Tuesday, May 7, 2013

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJERUHI WALIOUMIA KWA BOMU KANISANI OLASITI WANAOTIBIWA HOSPITALI YA MOUNT MERU ARUSHA

bo4 2de21
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu alipowasili katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti Jumapili iliyopita.
m1 
Taswira wakatia Rais Kikwete alipotembelea hospitali ya Mount Meru Mei 7, 2013  kufariji majeruhi wa mlipuko wa bomu katika kanisa la Olasiti jijini humo Jumapili iliyopita
PICHA NA IKULU
m2 m3 m4

RAIS KIKWETE AKIWA ARUSHA KUHANI MISIBA YA WALIOKUFA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA OLASITI

Rais  Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey  (10) nyumbani kwa wazazi wa marehemu katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita  Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. jijini Arusha Mei 7, 2013 PICHA NA IKULU bo2 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Joachim Assey (aliyekaa kushoto kwake) wakati akihani  msiba wa msichana Patricia Joachim Assey  (10) aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita katika  Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti  jijini Arusha Mei 7, 2013
bo3Mama Salma Kikwete akipungia wakati msafara wa Rais Kikwete ukiondoka baada ya kuhani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey  (10) katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu Jumapili iliyopita katika  Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti. katika kitongoji cha Majengo kata ya Elerai jijini Arusha Mei 7, 2013 bo11Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na  Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu  alipowasili katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti  Jumapili iliyopita. bo17 Wananchi wakimuaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete baada ya kumtembelea  Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu  katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti  ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, bo18 
 Rais  Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa kijana James Gabriel (16) aliyefariiki katika  shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita
Rais  Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakihani msiba wa marehemu   Regina Longino Kurusei (45), mkazi wa Olasiti aliyefariiki katika  shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Jumapili iliyopita.

bo23

 ............................................................................................................

MH. PINDA: VYOMBO VYA USALAMA VIACHIWE KAZI YAKE

DSC_0280
Waziri mkuu mh.  Mizengo Pinda amewataka watanzania kuwa watulivu
wakati uchunguzi wa tukio la shambulio la bomu lililotokea katika
kanisa la Mtakatifu Joseph jimbo la Arusha ukiendelea.
Waziri mkuu ameyasema hayo wakati akitoa taarifa za awali juu ya tukio
hilo bungeni , na kusema suala hilo sio la kushabikia kisiasa badala
yake watoe ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kuwanasa
waliohusika.
Licha ya watu watatu kupoteza maisha , Waziri mkuu amesema  hali ya
majeruhi wa mkasa huo inaendelea vizuri ambapo 24 kati ya  66
wameruhusiwa baada ya kupata nafuu.
 Aidha mh.  Pinda amesema mpaka hivi sasa , vyombo vya usalama
vinaendelea na uchunguzi iwapo bomu hilo la kurushwa kwa mkono
lilitengenezwa kienyeji au kiwandani.
 Katika hatua nyingine Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Shamsi Vuai Nahodha ametoa wito kwa wananchi na viongozi wa dini kutoa
ushirikiano kwa kupinga mauaji yanayoendelea hapa nchini.
Mpaka hivi sasa watu wanane wamekamatwa ambapo wanne wana asili ya
kutoka Uarabuni na wengine ni  watanzania wakihusishwa na tukio hilo .......................................................................................................

Bomu Arusha: Pengo afichua siri

pengopix 2bab9
Kadinali Pengo alisema amepata taarifa kutoka kwa watu ambao hana na shaka nao.
"Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo," alisema Kadinali Pengo na kuongeza:

"Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu," alisema Pengo.
Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.
"Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani," alisema Pengo.
Alisema kujaribu kuficha ukweli na kupotosha ni njia sahihi kwa ibilisi kuleta vurugu katika jumuiya ya watu na ieleweke hivyo.
"Naomba kila mtu akubaliane na tamko langu haidhuru pana kosa, amani ya taifa letu ni jambo la msingi na amani itajengwa tu iwapo kila mtu anayehusika atakuwa tayari kusema ukweli kama ulivyo," alisema.        :chanzo Mwananchi

.............................................................................................................................
BAADHI ya Wananchi Mkoani Mbeya wamelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kuendelea kusambaratisha na kumaliza kabisa mtandao wa ujambazi kutokana na majambazi wengi kukamatwa na wengine kuawa.
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio Julius Kaijage akimkabidhi pikipiki mbili na matairi 4 ya gari pamoja na mabati mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro vifaa hivyo vyote vimetoka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiongea na wadau mbali mbali kwenye hafla fupi ya kupokea misaada toka kwa wadau wa ulinzi mkoani hapa
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha analiwezesha kwa hali na mali.
Meneja wa Benki ya NMB kanda ya nyanda za juu kusini Bi.Lucresia Makirie amesema benki yake imetoa msaada Pikipiki tatu kusaidia jeshi hilo ili zisaidie katika ulinzi shirikishi katika mkoa wa Mbeya
Kamanada wa Polisi Mkoani Mbeya Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya upo katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi hilo .
Picha ya pamoja



BAADHI ya Wananchi Mkoani Mbeya wamelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kuendelea kusambaratisha na kumaliza kabisa mtandao wa ujambazi kutokana na majambazi wengi  kukamatwa na wengine kuawa.
  
Pongezi hizo zimekuja Siku moja baada ya Jeshi hilo kuwauwa watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika majibizano ya kurushiana risasi kati ya Askari na majambazi hayo katika tukio lililotokea katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya.
  
Katika kuhakikisha Jeshi hilo linaendelea  kufanya kazi katika mazingira mazuri na kwa mafanikio  na kuunga mkono juhudi zao, Wadau mbali mbali  leo  wamejitokeza kulichangia jeshi hilo katika Hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoani hapa.
  
Hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Jumla ya Shilingi Milioni 28 zilipatikana vikiwemo vifaa mbali mbali.
  
Mwenyekiti wa kikosi cha Mafanikio cha kuchangisha fedha na michango ya kuliwezesha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika Mazingira mazuri, Julius Kaijage amesema Askari wa Jeshi la Polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha analiwezesha kwa hali na mali.
  
Katika Hafla hiyo Jumla ya Pikipiki tano zilinunuliwa ambapo kati ya hizo Tatu zimetolewa na Benki ya Nmb kwa thamani ya Shilingi Milion 5.4, wakati kamati ikinunua pikipiki Mbili kwa Thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki Nane.
  
Mbali na michango hiyo pia Wakala wa Majengo mkoa wa Mbeya (TBA) imetoa mabati 22 ya Geji 28 yenye thamani ya Shilingi 460,000/=, pia kamati ya Mafanikio imenunua Matairi nane yenye thamani ya Shilingi Milioni 3,020,000/=,pamoja na mafuta kwa ajili ya magari ambayo ni Lita 360 kwa Mwaka zilizoahidiwa na kampuni ya G4S.
  
Mbali na pongezi hizo Wananchi hao wamemshauri Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani mbali na kupambana na uhalifu katika Mkoa wa Mbeya na kuwasisitiza watu wanaofanya shughuli zisizokuwa na uhalali kuacha mara moja au kuhama Mkoa pia wapendekeza kufanya ziara za kushtukiza katika Vituo vidogo vya Polisi.
Kwa upande wake Kamanada wa Polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amewapongeza wadau mbalimbali waliojitokeza kulisaidia jeshi hilo ambapo amewahahakikishia wananchi wa mkoa huu kuwa kwa sasa mkoa wa mbeya upo katika mazingira salama kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wananchi na jeshi hilo .
Na Mbeya yetu
.................................................................................................................

Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kusambazwa



Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Charles Kitwanga 
Na  Mwandishi Wetu  (email the author)
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Magreth Mkanga (CCM) aliyetaka kujua lini mkongo utaanza kutumika, kama utasaidia kupunguza gharama za mawasiliano na pia Serikali imejiandaa vipi kuwawezesha wananchi kunufaika na mkongo huo hata wale wasio na uwezo

Dodoma. Serikali ipo katika mpango wa utekelezaji wa mradiwa usambazaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano awamu ya tano.
Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk Charles Kitwanga ambaye alisema mradi huo unalenga kuziunganisha wizara, idara, vyuo, shule, hospitali na taasisi za umma kwenye mkongo.
Alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni taasisi hizo kushindwa kujiunganisha kutokana na uwezo mdogo wa kifedha,ambapo alisema tangu Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ulipoanza kutumika umesaidi kushusha gharama za mawasiliano kwa watumiaji.
Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Magreth Mkanga (CCM) aliyetaka kujua lini mkongo utaanza kutumika, kama utasaidia kupunguza gharama za mawasiliano na pia Serikali imejiandaa vipi kuwawezesha wananchi kunufaika na mkongo huo hata wale wasio na uwezo.
Naibu Waziri alitoa mfano kushuka kwa gharama za kusafirisha masafa kwa asililimia 99 kutoka Dola za Marekani 20,000 kwa mwezi kwa umbali wa kilometa 1,000 kwa mwendo kasi wa Megabits mwaka 2009 hadi kufikia Dola za Marekani 160 kwa mwezi kuanzia mwaka 2011.
“Huduma za intaneti zimeshuka kutoka Sh36,000 kwa Gigabyte moja mwaka 2009 hadi Sh9,000 kwa Gigabyte moja mwaka 2013 sawa na kushuka kwa asilimia 75,” alisema
...................................................................................................................................................................................................................

FBI watua Arusha kusaka magaidi



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi na Waumini wa Kanisa Katoliki la Olasiti Jijini Arusha May 7,2013 alikokwenda kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 6,2013 na kusababisha vifo na majeruhi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa Pole Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Josephat Lebulu (kushoto ) na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu, Francisco Montecillo (katikati), May 7,2013 baada ya kutembelea Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha ambako May 6,2013 ulitokea mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono na kusababisha vifo na majeruhi.
Makachero wa FBI wawasili Mjini Arusha kusaidia Polisi Tanzania kusaka magaidi
Makachero wa FBI kutoka Marekani wamewasili nchini Tanzania kusaidia katika upelelezi wa shambulizi la bomu lililotekelezwa katika kanisa katoliki mjini Arusha siku ya jumapili.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza akiwa mjini Arusha anasema makachero hao wa FBI wako Tanzania kusaidiana na Jeshi la wananchi wa Tanzania na Polisi kutafuta undani wa tukio hili ambalo limeishtua na kuiweka serikali ya Tanzania katika wakati mgumu.
Wakati huo huo wakuu wa serikali wakishirikiana na viongozi wa kidini wameandaa mkutano utakaojumuisha viongozi wapatao 200.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq amewaambia wanahabari kuwa wamelazimika kuandaa mkutano huo wa siku mbili kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete.
Mkutano huo utajadili uhusiano bora baina ya wakrito na waislamu.

....................................................................................................................

Mwanamume akikosa mtoto hupata huzuni zaidi kuliko mwanamke



 
Na Kalunde Jamal, Mwananchi  (email the author)
DONDOO MUHIMU
Utafiti ulihusisha watu 108, kati yao 27 walikuwa wanaume na  81 wanawake.Ulifanyika kwa kukusanya maoni katika mtandao, midahalo na kujaza madodoso.Walioshiriki walikuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 66.
Wenye umri usiopungua miaka 41 ndiyo walijibu maswali hayo.Waliosema wanahitaji watoto
Wanaume asilimia 59 na wanawake ni asilimia 63.
Sababu  za kutaka watoto
Asilimia 38 ya wanaume walihitaji mtoto kwa kuwa hawakuwa na mtoto kabisa, huku asilimia 27 tu ya wanawake ndiyo walikuwa hawana watoto kabisa.
Idadi ya wasio na watoto
Kati ya kila wanaume wanne  mmoja hana kabisa mtoto, ikilinganishwa na asilimia 18 ya wanawake ambao hawana watoto.
Utafiti huo umebainisha kuwa asilimia 55 tu ya wanaume ndiyo walikuwa wanataka kuongeza watoto, ukilinganisha na asilimia 59 ya wanawake ambao walikuwa wanahitaji kuongeza.Utafiti mdogo uliohusisha wanawake na wanaume 125 ambao tayari wana watoto unaonyesha kuwa pamoja na wanaume kupata madhara bado hawapendi kuwa na watoto wengi kama wanawake. Wataalamu wa Saikolojia Tanzania waunga mkono matokeo ya utafiti huo.
reTofauti na mazoea na mtazamo wa wengi kwamba mwanamke ndiye anayeumia zaidi akikosa mtoto, wataalamu wamegundua kuwa anayeumia zaidi kwa kukosa mtoto ni mwanamume.

Utafiti huo umeonyesha kuwa wanaume wanahitaji mtoto sawa sawa na wanavyohitaji wanawake, lakini wao wanaumia zaidi wanapokosa bahati ya kupata mtoto.
Wataalamu hao wamebaini kuwa sababu kubwa zinazowafanya wanaume wajisikie vibaya zaidi wanapokosa watoto ni tamaduni za toka enzi kuwa wao wanaweza kila kitu na msukumo wa familia.
Tofauti na wanawake, ambao wanahitaji mtoto kwa ajili yao binafsi kwa asili ya kuumbwa kwao, hali ambayo kitaalamu inajulikana kama ‘biological urge’.
Taarifa za utafiti huo ulioongozwa na Robin Hadley, wa Chuo Kikuu cha  Keele, ukishirikisha wanaume 27 na wanawake 81, ambao hawajapata mtoto, uliwasilishwa mbele ya Wanasaikolojia wa Taasisi ya British Sociological Association,  ya Uingereza.
Waohitaji zaidi watoto
Kwa idadi hiyo waliosema wanahitaji watoto ni wanaume asilimia 59 na wanawake ni asilimia 63.
Nusu ya wanaume walisema kukosa mtoto kunawafanya waonekane tofauti kwenye jamii, huku wanawake wakisema wanahitaji watoto ili waje kuwasaidia baadaye.
Utafiti huo ulibaini kuwa asilimia 38 ya wanaume walihitaji mtoto kwa kuwa hawakuwa na mtoto kabisa, huku asilimia 27 tu ya wanawake ndiyo walikuwa hawana watoto kabisa.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa wanaume wanajisikia vibaya zaidi kukosa watoto kwa sababu asilimia ya wasio na watoto ni wanaume,tofauti na wanawake ambao wakati mwingine hubahatika kupata mmoja au wawili.
Tafiti hizo zilionyesha kuwa kati ya kila wanaume wanne  mmoja hana kabisa mtoto ikilinganishwa na asilimia 18 ya wanawake ambao hawana watoto.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa asilimia 56 ya wanaume hawana watoto kabisa, ikilinganishwa na asilimia 43 ya wanawake ambao hawana.
Akizungumzia utafiti wake Dk Hadley, anaeleza kwamba  amegundua kuwa kati ya wazazi wawili aliye kwenye hatari ya kukosa mtoto kabisa ni mwanaume, huku akiumia zaidi anapopatwa na hali hiyo kiasi cha kuwa na hasira, kujisikia vibaya mbele za watu, kujitenga na jamii, kuwa na wivu na mambo yanayofanana na hayo.
Wanawake kupenda watoto
Anabainisha kuwa hiyo ndiyo sababu inayowafanya wanawake wapende kupata watoto kuliko wanaume ili kuwaondoa kwenye matatizo hayo, ambayo mara nyingi husababisha familia nyingi kusambaratika bila kujali zilikuwa kwenye maelewano ya kiasi gani.
Alisema kwamba utafiti huo ulifanyika kwa njia ya kukusanya maoni kwenye mtandao, midahalo, kujaza dodoso za majibu na ulihusisha watu wenye umri wa kati ya miaka 20-66 huku wengi waliojibu maswali hayo walikuwa na umri usiopungua miaka 41.
....................................................................................................................................................................................................

DAWA FEKI NA MBEGU ZA MAZAO ZAZAGAA MBEYA

Mkuu wa wilaya Mbeya Norman Sigalla
*Wakulima wauziwa unga wa matofali kama dawa
*Mahindi yapakwa Coper kulaghai wakulima

DAWA feki zimezagaa katika maduka mbalimbali ya pembeje za kilimo mkoani Mbeya na kuendelea kutajirisha wafanyabiashara wasio waaminifu, imebainika.
Uchunguzi wa kina uliofanywa kwa miezi sita sasa, umebaini kuwepo kwa dawa feki za kuhifadhia nafaka hasa mahindi na maharage.
Wafanyabiashara hao, ambao baadhi yao kwa sasa hawakamatiki kutokana na utajiri walioupata kwa njia hiyo, wamefikia hatua ya kusaga matofali yaliyochomwa  kisha unga wake kuhifadhiwa kweye mifuko kama dawa za kuulia wadudu wanaoharibu mimea na matunda ya Kahawa.
Dawa aina ya Red Copper baadhi ya wafanyabiashara wanauza kwa ujanja unga wa matofali ya kuchomwa kisha kuweka unga huo kwenye mifuko na kuuza kwenye maduka yao huku Copper ya kuhifadhia mbegu za pamba wanauza kama Copper ya kutibu magonjwa ya kahawa aina ya CBD.
Copper hiyo wakulima wakiikoroga kwenye maji inatuama kwasababu siyo Copper halisi ya kuchanganya na maji lakini wengi wanaitumia kwasababu ni bei rahisi na hawana elimu ya kutosha kuhusu dawa hizo.
Kwa upande wa mbolea, wanachukua mbolea aina ya minjingu ya punje na kuweka katika mifuko ya Dap kwani Dap ina bei kubwa kuliko minjingu.
Wanafanya hivyo kwasababu mkulima anapotumia mbolea hiyo hawezi kugundua mpaka pale mazao yatakapokuwa yameanza kuharibika yakiwa shambani.
Mbegu za mahindi, wamekuwa wakichukua mahindi ya kawaida na kuyachanganya na Copper ya kuhifadhia mbegu za pamba na kopa ya kawaida kisha kuhifadhi kwenye mifuko ya makampuni ya utafiti na kuwauzia wakulima.
Kuwepo kwa mchezo huo mchafu kwa ajili ya kujitajirisha unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara, mtaalam wa masuala ya pembejeo kutoka kampuni ya Bager, Alex Swilla anathibitisha kuwepo kwa mchezo huo mchafu huku serikali ikiendelea kufumbia macho.
Anasema mbali na mbolea na mbegu hizo kuchakachuliwa, wafanyabiashara hao pia wanachakachua na sumu ambapo jina la sumu linalokuwepo kwenye kopo ni tofauti na dawa inayokuwemo ndani.
‘’Kwa upande wa sumu, wanachukua dawa aina ya Sumision na kuweka katika makopo ya sumu aina ya Daksban’’alisema Swilla.
Alisema hali hiyo imeendelea kushika kasi kutokana na mambo mawili, likiwemo suala la rushwa kwa wakaguzi au wakaguzi hao kutokagua kabisa maduka ya pembejeo hizo za kilimo ama kukaa muda mrefu bila kufanya ukaguzi hali ambayo inawapa mwanya wafanyabiashara hao kuendelea na mchezo huo.
Hata hivyo, imebainika kuwa kutokana na ubora wa pembejeo za ruzuku kutoka serikalini, baadhi ya wafnyabiashara hawakuwauzia wakulima kutokana na bei yake kuwa kubwa hivyo mbolea hizo waliziuza kwa bei kubwa tofauti na maelekezo ya serikali lakini serikalini hakuna aliyejali.

 ....................................................................................................................

Moyes kocha mpya Man united, Ferguson kuwaaga mashabiki jpili

fejinew 4695d
Sir Ferguson
feji1 66431
Sir Ferguson
feji2 44480
feji 09948

Sir Alex Ferguson anajiandaa kuhitimisha miaka yake 27 ya kuifundisha Manchester United.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 71 anajiandaa kuuga umati wa mashabiki Uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya mechi ya United dhidi ya Swansea, wakati watakapokabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu England, hilo likiwa la 13 chini ya Ferguson.
Mazungumzo yanaendelea kumsaka mrithi wake na kocha wa Everton, David Moyes ni miongoni mwa wanaopewa nafasi. Chanzo: binzubeiry
....................................................................................................................................................

No comments: