MKUU WA CHUO CHA MPUGUSO KULIA KATIKATI MKUU WA WILAYA CHRISPIN MEELA NA ANAYE FUATA NI MWENYEKITI WA BODI YA CHUO MPUGUSO MZEE MKISI |
WADAU WA ELIMU NA WAPILI KUTOKA KUSHOTO MBELE NI MKUU WA CHUO CHA UALIMU TUKUYU MATHIAS MVULA |
BAADHI YA WANACHUO WALIOHITIMU CHUO CHA UALIMU MPUGUSO TUKUYU |
............................................................................................................
HAPA LEO NINA SAFARI YA KWENDA DSM HADI MOSHI KCMC SAFARI INAANZA MCHANA HUU TUOMBEANE WADAU WA KINGOTANZANIA
GFC- TANZANIA YAPENYA NUSU FAINALI PAN-AFRICAN GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE
GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™
MSIMU WA TATU
ROBO FAINALI – EP7 winners & hype EP 8
*STOP PRESS* *STOP PRESS* *STOP PRESS* *STOP PRESS* *STOP PRESS* *STOP PRESS*
*WATANZANIA NA WAKENYA WAINGIA NUSU FAINALI*
Mai
mosi, Dar es Salaam; Jana usiku timu kutoka Kenya na Tanzania
ziliwakilisha vizuzi Afrika mashariki katika sehemu ya saba ya
GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™. Timu ya Kenya ilifanikiwa kuzishinda timu
nyingine na kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa Guinness.
Kenneth kamau na Wills Ogutu wote kutoka Nairobi wamefuzu nusu fainali
pamoja na watanzania Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad ambao walipata
nafasi ya pili jana usiku.
Timu
hizi mbili kutoka Kenya na Tanzania sasa zina nafasi ya kuwakilisha
Afrika mashariki na kushinda hadi dola za kimarekani 250,000 pamoja na
kuvikwa taji la ushindi wa Pan-African, watakapoendelea hatua z juu
zaidi. Timu hizi zitahitaji kujiandaa vizuri zaidi na kujiamini ili
kufanya vizuri katika hatua ya nusu fainali.
Timu
zingine nne zitakutana katika robo fainali ijayo ili kuwania nafasi ya
kuingia nusu fainali ya mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.
Usikose
kuangalia robo fainali za Pan-African kupitia televisheni za ITV na
Clouds TV ambapo timu za Africa Mashariki zinapokutana na timu na timu
zingine kutoka Afrika Magharibi huku ukiburudika na kinywaji cha
GUINNESS.
Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
GUINNESS
FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na
kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia
kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV
kila siku ya Jumatano usiku.
Tafadhali kunywa kistaarabu – Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
....................................................................................................................................................
SERIKALI YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO KWA WAKUU, WAMILIKI WA SHULE NA VYUO
Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa
wakuu na wamiliki wa shule na vyuo binafsi kwa minajili ya kuboresha
sekta ya elimu haoa nchini.
Akizungumza
na viongozi wa TAMONGSCO Rais Kikwete amesema sekta binafsi ina
mchango mkubwa wa kuinua elimu hapa nchini hivyo jitihada za pamoja
zinahitajika katika kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza
Rais
Kikwete aliwataka wamiliki na wakuu wa shule na vyuo binafsi kupunguza
ada kubwa wanazotoza kwa wanafunzi ili watanzania wengi hasa wa kipato
cha chini waweze kupata fursa ya elimu.
Aidha
Mheshimiwa Rais alisema serikali iko katika Mchakato wa kutunga Sera
Mpya ya Elimu baada ya ile ya mwaka 1995, umefikia katika hatua za
mwisho na kinachosubiriwa sasa ni maoni ya Wabunge ili Sera hiyo
ikamilishwe na kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu.
Wakati
huo huo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Taasisi ya Elimu
Tanzania itaanza maandalizi ya kupitia upya mitaala ya elimu nchini ili
nayo ilingane na malengo ya Sera Mpya ya Elimu,mahitaji ya maendeleo
nchini na duniani kwa ujumla.
Licha
ya changamoto zinazoikabili sekta ya elimu serikali kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali wa elimu imeongeza sekta hiyo ambapo kuna wanafunzi
zaidi ya milioni nane katika shule za msingi,zaidi wanafunzi milioni
moja na laki nane kwa shule za sekondari na zaidi ya laki moja na
sitini elfu kwa upande wa vyuo vikuu.
WAKATU HUOHUO
Na Gervas Mwatebela, Dar es salaam
Wadau
wa elimu wametakiwa kutoa ushirikiano wa dhati kwa taasisi za sekta
hiyo kwa minajili ya kuboresha hali ya elimu hapa nchini.
Mwenyekiti
wa mfuko wa kijamii wa walimu TGTF bwana Ephraim Mwikuka alisema
mazingira ya sasa ya elimu yana changamoto kubwa kwa upande wa waalimu
na wanafunzi hivyo kuhitaji nguvu za pamoja kuzitatua.
Mwenyekiti
huyo aliongeza kuwa TGTF imejipanga kushirikiana na serikali na jamii
katika kuboresha mazingira ya elimu ya msingi na sekondari hapa nchini.
Bwana
Mwikuka amewataka watanzania kuacha kulalamika bali wachukue hatua
katika kukabiliana na taasisi,jumuiya na serikali kwa ujumla kutatua
changamoto za kielimu katika jamii.
Aidha
Mwikuka aliongeza kuwa elimu ni msingi wa taifa lolote hivyo ni lazima
wadau kwa kushirikaiana na watanzania kuonesha juhudi za makusudi
kuendeleza elimu na si kuibua lawama zisizokuwa na msingi wowote.
..........................................................................................................................................................
No comments:
Post a Comment