA MVUA SIJAPATA HA CHEMBE YA KUUONA MLIMA ZAIDI YA MAWINGU NA MVUA ISIYOKATIKA

KIUKWELI KAZI YA ASKALI WA BARABARANI MIE SIKU HIZI WALA SIELEWI KABISA SIJAJUA WAKIWA KATIKA MAJUKUMU YAO HUWA WANAPASWA KUFANYA NN ZAIDI YA KUKUSANYAWAKIJUACHO UKIZINGATIA SAFARI YANGU ILIKUWA NI YA MWENDOMLEFU HUKU NIKI NIKISHANGAA UWEPO WA VITUO VYA ASKALI TRAFKI WENGI BARABARANI HUKU KARIBU WOTE WAKISIMAMISHA GALI WANAULIZA LESENI NA KADI

MOSHI

NIKIPATA BARAKA ZA MCHUNGAJI ENENDA KWA AMANI MKAMTUNZE MTOTO WA WATU MIE NIKAITIKIA KUWA AMEN

NIMEAMBIWA NA MCHUNGAJI  TUKAKUTUNZE NAMI KWAKUWA NDIO MKUBWA KATIKA FAMILIA YA MWALWEGA NITAWAAMBIA MANENO NILIYOAMBIWA NA MCHUNGAJI NA PIA MAJIBU YAKO KUWA .. NITAKWENDA. KARIBU DR MAGE KATIKA FAMILIA YA MCHUNGAJI MWALWEGA

HAWA KIUKWELI WAMEFURAHI SANA KULIA DADA FARAJA , NURU AMBAYE NDIE MKE WA BARAKA MEJAH, SHEM TAMARI MWENYE SUTI NDIE MEJAH

KULIA DADA RHOTINA, MAMAMDOGO NA KUSHOTO NDIYE MAMA YETU MCHUNGAJ RUTH MWALWEGA



KULIA NI IKUPILIKA MWALUMULI AKITETA JAMBO NA MAMA ILA SIELEWI KWANINI ALIKUWA ANASHIKA MDOMO HUKU ANAONGEA NA MAMA

UWEZO ANA MARAFIKI WAWILI AMBAO HAWA NI
UWEZO AKIWA NA KIFWAMBA

WATU WALIPENDEZA SANA NA WENYE FURAHA SANA MAANA NDIO RAHA YA KUOA

MEZA KUU YA WAOAJI

KWA UNYENYEKEVU MKUBWA MAMA MCH MWALWEGA AKIONGEA NA WAZAZI NA WAALIKWA, KARIBUNI MBEYA


ENG UWEZO AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA KWENYE SHEREHE  YA SENDOFF

BARAKA MEJAH AKITAMBULISHA UKOO WA MCHUNGAJI MWALWEGA KWA WAGENI WAALIKWA HUKU UWEZO AKIWA MAKINI SANA KUSIKILIZA

HII NDIO HESHIMA YA MCHAGA KWENYE SHEREHE


SHEREHE ILIKUWA NZURI NILIJIFUNZA MILA MILA NA DESTURI ZA KUOA UCHAGANI
 ..................................................................................................................................................................

SERIKALI: SH. BILIONI 876.3 KUTATUA MSONGAMANO MAGARI DSM

HAPA NI UBUNGO DSM UJENZI UKIENDELEA


KAZI ZINAKWENDA BARABARA YA MABASI YAENDAYO KASI

Gianttrafficjam

Na Immaculate Makilika- Maelezo
SERIKALI imesema   inatekeleza miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam yenye thamani ya sh. bilioni 876.336   katika barabara ya Al Hassan Mwinyi ambapo watumiaji wa barabara hiyo hutumia takribani saa moja na nusu kufika Osterbay polisi hadi daraja la Salender hususani mida ya asubuhi saa moja hadi saa tatu.
 Hayo  yalisemwa leo Bungeni na  Naibu Waziri wa Ujenzi   Gerson  Lwenge Naibu  wakati    akijibu swali  Mbunge  wa Jimbo la  Temeke  Abasi Zuberi Mtemvu  lililouliza kuwa  Je,Serikali inaweza kutoa ufafanuzi juu ya ufumbuzi wa tatizo la msongamano huo?
 Alisema   kuwa  inayolenga kutatua tatizo hilo ,ikiwemo miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo ambayo ni  kama ifuatavyo;.Barabara ya Kimara –Kivukoni (fire),Fire-Kariakoo na Magomeni –Morocco (Sh.  bilioni 240),Karakana na vituo vya mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) pamoja na kuhamisha nguzo za umeme(sh. bilioni 47.90).
 Nyingine ni  Barabara ya Mwenge – Tegeta(sh.  bilioni 88.00),Barabara ya Kilwa (Kilwa Road) Bendera Tatu-Mbagala Rangi Tatu ,(sh.  bilioni 35.16),Daraja la Kigamboni (sh. 214.64).Flyover ya TAZARA,Serikali ya Japani imetoa msaada wa fedha kwa ajili ya usanifu,.Barabara ya Gerezani (Bendera –Tatu-KAMATA),Serikali ya Japani imetoa  msaada wa fedha kwa  ajili ya ujenzi.
 Barabara ya Mandela (sh. bilioni 61.25) na.Barabara ya  Wazo Hill –Bagamoyo-Msata (sh. bilioni 89.61).
 Waziri  huyo  alisema  ujenzi wa mabasi yaendayo haraka(BRT) kutoka Morocco kwenda Magomeni hadi Kivukoni na Kimara yatapunguza msongamano wa magari kati ya Osterbay Polisi na Daraja la Salender.
 Aliongeza kuwa katika mipango ya baadae ,Serikali itaangalia uwezekano na kujenga barabara ya juu  (viaduct) pande zote za daraja ,kujenga daraja lingine pembeni mwa daraja la Salender au kujenga njia mbadala (salender bridge Bypass) kutokea Kenyata Drive  kuunganisha na Ocean Road.
.................................................................................................................................................................


Dkt. Shein azindua mbio za mwenge wa uhuru, Pemba



 

shain3 c8939
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Mohamed Shein,akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge Juma Ali Sima,(kushoto) kutoka Mkoa wa Kusini Unguja,baada kuzindua rasmi mbio hizo Kitaifa huko Chokocho Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo.

shain b1637
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Mohamed Shein,akizindua mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa kwa kuuwasha huko Chokocho Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba leo,(kulia) Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Tanzania Bara,Dkt.Fenelle Mukangara,na Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Zainab Omar Mohamed,(kushoto). Chanzo: Ramadhani Othman, Ikulu
................................................................................................................................................................


No comments: